Je, ni sahihi Tanzania kuendelea na uhusiano wa kawaida na Rwanda wakati tuko vitani na nchi hiyo DR Congo?

kmbwembwe

JF-Expert Member
Aug 16, 2012
10,436
7,225
Nchi ya Rwanda chini ya Kagame imekua kwa muda mrefu ikishutumiwa kukisaidia kikundi cha kijeshi cha Watutsi cha M23 kinachotaka kulidhibiti jimbo la kivu mashariki ya congo. Rwanda imekua ikikanusha kusaidia M23 lakini ukweli imekua na majeshi yake yakiungana na waasi hao kudhibiti maeneo ya madini ambapo madini yanaporwa na kuingizwa Rwanda ambapo yanasafirishwa nje kama mazao ya nchi hiyo.

Hivi karibuni Kagame baada ya kugeukwa na wafadhili wake wakuu Marekani na nchi za magharibi kwenye kuihujumu congo amekubali huku akihamaki vikali ana majeshi kivu na kutoa sababu za kuonesha ukabila na umbari wa kitutsi ndio sababu ya rwanda kuweka majeshi congo. Wafadhili hao pia wameonyesha kutambua mauaji ya kimbari hayakua kwa watutsi tu ila kwa wahutu yakifanywa na jeshi la kagame.

Rwanda imekua kikwazo cha amani kivu na imeendelea kupora madini na kutaka kuweka utawala wa watutsi wachache kivu kama ilivyo rwanda. Inaelekea malengo ya muda mrefu ya Kagame ni kupora jimbo la kivu na kulifanya sehemu ya Rwanda inayotawaliwa na watutsi walio wachache eneo hilo. Hiyo ni dalili mbaya kuwepo amani eneo la maziwa makuu.

Kutokana na udhaifu wa uongozi congo nchi hiyo imeomba msaada nchi za SADC kuisadia kupambana na waasi hao wa kitutsi na jeshi la Rwanda. Rwanda hivi karibuni wameshambulia kikosi cha tanzania congo na kuwaua askari zetu watatu huko. Nchi hiyo ambayo haina bahari inategemea bandari za Tanzania kwa kiasi kikubwa. Silaha kwa jeshi lake zinapita bandari za tanzania. Je, ni sahihi kuendelea kuruhusu nchi hiyo chokozi kuendelea kuingiza silaha kupitia nchini kwetu wakati ukweli tuko nao vitani?
 
Sio mtabiri
Dunia inaenda kuwa sehemu mbaya sana ya kuishi.
Vita itakuwa kila mahali
 
Your opinion is not a fact! Ndio maana mpaka sasa hakuna mgogoro wowote waki diplomasia baina ya nchi izo mbili.
 
Back
Top Bottom