Mwanza: Yaliyojiri Mkutano wa Hadhara wa CHADEMA baada ya kuondolewa zuio la mikutano

Molemo

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
14,534
13,225
Ni asubuhi tulivu siku ya Jumamosi tarehe 21 Januari hapa Jijini Mwanza.

Macho na masikio ya Watanzania yanaelekezwa hapa Jijini Mwanza kutakakofanyika shughuli kubwa ya kisiasa ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo.

Chadema Leo inazindua Rasmi mikutano ya kisiasa baada ya kuzuiwa kwa miaka saba kinyume kabisa na Katiba kwa tamko la aliyekuwa Rais wa Tanzania John Magufuli.

Rais wa Sasa Samia Suluhu Hassan aliamua kuondoa zuio hilo haramu kutokana na Maridhiano ya Kitaifa yaliyoasisiwa na yeye Rais pamoja na Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe.

Freeman Mbowe atafanya uzinduzi huo wa mikutano kitaifa hapa Jijini Mwanza katika viwanja vya Furahisha.

Pia katika tukio jingine Chadema leo inaadhimisha miaka 30 tangu kusajiliwa kwake mnamo mwaka 1993

Kwa muda wa wiki nzima habari kubwa katika jiji la Mwanza na viunga vyake ni kuhusu Mkutano huu ambao unatarajiwa kuvutia maelfu kwa maelfu ya wananchi wa jiji hili na mikoa jirani.

Molemo Media tunatarajia kuwaletea mubashara matukio yote muhimu yatakayoendelea hapa Jijini Mwanza kabla na wakati wa Mkutano huo mkubwa wa hadhara.

Karibuni Sana!

====

UPDATES:
Muda huu wa saa 7 mchana tayari Uwanja wa Furahisha unapendeza.Maelfu ya wananchi wanaendelea kumiminika katika viwanja hivi kutoka kila pembe ya Jiji la Mwanza. Shauku kubwa ya wananchi ni kumsikiliza Mwenyekiti wa Chadema Taifa Freeman Mbowe ambaye ni kipenzi kikubwa Cha watu wa Kanda ya ziwa

Mwenyekiti Freeman Mbowe Yuko kwenye msafara mkubwa wa maandamano ya wananchi kutoka eneo la Buhongwa umbali wa Kama kilometa 20 hivi kuja hapa kwenye viwanja vya Furahisha. Msafara wa Mbowe umetanguliwa na Pikipiki nyingi za vijana wa Jiji la Mwanza huku wananchi wakiwa wamejipanga kando ya Barabara wakipunga mikono.Mwenyekiti Mbowe Yuko kwenye gari la wazi

Mbowe awasili viwanja vya Furahisha;

Mgeni Rasmi ambaye ni Mwenyekiti wa Chadema Taifa Freeman Mbowe amewasili katika viwanja vya Furahisha majira ya saa 8 na nusu akiwa ameambatana na Katibu Mkuu John Mnyika pamoja na Manaibu Katibu wakuu wakiwemo wajumbe mbalimbali wa Kamati Kuu.

Mbowe amelakiwa na umati mkubwa wa watu hapa Furahisha huku Uwanja ukilipuka kwa shangwe kubwa zikiimbwa nyimbo mbalimbali za Hamasa

Mkutano wafunguliwa Rasmi
Viongozi wa dini wamekaribishwa kuongoza maombi wakiwemo Makamu Mwenyekiti wa Makanisa ya Kikristo aliyeombea Mkutano kwa Niaba ya Wakristo pamoja na Sheikh Ally aliyeomba kwa Niaba ya dini ya Kiislamu

Mwenyekiti wa Mkoa wa Mwanza ametoa salamu fupi za kuufungua Mkutano huo kwa kusema wanachadema Mwanza watakuwa Kama nyuki wa kusambaza habari ya Ukombozi wa nchi.

Baada ya hapo amefuatia Katibu wa Kanda ya Victoria kwa utambulisho

Salaam za Viongozi mbalimbali;
Aliyekuwa mbunge wa Mbeya Mjini Joseph Mbilinyi maarufu Kama Sugu amekaribishwa kutoa salaam na kuutumbuiza umma kwa nyimbo zake mbili ambazo zimeshangiliwa Sana na wananchi

Baada ya hapo amekaribishwa Katibu wa Baraza la Wanawake Catherine Ruge ambaye ameahidi kuhakikisha Wanawake wa Chadema wanatembea nchi nzima kuwasemea wananchi

