Mabomu ya Polisi yatanda Ubungo

Hvi soko la jioni halipo.afu ngoja wafukuzwe kwanza c wapenda mabadiliko.hawataki cdm ishike hatamu
 
Mkuu kuwahamisha wamachinga katika eneo lenye biashara ni KUKOSA AKILI YA BIASHARA..

Nilipiga kelele sana (hawa vichwa ngumu wa serikalini) wakati wanawaondoa wamachinga manzenze, mahakama ya ndizi na hata ubungo si support kabisa huu ujinga nitaeleza kwanini

a. Umajinga unatoa ajira isiyo rasmi kwa vijana wengi sana Tanzania dawa si kuwaondoa bali kuondoa zile nyumba, taasisi etc zilizokaribu na centres za wamachinga mfano. mazense serikali ilitakiwa inunue na kuhamaisha makazi ya watu pale na kuweka soko kubwa pale vilevile ubungo jengo la tanesco na maujinga yao waondoke wamachinga watengenezewe utaratibu wa kuwa na soko lao pale..

b. Turnover, in terms of cash transaction and services provided per day maeneo ya machinga ni kubwa sana ni uhai kwa taifa na kwa wananchi wake hasa kodi kwakuwa mazao na huduma zinauzwa maeneo hayo..

Serikalini tatizo lao hawajawahi kufanya kazi za biashara mtu amekuwa officer wa kufukuzia allowances hawezi kujua business preposition na faida itokanayo ndio maana wanaweza kuja na amri za kijinga kama hizo..ndio maana tunataka rais mmachinga sio professional politicians ..soma signature yangu
Sijakuelewa kuhusu Manzese, mbona wemejengewa paple pale karibu? Labda wewe ulitaka wajengewe pale darajani na si mita hamsini kutoka darajani kuelekea urafiki. Ok, tugeukie kwenye suala hilo la ubungo. Strategically, ubungo si mahali salama kabisa kwa mikusanyiko ya watu. Pale yale majenerator ni kama mabomu, na matransformer yaliyopo pale yanatumia mafuta ambayo yanaweza kusababisha milipuko. Kukusanya watu pale ubungo ni hatari sana kwa namna palivyo. Na kwa kifupi tu, wateja wa ubungo wanatokana na uwepo wa stendi ya daladala pamoja na mabasi ya mikoani. soon kituo cha mabasi ya mikoani kitahamia kibamba. Na kwa sababu za kiusalama kituo cha dala dala pia chaweza kuhama. But suala la kuwaondoa wamachinga pale naliunga mkono sana tu kutokana na mazingira ya pale yalivyo.
 
...kwa kuwa waliwafuga vibaka sawasawa kuondolewa, ht mi sintosahau eneo hilo.
 
Kwanini majereta yasihame badala ya watu wenye kuleta fedha wahame; manzenze yale makazi ya watu karibu na daraja ya kazi gani pale; pale panatakiwa pawe soko pande zote mbili; serikali iwaondoe wale wazee wenye makazi pale..

Biashara inalipa kwa serikali kuliko nyumba zao hizo hali kadhalika biashara ubungo inalipa kuliko majerata ya mgao.
 
Duh, haya bwana. Hivi pale ubungo wale wamachinga wakiweka zile meza wanalipia bei gani? Hivi unajua ni hasara kiasi gani ambayo serikali inapata kutokana na hizi biashara zisizo rasimi? Kwa mfumo wa biashara ya namna ile inakuwa vigumu sana kukusanya kodi. Hata hivyo, sidhani kama gharama za kuhamisha ile miundombinu ya tanesco pale inafanana na returns ambazo serikali itapata kutoka kwa wamachinga. Kuhusu manzese, suala la usalama umeliangalia? Ukizingatia ile ni barabara kuu?
 
