Lowassa: Tuko tayari kuingia vitani na Malawi...

Mkuu Jasusi nilidhani ni mimi mwenyewe nimeona upungufu huu wa wanasiasa wanaopenda kutumia kila nafasi inayojitokeza kwa faida za kisiasa.


Mimi nashangaa chain of command yetu iko wapi. Lowassa yeye ni nani kuzungumza kwa niaba ya JWTZ? Kamanda in Chief yuko wapi? Yaani Tanzania yetu imeshaparaganyika kiasi kwamba yeyote tu anaweza kuzungumza kwa niaba yake? Suala la vita au kuwa tayari kwa jeshi letu ni kamanda in chief peke yake anayeweza kulizungumzia. When was the last time you saw Lowassa inspecting a guard of honour?
 
Last edited by a moderator:
Lowassa anababaika sana.
Kauli ya mhe Membe ilitosha sana kuonesha msimamo wa nchi
Ila kwa kuwa anapenda publicity akaona na yeye atoe msimamo
 
Hizi ni kauli za kitoto kabisa, Hakuna ushujaa wowote kutoa kauli km hizo kwenye press! By the way there is a chain o f command na anaepaswa kuyazungumza hayo yupo ila HATUJAFIKA UKO kwani diplomcy imeenza...Ni vizuri kujiandaa kwa kuyaweka majeshi yetu ktk state of alert/emergency na sio kutangaza..Siku zote chokochoko km hizi za kina LOWASSA ndo hua zinazua mambo na kupelekea mambo kupalaganyika...Malawi ni jirani yetu na watanzania wengi tu wapo uko...Cha msingi tumeshatuma warning kupinga kwa njia z kidiplomacy lets wait and see the response and not otherwise!
 
Mkuu Jasusi, Lowassa ndiye M/Kiti wa Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama, hivyo anazo nguvu na mamlaka yote kuzungumzia hili!.

Kwa powers alizo nazo, anaweza kumsummon MFI (Membe), CDF (Mwamunyange), CIS (R.O) na IGP (Mwema).

Utakuwa umechanganya kati ya kuzungumzia uwezekano wa Tanzania kuingia vitani na powers za kutangaza vita!.

Mwenye mamlaka ya kutangaza vita ni Amiri Jeshi Mkuu pekee na hakuna ku delegate jukumu hili!, lakini kuzungumzia nia ya kuilinda mipaka yetu, any leader anaruhusiwa kusema!.

Naendelea kukumbushia posibility ya
"Jiwe Walilolikataa Waashi, Litafanywa Kuwa Jiwe Kuu la Pembeni!".

Pasco.


oh boy!
 
Jamani mimi naomba kuuliza tu, hii ni kauli ya Lowasa au ni kauli ya Kamati ambayo yeye ndio Mwenyekiti na ameongea kwa niaba ya kamati nzima? i mis some point here!



Lowasa ameunga mkono kauli ya membe ambayo Ndio kauli ya serikali yeye ameongea Kama mwenye kigoda wa kamati kuunga mkono kauli ya membe ambaye ndiye aliyeisemea serikali( Nadhani hapo point ni je kwanini kauli ya Lowasa iko strong compare na ya membe ambayo iko newtro?) jamani kwenye hili Tuweke tofauti na itikadi na ufisadi wetu pembeni Lowasa ni jembe basi tuu ni Izo kashfa na kuwa kondoo wa kafara otherwise he is a man of word kuliko viongozi wote walio madarakani include JK. Uyu Jamaa angetufaa sana kuwa comander I'n chief kuliko hata handsome boy wetu. Mwizi lakini mchapakazi na mwenye msimamo tofauti na handsome wetu mwizi, Hana msimamo na amekuwa akicheka hata msiba naona bora Lowasa kwa asilimia 100
 
Kuwen na uelewa, lowasa ni m/kiti wa kamati ya ulinzi na mambo ya nje, in case of anything beyond agreement diplomatically, rais atatangaza vita na siyo lowasa. Hata mvua inaanza kwa rasharasha. Akina lowasa ni rasharasha kabla ya mvua kutua. Pia tambueni kuwa vijana wanavaa kombati bila nishan, acheni wakazipate hizo za malawi jamani.
 
Swali la kizushi kwenu wadau wa JF. Ikiwa Malawi wakishika bango kudai nyasaland, wakenya nao wadai kanda ya kaskazini, waganda nao wadai bukoba alafu waungane je tutatokea mlango UPI? Sitamani iwe ivo ila tuchukulie Ndio imekuwa ivo itakuwaje? Ikumbukwe warombo walinyimwa Sukari wakapandisha bendera za Kenya rombo nzima na kushusha ya tz iyo ilikuwa ni sababu tosha ya kuwafungua wakenya masikio na wamesha anza kuchukua hatua za awali kwa kujenga uwanja wa ndege rombo mnalionaje hili wadau?
 
mzee mwanakijiji, you might be growing too old!. Kwa kawaida as one grows older is also expected to be wiser, nikukosoma siku hizi nakuona you are either becoming less wiser au inawezekana mimi ndio nashindwa to make sense hivyo uwezo wa uelewa wangu ndio unapungua kuweza kukuelewa!.

