Lowassa: Tuko tayari kuingia vitani na Malawi...

Haya ndio maneno aliyoshindwa kusema MEMBE juzi Bungeni. Sielewi nani alimwambia Membe awaite wa Malawi ''WENZETU'' wakati wao wanajiandaa kutupiga kivita.

Tangu lini adui akawa mwenzako?

Mbona unakuwa biased, na haya hapa chini yana tofauti gani na ya Membe

Watanzania na Wamalawi nindugu wa muda mrefu.

Mtu anayemwita adui "mwenzetu" na anayemwita adui ndugu tena wa muda mrefu, what's the difference.
 
Siamini hili; hii ndio sababu ya kwanini siamini anafaa kuwa Rais. Anazungumzia vita leo? kwa lipi hasa? wanataka kuescalate vitu bila sababu ya msingi. Hafai kuwa Amiri Jeshi Mkuu. Kama hii ni sababu ya kwenda vitani basi tumekosa viongozi kweli kweli!
Sikubaliani na wewe. Suppose hao wamalawi wanaingia ndani ya mipaka ya nchi tukae tu kimya?? kama hatutapigan kwa hilo tutapigana kwa lipi maana kwangu huo ni uchokozi usiovumilika.
 
Wapuuzi wakubwa hawa, wametuulia jeshi letu na maufisadi yao halafu wanakuja na maneno ya kujifariji. Vita ikianza wewe na huyo shoga yako na fisadi mwenzio mwende mkapigane.Jeshi linaagiza mavifaa mabovu ili mpate nafasi ya kufisadi halafu mnakuja kuwadanganya watanzania kuwa mna vifaa vya kisasa! $h#nz! wakubwa nyie.
Watanzania kwa kupigana kwa maneno hamjambo!

Hapa tayari umeshaua askari kumi wa Malawi.

Hot air kills!
 
I support Edward Lowassa,just like George W Bush are the kind of people wasiomumunya maneno when it comes to the issue of National Security
 
wamalawi mpaka sasa wamekaza ...hawataki kujadili hili swaa..wanadaia ziwa ni lao lote...
 
I support Edward Lowassa,just like George W Bush are the kind of people wasiomumunya maneno when it comes to the issue of National Security

Ni vizuri wale wa maneno matupu wakaelewa hivyo.
Mwalimu alikuwa categorically straight kwenye issues kama hizi
...sababu ya kumpiga tunayo..
...uwezo wa kumpiga tunao...
...nia ya kumpiga tunayo..
...tutampiga mshenzi huyu...

Ni bahati kuwa sababu zote za kuingia vitani hazijatimia, lakini the nation should wlk along this mood, na ndio maana Lowassa is right on this issue.
 
Nashindwa kuelewa jinsi viongozi wetu wanavyozungumzia kuiingiza nchi vitani kwa mbwembwe kipichi ambacho tukishuhudia kuwa suluhu ya migogoro sio vita bali majabiliano, nashindwa kuelewa kwani ni tuanze kufikiria vita na kuanza kujivunia uwezo tulionao katika vita badala ya kuweka nguvu katika majadiliano ya kutafuta suluhu ya mgogoro wa mpaka wa ziwa nyasa au malawi kama wente kuugombea wanavyota uitwe.

Tena najiula hawa viongozi wetu wametokea wapi kuja kujadili mambo ya vita wakati huu ambao tunaishudia nchi na dunia kwa ujumla vikiwa kwenye migogoro mikubwa ya kiuchumi. swali lingine linanijia kichwani kujiuliza hivi hizi garama za vita wakati ambapo tunashudia hata hospitali zetu zikiingia kwenye mgogoro na wahudumu wa sekta ya afya wakidai kuwa bhospitali hazina vifaa vya kuwahudumia wananchi kwenye sekta ya afya, Je majeruhi wa vita kati malawi na tanzania watatibiwa katika hospitali gani?.

hapo nipo ninapohisi kuwa serekali haiko makini juu ya hili, ingekuwa serekali iko makini juu ya hili basi kujitapa huko kuwa wako tayari kuingia vitani kungeanzia na huku kwenye vita juu huduma duni ya afya nchini ikiwemo ukosefu wa vifaa tiba na maslahi ya watendaji, mishahara ya wafanyakazi, vita dhini ya rushwa na ufisadi uliokidhiri katika nchi hii.