Kwa hili naipongeza halmashauri ya jiji pamoja na polisi ila nawakumbusha kuwa isiwe kama kazi ya zimamoto wametumia nguvu Nyingi na wakati wao mwingi kuwatoa kwa leo basi wasijisahau wakajiondokea na kesho tukawapata Hawa machinga wamerudi kwenye hayo maeneo tena,jamani swala la watu kujitafutia riziki ni sawa kabisa lakini ni lazima tufuate sheria na taratibu za nchi kanuni za biashara zifuatwe bila kuathiri mazingira biashara zifanyike sehemu rasimi.siyo uweke meza ama kibanda cha kuuza suruwali barabarani kisa eti serikali haijakujengea soko hii isiwe sababu ya wewe kuvunja sheria na taratibu za nchi,tafuta chumba jirani na eneo husika panga weka mali ndani uzia ndani ya chumba kwa ustaarabu na jiji ama miji,barabara zetu ziwe safi kwa matumizi husika
 
Mkuu usalama si tatizo mkuu barabara kuu ndio hasa sehemu ya kufanya biashara sijaona mantiki yako labda uwe hujawahi kufanya business, barabara kuu nyumba za kuishi wapi na wapi pale panatakiwa maduka na biashara na soko la kisasa kabisa (manzense) kwasababu tuna maofficer wamesoma degree za biashara bila kufanya biashara kila siku kazi yao kuua masoko badala ya kuyaenzi hawajui masoko (au sehemu kuwa soko) ni kazi kubwa sana mkuu..

Ile miundo mbinu ya tanesco pale haifai kabisa kwanza ziko karibu na high way na makazi ya watu wanatakiwa wayapeleke hata katika kambi ya jeshi wakitaka..huko makongo juu kusiko na makazi na watu wengi kama ubungo ambako biashara inalipa

Mkuu returns ni kubwa sana kutoka kwa wamachinga a. ajira b. bidhaa zinazouzwa pale zote zinanunuliwa na vat inalipwa c. wengi wetu tuna leseni za biashara ndogondogo d. services huduma na idadi ya watu wanaotegemea huduma zetu kuanzia chakula cheap, nguo etc huwezi kulinganisha na mjengo wa tanesco na transfoma zake..

Maofisa wengi serikalini ni vilaza wa biashara wamekariri usafi, security etc. wanawaona wale vijana kama vile uchafu kwa vile wao walipomaliza shule waliingia ofsini hawajawahi kufanya biashara, wanatembea kwenye magari wanaona wale vijana ni bughudha etc..

MASOKO hayavunjwi yanaendelezwa; only in Tanzania MASOKO yanavunjwa sijawahi kuona ujinga kama huu.
 
Umeshiba maharagwe na allowance ya vikao wewe, jaribu kufanya biashara kwenye informal sector ndio utajua umuhimu wa eneo; sisi tuna usemi Mungu yuko karikooo, Manzense na Ubungo kwasababu hapo ndipo turnover za biashara zilipo; jiji wanatakiwa kupaendeleza pale na kuondoa vizuizi vyote vinavyohatarisha biashara ikiwemo hilo mjengo wa tanesco
 
kwa kweli kwa hili serikali naipongeza sana, waje hata mitaa ya Aggrey na Likoma kuna vijana wamejaza makomputa eti wanaingiza miziki, alafu mgambo hupita na kuwatoza elfu mbili, wakati huo kuna watu wanalipa kodi na wapo sehemu salama wanaathilika na hawa vijana kwa kisingizio cha ajira. Tuwe wastaarabu, tulipe kodi na serikali iwajibike na matakwa yetu muhimu.
 
Serikali ijitahidi kupanga mipango yake vyema hasa kwa kutenga maeneo kwa wananchi wake sio mpaka wananchi wajitafutie maeneo wao wenyewe.Wanazembea kugawa maeneo mpaka wananchi wanavamia sehemu halafu wanaibuka kama vile wametekenywa maeneo nyeti. Wajifunze kwa kuangalia maendeleo ya miji yetu hapo baadaye.
 
Kwa kweli mpango huu ni mzuri kwa usalama wa hawa wafanyabiashara, matumiaji na taasisi zinazomiliki maeneo hayo na maendeleo yetu. Mpango huu pia utatusaidia ktk zoezi la mipango miji.

