Madai ya mgomo Chuo kikuu Dar hayana upeo mkubwa

MAWAZO YAKO HAYATOFAUTIANI NA YULE MVIVU WA KUFIKIRI, EPHRAIM KIBONDE!
Kama viongozi wa serikali wenyewe wamekiri kuwa pesa hiyo ni ndogo kulingana na gharama za maisha ya sasa,,,,wewe umeibukia wapi na vimadai vyako vya kitoto!Infact wewe ndo unamawazo ya kitoto na kilimbukeni,,,embu kaa ufikirie,najua wewe ni kilaza ila fikiria hili:-
UNALINGANISHA KIPATO CHA WANAFUNZI NA MAASKARI??

KIMSINGI Mr. Kilaza tafuta kitu kingine cha kuzungumzia, NAONA ELIMU YAKO NI YA KUUNGAUNGA NA HAIJAKUSAIDIA HATA KIDOGO!!!!!!!!!!

jibu hoja!
 
hawa wanafunzi wanadai nyongeza ya shs laki moja na nusu kwa mwezi. kiasi hiki ni kidogo sana ukilinganisha na michango ya wazazi wao wanayotoa kwenye harusi kila mwezi. Wazazi wanatumia hela nyingi kusomesha watoto sekondari, ikifika chuo kikuu wanasema hawana uwezo. hii imekaaje? tupunguze michanggo ya kwenye harusi, kitchen party, komunio nk nk tuwekeze kwenye elimu. no shortcut to progress.
 
pesa inatosha kwa mwanafunzi yeyote (hata asiyejiweza) IKIWA ITATUMIKA SPECIFICALLY KWA MEALS AND ACCMDTN kama bodi walivyoitoa.
STATIONERY na FACULTY RQRMENTS ni elements nyingine za mkopo.
Mtanzania wa kawaida atakuelewa kama utaomba kuongezewa elements za kukopeshwa NA sio kusema kuwa unakula zaidi ya 4500 kwa siku. Tuko Tanzania jamani, kudai hiyo fedha ni anasa na atlast zinaumiza wazazi wetu wakulima na wafanyakazi.
Pesa haiongezwi from nowhere, kuna mahali itapunguzwa. Na viongozi wetu wa Africa wanapunguza toka kwa haohao maskini.
Kama nauli, vocha, nguo mnaona vina uzito wa kustahili kukopeshwa, JENGENI HOJA BODI IONGEZE THAT LOAN-ELEMENT.
Be wise, be patriot for your country!
 
kuendelea kuamini hiyo fedha inatosha(kwa meal&accomodation) bila kutoa mchanganuo wa matumizi yake ni ushabiki na ubishi usio na tija.
Labda nikuulize ni sekta ipi haswa ambayo serikali imepeleka hela ya kutosha?kwa sababu walimu au madaktari wakigoma utaambiwa fedha zinasomesha au zinanunuliwa dawa,kinachoonekana ni serikali kutumbua na kula bata kwa kodi za wananchi.
Madhara ya kuwaacha wanafunzi wateseke ni makubwa kwani watakapomaliza chuo itabidi waweke uzalendo kando na kufanya biashara.imagine daktari,nesi au mwalimu aanze kutoa huduma yake kibiashara zaidi tutafika?
 
Kueni makini na thread zenu, chambu kwanza unayoongea kabla ujafanya ulinganifu, kusema umesoma nje na hapa nchini nishaanza kuweka shaka, inaonekana mazingira ya elimu ya juu huyajui kabisa, uwezi tamka mathalani mtoto wa udsm yaani undergraduate afanye kazi na kusoma.. vyuo vingi vya nje unakuwa na kama masaa 15 kwa wiki then u cn manage mtoto wa udsm yupo ful tym until 8pm.. how cud this b pocbo... na doubt kama una elimu ya juu... FIKIRI KWANZA NDUGU, NI NGUMU SANA KWA 1ST DEGREE KUSOMA HUKU UNAFANYA KAZI, LABDA UENDE OPEN UNIVERSITY.
 
Kiwango cha posho ya Tsh 5000 kwa siku kwa mwanachuo kwa mazingira ya sasa kwa Tanzania, ni kiwango kinachoweza msaidia kama anaakili ya kupanga vizuri bajeti yake. Kama wanachuo wanataka kuishi kwenye hoteli za gharama au kifahari ni jukumu lao na wazazi wao kuongeza pesa za kujikimu kifahari. Kiwango cha Sh laki moja na nusu kwa mwezi kama yuko makini na kufikiria zaidi future yake anaweza panga vizuri bajeti na akaishi bila tatizo kubwa. Ila kama anataka awe anakwenda kula Hamburgers McDonalds ni juu yake na familia yako kuongeza matumizi.