Hivi kuna sababu nyingine yoyote ya nchi kuingia vitani ambayo ni kubwa zaidi ya nchi kutishiwa mipaka yake?.

Kuna justfied wars na unjustified wars!. Kwangu mimi kitisho cha malawi ni justified war!. El is right and he is the not only the one who can make the best president of this country but he is "the one and only best" ccm has!.

Kwa kauli kama hii, ni uthibitisho kuwa yeye tayari ndiye amiri jeshi wetu!. Who else?. Nani mwingine yoyote ameweza kujitokeza to stand firm on this national security threat?!.

Naendelea kusisitiza tuendelee kukosoa madhaifu na madudu ya serikali iliyopo kwa nguvu zetu zote, ila pia kama kuna mabaya 99 na zuri moja, hilo moja litajwe!.

Hii kauli ya el imekuja mahali pake at the right place at the right time!.

Pasco.

watu wa lowassa mmepata pa kutokea,eti kauli ya lowassa!hivi ni ya lowassa ama ya kamati anayoingoza?nahitaji ufafanuzi zaidi
 
Mwalimu Jk.Nyerere alikuwa na upeo wa ajabu sana wa kujua dhamira mbovu na uongozi usio na tija kwa baadhi ya watanzania kama Kikwete tumeshashudia wenyewe Lowasa naye huyo na watanzania tunatakiwa kuwa makini kushabikia vita, vita wanaweza usa pekee ambao siku zote wanapigania mbali kabisa na nchi yao lakini sisi na malawi pua na mdomo Lowasa kwao arusha na inawezekana hana ndugu mbeya, iringa,songea au rukwa sehemu ambazo lazima zitadhurika kwa uzarishaji na tanzania kuingia kwenye janga la njaa.
 
Ikibidi kuwachapa hao wapori pori inabidi wachapwe. Vita si ya kufurahia ila kama haki ni yetu lazima tuipiganie.
Vita vya kupambana na ufisadi ambao umepoteza maisha ya Watanzania wengi kuliko vita ya Kagera vimetushinda.Huhitaji mizinga wala ndege za kivita kupambana na adui huyu ufisadi kwa nini vimetushinda?
Tusijidanganye, Ukiona matamko kama hayo yanatolewa na mtu yeyote ujue serikali iko disorganized ni kama kundi la walevi bar kwamba kila mtu anaweza kusema apendalo na asilopaswa kusema ili Barmaid amwone anafaa.
Hawa wanasiasa wasituvunge. Jeshi letu sii moja tena! kuna tofauti kubwa sana ya kifikra kati ya Officers and men. Serikali na watu wake kwa sasa wako tofauti sana kifikra na kimtazamo. Katika hali kama hiyo vita viwe na hatua ya mwisho kutajwa.
Nakumbuka 1978 ushindi wa JWTZ ulirahisishwa na Raia wa Uganda kuchoshwa na Serikali ya Amin na kutoa siri na ushirikiano kwa jeshi letu. Sisi tumejiuliza kwa kiwango hiki cha utendaji wa serikali,Polisi wetu,viongozi watendaji wa ngazi zote (na CCM pia) wameweza ku maintain hali ya wananchi kuipenda nchi yao au wamedharau kiasi cha raia mipakani kutamani wangekuwa raia wa nchi hizo jirani?
Kwa tamko hilo la EL, kuna mawili, eitha anamdharau anayepaswa kutoa tamko au nchi hii inautawala wa kambale kila kambale ana ndevu hata mtoto au mama wote ndevu tuu.
,
 
EL ana-take advantage kwenye mfumo wenye uongozi ulio dhaifu from top to bottom, otherwise tamko lake hakupaswa kulitoa at this stage and minute.

tumeambiwa juzi tu hapa kuwa kulikuwa na delegation kutoka serikali ya malawi iliyohudhuria moja ya vikao vya bunge. jamani, kweli mtu anakuja harmlessly hadi chumbani kwako kukusalimia au kuongea na wewe kistaarabu lakini wewe unatoka huko nje unatangaza vita naye? ni sahihi kweli?

mwalimu nyerere (rip) alitangaza vita na amini, lakini hii ilikuwa ni baada ya kufanya necessary but failed "due diligence" kupitia AU (OAU wakati ule).
tusichanganye mambo na kilichotokea wakati ule. yes, mwalimu alikuwa mbabe.... lakini the old man knew what to do when and where!
 
