Maandamano ya CHADEMA Jijini Mwanza

Dada Regia, mimi mwanachama wa chadema. Lakini naanza kupata mashaka na agenda mliyonayo viongozi wetu hii ya kuandamana. Siogopi maandamano ila sidhani kama ni muda muafaka. Tumieni njia mbadala kuimarisha chama na sio hii inaleta mtazamo hasi na kukitenga chama na kundi flani kubwa la watu ambao kwa kiasi kikubwa kwa kutokuamini upinzani unaweza kufanya kile unachoahidi, waliipa kura ccm mwaka jana na kuirudisha madarakani japo wameshaichoka sana. Lazima tukubali ukweli, ccm bado inakubalika sana. Unaweza kuona Bungeni walivyofunika, ok hata ukisema walituibia viti 20 vya ubunge bado upinzani hauna nguvu. Maandamano na migomo haiwezi kuwang'oa kwa sababu ni wachache ndio wataunga mkono. Tena leo CCM wakiamka wakafunga mjadala wa Dowans, wakawafikisha mafisadi kadhaa kizimbani(kama ilivyofanya kwa kina Mramba), upinzani wote utanyong'onye. Hebu tutafute sera za kudumu tuachane na vivuli vya matukio ya mpito. Kwa hiyo staili yenu, mnapunguza kasi ya ukombozi wa Taifa hili. Muda wa maandamano sio sasa, msirubuniwe na wachache wanaowazunguka ambao ni waelewa, wasomi na walio karibu na vyombo vya habari. Watanzania wengi hawako pamoja na nyie hata kidogo. Na siku CCM ikiamua kutusambaratisha litakua ni pigo takatifu na hatutasimama tena. Mwambie Dk Slaa, ths will never work out!!

Kuwa mwanachama haina maana unaamini ktk kile ambacho chama hicho kinapigania/simamia. Watz wengi wanajiunga na chama si kwa sababu ya itikadi, bali kwa ajili ya vyeo, umaarufu na mkumbo. Je ni wanachama wangap wanajua sera na katiba za vyama vyao?

Nadhani muono hasi dhidi ya maandamano ni uoga tu. Ni nidhamu ya uoga ambayo imetamalaki miongoni mwa watz toka zamani. Mbona hutuambii njia mbadala? Mbona hujiulizi kipi kimefanya chadema kuinuka ghafla? Unaikumbuka operesheni sangara?

Maandamano ni njia pekee ambayo inaeleweka kwa CCM na ndio maana wanaruhusu kwa shingo upande. Kwa jinsi maisha yalivyo magumu, hatuwezi kuendelea kutumia mbinu zilezile za miaka yote,maandamano ndio strategy mpya inayoweza kututoa. Mtaji mkubwa wa chadema ni vjana ambao msimamo wao sio wa kutiliwa shaka wala kudanganywa na propaganda, hao wengine watakuja taratibu baada ya maisha kuwaonyesha ukatili.

Mwisho mimi sio mwanachama wa chama chochote na sitarajii kujiunga na chochote, ila chama cha ukweli chenye nia na uwezo wa kuwatoa wananchi nakijua na nakiunga mkono hata nikiwa ndotoni. Na pia nawaelimisha na kuhamasisha wengine waliokaribu yangu wakiunge mkono na kuchangia maendeleo yk.
 
182093_1470892587284_1682707865_914231_1937388_n.jpg

Picha hii siyo Mwanza.
 
Kweli tunataka mabadiliko! watanzania hatuombi bali tunataka katiba mpya kwa lazima! haki haiombwi mahali popote! haki inadaiwa!

Suala la katiba mpya sio mjadala tena. Serikali sikivu, kama Mh. Mbowe alivyoiita, imeridhia kwa moyo mmoja. Lililobaki ni wananchi kutulia na kutafakari kwa kina namna katiba mpya inavyopasa kuwa. Nafasi hii ni mhimu sana kwetu
 
libya wamepata zaidi ya hivyo unavyo sema uchumi nia mrama 11 kutuzidi!! Kachunguzwe akili, naskia kuna orodha ya wana ccm ambao wamechukuliwa mizukule na shekhe yahya, sije kuwa we ni mmoja wapo?