Tumepitia vyuo vya Tanzania na tumepitia vyuo vya mataifa makubwa, kwa ulinganifu katika masuala ya posho naweza sema kumbe Tanzania ni bora mwanafunzi anaweza pata posho hiyo kuliko vyuo vya nchi tajiri. Watu hatukulala usingizi ni darasa na kazi. Uwapo kazini wakati wa mapumziko ndo unafanya homework, hakuna kulaza damu.

Tusiwe watu wa kulaumu serikali katika kila kitu, tulaumu yale ya msingi lakini katika hili mimi binafsi nasema hapana.

Watanzania tuko wavivu mno wa kujituma na kufikiri. Mazingira yako huru mno kujishughulisha Tanzania kuliko mataifa yaliyoendelea.

Utakuta walimu wanakimbilia kufundisha shule za mijini, kumbe shule za vijijini zina nafasi zaidi kwa kujiongezea pato kwa kujishughulisha na kilimo au kufungua biashara ndogo ndogo kusaidia wanavijiji kupata bidhaa ambazo wanapata taabu kuzifuata mbali. Mshahara wake ungezalisha zaidi kuliko mijini anamalizia kwenye starehe na gharama kubwa ya maisha.

Athari wanazopata wanachuo katika migomo yao ni kubwa kwao wanafunzi kuliko viongozi wanaowanyooshea vidole wakati wanaishi maisha ya starehe, na waendapo vyuoni ni kwenda kuwapiga msasa wa kisiasa tu. Kinachofanyika sasa vyuoni ni kama cheer ambayo ni kufuata mkumbo tu na kulazimisha wasiotaka lazima wafanye vinginevyo watadhurika, huku ni kuwanyima wengine uhuru wao wa kujiamulia wanavyotaka. Haki ya uhuru ni uamuzi wa dhamira safi baada ya upembuzi yakinifu.

Serikali ina mengi ya kufanya si wanafunzi tu, elimu, mawasiliano, afya, na huduma nyingine za jamii. Hata Chama kingine kikitawala hakitamaliza matatizo hayo kwa siku moja.

Kwanza nashukuru baada ya kusoma ilibidi nizime computer nilale otherwise ningepewa "Total ban"
Mkuu,unadai elfu 5 inatosha?
Sawa,inategemea na unaitumia vipi either kama familia au kwa kula mlo mmoja kwa siku!

Sikiliza moja kati ya hoja za wanachuo,hii ni yangu na nawakilisha wengi sana

1.Sijapata hostel wala Main campus room,kwa sababu hiyo basi nimepanga chumba 360,000/= @mwaka,tunaishi wawii,so 180,000/= kwa mwaka
2.Tunapoishi ubungo,maji una nunua ndoo moja sh.500 hadi700 siku nyingine,unahitaji ndoo ngapi kwa siku?
3.Umeme kwa mwezi hadi december ilikuwa 6000/=,saivi 10,000/= kwa mwezi,--->120,000/= kwa mwaka
4.Unahitaji nauli kwenda chuo na kurudi kila siku
5.Unahitaji kula asubuhi,mchana,jioni (sh.ngapi kila mlo hapo?)
6.Ninasoma B.Sc in computer science,....laboratory hazifanyi kazi zote,nahitaji computer kwa ajili ya masomo yangu,faculty requirement nazopewa ni sh 60,000/= kwa mwaka,una nunua computer gani?
7....

Hayo yoooote ni mahitaji yaliyo ya muhimu,sijaongelea kununua vocha kwa ajili ya simu hapo,na katika mahitaji hayo yote inabidi ujibane na utumie 5,000/= kwa siku unayopewa kwa siku ili uweze kuyafanya!
Kwa mtazamo wako kweli unaweza kuishi dar hii kwa kiasi hicho cha hela?
 
Naomba wahusika (wanachuo) watueleweshe , tusitoe hukumu pasipo kusikiliza pande zote. Kila mtu ana haki ya kusikilizwa.
 