Baada ya serekali kukamilisha haya basi wanachi tungetoa baraka zetu kwa serekali kuingia vitani na malawi bila kuruhusu na kusisitiza juu ya kutoa fusra kwa majadiliano katika kutafuta suluhu ya mgogoro wa mpaka kati yake na malawi. Tena kwanini hili limekuja wakati huu inawezekana kuna kitu kinaendelea hapa duniani na miongoni mwavyo ni kutolewa kwa taarifa za uwezekano wa kuwepo mafuta katika ziwa hili.

serekali za Malawi na Tanzania lazima ziwe makini san juu ya hili isijekuwa kuna majinchi makubwa yanatusukuma sisi tuingie vitani ili wakati sisi tukizichapa wawo watoe sila watugawie huku wakichota rasilimali zetu na baada ya vita wakituacha tukinuka kwa madeni na hali mbaya ya kiuchumi, ukosefu wa chakula huku tukibakiwa na maandaki makubwa waliyochimba madini, mafuta, gasi na urani,
Tanzania duniani imekuwa ikisifika kwa amani na upatanishi wa nchi nyingi katika ulimwengu huu , hata Mwalimu aliwahi kuongoza tume za kutafuta ususluhishi katika nchi nyingi duniani, kipindi cha Karibuni tulishuhudi Kikwete akisaidia kwa karibu kupatikana kwa mwafaka katika taifa la karibu nasi hapahapa A.

Mashariki la Kenya na Dunia nzima walihsngaa maana Kikwete kaingia tu na mwafaka hapo hapo wakamuuliza alitumia mbinu gani? Hatimaye sasa baada ya kuwa marefarii kwa muda mrefu sasa ni zamu yetu kucheza sijui nani anatupulizia kipenga
 
Ikibidi kuwachapa hao wapori pori inabidi wachapwe. Vita si ya kufurahia ila kama haki ni yetu lazima tuipiganie.
 
Mkuu ni vyema kuweka msimamo wako dhahiri ili uende kwenye meza ya mazungumzo ukiwa na msimamo huo.....Fanya yote usichezee mipaka ya nchi.

Mkuu nimekuelewa kuweka msimamo ni sawa lakini hali ilivyo sasa amebakia JK kuamuru Jeshi lianze kazi. Hapo hakuna tena mazungumzo. Maana Malawi wametuchokoza. Tuna moja kati ya mbili, nguvu ya kuwafukuza kwa mabomu au kuwashitaki mahakamani. Sisi naona tunaamua nguvu kuliko mwafaka kwanza.
 
Ni vizuri wale wa maneno matupu wakaelewa hivyo.
Mwalimu alikuwa categorically straight kwenye issues kama hizi
...sababu ya kumpiga tunayo..
...uwezo wa kumpiga tunao...
...nia ya kumpiga tunayo..
...tutampiga mshenzi huyu...

Ni bahati kuwa sababu zote za kuingia vitani hazijatimia, lakini the nation should wlk along this mood, na ndio maana Lowassa is right on this issue.

Well said mkuu
 
Anachoongea Lowassa ni sawa kabisa ila tujitahidi sana kwanza njia za kidiplomasia kwani tukumbuke vita vya Uganda vilitugharimu kiuchumi na uchumi wenyewe huu ulioshikiliwa na mafisadi tuangalie sana isije ikatugharimu mpaka kizazi cha wajukuu zetu
 
Mungu ibariki tanzania yetu. ee Mungu tuepushe na hichi kikombe tusikinywe kwani madhara si mazuri hata tukishinda, ila kama ni mapenzi yako tukinywe, mapenzi yako yatimie katika jina la Yesu mwanao aliye hai. Amen.
 