Mwingine aliyepata nafasi ya kusalimia ni Mjumbe wa Kamati Kuu Suzan Kiwanga ambaye amesema watatumia miaka miwili iliyobaki kabla ya Uchaguzi mkuu kutembea nchi nzima

Peter Msigwa Mwenyekiti wa Kanda ya Nyasa alisema tatizo kubwa la nchi hii ni watawala kuwa na uelewa mdogo wa mambo ndiyo maana nchi inakwama

John Heche Mjumbe mwingine wa Kamati Kuu amesikitishwa na Serikali kutaka kuleta Bima ya Afya kwa wote huku huduma zikiwa mbovu na kusema suala muhimu siyo kulazimisha Bima ya Afya kwa wote Bali Huduma Bora kwa wote

Pia Heche amezungumzia kwa uchungu hoja i ya vijana wataochaguliwa kwenda chuo kikuu hawataruhusiwa kujiunga na elimu ya chuo kikuu endapo watakuwa hawajapata bima ya afya

Mnyika ahutubia;
Katibu Mkuu John Mnyika amekaribishwa na Naibu Katibu Mkuu Bara ili aweze kuhutubia.

Mnyika amesema Siku ya leo ina matukio mawili kwa pamoja, mosi ni uzinduzi wa mikutano ya hadhara, pili ni maadhimisho ya miaka 30 ya CHADEMA tangu Ipatiwe usajili wa kudumu

Katibu Mkuu wa Chadema ndugu John Mnyika amemuomba Mwenyekiti wa chama hicho Freeman Mbowe kuitangaza rasmi kuwa siku ya tarehe 21 January kila mwaka iwe ni siku ya Chadema Day ikiwa sehemu ya kumbukumbu ya chama hicho.

Mwaka huu wa 2023 ni mwaka wa uchaguzi wa ndani 6a chama. Ni mwaka wa kuchagua viongozi wa msingi, matawi, kata, majimbo, wilaya, mikoa na kanda na Taifa "Ukiondoa masuala mengine yote ya wananchi, ajenda yetu kuu ni kudai katiba mpya na tume huru ya uchaguzi"

Mbowe aanza kulihutubia Taifa mnamo saa 11 Jioni
Mwenyekiti Mbowe amekaribishwa na Katibu Mkuu kuuhutubia umma wa Mwanza na Taifa kwa Ujumla.

Mbowe anasema, "Serikali ya awamu ya tano ililigeuza taifa hili kuwa taifa la maumivu, mateso na misiba." "Nikiri kwamba sisi sote tuliomizwa na mateso ya viongozi wetu. wana-chadema wameumizwa. wana-ccm wameumizwa na wapo wana-ccm walionufaika na mateso hayo."

Mbowe anaendelea kusema "taifa letu halipaswi kuwa taifa la kuumuza kiongozi yoyote, mwanachama yoyote, mfuasi wowote wa chama chochote. taifa letu linapaswa kuwa taifa la watu walioungana, wanaoshikamana, wanaosimama katika misingi ya demokrasia."

Taifa hili limepitia mengi, Taifa hili linapaswa kuwa na watu ambao wameungana, wameshikamana na kusimama katika misingi ya demokrasia, utawala wa sheria na haki kwa wote" Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa CHADEMA Tanzania

Ninaposimama kama mwenyekiti na kiongozi wa CHADEMA kudai haki, sisimami kwa ajili wa wana CHADEMA bali nasimama kama kiongozi wa kudai haki kwa watu wote" Freeman Mbowetz

Naomba nilisisitize sana, tusijenge tabia ya kuwachukia wanachama wa CCM kwa sababu ya madhila tuliyopitia. Wajibu wetu ni kuwashurutisha kwa hoja ili watambue, ndani ya CHADEMA kuna haki, ustawi na fursa ya kumsaidia kila mmoja na akawa raia mwema kwa nchi yetu" Freeman Mbowetz

"Tunahitaji kukaa kama nchi kutambua kwamba nchi hii haiwezi kuendelea kwa kugawana vipande vipande. kuwepo eti na kipande cha chadema, kuna kipande cha ccm, kuna kipande cha udp

"Hatuwezi kuijenga CHADEMA leo ya kujenga chuki kwa Taifa letu. CHADEMA tuna kauli kuu inayosema 'No Hate No Fear'. Natangaza wazi kuwa chama hiki sio cha chuki. Hatuwezi kujenga utaifa wa nchi hii kwa kujenga chuki" Freeman Mbowe

"Katika kujenga dhana ya 'No Hate' (hakuna chuki), iambatane na dhana kwamba hatumuogopi mtu," Freeman Mbowe Mwenyekiti wa CHADEMA Tanzannia.

