Najua mengi yatachangiwa humu kuhusu tamko hilo la LOWASA. wengine watasema ni shujaa, wengine watasema ni zaidi ya Serikali, wapo watakaomponda kuwa anatapatapa, lakini ukweli ubaki pale pale kuwa VITA siyo jambo ka kukimbilia hata kidogo na hakuna haja ya kulishabikia kisias, Cha msingi tu, tuombe mambo yaishe salama. Wazee wetu, watoto wetu, akina mama wajawazito kupitia maombi yao watatutafuna na hakika wote tunaoshabikia tukifikiri ni njia mojawapo ya kujipatia umaarufu kisiasa tujiulize kama tunafanya hivyo ili iweje?Kama Kuna chama cha siasa au mwanasiasa anaona hii ni njia ya kujipatia umaarufu kwa kusema, Serikali inaogopa au CCM ni waoga na serikali yao, huyo hafai hata siku moja kujiita rais wa Tanzania. Mungu ibariki Tanzania, Mungu ibariki Afrika.