Taratibu ndugu zangu tuvumiliane hiyo ndiyo raha ya demokrasia na uhuru. TUongee lugha laini ujumbe mzito.
 
Dada Regia, mimi mwanachama wa chadema. Lakini naanza kupata mashaka na agenda mliyonayo viongozi wetu hii ya kuandamana. Siogopi maandamano ila sidhani kama ni muda muafaka. Tumieni njia mbadala kuimarisha chama na sio hii inaleta mtazamo hasi na kukitenga chama na kundi flani kubwa la watu ambao kwa kiasi kikubwa kwa kutokuamini upinzani unaweza kufanya kile unachoahidi, waliipa kura ccm mwaka jana na kuirudisha madarakani japo wameshaichoka sana. Lazima tukubali ukweli, ccm bado inakubalika sana. Unaweza kuona Bungeni walivyofunika, ok hata ukisema walituibia viti 20 vya ubunge bado upinzani hauna nguvu. Maandamano na migomo haiwezi kuwang'oa kwa sababu ni wachache ndio wataunga mkono. Tena leo CCM wakiamka wakafunga mjadala wa Dowans, wakawafikisha mafisadi kadhaa kizimbani(kama ilivyofanya kwa kina Mramba), upinzani wote utanyong'onye. Hebu tutafute sera za kudumu tuachane na vivuli vya matukio ya mpito. Kwa hiyo staili yenu, mnapunguza kasi ya ukombozi wa Taifa hili. Muda wa maandamano sio sasa, msirubuniwe na wachache wanaowazunguka ambao ni waelewa, wasomi na walio karibu na vyombo vya habari. Watanzania wengi hawako pamoja na nyie hata kidogo. Na siku CCM ikiamua kutusambaratisha litakua ni pigo takatifu na hatutasimama tena. Mwambie Dk Slaa, ths will never work out!!

Mimi nadhani juhudi zetu zingekuwa ni kushiriki katika kuunda katiba mpya itakayotoa suluhisho la kudumu. Maandamano yakizidi sana wananchi hatutakuwa na utulivu wa kutosha kuweza kutoa mchango mzuri katika uundaji wa katiba mpya.
 
Kwa hali ilivyo ni lazima watu waingie mtaani ili kupata barabara, hospitali, shule bora n.k kama ulivyo tambua.
Haki yako hupewi - unaichukua kwa nguvu.

Lakini katika mijadala yetu huko nyuma na hoja za wanaharakati matatizo haya tuliyonayo yatatatuliwa kama tukiandika katiba mpya itakayojenga Tanzania mpya. Serikali imekubali katiba mpya na wananchi wamekubali. Kwa nini badala ya kufikilia njia za kubahatisha za shoti kati tusiitumie hii furusa kuandika katiba nzuri iatakayojenga Tanzania mpya isiyo na umasikini na ufisadi?
 
You have raised important points but the truth remains and that is change require force - in science or sociology.

True, but force can be naked or clothed. Unless it is in emergence situation, legitimate change is that which is brought by clothed force.
 
Wee kweli bado upoupo, yaani CCM walipue mabomu makusudi halafu CHADEMA watoe hela kwa wahanga? Kwanini hao CCM wasitoe kutoka kwenye faida waliyoipata kutokana na hiyo milipuko? Maana kwa CCM milipuko na vifo vya watanzania, kwao ni dili na ndo wanapatia faida humo. Basi zinazozidi katika faida yao, wawasaidie hao wahanga wa mabomu.