Lakin tatizo langu ni nguvu na mbinu inayotumika. Hv serikali haijui kuwa wafanyabiashara hawa wanategemea biashara hizi kuishi wao na familia zao? Hivi haijui kuwa kwa kufanya hivi ni sawa na kukiuka haki zao za kuishi? Kwa nini wasingeandaa mpango wa kuwahamishia sehemu nyingine au kuwawekea mazingira bora zaidi ya kufanya biashara?

Na kuwaelimisha pia.
 
Mkuu usalama si tatizo mkuu barabara kuu ndio hasa sehemu ya kufanya biashara sijaona mantiki yako labda uwe hujawahi kufanya business, barabara kuu nyumba za kuishi wapi na wapi pale panatakiwa maduka na biashara na soko la kisasa kabisa (manzense) kwasababu tuna maofficer wamesoma degree za biashara bila kufanya biashara kila siku kazi yao kuua masoko badala ya kuyaenzi hawajui masoko (au sehemu kuwa soko) ni kazi kubwa sana mkuu..

Ile miundo mbinu ya tanesco pale haifai kabisa kwanza ziko karibu na high way na makazi ya watu wanatakiwa wayapeleke hata katika kambi ya jeshi wakitaka..huko makongo juu kusiko na makazi na watu wengi kama ubungo ambako biashara inalipa

Mkuu returns ni kubwa sana kutoka kwa wamachinga a. ajira b. bidhaa zinazouzwa pale zote zinanunuliwa na vat inalipwa c. wengi wetu tuna leseni za biashara ndogondogo d. services huduma na idadi ya watu wanaotegemea huduma zetu kuanzia chakula cheap, nguo etc huwezi kulinganisha na mjengo wa tanesco na transfoma zake..

Maofisa wengi serikalini ni vilaza wa biashara wamekariri usafi, security etc. wanawaona wale vijana kama vile uchafu kwa vile wao walipomaliza shule waliingia ofsini hawajawahi kufanya biashara, wanatembea kwenye magari wanaona wale vijana ni bughudha etc..

MASOKO hayavunjwi yanaendelezwa; only in Tanzania MASOKO yanavunjwa sijawahi kuona ujinga kama huu.
Mkuu nimekusoma vizuri comment zako.
Sidhani kama ni economical viable kuhamisha mitambo ya umeme, gridi ya taifa na mjengo wa Tanesco kwa ajili ya kuwapisha machinga. Is it sensible...!!!?? Tena machinga wenyewe pale wala hawalipi kodi, na kama wanalipa basi haiendi serikalini, na kama inwakwenda basi ni mia mbili mia mbili. Kweli..!?

Suala la usalama limeshazungumziwa na wachangiaji wengine, niongezee tu uwepo wa machinga pale una-entertain vibaka na matukio ya uhalifu kwa kiwango cha juu. Wengi wameshalizwa sana pale.

Niko against ccm lakini kwa hili siwalaumu. Kuhusu kutengewa maeneo tusitafute visingizio kila wakati, Machinga complex hadi sasa bado iko empty na badala yake jamaa wamejazana pale karume na hawataki kuhamia sehemu waliyopangiwa. Bado mtawalaumu ccm tu?? Wana madhambi yao lakini sio kwenye hili.

Ukiweka huduma sehemu na ikawa nzuri watu wataifuata tu. Mbona watu wanatoka Gongolamboto wanakwenda Mlimani City? Mbona watu wanatoka Kibamba wanakwenda Quality Centre?

Watanzania tujifunze kutii sheria na kufuata utaratibu. Ningependa kuona baada ya Ubungo ifuate manzese, mwenge na maeneo mengine yenye kero za namna hiyo.
 
naombeni picha wakuu kama kuna aliyeko karibu...na habari zaidi.
 
aha ha aha ah duh eti kama eapoti...BIg up maghufuli , sema hawa jamaa wartarudi ..sasaq ndio muda muafaka wa kuwatafutia sehemu nyingien
 
aha ha aha ah duh eti kama eapoti...BIg up maghufuli , sema hawa jamaa wartarudi ..sasaq ndio muda muafaka wa kuwatafutia sehemu nyingien

kumbe mambo yanawezekana?...ila sio suluhisho la kudumu...ni kwa visiku vichache tu.
 