Maneno mazuri lkn tuhakikishe njia za kidiplomasia zimeshindikana kabisa tukumbuke ita vya Uganda ambavyo mimi nijuavyo havikuwa vya lazima lkn vimetugharimu kiuchumi mpaka leo sasa angalia tz ya leo uchumi ulioshikiliwa na mafisadi
 
Haya ndio maneno aliyoshindwa kusema MEMBE juzi Bungeni. Sielewi nani alimwambia Membe awaite wa Malawi ''WENZETU'' wakati wao wanajiandaa kutupiga kivita.

Tangu lini adui akawa mwenzako?

mwenzie Lowassa amesoma mood ya nchi na ameamua ku grab the headlines vilivyo

so far as far as national security is concerned: LOWASSA 1 MEMBE 0

game inaendelea

Hii ni kauli ya mtu anayetaka kubaki kuwa relevant politically bila kupima ramifications. Top diplomat hakurupuki na ku-spit fire hata pale pasipostahili na wala nchi haijawa katika hali hiyo ya kuingia vitani wakati huu ambapo mazungumzo yanaendelea. Hata siku moja tamko la vita halitolewi na bunge, wala na mwenyekiti wa kamati ambaye kazi yake ni kushauri na hapa ndipo Lowassa na wafuasi wao wanaposhindwa kuelewa majukumu hasa ya Kamati. Kamwe yeye si waziri kivuli au waziri mbadala (japo angependa iwe hivyo). Uwezo wa kivita haupimwi na utayari wa jeshi lako kwa kupewa taarifa na majenerali bila kujua nguvu za adui.

Mimi nafikiri Membe alikuwa ana-respond kwa swali aliloulizwa na kulikuwa hakuna haja ya ku-spit fire. Ilitosha kutoa onyo na in any case, onyo sahihi na lenye effect ni lile linalotolewa kwa Serikali husika through diplomatic channels, siyo kwenye podium ya bunge au ukumbi wa Msekwa baada ya kuwakusanya waandishi wa habari. If he thought he was going to steal the show, he has unexepectedly exposed his immaturity and lack of diplomatic prowess in dealing with a neighbour. Vita huwa ni mambo ya last resort tena kwenye nchi kama yetu yenye changamoto nyingi za kiuchumi na kijamii.
 
Sitta aliongea kwa niaba ya Pinda....... na Lowassa ameongea kwa niaba ya J.K...........spati picha jins PINDA atakavyolia vita vikianza,mwoga huyu balaa
 
kitalolo,

Wengi wanaoshabikia kauli ya kichochezi ya Lowassa ni wale ambao wamezaliwa katika miongo mitatu hii na ambao hawajui ni kwa kiasi gani vita hugharimu. Hawakumbuki miaka 18 ya kujifunga mikanda, hatimaye ikageuka kuwa miongo 18. Lowassa atafute mtaji mwingine wa kisiasa, hili litamalizwa kwa diplomasia mahiri tuliyonayo.
 
Last edited by a moderator:
....Hizi ndio kauli za Kishujaa.... Siyo kama za MH. MEMBE na kulalamika eti' bajeti yangu HAITOSHELEZI...

.....JWTZ wote wapokwenye Morale ya KUKIAMSHA muda wowote...

Ikiwezekana Wananchi wote wa Lake NYASA wavalishwe KOMBATI na WAANZISHIWE Mazoezi mepesi mepesi kujiandaa kwa MAPAMBANO.. Viva Lowassa.

via M4C...
 
Wengi wanaoshabikia kauli ya kichochezi ya Lowassa ni wale ambao wamezaliwa katika miongo mitatu hii na ambao hawajui ni kwa kiasi gani vita hugharimu. Hawakumbuki miaka 18 ya kujifunga mikanda, hatimaye ikageuka kuwa miongo 18. Lowassa atafute mtaji mwingine wa kisiasa, hili litamalizwa kwa diplomasia mahiri tuliyonayo.

....Jaribu kuwa MZALENDO kwa kulitetea TAIFA lako kwa Njia zozote iwe kwa Diplomasia iwe VITA, yote JIANDAE NAYO...

Sio Unalaumu laumu kama Si MTANZANIA vile.

Hapo hakiangaliwi CHAMA, Dhehebu, Kabila, Rangi ,.. HAPA NI KUITETEA TANZANIA NA MIPAKA YAKE....

via M4C
 
Back
Top Bottom