Madai ya mgomo Chuo kikuu Dar hayana upeo mkubwa

Mimi naona tunatoka nje ya pointi. Suala la kulipa au kutolipa deni la Dowans halina uhusiano na kuongeza au kutokuongeza posho za wanafunzi. Yapo maeneo mengi mhimu zaidi ambako fedha hizo zingehitajika zaidi ya kupandisha posho za wanafunzi. Kwa mfano, matokeo ya kidato cha nne mwaka huu yanatisha. Moja kati ya sababu ni uchache wa walimu na vitendea kazi. Tungetarajia tuseme kwamba fedha hizo zitumike kuongeza mishahara ya walimu. Walimu wa shule ya msingi kwa mfano take home yao haizidi 5,000 kwa siku na wanafanya kazi

Halafu kumbuka pato hilo la mwalini ni kwa ajili ya kujikimu yeye na famijlia, kusomesha watoto, kusomesha watoto waliochuoni kama hao wanaodai nyongeza.
 
wewe hujasoma tanzania. Tanzania hakuna mabox ya kubeba au wazee wa kuwaangalia wakati wa likizo kama mnavyofanya huko "majuu".

wengine huwa wanaolewa huko,,, hayo mabox tukabebe kwa kikwete au? Kama waliomaliza wapo mtaani na ajira hawana..

Niko mazingira ya chuo daily. Nakutana nao karibu kila kona, ndani na nje ya chuo. Ni vijana ambao ni wadogo kiumri hata kifikra. Wanapenda maisha ya fasta. Hawataki kutoa jasho. Kama hawataki kutoa jasho katika kusoma watatoa jasho katika kutafuta hela? Ni mambo mangapi muhimu ambayo huwa wanayapigania kama si maslahi? Ndio maana wenzao wa COET wakawasusia mgomo wao.

Serikali huwa inaamua kukutana nao ili tu kuondoa kiwingu. Ni kweli hawana hoja za msingi sana. Wanataka kuishi kama wafanya kazi wakati hata hao wafanyakazi wanaishi kwa hiyo laki unusu kwa mwezi tena wakiwa na familia.

Miaka mitatu au minne si mingi kwa kukaa chuoni na kusoma. Serikali iwaongezee tu ila wajue kuwa madai yao si ya msingi sana. Wangeandamana kwa ishu ya DOWANS na katiba wangeonekana wa maana ZAIDI
 
Kitu kimoja muhimu tukielewe wengi wa wanachuo wapo katika kipindi kile cha mabadiliko ya umri kutoka utoto kwenda utu uzima (teenage turning into matured age). Na wanasaikolojia mnajua fika vijana wengi walio katika umri huo ilivyo ngumu kuelewa mambo mengi ya msingi. Na kabisa katika umri huo wengi ni rahisi sana kufuata mkumbo tu mradi wanafikiria maslahi yao. Most of them do not control themselves. Katika mataifa yaliyoendelea tunaona umri huo ndio ulioathirika zaidi katika matumizi ya madawa ya kulevya. Wanahitaji wanasaikolojia, na bahati mbaya vyuo vingi Tanzania havina vitengo vya wanasaikolojia kuwasaidia vijana, na kama vipo havitiliwi uzito unaostahili.

Hiyo ndio halihalisi kwani hata ushauri mzuri ambao wengi wanajitahidi kuwawa vijana wetu hawafungui akili kuupokea
 
Tumesoma Chuo tukipata 2500, Tuliishi nje ya Chuo. main Campus ngumu. Wengine walikuwa wanatoa Rushwa kupata main campus hosteli. .... Kwa sisi watoto wa Kimaskini ukishazoea Hosteli ukimaliza Tu shule utaanza pata tabu. ni vema ukaanza kuzoea kuishi na wananchi mapema. kwa pesa hio hio tuliweza fanya yote muhim ya chuo. na kulipa Kodi mtaani...na kuwasaidia wengine.. ..wapo wengine for the same amount waliweza nunua used computer...!!

Wengi wa wanafunzi hawana washauri. wanakwenda kimkumbo. Utakuta mtu anakwenda Nunua TV/Friji/Redio wakati anaweza nunua Computer used ikamsaidia kwa mambo mengi tu ya Masomo yake. Wengine wanaiga...na wengine ni Ujinga wa Kutoka Nje ya DSM anakuja DSM anavamia starehe, baada ya wiki boom alopewa anakuwa ameishiwa...!!!

Tatizo jingine la kuandamana wanafunzi wanataka wanafunzi waandame hata wale ambao hawataki kuandamana.msipoandamana Ugomvi...!!!
 
Vijana wana haki ya kudai posho kuwa Tshs 10,000.00 maana elfu tano haitoshi kabisa , pia ni mkopo ambao utarudishwa
 
Katika moja ya maoni yangu katika safu hii nilisema athari za migomo vyuoni mwadhirika ni mwanafunzi badala ya serikali au uongozi wa vyuo.
Haya Wanachuo wa Chuo cha Tumaini Dar Es Salaam (Kurasini) wamefukuzwa sababu ya mgomo, na wanaotaka kurudi waandike barua ya kujieleza kwa uongozi wa chuo na iwe imefika February 11 kwa njia ya posta. Hakuna mtu kukanyaga ardhi ya chuo.