Matokeo ya kushangilia ushindi wa CDM sana. Hakuna kurudi nyuma mabadiliko tu.
 
Ni operesheni kuwaondoa wamachinga
headline_bullet.jpg
Nao wajibu kwa kuwarushia polisi mawe

Ubungo(7).jpg

Askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU), akipiga bomu la kutoa machozi kuwatawanya wafanyabiashara ndogo ndogo, wakati wa operesheni ya kuwaondoa wafanyabiashara hao eneo la Ubungo jijini jana. Kushoto ni baadhi ya wafanyabiashara hao waliokuwa wakipambana na askari hao, wakishangilia kwa kuonyesha alama ya vidole viwili.(PICHA:OMAR FUNGO)

Mapambano yaliyohusisha mawe, mabomu ya machozi na maji ya kuwasha kati ya askari polisi na wafanyabiashara ndogondogo, maarufu kama “Wamachinga”, yalizuka jana na kusababisha tafrani na hofu kubwa miongoni mwa wakazi, wafanyakazi, wafanyabiashara na wapita njia katika eneo la Ubungo, jijini Dar es Salaam.

Mapambano hayo yalizuka baada ya askari polisi, wakiwamo askari kanzu wakishirikiana na wale wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni, kuendesha operesheni ya kuwaondoa wafanyabiashara hao katika maeneo hatarishi na yale yasiyoruhusiwa kufanya biashara katika maeneo mbalimbali ya Ubungo.

Maeneo hayo ni pamoja na kwenye kituo cha daladala cha Ubungo Mwisho, Ubungo Maji, Ubungo Mataa hadi darajani (Barabara ya Mandela), eneo la kituo cha kuzalisha umeme cha Songas na Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) hadi Riverside, Ubungo Mataa hadi darajani kwenda Chuo Kikuu cha Dar es Salaam -UDSM (Barabara ya Sam Nujoma) na Ubungo Mataa hadi Kituo Kikuu cha Mabasi Ubungo-UBT (Barabara ya Morogoro).

Askari hao wakiongozwa na baadhi ya maofisa waandamizi wa Jeshi la Polisi na walianza kuwaondoa wafanyabiashara hao katika maeneo hayo kuanzia saa 9.00 usiku wa kuamkia jana, kwa kuvunja na kuondoa meza na vibanda vinavyotumiwa na wafanyabiashara kuuza bidhaa zao.

Miongoni mwa meza zilizovunjwa na kuondolewa na askari hao katika maeneo hayo, ni pamoja na zile zinazotumiwa na wauza magazeti.

Hatua hiyo ilisababisha jana, wauzaji wa magazeti kulazimika kupanga magazeti chini, huku baadhi yao wakilalamikia hali hiyo.

ya kuondolewa katika maeneo yao ya kufanyia biashara, ilipingwa vikali na wafanyabaishara hao walioonekena kuwa na hasira na hivyo kuanza kuwarushia askari hao mawe kwa wingi na mfululizo.

Kwa jinsi mawe hayo yalivyokuwa yakirushwa kwa wingi na wafanyabiashara hao, yalionekana mithili ya kundi la ndege likiruka angani.

Mawe hayo yalianza kurushwa na wafanyabiashara hao katika eneo la Ubungo Maji kuanzia saa 1:00 asubuhi.

Katika tukio hilo, gari moja linalosadikiwa kuwa ni la polisi, lilivunjwa kioo.

Mbali na kurusha mawe, wafanyabiashara hao walifunga Barabara ya Mandela, katika eneo la Songas baada ya kuweka mawe makubwa kuzuia magari kupita.

Hali hiyo ilisababisha msongamano mkubwa wa magari kwa takriban saa moja.

Wafanyabiashara hao walidai kuwa wameamua kufunga barabara hiyo ili kushinikiza Mbunge wao Jimbo la Ubungo (Chadema), John Mnyika, aende eneo hilo kuwatetea wasiondolewe katika maeneo yao ya kufanyia biashara.

Hali hiyo ilionekana kuwazidi nguvu askari polisi wa kawaida, askari kanzu na wale wa Halmashauri ya Manispaa waliokuwa mstari wa mbele kuendesha operesheni hiyo dhidi ya wachuuzi hao.