Ndugu zangu tujadiliane, kulumbana na kubishana kadili tutakavyoweza lakini tusisahau kuzifunga speed governor ndimi zetu zisije kutoa maneno ya kijinai na yenye madhara. Kusema CCM au chama chochote au mtu yoyote kwamba amelipua mabomu ya Gongolamboto kwa makusudi ni kauli nzito. Ujuwe kwamba wapo tuliopoteza ndugu zetu wapendwa na wapo tuliopata majeraha makubwa. Maneno yoyote yanayoashiria kutaja kiini cha ulipukaji wa mabomu ni very sensitive na hayapaswi kusemwa kiutani utani bila kuwa na ushahidi.
 
Ni mwanzo mzuri wa vyama kufanya kazi za siasa bila kuingiliwa - vuguvugu hizi za kisiasa zinasaidia ku-articulate hisia na mawazo ya wananchi juu ya utendaji wa serikali; serikali makini italichukulia hili kama changamoto badala ya upinzani au uchochezi....
 
Kati ya watu wanaohitaji kuombewa na atolewe pepo wachafu ni ze marcopolo !!!!Hawa ni watu ambao akili yao haina akili.Bora uwe na mbuzi 6 utakula nyama lakini sio mtu mmoja wa kaliba hii!!!Wewe una upeo na maono kuliko maelfu ya watu hao!!Wenye elimu(slaa),wako hapo,wenye hela(mbowe,ndesambulo),wako hapo tusio na kitu tuko hapo tukidai maisha bora,umebaki wewe tu!!!wewe AMKA utoke shimoni!!!Ushindwe na ulegee kama umetumwa kawaambie tuko macho na bundi hatui juu ya bati
 
Hivyo wavihitajivyo yapatikana kwa kagoda,deep green,meremeta au malipo ya dowans? kungekuwa na serikali makini isoendekeza ufisadi yote yawezekana. msoandamana mna barabara hospitali na shule bora? una elimu kiasi gani hadi usielewe ukosefu wa maendeleo unatokana na nini?
Mnapoeza muda wa watu kufanya kazi. Watu wanataka barabara, hospitali, shule bora n.k. Hawataki maandamano.
Acheni uzushi, kahamasisheni shughuli za maendeleo.
 
Kwa hiyo maandamano ndio yataleta hospitali?
Vyama vinavyojifanya kujali kwa nini visihamasishe foundations zitakazofanya miradi ya maendeleo kwa mfano?
Maandamano feki ni unafiki tu!
Hhahahaha...Pale unapotaka kutukana lakin unashindwa kutukana na wivu wakutaka ingekuwa ni mafanikio ya upande uliopo...halafu unajikuta huko ulipo ndio hovyoooooo...Badilika nduguuu,Usingoje kubadilishwa...Siku utakayotaka kubadilika utajikuta umechelewa na kujutia muda uliopeteza...Tehhe..Nikuulize swali....We umefanya nini hata kimoja kusaidia jamii ambacho unaweza kujivunia au ambacho jamii inashukuru kwa mchango wako...ukianzia hapo kwako binafsi utaweza kuongeza nguvu katika kikundi ambacho unakiunga mkono.
Kumbuka Ili kujarubu kupata haki yetu Watanzania katika uongozi huu wa Thithiemu inabidi tutumie kanuni ya ng'ombe ya kupiga kelele ndipo watajua tunasikia kiu...Bila hivyo tutafia zizini....TAFAKARII NA KISHA CHUKUA HATUA SIO KUPINGA TUU...AGGGGHHRRRH..!!!Weee viippi!!
 
Mnapoeza muda wa watu kufanya kazi. Watu wanataka barabara, hospitali, shule bora n.k. Hawataki maandamano.
Acheni uzushi, kahamasisheni shughuli za maendeleo.
Kama watu hawataki maandamano mbona wamekuwa wakifurika kila sehemu? Hivi wewe mwana-CCM husomi upepo, hukuona jinsi Makamu wa Rais alivyokosa watu alipotembelea Mbeya hivi juzi? Kwa nini Makamu wa rais akose watu halafu CHADEMA wakusanye watu wengi? Akili kichwani mwako.
 
Back
Top Bottom