Mkuu.. Machinga Complex ni kipimo kizuri cha upungufu wa akili wa viongozi wetu.. Nilisema toka wakati wanaanza matayarisho kwamba kama nia ni hiyo wanayoisema basi itakuwa ni hasara.. Nadhani kulikuwa na personal interests ndo maana wakalazimisha..
Hili la ubungo kwangu mie naona Serikali kabla ya kutoa deadline wangewatafutia eneo mbadala ambalo liko ndani ya biashara.. Au wangeweza hata kununua eneo toka kwa raia na kulitenga kwa ajili ya wamachinga.. Kuwafukuza bila ya kujua wataenda wapi ni kuwaonea na kuwalazimisha kuingia katika vitendo vya uhalifu.. Serikali makini icingewaacha wajazane pale ndo waje kuwaondoa..
Nakubaliana na mdau hapa!