Hivyo, wakalazimika kuomba msaada kutoka askari polisi wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU).

FFU walifika eneo hilo wakiwa kwenye magari manne aina ya Land Rover na gari moja la kurusha maji yenye kemikali za kuwasha mwilini.

Askari hao wakiwa wamebeba mabomu ya machozi, bunduki za risasi za moto na zile za mipira pamoja na virungu tayari kwa mapambano, walianza kufyatua mabomu ya machozi na kurusha maji ya kuwasha kuwatawanya wachuuzi hao.

Wachuuzi hao pamoja na wapita njia, walianza kukimbia hovyo katika maeneo mbalimbali, huku watu waliokuwa majumbani wakijifungia ndani ya nyumba kunusuru maisha yao.

WATU 34 MBARONI

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Charles Kenyela, alisema watu 34; wanaume na wanawake, walikamatwa na polisi. Kati yao tisa walifikishwa mahakamani jana na waliobaki watafikishwa mahakamani leo.

Mabomu na maji hayo yalirushwa kwa dakika kadhaa, hali ilirejea kuwa shwari na magari kuruhusiwaa kuendelea na safari baada ya vizuizi vilivyokuwa vimewekwa barabarani na wachuuzi hao kuondolewa na polisi.

DC RUGIMBANA: OPERESHENI YA KAWAIDA
Baada ya hali kuwa shwari, Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Jordan Rugimbana, aliyekuwa katika eneo hilo, aliwaambia waandishi wa habari kuwa operesheni hiyo ni ya kawaida na kwamba, hawataruhusu wachuuzi kuyatumia maeneo hayo kufanya biashara.

Alisema katika kutekeleza amri hiyo, maeneo hayo sasa yatawekewa ulinzi kuzuia biashara kufanyika.

Naye Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Charles Kenyela, akiwa eneo la tukio, aliwataka wafanyabiashara kuondoka katika maeneo hayo na kwenda kule walikopangiwa na manispaa.

Alisema maeneo ya karibu na mitambo ya Tanesco waliyokuwa wanafanyia biashara ni ya hatari kwa vile unapita umeme mkubwa.

Kenyela alisema hivi asa ni marufuku maeneo yaliyokatazwa, kufanya biashara, si katika nyakati za mchana tu, bali usiku pia.

“Soko la saa 12 pia marufuku. Sasa we njoo usiku na vitunguu vyako hapa uone. Hatufanyi kwa nia mbaya, bali kwa faida yao (wafanyabiashara ndogondogo),” alisema Kamanda Kenyela.

Hata hivyo, dakika chache baada ya Rugimbana na Kamanda Kenyela kueleza hayo, wachuuzi hao walijikusanya karibu na eneo la darajani na kuanza kuimba nyimbo mbalimbali za kusifu juhudi za Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Julius Nyerere, huku wakitoa matamshi ya kupinga kuondoka maeneo waliyoondolewa.

Kitendo hicho kiliwatia hasira FFU ambao walianza kuwatawanya kwa kuwarushia mabomu ya machozi na kupiga hewani risasi za mipira.

Wachuuzi hao waliochanganyika na vijana wanaosadikiwa kuwa ni wabwia dawa za kulevya, maarufu kama ‘mateja’, walianza kukimbia hovyo kwa mara ya pili.

Hata hivyo, juhudi hizo za kujinusuru hazikufua dafu, kwani baadhi yao walitiwa mbaroni na polisi.

Baadaye, hali ilirudi kuwa shwari, lakini askari hao waliendelea kuweka ulinzi katika maeneo hayo.

Majira ya sasa 8:20, wachuuzi hao walirejea na kuchoma taili barabarabi, lakini polisi waliingilia kati na kuwasambaratisha tena.

Akizungumza katika kikao kati ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Saidi Meck Sadiki, viongozi wa Tanesco na Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamanda Kenyela alisema operesheni hiyo ilifanyika kwa amani na salama bila ya mtu yeyote kujeruhiwa wala kufa.

Alisema wamejiandaa kikamilifu kupambana na mfanyabiashara yeyote atakayejaribu kufanya biashara usiku katika maeneo yasiyoruhusiwa.