Funguka akili yako tafuta njia mbadala ya kuongeza kipato uwapo likizo.
Ulimwengu mzima hakuna anayeweza kujitosheleza kwa kutegemea msaada tu ila mwenyewe ufunguke akili namna gani uongeze ziada

1.Njia mbadala kama zipi?Unazani una akili zaidi ya wale watu zaidi ya elfu10 walio kuwa wanaandamana kudai nyongeza ya hela?
2.Nani kakwambia tunaomba msaada?
Huu ni "mkopo" dammit kama hujui nini kinaendelea au bahati mbaya hukubahatika kusoma chuo kikuu kaa kimya ukiongea sana utakuwa kama kibonde
 
Siasa za ujamaa zimetuharibu..kila kitu tunasubiri serikali, serikali, serikali.. kwa wanginewe tulioshuhudia nchi zengine mtu anajisomesha yeye mwenyewe..mchana anapiga mzigo, usiku anaenda kupiga kitabu..sisi tunataka kila kitu kiekwe mezani TULE.

Wewe pointi yako ni kutuambia kwamba "na mimi nimefika nchi za wengine" ok,tumejua!
Rudisha mawazo yako Tanzania na ujiulize viongozi woooote enzi hizo wanasoma walikuwa wanapata wapi hela kama sio ujamaa ambao leo unaona ni kinyaa kwako!
 
Nafikiri unajadili event badala ya concept..

Concept hapo ni kujitegemea sio mgawanyiko wa masaa ya kusoma mchana na usiku, na jinsi mtu atavojishikiza. Kujitegemea kwamba mtu kuwa proud kugharamia elimu yake. Kama huezi kutafuta walau fedha wakati wa semester au term, basi fanya hivo wakati wa likizo. Kama hiyo nayo huezi basi tafuta pesa kabla hujaanza masomo..hamna kisingizio hapo.

Wewe ulifanya lipi kati ya hayo kama ulibahatika kusoma?
Na kama ulisoma,ni chuo gani umesoma katika Tanzania?
Unajua likizo za wanachuo zilizo?week3 unafanya kazi gani ya kukupa hela ya kutumia chuo?
Wafanye kazi kwanza si ndio kutaka watu wazae,waolewe na kushindwa kwenda chuo baadae kwa sababu ya majukumu kuzidi?
Ni watu wangapi wana majukumu ya kifamilia wana tushauri "someni kwanza " kabla ya kila kitu!
Mmmmh
 
mchanganuo wako ni mzuri lakini uko more theoretical.
Mfano tuchukulie matumizi ya mwanafunzi ya kila siku.
1.chai na chapati 2=600/-
2.sahani ya wali na nyama=2000/-(mchana)
3.chipsi mayai=1500/-(jioni)
4.maji madogo 2,soda 1=1500/-
5.fedha ya chumba kwa siku=500/-
Jumla =6100/-
hapa unaona ile fedha wanayopata kwa ajili ya meal na accomodation(5000/-) haitoshelezi hata ujaribu kujibana kiasi gani,yaani usinywe bia wala humberger.
Si hivyo tu,ukweli uliopo mtoto wa mkulima kutoka tandahimba anapochaguliwa kuja chuo anatarajiwa kuchangia ada ya mdogo wake pale kijijini.kuna gharama nyingine za msingi ambazo mwanafunzi anakabiliana nazo mfano nauli ya kwenda chuoni kwa wale wanaoishi nje ya campus,stationaries kwani hela wanayopewa kwa mwaka ina uwezo wa kununua kitabu cha course ya semester 1 tu,radio hata ya mkulima tu,simu na vocha kwa mawasiliano,surawili na tai ili uonekane mwanachuo kweli.

Tanzania haijaweka mazingira ya wanafunzi kufanya part time job.hakuna viwanda vinavyofanya kazi usiku,lakini pia mwanafunzi wa chuo(form vi leaver) hana ujuzi wowote wa yeye kuweza kufanya kazi.kuna mradi kama mlimani city ungeweza kuajiri wanafunzi but sidhani kama unafanya hivyo.
Sidhani kama unafurahia kuona watoto wetu wa kike wanachuo wakijiuza pale posta.

Kwa ufupi madai ya wanafunzi yana msingi na yanahitaji kuangaliwa kwa umakini bila ushabiki wa kisiasa.
Mapendekezo:badala ya kutoa fedha ya meal&accomodation serikali kupitia board ya mikopo ikopeshe fedha ya KuJIKIMU ambayo itajaribu kuadress mahitaji muhimu ya mwanachuo.lakini hii isiwe kwa wanafunzi wooote isipokuwa wale wachache waliofaulu vizuri(div one na two).hii itaondoa migomo ya mara kwa mara.
Hii hela inatosha kama kule hostel kugekuwa na miundombinu amabayo inamwezesha kijana kujipikia.
Kwa mfano kama angekuwa anajipika mwenyewe asingehitaji kununua maji/soda angechemsha tu maji ya DAWASCO, sh.2000 ya lunch inatosha 1/2kg ya nyama, chai angenunu sukari na kupika mwenyewe maandazi/chapati kwa hiyo kwa siku angetumia sh.2000-4000 tu. Kutokana na hili wanafunzi wengi wa Tanzania wanapata shida sana wanapo kwenda kusoma nje kwa sababu hawajazoeshwa kujipikia.
 