Huyu bwana EL kwa kauli na maamuzi ya haraka (stahili kwa wakati stahiki) huwa nampa 100% na kwa jinsi anavyamua ni bora hata ndo angekuwa Rais wa hii nchi maana yule mtalii huwa hana kauli nzito kama ya huyu bwana zaidi utasiki "...sina hela hiyo ya kuwalipa; atakaye taka kazi aendelee, asiye taka aache"

Hata kwa hili angeweza sema "...wakitaka kuendelea waendelee, wakitaka waache; sina nguvu wala hela ya kuharibu kupambana nao".
My thinking
 
Kuwen na uelewa, lowasa ni m/kiti wa kamati ya ulinzi na mambo ya nje, in case of anything beyond agreement diplomatically, rais atatangaza vita na siyo lowasa. Hata mvua inaanza kwa rasharasha. Akina lowasa ni rasharasha kabla ya mvua kutua. Pia tambueni kuwa vijana wanavaa kombati bila nishan, acheni wakazipate hizo za malawi jamani.
Very good mzee, watu wanashindwa kuelewa kuwa we are building up pressure on the other side, forcing them to see our point of view.

Nashangaa sana watu wanaomshambulia EL katika hili.
Huko Israel, when it comes to matters of National Security , iwe Kadima, Party, Laobour na vyama vingine -msimamo unakuwa mmoja na ni wa kuteteta maslahi ya nchi.

Shame on the dithering commentators katika mada hii.
 
Maneno ya kujifurahusha hayo! Vijana wa JWTZ hawana morali hata kidogo ! Nani anaenda kupigana vita wakati dhuluma imetapakaa kila sehemu? Hata JWTZ kwenyewe kunafukuta moshi ndani kwa ndani kwa muda mrefu sasa.. Vijana wanaonewa , wanahujumiwa nafasi za masomo, posho halali Na mengine mengi.. Kwa maoni yangu kuingia vitani kipindi hiki imekula kwetu..
Naungana mkono na wewe.Kwanza uzalendo huu wa Lowasa unatoka wapi wakati ni yeye na wenzake tayari walishaisaliti nchi hii kwa njia za kifisadi lakini mbaya zaidi ni kwamba kama vita hii itapiganwa Watanzania tutambue kwamba tunaenda vitani tukiwa tumegawanywa na hawahawa akina Lowasa na Mimi nina wasiwasi vita hii kama itatokea itajenga mianya mingine ya kufisadi raslimali za Taifa hili.
 
Mbunge wa Monduli Edward Lowassa amedandia huja ya kuingia vitani na Malawi. Licha ya kuwa yeye ni mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama ya bunge hana uhalali wala mamlaka ya kusema kwamba tanzania imejiandaa kuingia vitani kama ikibidi. Hiki ni kiherehere ili aonekane na yeye bado yumo. Rais wa nchi ndiye mwenye mamlaka ya kufikiri kushauriwa na kuamua kama nchi iingie vitani au vipi. Labda anajitutumua baada ya kuona mpinzani wake ambaye ni kiongozi serikalini amezungumzia suala hilo lakini kimsingi huyu bwana has no business talking about the damn war
 
Atajifanya kusema yupo teyari kuingia vitani akifikiri hii vita niya waTz wote kama ile ya uganda, ninachotaka kumtaarifu tu ni kwamba kwa hali ya ufisadi sasa si wamoja tena kama ilivyokuwa awali bali tutawaachia mafisadi washirikiane na hao JWTZ huku sisi tukaa pembeni kushuhudia tena ikiwezekana tutawasaidia wamalawi kwani wao watawanufaisha wananchi wake kutokana na gase watakayoipata ila siyo Tanzania
 
Maneno ya kujifurahusha hayo! Vijana wa JWTZ hawana morali hata kidogo ! Nani anaenda kupigana vita wakati dhuluma imetapakaa kila sehemu? Hata JWTZ kwenyewe kunafukuta moshi ndani kwa ndani kwa muda mrefu sasa.. Vijana wanaonewa , wanahujumiwa nafasi za masomo, posho halali Na mengine mengi.. Kwa maoni yangu kuingia vitani kipindi hiki imekula kwetu..

Hawa wanyasa ni watu wenye akili sana kwani wameishasoma hali ya nchi kuwa morali yake iko chini sana na ndio maana wamechokoza; na mkifanya kosa kwenda vitani kama huyo fisadi EL anavyoshabikia , mtajilaumu nyie na kizazi chenu!! Kwanza ukilaza wenu umewafanya muizarau Malawi kuwa nchi ndogo haina nguvu, kumbuka Israel ni nchi ndogo na imezungukwa na maadui lukuki lakini inawapa wote kipondo, na waisrael wanawafadhili wanyasa huku nyie mnalala kitanda kimoja na waarabu!! Ngoma ndio ipo hapo, mkijaribu tu mwanamke mama Banda atawapa kipondo cha hamu bora mtumie diplomasia mpaka hapo mtakapomaliza kuiondoa ccm madarakani!!
 
Back
Top Bottom