Madai ya mgomo Chuo kikuu Dar hayana upeo mkubwa

Nadhani wenye madai UDSM (sio wote waliyasupport esp COET) Walistahili kuomba kiasi chao cha posho wanachopewa kiwe kinaangaliwa mara kwa mara kulingana na fluctuation za maisha na si kujiwekea kiwango fixed km walivyofanya...kwa kua kiwango kinatakiwa kipande ama kushuka kulingana na gharama za maisha kwa wakati!...pili mfumo huu wa kudai kwa kufanya fujo na kuharibu mali ni wa ki- analogue wakati sasa tunakaribia kuiacha digital!
 
Anasa zipo saana vyuoni, lakini je madai yao yanamsingi kimahitaji wawapo vyuoni?
Ama ni agenda fulani nyuma ya pazia?

Naomba kuuliza tu ili nijue.

Kama ungeiruhusu akiri yako ifikiri zaidi ya hapo usingeuliza hilo swali!
 
Wewe pointi yako ni kutuambia kwamba "na mimi nimefika nchi za wengine" ok,tumejua!
Rudisha mawazo yako Tanzania na ujiulize viongozi woooote enzi hizo wanasoma walikuwa wanapata wapi hela kama sio ujamaa ambao leo unaona ni kinyaa kwako!
Yeah nimefika nchi za watu .. jinyonge basi..

Nimesema wapi habari za kinyaa??nimesema wapi habari za viongozi??

Elewa kwanza context ya kitu unachokijibu..otherwise sie wengine tutaona unatafuta mtu wa kukufanyia DRE
 
Wewe ulifanya lipi kati ya hayo kama ulibahatika kusoma?
Na kama ulisoma,ni chuo gani umesoma katika Tanzania?
Unajua likizo za wanachuo zilizo?week3 unafanya kazi gani ya kukupa hela ya kutumia chuo?
Wafanye kazi kwanza si ndio kutaka watu wazae,waolewe na kushindwa kwenda chuo baadae kwa sababu ya majukumu kuzidi?
Ni watu wangapi wana majukumu ya kifamilia wana tushauri "someni kwanza " kabla ya kila kitu!
Mmmmh

Nerejea kukwambia tena..usikurupukie kujibu hoja kabla hujajua context yake..Hoja hapo ni kuwa na mentality ya kujitegemea..usidhanie ni wanafunzi tu wenye mahitaji, na virtually hata ukiwa dumb kiasi utagundua serikali haina hiyo capacity ya kulipa mtu kadiri ya anavotaka..btw, ni mkopo tu huo na wala serikali hailazimiki kuwalipa..unapoomba kitu sdio lazima upewe, hata ukienda benki kukopa huombi tu kama mlevi lazma ukidhi masherti fulanifulani..its commonsense..Hata sisi tulisoma ktk mazingira hayohayo..i tell what ..mie ela yangu ya mkopo wa kwanza zaidi ya nusu nilimpa mama yangu Hawa binti Juma ili kulipa mkopo wa kibanda alichokua anakaa na mimi kubakiwa na 50% iliosalia, wakati some other fellow students walitumia zile ela ndani ya wiki moja zikaisha!..huezi kumuiga tembo kunya..wewe kama unataka kusoma fanya mipango mapema..enzi za ujamaa kudhani serikali ndio baba ndio mama imeshapita.
 
Mkuu hao jamaa ni much know wamefika ulaya! ulaya my foot!

NONSENSE. Hivi mtu kutoa views zako ndio umekuwa much-know?? na wewe mbona unatoa view zako na ww ni much-less au much-upupu??

Leo hii mimi nakatwa mkopo nilioutumia kusoma UDSM, hivi is this not very right opportunity ya bodi ya mikopo ku-make profit kubwa!! wapewe hiyo elfu kumi waweke interest jamaa wakianza kazi wanakatwa life goes on like that! nimesoma Canada 90 perceny ya wanafunziw anategemea mikopo na scholarship...no time to work labda ukiwa summer, siku nyingine ni assignments na lectures they keep you busy to the maximum
Wapewe 10K kutoka wapi? mkopo ni mkopo, haulazimishwi, u take it or you leave it, kama unaona mkopo haukutoshi nenda kwa mkopaji mwengine, simple tu, sioni what the farce is all about.. It is commonsense serikali haina hiyo hela, na hata kama inayo-yapo majukumu mengine ya muhimu na ya muda mrefu..kudhani kwamba serikali inaeza ikaamka tu katikati ya mwaka wa fedha na ku-double the posho is idiotic nortion to begin with..the so called wasomi na their lekchara Waberoya should know this, its so basic!

kwa bahati na fundisha UDSM, haingii akilini kama sio unafiki mtu kusema eti 5000 inatisha kwa siku!!!! kuanzia nauli, chakula na malazi , forget other things!!!

Yeah yeah unafundisha UDSM big deal..does that make you an authority in this context?

wamekuja na hoja ya kufanya kazi, nimewauliza je elimu yetu ya kutoka primary imemfungua mtu uwezo wa kufanya kazi --i mean kujiajiri? au hata kuajiriwa ni sehemmu gani wanazopokea wanafunzi na kukubali part time basis... watu saa kumi wanafunga maofisi, sisi tunamaliza kufundisha mpaka saa 2 usiku siku nyigine!!

Hatuna utaratibu wa kufanya kazi usiku nchi hii, kama kazi za usafi n.k lakini assume wana ji-engage kufanya kazi usiku je wanapata wapi muda wa kujisomea, kumbuka we have system ya ku-disco ambayo nje vyuo vingi vya nje havina!!!!

there are so many challenges kulinganisha bongo na abroad ni makosa makubwa kutokana na culture, muda, mentality na system ya education. bahati mbaya hawaji system ya mlimani wameisikia tu

Kwa hiyo wewe peke yako ndio umesoma Tz?
Hoja imeshaijibiwa hii...kwa mkifupi hakuna formula ya kuji-subsidize mtu..kila mtu kwa nafasi yake na muda wake anajua anaishije na anapata vipi pesa..dunia haiwezi kusimama kukusubiri wewe umake-up your mind. Kuna kukata magogo, uvuvi, kuosha madish, kuuza vocha, kilimo , ufugaji, kufundisha twisheni madogo etc etc..

Haidhuru kama unafundisha UDSM na mentality yako ni potofu kiasi hiki na kushindwa kuona big-picture nasikitika hao wanafunzi wako watakuwa ktk hali gani..no wonder wanataka walipwe 10,000 kana kwamba serikali yao inapata fedha za majini from somewhere. Sijui umesoma lini , lakini nakumbuka sie kipindi tuna soma tulikuwa tunapata mkopo ni Muhimbili na main Campus kama sikosei na SUA au Mzumbe..na wanachuo walikuwa wachache..leo kuna body ya mikopo na kila mwanafunzi anaruhusiwa ku-apply mkopo na idadi ya wafaidika na mikopo imeongezeka maradufu, this means situation is more tricky.

Hata kama ningekuwa prezidaa leo hii, hii ishu ya posho isingekuwepo kwene to-do list yangu ya vitu 100 vya kwanza.
 
Binafsi naeza kusema they should have made a request to yhe government ili wapate kuongezewa,.tunaeza kusema kuwa 5thousand inatosha but with the current life in tz ni ngumu kwakweli,bei ya vitu inaongezeka every day!.the fixed amount ya 5thousand sio fair in relation to the inflation..kuna mahitaji mengi tu that some people who are totally poor and only depend on the loan for their survival that makes 5000 not sufficient.
 