Mkubwa hivi unajua mazingira ya shule za vijijini kweli???? Unajua shughuli za kilimo zinavyofanyika vijijini na jinsi zinavyolipa???? Unajua purchasing power ya wanavijiji wa kweli huko vijijini??? Nina mashaka kama unafahamu hayo yote.

Otherwise usingezunguzia hayo uliyoyazungumzia kirahisi hivyo.....

Watu kama hao ndo washauri wa serikali yetu usiwashangae,ni pumba kwanzia mawazo yao hadi wao wenyewe
 
1.Njia mbadala kama zipi?Unazani una akili zaidi ya wale watu zaidi ya elfu10 walio kuwa wanaandamana kudai nyongeza ya hela?
2.Nani kakwambia tunaomba msaada?
Huu ni "mkopo" dammit kama hujui nini kinaendelea au bahati mbaya hukubahatika kusoma chuo kikuu kaa kimya ukiongea sana utakuwa kama kibonde

Wewe pointi yako ni kutuambia kwamba "na mimi nimefika nchi za wengine" ok,tumejua!
Rudisha mawazo yako Tanzania na ujiulize viongozi woooote enzi hizo wanasoma walikuwa wanapata wapi hela kama sio ujamaa ambao leo unaona ni kinyaa kwako!

Mkuu hao jamaa ni much know wamefika ulaya! ulaya my foot!

Leo hii mimi nakatwa mkopo nilioutumia kusoma UDSM, hivi is this not very right opportunity ya bodi ya mikopo ku-make profit kubwa!! wapewe hiyo elfu kumi waweke interest jamaa wakianza kazi wanakatwa life goes on like that! nimesoma Canada 90 perceny ya wanafunziw anategemea mikopo na scholarship...no time to work labda ukiwa summer, siku nyingine ni assignments na lectures they keep you busy to the maximum

kwa bahati na fundisha UDSM, haingii akilini kama sio unafiki mtu kusema eti 5000 inatisha kwa siku!!!! kuanzia nauli, chakula na malazi , forget other things!!!

wamekuja na hoja ya kufanya kazi, nimewauliza je elimu yetu ya kutoka primary imemfungua mtu uwezo wa kufanya kazi --i mean kujiajiri? au hata kuajiriwa ni sehemmu gani wanazopokea wanafunzi na kukubali part time basis... watu saa kumi wanafunga maofisi, sisi tunamaliza kufundisha mpaka saa 2 usiku siku nyigine!!

Hatuna utaratibu wa kufanya kazi usiku nchi hii, kama kazi za usafi n.k lakini assume wana ji-engage kufanya kazi usiku je wanapata wapi muda wa kujisomea, kumbuka we have system ya ku-disco ambayo nje vyuo vingi vya nje havina!!!!

there are so many challenges kulinganisha bongo na abroad ni makosa makubwa kutokana na culture, muda, mentality na system ya education. bahati mbaya hawaji system ya mlimani wameisikia tu
 
Madai ya wanafunzi vyuo vikuu ni utoto, ulimbukeni . ni vigumu eti leo mwanafunzi alipwe elf 10 kwa siku huku mfanyakazi Polisi, Mwalimu na wafanyakazi wengine wakilipwa elf 4 kwa siku.

Mtoto aliyeamaliza kidato cha 6 juzi na kujiunga chuo eti leo andai mapesa mingi kiasi hicho.anataka alipwe au kwa jina la kisomi mkopo wa elf 10 kwa siku . Lkn bado maraha, amstarehe wanayofanya vyuoni hazitasaidia, hazittaosha na matatizo yatazidi. vimwana na vibaba vitazidim kulala vyumba vya wanafunzi kama mabibo kufanya majabozi , kwani baadhi yao huona wakiwa chuoni ndio mwanzo wa maisha ya juu.