Nawashauri wanachuo tulieni na sikilizeni wanachowaambie, maana hakuna mafanikio bila kupitia taabu na masumbuko
 
Halafu basi mikopo yenyewe wanayopewa hakuna hakika kama watalipa maana baada ya kuhitimu chuo hawana hakika ya ajira, na kama watajiari nani atakayefuatili mkopo?
 
Kwa hayo hata upewe 30,000/= kwa siku haitakutosha. Hebu jaribu kufikiria hali halisi ya nchi sidhani kama hata aje rais yupi ataweza kuhakikisha ulipwa kwa kufikiria hayo.

Nchi nyingi za ulaya wameshaachana na maswala ya kuratibu mikopo kwa wanafunzi wanatoa scholarship na mfano mzuri ni wenzetu Uganda na Kenya. Swala la mikopo ni la financial intitutions kama mabenki na sacos. Hii itamweka mwanafunzi kuona mazingira yake halisi na kukopa kwa kadiri ya uwezo na mahitaji yake bila manung'uniko. na hii itasaidia sana katika kukusanya madeni ili na wengine wapate pia itakuwa fair kuliko ifanyavyo bodi ya mikopo hapa kwetu TZ.
 
Nafikiri unajadili event badala ya concept..

Concept hapo ni kujitegemea sio mgawanyiko wa masaa ya kusoma mchana na usiku, na jinsi mtu atavojishikiza. Kujitegemea kwamba mtu kuwa proud kugharamia elimu yake. Kama huezi kutafuta walau fedha wakati wa semester au term, basi fanya hivo wakati wa likizo. Kama hiyo nayo huezi basi tafuta pesa kabla hujaanza masomo..hamna kisingizio hapo.
kazi ziko wapi? hao waliohitimu hawana kazi, wengine mishahara hawajalipwa mfano walimu wanadai mishahara yao, unamwambia aende kufundisha shule za kata, wakati walimu wenyewe wanacheleweshewa mishahara yao. Tueleze kazi ziko wapi waende hawa watoto wakafanye. Kazi za bongo technical know who.
 
Kwa hayo hata upewe 30,000/= kwa siku haitakutosha. Hebu jaribu kufikiria hali halisi ya nchi sidhani kama hata aje rais yupi ataweza kuhakikisha ulipwa kwa kufikiria hayo.

Nchi nyingi za ulaya wameshaachana na maswala ya kuratibu mikopo kwa wanafunzi wanatoa scholarship na mfano mzuri ni wenzetu Uganda na Kenya. Swala la mikopo ni la financial intitutions kama mabenki na sacos. Hii itamweka mwanafunzi kuona mazingira yake halisi na kukopa kwa kadiri ya uwezo na mahitaji yake bila manung'uniko. na hii itasaidia sana katika kukusanya madeni ili na wengine wapate pia itakuwa fair kuliko ifanyavyo bodi ya mikopo hapa kwetu TZ.
Umenena vyema. Je mafisadi watakula wapi? Huu ni mradi wa watu wewe hujui bado? Hapo watu wanakula na kusaza. Hapa kwetu ukitoa wazo lenye mwanya wa kula ndo linalofanyiwa kazi si wazo la kusaidia kuondoa kero. Hawa wa kwetu wameshindikana. hatuna njia nyingine ila tu ya kuandimana na kuwaondoa kama Misri.
 
Siasa za ujamaa zimetuharibu..kila kitu tunasubiri serikali, serikali, serikali.. kwa wanginewe tulioshuhudia nchi zengine mtu anajisomesha yeye mwenyewe..mchana anapiga mzigo, usiku anaenda kupiga kitabu..sisi tunataka kila kitu kiekwe mezani TULE.

Hii mail umeandika ukiwa wapi ndugu yangu. Tanganyika hii utapata wapi kazi za muda za usiku? Labda ukahaba kwa kinadada. Hao waliomaliza chuo wenyewe hawana kazi ije kuwa hao ambao bado wapo chuo?
 
Nilipokuwa shule ya msingi na sekondari licha ya kufanya vibarua nilikuwa nalima shamba la mahindi, mavuno yake yalitosha kununulia sare za shue na kubakiza za kununulia mihogo ya lunch. Vijana hawataki kujishughulisha, eti wanataka vibarua vya kuuza maduka na maofisini.
Nendeni mkaombe mashamba ya kulima mpata mshiko
 
Mengi yamesemwa na yataendelea kusemwa. Ukweli ni kwamba mahitaji ya mwanaadamu huwa hayawezi kutoshelezeka. Leo unapata 5,000 unaziona hazitoshi na unafanya mchanganuo wa matumizi kuonesha zisivyo tosha. Kesho ukupewa 10,000 pia utaonesha hazitoshi na utatoa mchanganuo wa kuunga mkono hoja yako. Cha mhimu tuhitaji kwa mujibu wa hali yetu ya uchumi. Tuangalie watu wa kawaida wanaishije na kwa vipato gani. Tukiona kama kutokana na hali halisi ya uchumi na maisha ya watanzania ni haki kwetu kupewa 10,000/= kwa mwezi basi tuwasilishe maombi yetu serikalini kwa hekima na busara
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom