pefla
Senior Member
- Jan 31, 2012
- 105
- 74
ELIMU ILIFIA CHUO KIKUU au ILIZIKWA CHUO KIKUU?
Imeandikwa na ASKOFU BAGONZA
Mzee Jenerali Ulimwengu kasema vyuo vikuu vyetu ni kama Extended High School. Anayebishi anitafute. Sababu ni nyingi kama idadi ya wajinga wetu waliosoma vyuo vikuu.
1. Tulipokuwa na Chuo Kikuu kimoja, tulifuta ujinga kwa asilimia 85. Sasa tuna vyuo vikuu zaidi ya 50, tuna wajinga wengi mitaani na maofisini kuliko enzi ya chuo kikuu kimoja.
2. Vyuo vilitengeneza wanasiasa na viongozi makini. Waliposhika madaraka wakapiga marufuku mijadala ya kisiasa na kijamii katika vyuo vikuu.
3. Wakati ule wanafunzi wa vyuo vikuu waliwahoji watawala, siku hizi watawala wanawahoji wanafunzi wa vyuo vikuu.
4. Vyuo vikuu vilizalisha wachambuzi na watafiti. Siku hizi vinazalisha ma-chawa na wapiga debe. Hata mbunge mwenye darasa la saba anaajiri wapiga debe kutoka chuo kikuu. Nampongeza.
5. Kuna tofauti ndogo inayotenganisha uchawa na ujinga. Wote wanazalishwa katika vyuo vikuu. Mmoja anaishi ofisini na mwingine anaishi mitaani akiunga mkono asiyoyajua.
6. Elimu ya wakati ule ilichochea uasi mtakatifu (holy rebellion). Hii ya sasa inachochea woga na utii usiomnufaisha anayetii.
Nini kilitokea?
Waliohitimu chuo kikuu walienda kuua elimu kuanzia shule za msingi. Vyuo vikuu vikageuka kuwa mhanga wa mafanikio yake. Kwa hiyo elimu ilifia chuo kikuu na kuzikwa chuo kikuu.Shule za Msingi na sekondari ni vitalu vya uzalishaji unaoenda kukuzwa chuo kikuu.