Lowassa na siasa za makanisani?

Mim ni mkatoriki lakin siungi mkono Lowasa kualikwa kwenye hiyo harambee! Hovyo kabisa hizi dini za siku hizi hakuna kitu,wanawaza hela tu!

Kanisa Katoliki sio dini za siku hizi. Ooopps kwanza umesema wewe ni mkatoriki hiyo ndio itakua ya siku hizi.
 
Mim ni mkatoriki lakin siungi mkono Lowasa kualikwa kwenye hiyo harambee! Hovyo kabisa hizi dini za siku hizi hakuna kitu,wanawaza hela tu!

Kanisa Katoliki sio dini ya siku Hizi ni Kanisa la kwanza duniani. Ok wewe umesema ni Mkatoriki hiyo ndio itakua dini ya siku hizi.
 
Hekalu langu limekuwa pango la wanyang'anyi...mie ni muumini wa katoliki ila kwa hili mauti yataliandama kanisa hili,tunajenga ama tunabomoa?
 
Mimi ni mkatoliki na ninajua kuwa Lowasa hajawahi kualikwa kwenye dhifa za namna hii kwenye majimbo mengi. Niambieni ni lini mliwahi kusikia kuwa Lowasa amealikwa kwenye kuongoza dhifa ya Kanisa Katoliki kama ambavyo ameitwa huko Mwanza. D'Salaam ndiyo makazi ya Lowasa. Mke wake Regina si tu ni mkatoliki mwenzetu bali ni mshiriki mkuu wa mambo ya Kanisa na hadi ametunga kitabu kuhusu ziara yao kule Israel. Lakini jiulizeni kwamba ni lini Edward Lowasa binafsi alipewa nafasi jimboni D'Salaam kama anayopewa huko Mwanza?

Kanisa Katoliki limekuwa ni linaongozakatika kuupinga ufisadi. Askofu wa Jude Thaddaeus wa Dodoma alitoa pongezi kwa wanasiasa walioufichua ufisadi. Askofu huyo alitoa pongezi hizo siku ya kumsimika Askofu Msonganzila kama askofu mpya wa Musoma. Kumbuka ilikuwa ni miezi mitatu baada ya Dr. Slaa kutamka list ya mafisadi na vilevile mwezi mmoja kabla Lowasa hajajiuzulu mwenyewe kwa kushindwa kujitete bungeni kwa tuhuma za ufisadi wa RICHMOND zilizotafitiwa na timu ya Dr. Mwakyembe.

Wakati askofu Jude Thadaesu anatoa pongezi kwa kina Slaa alikuwa askofu wa Dodoma lakini alisoma pongezi zile kama rais wa Baraza la Maaskofu wa Tanzania. Leo, askofu Jude Thaddeus hayuko Dodoma bali sasa yuko Mwanza! Bado ni rasi wa Baraza la Maaskofu!
Halafu hukohuko Mwanza ndiko Lowasa ameanza kuonyesha anakubalika ndani ya Kanisa Katoliki!

Hapa tunahitaji umakini wa hali ya juu. Kwanza nina wasiwasi kama askofu amejulishwa mapema kuhusu uchangiaji huo. Wenye kujua namba za Jimbo Kuu la Mwanza bado siku ya kesho inaweza kutumika kuulizia ofisini kwake kama kweli anajua.

Lowasa hajathibitika kuwa ni fisadi. Lakini hajawahi kukanusha kutohusika na RICHMOND inayotutesa hadi kesho. Kwa nini aliitupilia mbali nafasi ya kujitetea bungeni ambapo ilikuwa ni nafasi ya nzuri ya kujisafisha mbele ya umma kuliko kutumia njia zingine.

Kanisa Katoliki limepinga sana ufisadi. Kama mafisadi hawajaakmatwa na bado kuna wale wanatuhumiwa kwa ukaribu, leo Kanisa linaenda kujiweka karibu nao. Ukweli ni kwamba Kanisa Katoliki linajiweka katika mahala pagumu kwenye vita hii y ufisadi. Lisijilaumu pale litakapoanza kuulizwa "mbona watuhumiwa mnawaalika wanapowachangia hizo pesa zao".

Ninalifahamu hili kanisa langu kuhusu mambo ya ushoga (homosexuality). Ni moja ya maknisa machache kama si pekee ambalo linapinga kwa ukali suala la ushoga. Ninalipongeza liendelee hivyo. Lakini kama linapinga ushoga na hajakamatwa mtuhumiwa wa ushoga basi ina maana kuwa kuwa mtuhumiwa wa ushoga hakumfany mtuhumiwa asikubaliwa na kanisa kuongoza harambee.

