Mimi nashangaa chain of command yetu iko wapi. Lowassa yeye ni nani kuzungumza kwa niaba ya JWTZ? Kamanda in Chief yuko wapi? Yaani Tanzania yetu imeshaparaganyika kiasi kwamba yeyote tu anaweza kuzungumza kwa niaba yake? Suala la vita au kuwa tayari kwa jeshi letu ni kamanda in chief peke yake anayeweza kulizungumzia. When was the last time you saw Lowassa inspecting a guard of honour?
Huyu Mmasai hapo ndipo ninapompendea katika maamuzi magumu. Huwa haumi maneno.
Kwa mara ya kwanza nakubaliana na Lowassa katika tamko thabiti na lisilo la kumung'unya maneno.
Tunatumaini ndugu zetu wa Malawi watatuelewa vizuri katika hili.
Wakato mwingine si vibaya kutunisha misuli jirani anapoleta chokochoko.
Nashukuru Mungu mpango wa reserve army wa JKT nao unaanza karibuni.
Ikibidi kuingia vitani jeshi letu liko vizuri sana na kama ilivyo ahadi yao (JWTZ), wako tayari kulinda mipaka ya nchi yetu hadi tone la mwisho. Tunasali sana tusifike hapo, - alisema Lowassa..
Acha nidhamu za woga. JWTZ wenyewe wana hamu ya kupigana.
Lakini vita siyo kitu cha kushangilia hata kidogo. Inaweza kutuathiri sana. Kwangu mimi naona ni mapema sana kuanza kufikiria hili la kupigana. Juhudi za kidiplomasia zingetumika kwanza kutatua huu mgogoro.
mbona sijaona pahala wamalawi wamesema hawataki hao uliowataja wanufaike na ziwa Nyasa?can you back up you claims?suluhisho la mgogoro ni lipi?huu mgogoro ulivyo,mwenye kuwa juu ni mwenye influnce at the time being,kama mama Clinton yuko nao,wala msijisumbue,kamateni mafisadi kwanza,nchi itarudi kwenye msitari,"umma" utalinda nchi.Kuna pahala panshinda nguvu ya umma?jeshi lipo lakini hata recruiting inafanyika kwenye umma wa wananchi,na sapoti ya vita pia.Hatuna nguvu za "big nations" kujiamulia bila sapoti kubwa ya wananchi.Halafu matatizo tuliyonayo ni makubwa kiasi kwamba kupostpone hii issue ni more relevant.
Mimi nashangaa chain of command yetu iko wapi. Lowassa yeye ni nani kuzungumza kwa niaba ya JWTZ? Kamanda in Chief yuko wapi? Yaani Tanzania yetu imeshaparaganyika kiasi kwamba yeyote tu anaweza kuzungumza kwa niaba yake? Suala la vita au kuwa tayari kwa jeshi letu ni kamanda in chief peke yake anayeweza kulizungumzia. When was the last time you saw Lowassa inspecting a guard of honour?
Kutokana na chokochoko waziletazo nchi jirani ya Malawi na kupitia kauli za viongozi wetu Mh.Membe wakati anawasilisha Budget yake na Mh. Lowasa kupitia kikao cha siri cha Kamati yake sasa wakati umefika wa kulipia matumizi ya jina hilo la Makamanda.
Ikitupasa kuingia vitani basi nashauri wale wote wajigambao kuwa makamanda,wazalendo wa kweli na wapigania haki ni wakati wao kusonga front kama chambo ili wakainusuru Mipaka ya Nchi yetu.
Kazi kwenu kombania ya Green Guard, Blue guard na Wazee wa gwanda.