"Nampongeza Rais Samia Suluhu kwa kukubali maridhiano. wapo watu wanatamani maridhiano yasifanikiwe. wao wanafaidi maisha nje ya maridhiano. samia alikubali nia ya maridhiano kinyume na matakwa ya chama chake. "Huyu rais akakubali nilichompendekezea kwa niaba yenu wote watu wa chadema. halafu, eti kuna watu wanataka nimtukane rais huyo. sitofanya kitu hicho kamwe."

Kwa pamoja tuna wajibu wa kujadiliana yapi ni mambo ya msingi ya kuyafanya ili kulipeleka Taifa letu katika Taifa lenye furaha, ustawi na haki kwa kila mtu" Freeman Mbowe Mwenyekiti wa CHADEMA Tanzannia

Freeman Mbowe Mwenyekiti wa CHADEMA Tanzannia, "yaani nyinyi [chadema] badala ya kunipongeza mbowe, mnakuja na mambo ya kiharamia, mnasema: 'mbowe karamba asali.' nyinyi mko noma sana aisee, yaani mko noma washkaji."

Freeman Mbowe, "yaani [chadema] mnaanza kusema kwamba eti mbowe karamba asali! hivi nyinyi mnajua mbowe nimepoteza bilioni ngapi kwa kuwa mwana-chadema? mnakubali kutunza propaganda za kitoto, kwamba eti mbowe karamba asali, hataki katiba mpya."

Freeman Mbowe, "wanachama wa chadema, wakiwemo viongozi wangu wakuu, wanasema: 'Mbowe anafanya usiri hatuambii. mwenyekiti mbowe yupo ikulu kila siku. hii mi-ccm siyo mijitu ya kuamini. mheshimiwa Mbowe karamba asali.'"

Katika miaka yangu 30 ya kupigania Taifa hili natamani nitakapoacha uongozi, niache Taifa langu, nchi yangu, watoto wangu, wajukuu wangu wakiwa wanapendana, wanaoshikamana na kuitafuta kesho yetu pamoja," Freeman Mbowe.

Freeman Mbowe, "Yaani kama kitu kimeshawahi kuniumiza katika historia yangu ya miaka 30 ya utumishi wa chama hiki ni kuwepo kwa mtu yoyote anayeweza kufikiria kwamba mimi freeman aikaeli mbowe eti naweza nikaramba asali ya aina yoyote ile, nikausaliti umma wa Watanzania.

Mamilioni ambao nimeteseka kwa miaka 30 kuwapigania. nilivumilia kwa sababu nilisema nina mambo makubwa ya kuyatafuta kuliko kauli za kipropaganda."

Freeman Mbowe,"nimesafiri kwenye safari hii kwa maumivu makubwa. nimepoteza mabilioni ya fedha. muda wangu wa maisha uliobaki ni mdogo kuliko nilioupoteza katika harakati za kutetea haki za wananchi na ndugu zangu."

FB_IMG_1674313698813.jpg
FB_IMG_1674313701433.jpg
FB_IMG_1674313704476.jpg
FB_IMG_1674313707231.jpg
 
Ni Asubuhi tulivu siku ya Jumamosi tarehe 21 Januari hapa Jijini Mwanza.

Macho na masikio ya Watanzania yanaelekezwa hapa Jijini Mwanza kutakakofanyika shughuli kubwa ya kisiasa ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo.

Chadema Leo inazindua Rasmi mikutano ya kisiasa baada ya kuzuiwa kwa miaka saba kinyume kabisa na Katiba kwa tamko la aliyekuwa Rais wa Tanzania John Magufuli.

Rais wa Sasa Samia Suluhu Hassan aliamua kuondoa zuio hilo haramu kutokana na Maridhiano ya Kitaifa yaliyoasisiwa na yeye Rais pamoja na Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe.

Freeman Mbowe atafanya uzinduzi huo wa mikutano kitaifa hapa Jijini Mwanza katika viwanja vya Furahisha.

Pia katika tukio jingine Chadema leo inaadhimisha miaka 30 tangu kusajiliwa kwake mnamo mwaka 1993

Kwa muda wa wiki nzima habari kubwa katika jiji la Mwanza na viunga vyake ni kuhusu Mkutano huu ambao unatarajiwa kuvutia maelfu kwa maelfu ya wananchi wa jiji hili na mikoa jirani.