Hivyo, Tanzania kuna watuhumiwa wengi tu wa ushoga. Baadhi yao ni matajiri. Maadam hawajatiwa hatiani basi tutarajie nao siku moja tusikie wakiitwa kwenye Parokia mojawapo ili kuongoza harambee! Tusilalamike ikifika huko.

Kanisa lingejifunza kupitia kwenye scandal ya Freemasons. Kitendo cha jamaa wa freemasons kuwa karibu na viongozi wa kanisa katoliki kunalitesa na hadi kuna watu wengi tu wanaamini kuna uhusiano mkubwa wa Freemasons na Ukatoliki.

Haijapita miaka miwili wenzetu nadhani walutheri walikataa hela ya Rostam Azizi. Naikumbuka issue ile ambapo ilibidi viongozi wa Kanisa waingilie kati na kusema Rostam alialikwa na kikundi cha kwaya na si viongozi wa Kanisa. Kama sikosei ilibidi kile kikundi kirudishe hela zile kwa Rostam na kuomba samahanani.

Je, haya si mazingira yaleyale kama ya case ya Rostam na walutheri wale. Nimelisoma gazeti na mleta mada hajakosea hata nukta. Lakini kama mmesoma vizuri hakuna palipoandikwa kwamba Paroko amemualika Lowasa. Kwa mazingira yaleyale yaaliyopita kwa Rostam, basi inawezekana huyu mwenyekiti wa Parokia ambaye ni mlei ameandaa jambo zima na labda Paroko au padri wa pale ameshirikishwa mwishoni sana.

Kama Paroko hana taarfia basi hata askofu Jude Thadeus wa jimbo hilo inawezekana habari hii ndiyo inamtaarifu.

Habari inaeleza kuwa Lowasa anaushawishi ndicho kigezo cha kumualika hapo parokiani. Hivi lina ukweli hili? Kama ni hivyo mbona hamjasikia Kanisa Katoliki likimualika Reginald Mengi. Ukweli nikwamba kama ninavyoshangaa Lowasa kualikwa nitashangaa kusikia Kanisa Katoliki kumualika Mengi tangu siku Mengi alipotamka kwamba viongozi wa dini wahimize uvaaji wa Condom.

Hayo ndiyo yangu.
 
Sidhani kama kuna ukweli ktk hili. na kama likitokea kuwa kweli nadhani kanisa litakuwa limekwisha kabisa. Yaani sipati picha na sina uhakika kama hizi taarifa zimemfikia Pengo na maaskofu wengine wa kanisa langu hili zuri, mweeeeeee! Lowassa kuchangia kanisa katoliki,oooopssssssss! an abomination of the century, pheeeeeeeeeeeeeeeew! Tusubiri tuone kama ni kweli!
 
********************* Source: TANZANIA DAIMA Date=TODAY Page. 06 ********************* Waziri Mkuu mstaafu, Edward Lowassa, anatarajiwa kuongoza harambee ya kuchangisha zaidi ya shs. millioni 150 katika Kanisa Katoliki, Parokia ya Nyakato, Jimbo Kuu la Mwanza. -Akizungumza na Tanzania Daima jana ofisini kwake, Mwenyekiti wa Kamati ya ujenzi wa Kanisa hilo, Pastory Masota, alisema harambee hiyo itafanyika Jumapili wiki hii. -"Tumemwalika Lowassa kufanikisha harambee yetu, maana ni mtu mwenye mahusiano mazuri na jamii yote. Harambee itakuwa Jumapili wiki hii pale kanisani Nyakato National". "Ukitaka kufanikisha jambo lazima utafute mtu anayependa ushirikiano na maendeleo kwa ujumla. Lowasa amekubali mwaliko wetu na atakuja" alisema Masota. Alisema kuwa kanisa hilo lina uwezo wa kuchukua waumini 1,350 kwa wakati mmoja. Masota alisema harambee itatanguliwa na misa takatifu kuanzia saa 04:30 hadi saa 05:00 asubuhi, na wageni mbalimbali wa Serikali wamealikwa kutoka mikoa yote ya kanda ya Ziwa, Arusha na D’Salaam. Alisema anaamini siku hiyo kanisa litafanikiwa kutokana na ushawishi unaokubalika wa kiongozi huyo. Hadi sasa kanisa hilo limetumia zaidi ya shs. Million 170 na kwamba harambee hiyo itafanikisha kukamilisha ujenzi wa kanisa hilo ambalo ni la kwanza kwa ukubwa kujengwa bila bila ufadhili toka nje ya nchi.
...Mkono mtupu, haulambwi.

...Mwenyekiti yuko sahihi.
 
Jitahidini kuwaelewa wakatoliki na falsafa za dini hasa wakristo juu ya wadhambi,hata yesu aliwahi kusema ya kwamba hakuja kwa watu wema bali wadhambi,kumbukeni falsafa ya dini na ya siasa zina tofauti kubwa.dini inawataka wadhambi ili iwatoe huko kwenye dhambi lakini ukweli wa siasa ni kuwakana wadhambi japo mambo ni tofauti kidogo kwa chama cha magamba CCM.Japo sina hakika na lengo hasa la kuitwa kwa Lowasa huko MWZ tukiachilia mbali kumchuna fedha ambazo zimetokana na kuwaibia wananchi wa TZ, sijapata picha halisi na wala mantiki ya kumwalika Lowasa,binafi sina haja hat ya shilingi kumi yake kutokana na yale aliyoyafanya ndani ya TZ
 
Sidhani kama kuna ukweli ktk hili. na kama likitokea kuwa kweli nadhani kanisa litakuwa limekwisha kabisa. Yaani sipati picha na sina uhakika kama hizi taarifa zimemfikia Pengo na maaskofu wengine wa kanisa langu hili zuri, mweeeeeee! Lowassa kuchangia kanisa katoliki,oooopssssssss! an abomination of the century, pheeeeeeeeeeeeeeeew! Tusubiri tuone kama ni kweli!

Ndiyo maana nimesema kwamba binafsi sijawahi kusikia Edward Lowasa akialikwa kuongoza harambee kwenye jimbo la D'Salaam ambalo ni la Pengo. Kama wapenzi wa Lowasa wamefanikisha move hii basi kigezo kitakuwa kwamba Rais wa Baraza la Maaskofu ambaye ni askofu wa Mwanza amemkubali Lowasa.

Unadhani ikitoka picha hiyo, tutasema nini? Wana akili sana watu wa Lowasa katika kutafuta kukubalika kwenye jamii.
 
Sioni ubaya wowote hapo.

Unaweza ukaliona katika mtazamo huo, ila mimi nadhani kwa jinsi huyu Bw. Lowassa alivyotokatoka ktk utumishi wa Umma, Mwenyekiti wa Parokia hawezi kusema huyu Bw. Lowassa ana mahusiano mazuri na jamii au jamii inamkubali, jamii gani anayoizungumzia huyu Mwenyekiti???Jamii hii ni ya sisi Watanzania tulioingizwa mjini na Lowassa na Kundi lake la Wahuni?? Mi nadhani aseme yeye kwa ajili ya tamaa zake za hela ameamua kumualika huyo bwana kwakuwa anafahamiana kwa ukaribu na mafisadi hivyo mafisadi wengi watakuja kutoa fedha haramu hapo kanisani. Under normal circumstance Padri anadhani wachangiaji watatoka wapi kama wana nyakato wameshindwa???Mwenyekiti kapima kaona wananyakato hawana hela hivyo kaamua kusaka hata Fedha haramu ili mradi kanisa lijengwe.

Kanisa litakufa kwa sababu ya tamaa zake za pesa. sasa hivi kama huna pesa huwezi kuwa kiongozi wa kanisa na wala hutothaminiwa. Wenzetu ulaya kanisani hawaendi kwa wingi kama Africa, nadhan walishaona jinsi kanisa linavyopotoka. Kanisa endeleeni kutamani fedha haramu halafu muone mtapoishia. Mungu pia alikataa Sadaka ya Cain kwani alikuwa mchakachuaji. Au katika hili mlilolifanya, Biblia zenu hazina huo mstari wa Cain na Abel???? Kama kanisa mnatamaa hivi, mtashindwa kukemea wafanya maovu.Na ndivyo hali ilivyo hivi sasa. Au mwenyekiti na wewe na Fisadi??

Yupo wapi Mtikila. alikuwa anabweka sana na ufisadi, Rostam akatoa ushahid kuwa Mtikila alimfwata akamkopa hela. Hadi leo Mtikila analiapproach suala la ufisadi kwa aibu sana. Kanisa acheni njaa na tamaa za kipumbavu.
 
Hizi dini ni unafiki tu siku hizi ndio maana waumini wanapungua kila siku kwa mambo kama haya.
 
Hekalu langu limekuwa pango la wanyang'anyi...mie ni muumini wa katoliki ila kwa hili mauti yataliandama kanisa hili,tunajenga ama tunabomoa?
Hii ni dalili kuwa kanisa limeanza kuongozwa na wahuni, wenye uchu wa pesa haramu.
 
Kama swala la ufisadi wa Richmond ndo kikwazo kwa Lowasa kualikwa kweye shughuli za kijamii likiwemo hilo la la kuchangia ujenzi wa "Jengo la Kanisa" basi itabidi Kikwete asialikwe kwenye shughuli yoyote ya kijamii!kwa kutenda haki huwezi kumtenganisha Kikwete na Richmond kama vile ambavyo huwezi kumtenganisha na ufisadi mwingine wowote mkubwa nchini!
Simtetei Lowasa ila sioni pia kama ni haki kumvalisha kitanzi peke yake! Nawasilisha!
 
The job that he does best...why don't we make fund raising his permanent job?
 
Hii ni dalili kuwa kanisa limeanza kuongozwa na wahuni, wenye uchu wa pesa haramu.

Harambee si sehemu ya misingi ya imani ya kikatoliki, kwa hiyo kilichofanywa huko mwanza ni njaa za watu wachache wanaotumia kanisa kujifaidisha.
 
Mim ni mkatoriki lakin siungi mkono Lowasa kualikwa kwenye hiyo harambee! Hovyo kabisa hizi dini za siku hizi hakuna kitu,wanawaza hela tu!

Tatizo lakujifanya mkatoliki kuliko papa ndio hilo!
Usichanganye dini na siasa,huenda wewe ni mkatokaliki kwa ubatizo after then zero thts why unaongea upupu!
Sasa katiba ya dhehebu lako bible hem reffer kifungu chochote cha bible kutetea hoja yako yakupinga hilo,tena si a ajabu ukitafakari matendo yako hata roho yako inaweza kusuta!
 
Asiye na dhambi na awe wa kwanza kumrushia jiwe.

Mkuu hata mimi nimeanza kuamini huyu mzee amekua anabebeshwa lawama nyingi lakini simbaya hivyo kama hawa ambao wako radhi kutumia nguvu ya dola kutuua,kututia vilema na kutufanyia madhila yoyote ilimradi waendelee kubakia madarakani!
 
acheni kupotosha, hamjui maandiko? yesu alikula na wenye dhambi na alisema
amekuja ulimwenguni kwa ajili ya wenye dhambi wapate kuokoka kwa neno lake.
mnakumbuka historia ya zakayo? Paulo alikuwa mpinga kristo na kanisa sasa ni mwl
wa kanisa Yesu mwenyewe alimtuma kuhubiri neno lake,
Tujiulize kwa nn alipenda kushiriki na wenye dhambi na sii mafarisayo wanafiki?
kwann alichagua mitume wenye dhambi kama Mathayo aliekuwa mtoza ushuru kazi iliolaaniwa
na jamii yote lkn yesu alimpenda na leo hii twasoma injili za mathayo.mifano ni mingi.

kwa lowasa mmejuaje kama ni mpango wa Mungu wa kumtakasa
msije mkashangaa akakiri madhambi yake na akaja kuwa msaada mkubwa
ktk harakati zetu za kudai taifa jipya,Tanzania mpya na uchumi mpya.
Kanisa kama Yesu halijaangalia makosa yake kumwaalika bali limeangalia heshima yake
kama kiongozi alietambuliwa. Huenda j2 ikawa siku nzuri kwa wanaharakati na akatangaza mageuzi mapya.
lets pray for that. Tujiulize kwa nn basi KKKT hawajamtenga kama ana dhambi ina maana wao hawamwoni?
Msimhukumu sana kana kwamba sisi hatuna dhambi,wengi wetu wazinzi,wezi wa wake za watu,
wezi wa rasilimali maofisini,walaghai,nk nk kweli asie na dhambi na awe wa kwanza kumrushia Lowasa jiwe.kama yupo hapa aseme......
 
Nguvu zimeniishia kabisa kumpinga Lowassa,kama amekubalika na wakatoliki huyo ndio ris wetu jamani,tepende tusipende,wengi tegemeo letu lilikua ni kanisa katoliki kutokana na msimamo wake na huwa haliingiliki kirahisi kama masheikh wetu wa bakwata,sasa kama bwana Ngonyani Lowassa kafanikiwa kuingia madhabauni basi tupende tusipende huyo ndio rais wetu!!!!!!nasikitika sana lakini hakuna la kufanya!najiandaa tu na mimi kuanzisha gazeti langu kwa ajili ya kuigonga serikali yake,gazeti nitaliita "POLITICO" mniunge mkono sasa na nyie,maana litakua kama jamii forum ilivyo,yeyote ataruhusiwa kuweka habari yake mradi iwe toka chanzo cha uhakika!sitakua kama kubenea na mwanahalisi lake!
 
Back
Top Bottom