Jamani tunapo jadili vitu ambavyo ni vya muhimu inatubidi tuwe makini na tusihusishe ushabiki, aidha wa kichama au wa kidini. suala la Candid kusema kwamba ''mgomo wa chuo kikuu hauna upeo'' na kuanza kulinganisha chuo kikuu chetu na vyuo vya nje linatupa mashaka kuwa yawezekana Candid hajasomea Tanzania au lah Candid sio mwenzetu kikipato au kuna uhusiano wa karibu kati yake na matatizo yanayokumba vyuo vikuu vyetu (yaani ni official katika serikali). Tusipotoshwe na watu kama hawa. Watu ambao hawajui hata mpangilio wa vipindi katika Vyuo vikuu vetu. eti wanafunzi wafanye part time!!! kuna muda wa part time vyuoni? mtu umeanza vipindi saa moja asubuhi na kipindi cha mwiisho saa mbili usiku utapata part time?. Candid soma kwanza mfumo wa elimu katika vyuo vikuu vyetu ndio uanze kuchangia hoja zinazohusu vyuo vikuu vyetu lasivyo usichangie kabisa utajishushia heshima yako mbule kwa sababu utatupa wasiwasi na kiwango chako cha elimu.
 
Ifike mahali tujadili mambo kutokana na uzito wa mambo yenyewe, isiwe tu kuropoka na kujaza kurasa za jf, niko katika maeneo ya chuo kikuu kwa miaka mitano sasa, sh 5000 haitoshi kabisa, gharama za copy, ubwabwa, maji ya uhai lita5,yamepanda mpaka sh 1500 kutoka shs1000,maeneo ya mabibi hostel,kwingine sijui
pia ikumbukwe kuwa huu ni mkopo na sio malipo kama baadhi ya wachangiaji wanavyoiita, kwa hiyo ni bara anayekupa mkopo akukopeshe thamani inayokutosha coz utailipa.
kuhusu hoja ya watumishi kwenda vijijini, hivi mtoa hoja we unavijua kweli vijiji vta tz? au kwa vile umesoma abroad unafikiri vijiji vya tz ni sawa na 'texas'? tafakari kiasi alafu ulete mada,sisi tutachangia, tusiwe wepesi kuwalaumu vijana.
 
Yeah nimefika nchi za watu .. jinyonge basi..

Nimesema wapi habari za kinyaa??nimesema wapi habari za viongozi??

Elewa kwanza context ya kitu unachokijibu..otherwise sie wengine tutaona unatafuta mtu wa kukufanyia DRE

DRE?? Shusha jazba kidogo.punguza matisho na ujadili hoja.
 
Kwa Tanzania haiwezekana kufanya "undergraduate" wakati unafanya kazi!!! Unless "ufanyiwe" sehemu kubwa ya "home work" na wanafunzi wenzako!
 
Siasa za ujamaa zimetuharibu..kila kitu tunasubiri serikali, serikali, serikali.. kwa wanginewe tulioshuhudia nchi zengine mtu anajisomesha yeye mwenyewe..mchana anapiga mzigo, usiku anaenda kupiga kitabu..sisi tunataka kila kitu kiekwe mezani TULE.

Una heri wewe uliye na uwezo wa kwenda nje (Wengi wetu pasipoti hatuna). Hata kama wangetaka wafanye kazi mchana au usiku, hiyo kazi yenyewe iko wapi? Waliomaliza digrii zao hawana kazi, sembuse ambao bado wanasoma? Labda tuwashauri wawe wakabaji au waibe kwa kutumia mtandao. Ulaya ni tofauti na hapa kwetu.
 
Naona unatafuta kufanyiwa DRE, hivi wewe ndio umepewa kifaa cha kupimia hoja JF?

we bwana mdogo mbona unapenda sana hilo neno la DRE?
Ushawahi kupigwa SOAP ENEMA wewe?
Usilete ujuaji hapa jf.kuna wajuaji zaidi yako.&a$$€h0&le3.
 
Mimi nadhani kijana mpaka anafika chuo kikuu anakuwa ameshakuwa mtu mzima. Tunapotoa madai lazima tizingatie hali halisi pamoja na uzalendo. Fikiria kama mzazi wako ninalipwa mshahara wa shilingi 200,000 kwa mwezi, nimeweza kukusomesha hadi umefika chuo kikuu, nimesomesha wadogo zako wako sekondari, nimelipa kodi ya nyumba na kugaramia chakula cha familia, leo vipi wewe ushindwe kutumia 5,000 kwa chakula tu? Wewe unatumbo kiasi gani la kushindwa kutosheka kwa chakula na kinywaji cha 5,000 kwa siku? Ningetarajia uandamane ili mshahara wa mzazi wako upande zaidi ili wadogo zako wasome zaidi. Wenzako wakati tunasoma chuo kikuu miaka kadhaa iliyopita tulikuwa tunapewa 1,500 kwa siku na tuliweza kula, kunywa na kujibana bana ili kuchangia ada za wadogo zetu.

