Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,812
11,989
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akishiriki Mkutano Maalum wa Baraza la Vyama va Siasa na Wadau wa Demokrasia katika ukumbi wa JNICC leo tarehe 11 Septemba, 2023 katika viwanja vya Ikulu, jijini Dares Salaam.


Kituo cha TCD kinafanya kazi vizuri tangu Rais Samia aingie madarakani, na ndie amekipa uhai. TCD ilifanya mkutano na wadau kujadili hali ya demokrasia kuelekea chaguzi za 2024 na 2025, baada ya kujadili kuna mambo tulifanyia maazimio na tutayaleta hapa.

Kuhusu Katiba, mchakato wa kupata katiba mpya uweze kuendelea, lakini kwa muda uliopo huenda tunaweza tusipate Katiba Mpya. Lakini mabadiliko ya katiba yanaweza kufanyika ikiwemo kufanya mabadiliko kifungu cha 74 cha Katiba ili tume huru iweze kusimamia uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024 na Uchaguzi Mkuu 2025.

Pawepo mgombea binafsi, kufanyia marekebisho kifungu cha 39 (2) cha katiba ya sasa kuhusu Rais na kifungu cha 67(1) kuhusu wagombea ubunge. Kuwa Rais atangazwe akishinda kwa zaidi ya 50% ya kura kwa hiyo kurekebisha kifungu cha 41 (6) na uchaguzi wa Rais uweze kuhojiwa mahakamani hivyo kubadilisha kifungu cha 41 (7).

JENISTA MHAGAMA, WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU (SERA, BUNGE NA URATIBU)
Amemshukuru Rais Samia kwa kukubali kuwa mgeni rasmi kwenye mkutano huu.

Kwenye siku tatu za Mkutano huu, wajumbe watashiriki kujadiliana ni namna gani taifa letu litaimarisha na kuboresha demokrasia hapa nchini.

Pia, tathimini ya maoendekezo ya kikosi kazi yatajadiliwa kwenye mkutano huu.

Rais Samia amedhihirisha kuwa ni kiongozi anayezingatia utawala bora na kutenda haki kwa watanzania wote.

SAMIA SULUHU HASSAN, RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
Leo tunapokutana na kuzungumza mapendekezo ya kikosi kazi ni mapendekezo ambayo wote wadau wa siasa nchini wameyaleta kwa pamoja.

Tutapishana tu kwa jinsi ya kusukuma utekelezaji, huyu anataka kalileta leo lifanywe kesho, mwingine ana subira kidogo, lakini wote maono yetu ni kama yanaenda pamoja.

Tayari Serikali imeanza kuchukua hatua ya baadhi ya mapendekezo ya kikosi kazi na mnayajua, kwa mfano kuruhusu Mikutano ya hadhara, tayari imeruhusiwa watu wanakwenda na tunawasikia yanayosemwa huko.

Lakini pia tulishauriwa kuunda kanuni za kuendesha hiyo mikutano ya hadhara, zimeundwa na zinatekelezwa, hilo limeshafanyika.

Lakini pia kuna jambo mahsusi ambalo ndio kila mtu analisubiri la katiba, marekebisho ya katiba yetu ambalo nalenyewe limeanza kufanyiwa kazi na pengine mkutano huu ni kuelekea huko pia.

La mikutano ya hadhara, tumeruhusu tukiwa na nia ya vyama vya siasa vizungumze wananchi wasikie sera zao, mada zao, mipango yao ili vyama vikue na virudishe watu wale walio wapoteza, vyama visimame, viwe madhubuti, tukienda kwenye uchaguzi kila chama kimejijenga vya kutosha na ndio maana ya kutoa fursa hii ya mikutano ya hadhara.

Hatukutoa fursa ile watu wakavunje sheria, watu wakasimame kutukana, watu wakasimame kukashfu, watu wakasimame kuchambua dini za watu. Lakini sishangai kwanini haya yanatokea, kwa sababu ya kuzungumzwa hakuna.

Tulianza na katiba, tukaenda ikakatika katikati, bandari imeenda sasa katiba tena. Tumieni hiyo fursa kajijengeni kwa wananchi, elezeni sera zenu, mtafanya nini, ili wananchi warudi wawaunge mkono ili tukienda kwenye uchaguzi vyama vyote vimejijenga vizuri.

Uendeshaji wa Tanzania unahitaji fikra za kila mtu, hakuna mtu mwenye hati ya kuimiliki, hata kitoto kilichozaliwa yeye kina haki, ili tuendeshe vizuri kila kundi litoe mawazo tuendeshe nchi yetu.

Niseme tena, fursa hii iliyotoka isiende kuharibu neema na baraka aliyotupa Mungu. Isiende kuharibu misingi ya uendeshaji nchi hii wazee wetu waliyotuachia.

Lingine, hakuna aliye juu ya sheria. Kila anayefanya makosa sheria itamshika. Kama umekiuka sheria, sheria itakushika. Ajenda yetu kubwa kama watanzania ni kudumisha amani, umoja na mshikamano wa kitaifa.

Tulitoa uhuru wa maoni, maoni mengi sana yanatoka kwa watanzania, tunayaona, mazuri tunayachukua na mengine unayapima maoni yao. Nina kikundi maalumu kinachoangalia maoni yote maoni na kuchukua yale mazuri na kuyaweka kwenye mipango yetu kuyafanyia kazi.

Kuna uhuru wa maoni lakini huu uhuru wa maoni una mipaka yake, sio tu kisheria, hata kibinadamu.

MAPENDEKEZO: PROF. MUKANDALA, MWENYEKITI WA KIKOSI KAZI

Hapa ninawasilisjha mapendekezo tu. Na ninayawasilisha kama yalivyopitishwa na kikosi kazi. Sitabadilisha chochote, nitayafikisha kama yalivyokubaliwa na kikosi kazi.

Kuhusu mikutano ya vyama vya siasa, Kikosi Kazi kilipendekeza kuwa:
a) Kikosi kazi kilipendekeza kuwa mikutano ya hadhara ya vyama vya siasa iruhusiwe kufanyika kwa mujibu wa katiba na sharia.

b) Mikutano ya ndani ya vyama vya siasa iendelee kufanyika bila vikwazo vyovyote.

c) Yafanyike mabadiliko ya sheria ili kuhakikisha nmikutano ya hadhara inafanyika kwa ufanisi. Sheria hizo ni pamoja na Sheria ya Vyama vya Siasa, sura ya 258; Sheria ya Jeshi la Polisi

Kuhusu Demokrasia ndani ya Vyama vya Siasa, Kikosi Kazi kilipendekeza kuwa:
a) Sheria ya Vyama vya Siasa ifanyiwe marekebisho ili kulipatia Baraza la Vyama vya Siasa, linaloundwa na vyama vyenyewe mamlaka ya kulishulikia suala la uvunjifu wa maadili ndani ya vyama vya siasa kupitia Kamati yake ya Maadili – yaani vyama vyenyewe vijisimamie.

b) Msajili wa Vyama vya Siasa aandae Mwongozo wa Uchaguzi wa ndani ya Vyama vya Siasa

c) Kuwe na Masharti kwamba idadi ya jinsi moja katika vyombo vya maamuzi ya chama cha siasa isipungue asilimia 40

d) Kukitaka kila chama cha siasa kuwa na Sera ya ushirikishwaji wa watu wenye ulemavu katika shughuli za chama husika

Kuhusu Ruzuku kwa Vyama vya Siasa inayotolewa na Serikali, Kikosi Kazi kilipendekeza kuwa:
a) Mfumo wa sasa wa kugawa Ruzuku ya Serikali kwa vyama vya siasa uendelee, isipokuwa asilimia 10 ya fedha za ruzuku kwa vyama vya siasa zinazotengwa katika bajeti ya serikali yam waka wa fedha husika,igawiwe sawa kwa vyama vyote vya siasa vyenye usajili kamili kwa vigezo vifuatavyo:

1. Chama kiwe na usajili kamili
2. Chama kiwe kimefanyiwa uhakiki na Msajili wa Vyama vya Siasa na kutibitishwa kwamba vinakidhi vigezo vya usajili kamili
3. Chama kiwe kimeshiriki Uchaguzi Mkuu angalau mara mbili tangu kupata usajili kamili
4. Katika mwaka wa fedha ulipita, chama husika kisiwe kimepata hati chafu ya mahesabu toka kwa CAG
5. Ruzuku itumike kuendesha ofisi za makao makuu, ofisi ndogo au ofisi kuu ya makao makuu ya chama cha siasa husika

b) Sheria ya vyama vya siasa itamke kuwa asilimia 20 fedha ya ruzuku inayotolewa na serikali katika mwaka wa fedha, igawiwe kwa vyama vya siasa vyenye madiwani wa kuchaguliwa katika kata kwa mijibu wa uwiano wa idadi ya madiwani hao ambao kila chama kinao, kwani kwa sasa sharia haijatamka kiwango chochote, bali imempa mamlaka waziri mwenye dhamana kuamua.

SerikalI iongeze fedha za bajeti ya ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa kwa ajili ya uendeshaji wa shughuli za Baraza la Vyama vya Siasa ili liweze kutekeleza majukumu yake ipasavyo, ikiwemo jukumu linalopendekezwa la kusimamia maadili ya vyama vya siasa.

Kuhusu Uhuru wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Kikosi Kazi kimependekeza kuwa:
a) Tume ya Taifa ya Uchaguzi isilazimike kufuata amri ya mtu yoyote, idara yoyote ya serikali, maoni yoyote ya chama cha siasa, taasisi, au asasi yoyote.

b) Utendaji wa Tume ya Uchaguzi uruhusiwe kuhojiwa kwenye mahakama ya juu pale itakapoanzishwa ili kuongeza uwajibikaji
  • Kuhusu uteuzi wa wajumbe wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Kikosi Kazi kilipendekeza kuwa utaratibu ufuatao utumike kuwapata wajumbe wa Tume hiyo:
  • Kuwe na kamati ya Uteuzi ya Wajumbe wa Tume itakayokuwa na wajumbe wafuatao:
  • Jaji Mkuu JMT – Mwenyekiti
  • Jaji Mkuu Z’bar – M/Mwenyekiti
  • Kamishna wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma - Tz Bara
  • Mwenyekiti wa Tume ya Maadili ya Viongozi wa Umma – Z’bar
  • Mwenyekiti wa Tume za Haki za Binadamu
  • Wajumbe wawili watakaoteuliwa na Jaji Mkuu wa JMT baada ya kupendekezwa na TLS na Chama cha Wanasheria Z’bar
c) Sifa za mtu kuwa Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti na Mjumbe wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi ziainishwe

d) Nafasi ya Mjumbe wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi itangazwe na Mtanzania yeyote mwenye sifa aruhusiwe kuwasilisha maombi kwa kamati ya uteuzi ya kuwa mjumbe wa Tume.

e) Kamati ya Uteuzi ifanye usaili ya watu waliowasilisha maombi ya kuwa wajumbe wa Tume ya Taidfa ya Uchaguzi na kupendekeza kwa Rais majina ya watu wanaostahili kuteuliwa kuwa wajumbe wa tume

f) Kamati ya Uteuzi itawasilisha kwa Rais majina manne zaidi ya idadi ya nafasi zilizohitajika kujazwa

g) Rais ateue wajumbe wa tume miongoni mwa majina yaliyowasilishwa kwake na kamati ya uteuzi

Mapendekezo haya unaweza kuyasoma zaidi hapa: Mapendekezo 19 ya Kikosi Kazi cha Rais Samia kuhusu uendeshaji Siasa nchini

UTEKELEZAJI: DKT. JIM JAMES YONAZI - KATIBU MKUU, OFISI YA WAZIRI MKUU (SERA, BUNGE NA URATIBU)

Serikali imemaliza uchambuzi wa mapendekezo yote ya kikosi kazi na yote yameanza kufanyiwa kazi na serikali.

Utekelezaji umegawanyika katika maeneo matatu:
  • Yale yanayogusa moja kwa moja katiba iliyopo
  • Yale yanayohusu na kuhitaji utungaji wa sheria mpya, au marekebisho ya sharia zilizopo au kutungwa na kurekebisha kanuni
  • Yale yanayohusu hatua za kiutawala ambazo haziusishi masuala ya kikatiba na kisheria
Kuhusu mikutano ya hadhara na mikutano ya vyama vya siasa, Kikosi kazi kilipendekeza mikutano hiyo iruhusiwe kufanyika na mikutano ya ndani iendelee kufanyika bila vikwazo vyovyote

Pendekezo hili limefanyiwa kazi na utekelezaji wake unaendelea. Aidha, ili kuhakikisha mikutano ya hadhara inafanyika kwa ufanisi, serikali ilishatunga kanuni za kuratibu mikutano ya hadhara ya vyama vya siasa ambazo zilianza kutumika 17 Machi, 2023

Kuhusu Demokrasia ndani ya Vyama vya Siasa, serikali imetekelezwa na serikali kupitia mapendekezo ya Muswada wa Marekebisho ya Sheria ya Vyama vya Siasa ambao unakusudiwa kuwasilishwa na serikali bungeni katika mkutano wa 13 wa Bunge utakaoanza tarehe 31 Oktoba, 2023. Baada ya Muswada kutiwa saini na Rais, baadhi ya masuala yatatiliwa mkazo kupitia kanuni na miongozo.

Kuhusu Ruzuku kwa Vyama vya Siasa, pendekezo hili limefanyiwa kazi kupitia Muswada wa marekebisho ya vyama vya siasa ambao unakusudiwa kuwasilishwa na serikali bungeni. Mswada huu utawasilishwa tarehe 31 Oktoba, 2023. Baada ya Muswada kutiwa saini na Rais, baadhi ya masuala yatatiliwa mkazo kupitia kanuni na miongozo.

Kuhusu Tume ya Taifa ya Uchaguzi, pendekezo hili limefanyiwa kazi kupitia Muswada wa marekebisho ya vyama vya siasa ambao unakusudiwa kuwasilishwa na serikali bungeni. Mswada huu utawasilishwa tarehe 31 Oktoba, 2023 katika kikao cha 15 cha Bunge.

Kwa Mwendelezo wa Mkutano (siku ya pili), bofya hapa: Abdul Nondo: TAMISEMI haipaswi kusimamia uchaguzi, haitotenda haki
 
Kama anaamini katika demokrasia lazima aonyeshe kwa vitendo, aache ukandamizaji wa upinzani, kama alivyoapa kulinda katiba atimize wajibu wake, kamata kamata isiyo na msingi iachwe, na sasa umefika wakati wa kukubali kukoselewa, kama anavyokosolewa kuchemka kwake kwenye suala la Dipiwedi, Kukubali udhaifu sio dhambi, mabadiliko ya katiba ni ya wananchi sio CCM,CCM waache kuhodhi katiba. lakini lazima tuwe na mahakama ya Katiba katika mapendekezo ya katiba mpya.
 
Kama anaamini katika demokrasia lazima aonyeshe kwa vitendo, aache ukandamizaji wa upinzani, kama alivyoapa kulinda katiba atimize wajibu wake, kamata kamata isiyo na msingi iachwe, na sasa umefika wakati wa kukubali kukoselewa, kama anavyokosolewa kuchemka kwake kwenye suala la Dipiwedi, Kukubali udhaifu sio dhambi, mabadiliko ya katiba ni ya wananchi sio CCM,CCM waache kuhodhi katiba. lakini lazima tuwe na mahakama ya Katiba katiba mapendekezo ya katiba mpya.
Amen
 
Kama anaamini katika demokrasia lazima aonyeshe kwa vitendo, aache ukandamizaji wa upinzani, kama alivyoapa kulinda katiba atimize wajibu wake...
Naamini si lengo la Rais kuminya Democrasia, isipokuwa kuna wahuni ambao kwa haraka haraka ni kama wanataka kuonesha wanamsaidia Rais ingawa kiuhalisia sio kweli.

Mh. Rais awaite na kuwakanya ili kutoendeleza negativity zinazoharibu umoja wa kitaifa na maridhiano kwa sababu hata wakati Mh. Rais anafanya maridhoani hawajui what was her good intention.
 
Naamini si lengo la Mh.Rais kuminya democrasia, isipokuwa kuna wahuni ambao kwa haraka haraka ni kama wanataka kuonesha wanamsaidia Mh. Rais ingawa kiuhalisia sio kweli!
Rais awaite na kuwakanya ili kutoendeleza negativity zinazoharibu umoja wa kitaifa na maridhiano kwa sababu hata wakati Mh. Rais anafanya maridhoani hawajui what was the Good intention ya Mh. Rais!!
Hili nakubaliana na wewe.
 
SSH aache hadaa na utapeli. Hata kubadilisha sheria ya tume ya uchaguzi amashindwa.

Juzi amemteua mkwe kwenda tamisemi kusimamia uchaguzi wa serikali za mitaa wakati mapendekezo ya hii tume mbovu iliyopo ilikuwa ni chaguzi zote zisimamiwe na tume ya uchaguzi.

She is all talk no action, atafika 2025 hakuna alichotimiza zaidi ya makongamano.
 
Naamini si lengo la Mh. Rais kuminya Democrasia, isipokuwa kuna wahuni ambao kwa haraka haraka ni kama wanataka kuonesha wanamsaidia Mh. Rais ingawa kiuhalisia sio kweli.
Mh. Rais awaite na kuwakanya ili kutoendeleza negativity zinazoharibu umoja wa kitaifa na maridhiano kwa sababu hata wakati Mh. Rais anafanya maridhoani hawajui what was her good intention !!
Wahafidhina wa CCM wanamtesa mama haswa Nape Nauye
 
SSH aache hadaa na utapeli. Hata kubadilisha sheria ya tume ya uchaguzi amashindwa.

Juzi amemteua mkwe kwenda tamisemi kusimamia uchaguzi wa serikali za mitaa wakati mapendekezo ya hii tume mbovu iliyopo ilikuwa ni chaguzi zote zisimamiwe na tume ya uchaguzi.

She is all talk no action, atafika 2025 hakuna alichotimiza zaidi ya makongamano.
Mnafiki sana huyu mama! Afu anadhani wa TZ wote ni wajinga!
 
Back
Top Bottom