Molemo Media tunatarajia kuwaletea mubashara matukio yote muhimu yatakayoendelea hapa Jijini Mwanza kabla na wakati wa Mkutano huo mkubwa wa hadhara.

Karibuni Sana!
Molemo habari za siku nyingi. Angakau leo nimekusoma. Ulipotea kabisa.
Naomba hakikisha picha su video zitumwazo zisomeke. Mara nyingi ukutumia app baadhi huwa hazisomeki. Inaelekeza tu fungua, fungua..... hadi unaghairi

Sent from my SM-G977B using JamiiForums mobile app
 
Vyema tujue agenda zao zitakuwa zipi..

Ukiondoa hali ya ugumu wa maisha inayoambatana na bidhaa hasa nafaka kupanda bei kila siku, Katiba Mpya inatakiwa kuwa ajenda ya kudumu.

Ni vyema hilo dai wakaliwekea time limit, ili kuzuia uwezekano wa kwenda kwenye uchaguzi wa S/M 2024 tukiwa na Katiba iliyopo, kama hawatafanikisha hilo, wajiandae kupigwa kwenye uchaguzi mkuu 2025 endapo watashiriki.
 
.Molemo Media tunatarajia kuwaletea mubashara matukio yote muhimu yatakayoendelea hapa Jijini Mwanza kabla na wakati wa Mkutano huo mkubwa wa hadhara.

Karibuni Sana!
Mkuu Molemo, asante sana, tutafuatilia live kutokea hapo Uwanja wa Furahisha, naamini besides live ya Molemo Media, pia kutakuwa na live za mainstream media ambazo zina national wide coverage kama TBC, ITV, Star TV, Channel Ten, na Azam TV.

I wish Chadema all the best, leo ni kweli macho na masikio ya Watanzania wote, hadi wale "jamaa zetu" ni viwanja vya Furahisha, huku wengi wakiwa very high expectations na ku anticipates kuwa Mbowe atakiwasha!, huku tunaojua ukweli tunajua hawezi kukiwasha kufuatia wema mkubwa Mama aliomtendea, licha ya kumfutia kesi na kumuachia huru, pia Mama amekuwa mwema zaidi kwa kum icapacitate kwa capacity building kuwazesha mambo yawe, ikiwemo funding some activities including vikao na trips ikiwemo overseas, hivyo haitegemewi shukrani ya punda, Mbowe ni muugwana na mtu wa shukrani hivyo leo Samia atashukuriwa.
P
 
Mkuu Molemo , asante sana, tutafuatilia live kutokea hapo Uwanja wa Furahisha, naamini besides live ya Molemo Media, pia kutakuwa na live za mainstream media ambazo zina national wide coverage kama TBC, ITV, Star TV, Channel Ten, na Azam TV...
Sijui kwa nini baada ya kumtoa Shaka hawajakuweka wewe bali wakamuweka Mjema, unajua sana propaganda based on UONGO.

Sent from my SM-A125F using JamiiForums mobile app
 
Ni Asubuhi tulivu siku ya Jumamosi tarehe 21 Januari hapa Jijini Mwanza.

Macho na masikio ya Watanzania yanaelekezwa hapa Jijini Mwanza kutakakofanyika shughuli kubwa ya kisiasa ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo.

Chadema Leo inazindua Rasmi mikutano ya kisiasa baada ya kuzuiwa kwa miaka saba kinyume kabisa na Katiba kwa tamko la aliyekuwa Rais wa Tanzania John Magufuli.

Rais wa Sasa Samia Suluhu Hassan aliamua kuondoa zuio hilo haramu kutokana na Maridhiano ya Kitaifa yaliyoasisiwa na yeye Rais pamoja na Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe.

Freeman Mbowe atafanya uzinduzi huo wa mikutano kitaifa hapa Jijini Mwanza katika viwanja vya Furahisha.

Pia katika tukio jingine Chadema leo inaadhimisha miaka 30 tangu kusajiliwa kwake mnamo mwaka 1993

Kwa muda wa wiki nzima habari kubwa katika jiji la Mwanza na viunga vyake ni kuhusu Mkutano huu ambao unatarajiwa kuvutia maelfu kwa maelfu ya wananchi wa jiji hili na mikoa jirani.

Molemo Media tunatarajia kuwaletea mubashara matukio yote muhimu yatakayoendelea hapa Jijini Mwanza kabla na wakati wa Mkutano huo mkubwa wa hadhara.

Karibuni Sana!
CHADEMA for real.. CHADEMA 4ever!
chadema_770_414shar-50brig-20.jpg
 
Back
Top Bottom