Kamanda wa Kanda hiyo, Suleiman Kova, alisema operesheni hiyo ni mwanzo wa kutatua kero jijini Dar es Salaam.

Hata hivyo, aliwataka wafanyabishara hao kutokata tamaa, badala yake waende kuendelea na biashara katika maeneo yaliyoandaliwa na ili kujenga nidhamu nchini na kuonya kuwa hawatamvumilia yeyote atakayejaribu kufanya biashara katika maeneo yasiyoruhusiwa.

Sadiki alisema operesheni iliyoanza jana, ni tukio la awali katika operesheni zinazotaka kufanywa na serikali jijini Dar es Salaam.

Sadiki alisema Ubungo imekithiri uvamizi wa maeneo nyeti unaofanywa na baadhi ya watu kwa kisingizio cha wafanyabiashara au wajasiriamali ambao alisema wanasahau ujasiriamali unaweza kubadili sura ukawa na madhara.

Alisema operesheni hiyo si nguvu ya soda kama itakavyodhaniwa na baadhi ya watu, bali itakuwa ya kudumu katika maeneo yote yasiyoruhusiwa, ikiwamo kituo cha daladala cha Mwenge ili kurejesha nidhamu na usalama mkoani Dar es Salaam.

“Wapo wajasiriamali, lakini wengine ni wezi tu, ndio hao hao wanajihusisha na dawa za kulevya na bhangi,” alisema Sadiki.

Katika hatua nyingine, Sadiki aliwataka watu wote waliojenga katika maeneo ya njia za umeme kuondoka mara moja kwa hiari kwa vile maeneo waliyojenga ni nyeti, vinginevyo wataondolewa kwa nguvu.

Alisema serikali imekwishamuagiza Mkurugenzi Mtendaji wa Tanesco kupeleka orodha ya watu wote waliojenga katika maeneo hayo.

MKURUGENZI TANESCO: TUNAJADILIANA NAO

Mkurugenzi Mtendaji wa Tanesco, William Mhando, alisema wanaendelea na majadiliano na watu hao kama majirani kuhusu suala hilo.

Sadiki pia aliwataka watu wote wanaochimba mchanga na kokoto maeneo ya Pugu, katika msitu wa Kazimzumbwi, kuanzia leo, waache mara moja kuchimba kwa vile hayo ni machimbo haramu na kunaharibu mazingira.

Alisema machimbo hayo ni haramu kama biashara ya dawa za kulevya na kwamba, wanaochimba hawajapewa kibali na halmashauri na wala manispaa haipati hata senti moja.

CHANZO: NIPASHE
 
Sadik alikwina? yaani miaka yote hiyo hakukua na nyaya au ni mpango mkakai wa kupunguza makali ya wapinzani?
 
Wilaya ya Kinondoni imewataka wachuuzi wanaoendesha shughuli zao eneo la kuzunguka kituo kikuu cha umeme Ubungo, stendi ya daladala Ubungo na Mwenge, waondoke katika maeneo hayo kwa kuwa wamekuwa wakihatarisha usalama wa matumizi sahihi na bora wa maeneo hayo.

Tamko hili linaungana na wito wa Shirika la Umeme nchini (Tanesco) la kuwataka wachuuzi hao waondoke Ubungo kwa sababu mbali ya kuhatarisha maisha yao, pia wanahatarisha usalama wa mitambo mikubwa ya umeme iliyoko

eneo la Ubungo, wametoa mfano wa kikosi cha zima moto na ukoaji kushindwa kuzimwa moto uliolipuka kwenye moja ya transfoma zake kituoni hapo kwa sababu kukosa sehemu ya kupita.

Ni kweli, wachuuzi hawa wamekuwa ni kero kwa watumiaji wengine wa barabara, usalama wa kituo kikuu cha umeme cha Ubungo, lakini pia kusababisha msongamano usiokuwa wa lazima katika maeneo hayo, hivyo kuwa kivutio kikubwa cha vibaka.

Tunaamini kuwa wachuuzi wana maeneo mahususi ambayo yametengwa kwa ajili ya kuendesha shughuli zao, kama vile kwenye masoko yaliyojengwa kwa kazi hiyo, tunaamini kuendelea kuchuuza kwenye maeneo ya waenda kwa

miguu, kwenye vituo vya daladala na kugeuza uzio wa kituo kikuu cha umeme cha Ubungo kuwa eneo la kuchuuza kila aina ya bidhaa, ni kuhatarisha usalama wao na wa wakazi wengine wa Jiji la Dar es Salaam.
Tunaunga mkono juhudi za kuwataka wachuuzi hawa warejee kwenye maeneo yanayoruhusiwa kuendesha shughuli zao, ili wafanye kazi zao bila kubugudhiwa lakini pia bila kuleta bugudha kwa watu wengine.

Tunalaani vitendo vya kukatana mapanga

Mwishoni mwa wiki iliyopita wabunge wawili mkoani Mwanza na watu wengine watatu mkoani Mbeya, walicharangwa mapanga na watu wanaominiwa walikuwa wanasukumwa na sababu za kisiasa, vitendo ambayo mbali ya kuwaletea

madhara makubwa mwilini, pia vimechafua sura ya taifa mbele ya jumuiya ya kimataifa jinsi tunavyendesha siasa zetu.

Ingawa polisi hawajasema chanzo cha matukio haya ni nini, waliojeruhiwa wamesema vitendo hivyo vimetokana na uhasama wa kisiasa. Wabunge, Highness Kiwia wa Ilemela na Salavatory Machemuli wa Ukerewe, walivamiwa usiku wa kuamkia Jumapili siku ambayo uchaguzi mdogo wa udiwani kata ya Kirumba ulikuwa unafanyika.

Kundi la watu wengine watatu nao lilicharangwa mapanga na kuumizwa sana sehemu mbalimbali za mwili ambako walishonwa majeraha yao, siku ya uchaguzi mdogo wa diwani wa kata ya Kiwira. Sababu za kisiasa zinatajwa kuwa chanzo.

Hadi sasa hali ya Kwia inaelezwa kuwa mbaya kutokana na majera aliyopata kichwani, na angali akipatiwa matibabu katika hospitali ya taifa Muhimbili ambako alihamishiwa akitokea Bugando, Mwanza.

Tunaelewa kwamba katika mfumo wa vyama vingi vya siasa kuna joto kubwa la kusaka kura hasa kipindi cha uchaguzi kinapokaribia, kwa maana hiyo ushindani wa hoja ni jambo linalotarajiwa ili kupata ridhaa ya wananchi.
Hali hii ya ushindani wa kisiasa katika kujenga hoja, kuuza sera ndiyo mambo yanawapa nafasi wananchi kupima nani apewe kura na kinyume chake.

Sheria ya vyama vya siasa na ile ya uchaguzi zimeeleza wazi kuwa vyama vya siasa vitaomba ridhaa ya wananchi kwa kuomba kura, si kuwatisha, si kutumia vurugu, si kwa kucharanga wengine mapanga na si kwa njia nyingine yoyote ya hila.

Kwa hiyo, wale wote waliosahau kuwa taifa hili halishabikii utumiaji wa mabavu kupata kura, hakika wamelitia doa kubwa taifa hili mbele ya wapenda amani wote duniani.
Ndiyo maana sisi tunachukua fursa hii kulaani kwa nguvu zetu zote wale walioamua kuendesha uhalifu wa kuwacharanga wenzao mapanga kwa kisingizo chochote kile.

Tunalaani kwa kuwa tunaona wazi kuwa huu ni mwanzo wa kujenga utamaduni wa kuumizana katika siasa.
Tutafarijika sana kama wahusika wote wa kadhia hizi watatiwa nguvuni na kufunguliwa mashitaka katika mahakama

zetu ile iwe fundisho kuwa siasa za kukatana mapanga si utamaduni wa Watanzania na kwa maana hiyo haziwezi kuungwa mkono na hakika hazivumiliki.
Tunalaani wote walioendesha vitendo hivi na tunaomba sheria ichukue mkondo wake ili kuvikomesha.

CHANZO: NIPASHE
 
Back
Top Bottom