Simu ya bei kubwa, redio kubwa chumbani, friji, tv na mambo mengine ya anasa huku familia zao zikila muhogo mchugu na dagaa. huku wanafunzi hao wakitoka familia maskini wakitumia fedha hizo kw anasa. Club zote za pombe na vinywaji vichafu wakifurika, disko, muziki na maisha ya ajabu yakiwa ndio maisha yao ya kila siku, wengine wakina mji huku wakiwa n elf 5 kwa siku huona tayari ajira kwao

Sasa wewe ndo kibonde mwenyewe,na kama sio kibonde basi mawazo yako yana matatizo sanaaaaa!
Huyo polisi kasoma hadi wapi hadi alingane hela na mwanachuo?
Huyo mwalimu wa elf4 unae muongelea na huyo mfanyakazi wamesoma hadi level gani wakapewa hizo hela?
Kama wanalipwa hela ndogo kiasi hicho na bado wanakaa kimya basi na wasi wasi na "akili na elimu zao"!
Tunasoma ili tujue jinsi ya kujitetea katika kila hali,kama unawaita wamesoma hao polisi,walimu nk na bado wanaonewa wamefyata mkia shauri zao,kama unaona wivu kuzidiwa hela na mwanachuo kajinyonge maana 10,000/= iko njiani mkuu
 
Hii hela inatosha kama kule hostel kugekuwa na miundombinu amabayo inamwezesha kijana kujipikia.
Kwa mfano kama angekuwa anajipika mwenyewe asingehitaji kununua maji/soda angechemsha tu maji ya DAWASCO, sh.2000 ya lunch inatosha 1/2kg ya nyama, chai angenunu sukari na kupika mwenyewe maandazi/chapati kwa hiyo kwa siku angetumia sh.2000-4000 tu. Kutokana na hili wanafunzi wengi wa Tanzania wanapata shida sana wanapo kwenda kusoma nje kwa sababu hawajazoeshwa kujipikia.

Hakuna hiyo miundombinu tena ni kosa la jinai kupika kwenye vyumba vya chuo, nje is ok, utakuta hizi facilities zote zipo
 
Sasa wewe ndo kibonde mwenyewe,na kama sio kibonde basi mawazo yako yana matatizo sanaaaaa!
Huyo polisi kasoma hadi wapi hadi alingane hela na mwanachuo?
Huyo mwalimu wa elf4 unae muongelea na huyo mfanyakazi wamesoma hadi level gani wakapewa hizo hela?
Kama wanalipwa hela ndogo kiasi hicho na bado wanakaa kimya basi na wasi wasi na "akili na elimu zao"!
Tunasoma ili tujue jinsi ya kujitetea katika kila hali,kama unawaita wamesoma hao polisi,walimu nk na bado wanaonewa wamefyata mkia shauri zao,kama unaona wivu kuzidiwa hela na mwanachuo kajinyonge maana 10,000/= iko njiani mkuu

well said!!!
 
Hii hela inatosha kama kule hostel kugekuwa na miundombinu amabayo inamwezesha kijana kujipikia.
Kwa mfano kama angekuwa anajipika mwenyewe asingehitaji kununua maji/soda angechemsha tu maji ya DAWASCO, sh.2000 ya lunch inatosha 1/2kg ya nyama, chai angenunu sukari na kupika mwenyewe maandazi/chapati kwa hiyo kwa siku angetumia sh.2000-4000 tu. Kutokana na hili wanafunzi wengi wa Tanzania wanapata shida sana wanapo kwenda kusoma nje kwa sababu hawajazoeshwa kujipikia.

Mkuu,najipikia mimi na natumia jiko la gesi hapa!
Siku nikipika naweza tumia hata sh.3000!
Lakini angalia gharama zingine hizo za kuishi mtaani,siku nisipo pika hapo natumia hadi 6000!
Sasa hata kupika saivi ni kero kabisa,gesi imepanda mara mbili,.....hela iko pale pale elf5 shit
 
Anasa zipo saana vyuoni, lakini je madai yao yanamsingi kimahitaji wawapo vyuoni?
Ama ni agenda fulani nyuma ya pazia?

Naomba kuuliza tu ili nijue.

We unavuta bange lazima,maana hujui unasimamia nini!
 
hebu changanua hiyo 5000 jinsi wewe ungeitumia kwa siku.

usiweke unafiki.

usi-assume kuwa uko mwaka wa pili, tatu au nne (hawa hawana garantii ya kupata vyumba kwenye mabweni ya chuo).

assume kuwa unaishi main campus au mabibo hostel.

You are a great thinker man!
 
Back
Top Bottom