Mimi nadhani
 
wakati unalipwa sh 1500 sukari,maji na chapati zilikuwa sh ngapi?na sasa hivi ni sh ngapi.proportionally sema ulikua unatumia % ngapi kwa chakula na malazi?
 
WEWE UMELOGWA NA KAMA WEWE SIO BASI BABAKO NI FISADI AU BASI UME IKOSA ELIM YA CHUO KIKUU ELFU 5000 KWA MAITAJI YA LEO NI SAWA NA 0 HIVYO WANA MADAI YA MSINGI NA WADAI MPAKA KIELEWEKE:msela:
 
Sasa huu ufisadi wa jakaya na uu ubepari ndio wenye tija kwako na pili wewe umejisomesha elim yajuu au umetumwa kupunguza makali
 
Du hapana kabisa kuwalipa 330,000/= kwa mwezi wakati hatuna hakika watafaulu wote na kuanza kazi ni unafiki. Kazi wajitafutie wenyewe km wengine tulivyofanya na vyumba ni jukumu lao km mabibo pamejaa. Hivi hiyo hela itatoka wapi? kila mwaka wanaongezeka na Watanzania ndio wanaowakopesha kwanini JKT isingerudi ? wajifunze Uzalendo kula kulala kusoma wangevijua iko siku tutashindwa wadhibiti hawa vijana

Hivi ni jukumu la serikali kupeleka watu vyuo vikuu. Huyo serikali ni nani? Tatizo ni kuwa hawa wanafunzi wanesahau kuzungumzia Taifa wanazungumzia serikali. Hwa ni watoto wa serikali? Nci nyingine hawajiingizi kwenye tuition. Wanachojua ni kukupa admission, wewe utajua utakapopata ada. Huku bodi ya mikopo mtu angeenda mwenyewe akachukua mkopo wake, akatoa dhamana mwenyewe. Usipolipa wanakuondoa kwenye system hata library huwezi kuingia! Kama walivyosema wachangiaji wangine, watu ahapa hawajui kitu kinachoitwa "work study" Badala ya kuajiri watu kutoka mitaani kufanya kazi cafeteria, library, janitorial n. k., wanaajiri wanafunzi ambako ndiko wanapopata fedha ya kujikimu na hata kulipa tuition. Ukikosa fedha ya kula huendi serikalini. Hii kitu iko Marekani katika vyuo karibu vyote. Watu wanafanya kazi usiku na mchana muda ambao hawana vipindi. It is time they stop demanding salaries without working and do some serious work to sustain themselves. Hizi laki tato na elfu thelathini ni fedha amazo wanalipwa baadhi ya watumishi wa umma, hata waliomaliza shahada ya kwanza chuo kikuu (nina ushahidi!!!), tena wana familia na wategemezi. Hawa wanafunzi wanaishi maisha mazuri kuliko hata baadhi ya walipa kodi ambao ndio wanaochangia hizo fedha. Kama unabisha, tembelea makazi ya baadhi yao!!
 
Mpendwa huku TZ wanafanya kazi usiku na mchana??
Unajua ratiba za masomo mlimani?
Unajua hivyo vyuo huko USA havina disco na hapa kwetu disco ndio ujiko wa baadhi ya maprofessa
Unajua kuwa elimu ya kutoka primary to university ina mchango mkubwa kumfungua mwanafunzi kujitegemea? system yetu ya elimu ikoje?

Unachosema ni sawa kabisa ila hiyo ni USA, unapolamismisha na hapa iwe hivi ili hali tunaona is impossible ndipo hoja zinapokuwa zinakinzana kwa mbali sana!!

cheers!!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom