Maandamano ya CHADEMA Jijini Mwanza

Mnapoeza muda wa watu kufanya kazi. Watu wanataka barabara, hospitali, shule bora n.k. Hawataki maandamano.
Acheni uzushi, kahamasisheni shughuli za maendeleo.


Pole sana! Nadhani ww ndio unapoteza muda wako kwa kufuatilia mambo usiyoyajua!
 
Viajenda vya kuchupia chupia na kuleta fujo tu, mara hii mnachokitegemea kitokee Mwanza, kama kule Arusha, hakitatokea, labda mkitafute wenyewe, hakuna wa kuwaopoweni, mtapiga makelele mchana na usiku mtatafuta vitanda mlale!

Sasa mbona inakuwasha??? Mpaka kieleweke tu!!!!!
 
Sasa hiyo itakuwa definition ya CCM au Mafisadi au wote kwa pamoja!vipi yakiitwa maandamano inakuwa kama msumari unaochoma kotekote!pole sana !!

Asante mkuu, Linawachoma sana. Na ba do! Moto mkubwa huanza polepole. hata mbuyu ulianza kama mchicha...
 
Maandamano ya wafuasi wa CHADEMA huko Mwanza yakiongozwa na viongoziwao Dr. Slaa, Mh. Mbowe na wabunge wa chama hicho yawa na amani kubwa pasipo na vurugu. Source- Radio 1
 
CDM mnatumia vibaya KODI zetu...saa nane ni saa ya watu kuwa makazini kutafuta riski.

Kazi zipi wewe? mbona unakuwa mnafiki, kodi zako anatumia vibaya Kikwete kwenda kubembea Jamaica na mwanae Riziwani kuwewa escort ya kwenda airport, na Salma misafara mikubwa kwenye ziara zisizo na kichwa wala miguu, subirini Mungu anajua nani mwongo nani mkweli, na haki haipatikani bila kutafutwa.
 
huyu mbweha sijui anajiita ze..makopo.. hana jipya ni saa na ma...la.ya tandale
 
Nyie CCM hata hotuba tu mnaandamana eti kuunga mkono inawasaidia nini mbona huwa hamsemi ni matembezi ya kuunga mkono hotuba.

Think Big...

Kunatofauti gani kati ya hilo na hili linalofanyika leo Furahisha?

Tofauti pekee ni kuwa wale wa CCM wanatembea "baada ya hotuba" wakati hawa wa Chadema sasa wanatembea "kabla ya hotuba".

Wote hao wanafanana juu ya jambo la msingi..."Hawana jambo la msingi wanaloliamini wala wanalolihitaji", wakishahutubiwa na kusikiliza mikutanoni yamekwisha wanarudi zao kwao.
 
Bravo Mh. Mtema

Big up CHADEMA and Poeplesssssss powerrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrr.

May God bless you and all Tanzanians.
 
Hamjawahi kuhamasisha hata ujenzi wa shule ya kata, kazi yenu kuandaa maandamano tu. Huo ni unafiki wa kisiasa, hamna moyo wa kweli wa kuleta maendeleo Tanzania.

Duh sijawahi kuona mtu kama huyu jf, nashindwa kumwelewa hivi wewe unafuatilia shughuli za cdm jaribu kufuatilia kwanza usilete utumbo hapa, unakera afadhali ufumbe domo
 
Fedha ingewasaidia sana wahanga wa hayo mabomu kuliko kutumika kwenye maandamano, taifa kwanza

Wee kweli bado upoupo, yaani CCM walipue mabomu makusudi halafu CHADEMA watoe hela kwa wahanga? Kwanini hao CCM wasitoe kutoka kwenye faida waliyoipata kutokana na hiyo milipuko? Maana kwa CCM milipuko na vifo vya watanzania, kwao ni dili na ndo wanapatia faida humo. Basi zinazozidi katika faida yao, wawasaidie hao wahanga wa mabomu.
 
Kama kuna anayeweza kunitajia kitu kimoja kilichopatikana kwa chama fulani cha siasa Tanzania kwa njia ya maandamano aweke hapa. Kila siku mnaandamana na kutoa hotuba zisizo na tija halafu jioni mnarudi nyumbani. Mantiki yake nini sasa?
Hivi huwa mnakaa na kuevaluate mafanikio yanayopatikana kutokana na hayo maandamano?

Matokeo ya uchaguzi ya majimbo yafuatayo yalipatikana baada ya wafuasi wa chadema kuandamana:

Mwanza
Ubungo
Kawe
Arusha

Wanafunzi wa vyuo vikuu wameshajua siri ya maandamano ndio sababu kila wakicheleweshewa pesa wanaandamana na kesho yake zinawekwa kwenye account. Maandamano JUUUUUUUUU.
 
Nimemuona Dr. Slaa hapo kwenye picha, inaonesha kama kachokaaaa, wamembebesha dunia babu watu roho riziki yake sasa du, watu wabaya!!!
 
Mods badilisheni heading ya hii thread, yanayotokea Mwanza siyo MAANDAMANO ni MATEMBEZI YA AMANI.

MAANDAMANO hupata suluhisho i.e Tunisia, Egypt na sasa Libya, MATEMBEZI hutafuta suluhisho i.e ARUSHA
 
Hao vibwengo ni kuachana nao wala mhihangaike kujibizana nao! Pipoz pouwaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa

Take 5 Rev.

Nashangaa watu wanakimbizana na vichaa kwenye JF. Hao wahuni sijui walevi wanaopinga maendeleo achaneni nao ni watoto wa fisadi. Bila ufisadi wanaona maisha yao yako hatarini.

Tusiwajibu.
 
Back
Top Bottom