Maandamano ya CHADEMA Jijini Mwanza

Regia Mtema

R I P
Nov 21, 2009
2,970
863
Wakuu yale maandamano ya CHADEMA katika Kanda ya Ziwa ndio yameshaanza.Maandamano yameanzia Buzuruga kuelekea uwanja wa Furahisha.Watu ni wammejitokeza kwa wingi wa jinsia na rika zote.Kwabahati mbaya sijakaa kwenye position nzuri ya kurusha picha lakini nikipata fursa nzuri nitazirusha.

Aluta Continua.

From kwenye Maandamano Mwanza

Regia E Mtema
Waziri Kivuli-Kazi na Ajira

PICHA ZAIDI, fuatilia hii thread - PICHA: Maandamano ya CHADEMA Mwanza

182093_1470892587284_1682707865_914231_1937388_n.jpg

HPIM0916.jpg
HPIM1103.jpg

HPIM1104.jpg
HPIM1105.jpg

HPIM1098.jpg
HPIM1099.jpg

HPIM1100.jpg
HPIM1101.jpg

HPIM1106.jpg
HPIM1108.jpg

HPIM1109.jpg
HPIM1111.jpg

HPIM1113.jpg
HPIM1114.jpg

HPIM1116.jpg
HPIM1115.jpg

HPIM1279.jpg
HPIM1119.jpg

HPIM1118.jpg
HPIM1121.jpg
 
Ahsante mkuu, Je hakuna dhoruba kali toka kwa watawala juu ya maandamano hayo?
 
Mnapoeza muda wa watu kufanya kazi. Watu wanataka barabara, hospitali, shule bora n.k. Hawataki maandamano.
Acheni uzushi, kahamasisheni shughuli za maendeleo.
 
Wakuu yale maandamano ya CHADEMA katika Kanda ya Ziwa ndio yameshaanza.Maandamano yameanzia Buzuruga kuelekea uwanja wa Furahisha.Watu ni wammejitokeza kwa wingi wa jinsia na rika zote.Kwabahati mbaya sijakaa kwenye position nzuri ya kurusha picha lakini nikipata fursa nzuri nitazirusha.

Aluta Continua.

From kwenye Maandamano Mwanza

Regia E Mtema
Waziri Kivuli-Kazi na Ajira
Endelea kutujuza tafadhali...
 
Mnapoeza muda wa watu kufanya kazi. Watu wanataka barabara, hospitali, shule bora n.k. Hawataki maandamano.
Acheni uzushi, kahamasisheni shughuli za maendeleo.

Mkuu,
Jambo muhimu kabla ya ku-criticise ni kujiuliza...ni nini kiini/theme ya maandamano ya mwanza? What are they demanding for?
Baada ya majibu...hapo tunaweza ku-conclude aidha negatively au positively.
 
Hamjawahi kuhamasisha hata ujenzi wa shule ya kata, kazi yenu kuandaa maandamano tu. Huo ni unafiki wa kisiasa, hamna moyo wa kweli wa kuleta maendeleo Tanzania.
 
Mnapoeza muda wa watu kufanya kazi. Watu wanataka barabara, hospitali, shule bora n.k. Hawataki maandamano.
Acheni uzushi, kahamasisheni shughuli za maendeleo.

Unafikiri maendeleo yanakuja pasipo kuhangaika. Tanzania hakuna maendeleo pasipo kuandamana.
 
mheshimiwa hebu tujuze kuna kama wabunge wangapi na viongozi wa kitaifa wa mwanza
 
Mnapoeza muda wa watu kufanya kazi. Watu wanataka barabara, hospitali, shule bora n.k. Hawataki maandamano.
Acheni uzushi, kahamasisheni shughuli za maendeleo.

Ni wewe tu ndiyo unaogopa nguvu ya umma (maandamano). Unafaidika na uozo uliopo nn?

Maandamano yanadai matumizi makini zaidi ya raslimali za nchi yetu, ili kiasi kinachookolewa kikajenge hizi barabara, hospitali, shule unazozisema.

Hongera Mwanza. Huu uwe ni mwanzo tu. Inahitajika sustained pressure kuwasambaratisha hawa mafisadi.
 
Mkuu,
Jambo muhimu kabla ya ku-criticise ni kujiuliza...ni nini kiini/theme ya maandamano ya mwanza? What are they demanding for?
Baada ya majibu...hapo tunaweza ku-conclude aidha negatively au positively.

Cha msingi sio kujua theme bali ni kujiuliza jamii itanufaika vipi na maandamano hayo na je, jitihada zinazotumika kuandaa maandamano zisingeweza kutumika kuleta manufaa zaidi? Hawa wote wanafiki tu!
 
Mnapoeza muda wa watu kufanya kazi. Watu wanataka barabara, hospitali, shule bora n.k. Hawataki maandamano.
Acheni uzushi, kahamasisheni shughuli za maendeleo.

Kama wanaotakiwa walete hizo hospitali, barabara, nk wako kimya uendelee kusubiri hadi lini???
 
Cha msingi nini wewe mshamba tu kwani wanaoandamana sio wana jamii? Muhuni wewe na mkeo
 
Ni wewe tu ndiyo unaogopa nguvu ya umma (maandamano). Unafaidika na uozo uliopo nn?

Maandamano yanadai matumizi makini zaidi ya raslimali za nchi yetu, ili kiasi kinachookolewa kikajenge hizi barabara, hospitali, shule unazozisema.

Hongera Mwanza. Huu uwe ni mwanzo tu. Inahitajika sustained pressure kuwasambaratisha hawa mafisadi.

Kwa hiyo unadhani baada ya maandamano hayo uchwara bajeti ya nchi itabadirishwa?
Nothing will be achieved by those maandamano other than media attention!
 
Vipi maandamano ya chadema huko rocky city shwarii,naombeni wadau wa ukanda huo mtupe yaliyojiri au yanayoendelea kujiri!!!!!!!!!.
 
Mnapoeza muda wa watu kufanya kazi. Watu wanataka barabara, hospitali, shule bora n.k. Hawataki maandamano.
Acheni uzushi, kahamasisheni shughuli za maendeleo.

Wewe ukome kabisa na upotee unaonyesha una u- MANIAC fulani kichwani mwako.

kawaulize wajomba zako BI ALI NA MUBARAK watakuambia km kweli watu walipoteza mua wao au la, pia shemjio Gadafi sasa hatoki ndani anatumia mtondooo
 
Kama wanaotakiwa walete hizo hospitali, barabara, nk wako kimya uendelee kusubiri hadi lini???

Kwa hiyo maandamano ndio yataleta hospitali?
Vyama vinavyojifanya kujali kwa nini visihamasishe foundations zitakazofanya miradi ya maendeleo kwa mfano?
Maandamano feki ni unafiki tu!
 
Back
Top Bottom