CPT wasema Katiba Mpya ni Kipaumbele Alfa na Omega, Wataja Vipaumbele 28 vya Dira ya Taifa Kuelekea 2050

Mama Amon

JF-Expert Member
Mar 30, 2018
2,021
2,478
1700419364305.png

Profesa Kitila Alexander Mkumbo, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, Waziri mwenye dhamana ya kusimamia utendaji wa kazi za Tume ya Mipango
Chama cha Wanataaluma Wakristo Tanzania (CPT) kimeadhimisha kwa kishindo kumbukizi ya miaka 40 tangu kilipoasisiwa na wanataaluma wakristo mwaka 1982.

Tukio hilo limeambatana na uzinduzi wa kitabu kipya chenye kupendekeza nguzo 28 katika ujenzi wa Taifa la Tanzania.

Kitabu hiki ni mchango wao wa kitaaluma katika mchakato wa maandaizi ya Dira ya Taifa ya Maendeleo kuelekea mwaka 2050. Nakala pepe ya kitabu hiki imeambatanishwa hapa chini.

Sekta za kimkakati tano zatajwa

Akiongea katika ukumbi wa Vijana wa Don Bosco, Upanga jijini Dar es Salaam, Jumamosi ya tarehe 18 Novemba 2023, Mwenyekiti wa CPT, Thomas Brash, ambaye kitaaluma alijitambulisha kama Mwanasheria, alisema kwamba, wanataaluma wametafiti na kuandika kitabu hiki ili kukazia umuhimu wa malengo matano ya kimkakati. Malengo hayo ni:
  1. Kujenga Uchumi Mpana na Shirikishi,
  2. Kuimarisha utawala Bora na Kujenga Taasisi Imara,
  3. Upatikanaji wa Huduma Muhimu za Jamii kwa Wote,
  4. Kutunza Mazingira na Kuendeleza Uadilifu wa Uumbaji, na
  5. Kuendeleza Mahusiano Mazuri ya Kikanda na Kimataifa.

Vipaumbele vya kimkakati 28 vilivyotajwa

Kwa mujibu wa kitabu hiki ambacho kimebatizwa jina “Mchango wa Wanataaluma Wakristo Tanzania Kuelekea Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050,” mchanganuo wa vipaumbele vyote 28 vilivyotajwa kitabuni, kila lengo likiwa limebeba shabaha zake ni kama ifuatavyo:

I. Kujenga Uchumi Mpana na Shirikishi

  1. Kuweka mwelekeo Mpya katika Kukabiliana na Umaskini
  2. Kuondokana na Kilimo cha Kujikimu
  3. Kuchochea Kasi ya Ukuaji wa Uchumi kwa Kuzingatia Manufaa kwa Jamii Pana
  4. Kuboresha Mazingira ya Uwekezaji na Uendeshaji Biashara
  5. Kubuni Mkakati wa Madini Mahsusi
  6. Kubuni Fursa Mpya za Kiuchumi
  7. Kupanua Manufaa ya Miradi Mikubwa ya Maendeleo kwa Wananchi
II. Kuimarisha utawala Bora na kujenga Taasisi Imara
  1. Kuendeleza Mchakato wa Katiba Mpya
  2. Kufanya Mapitio ya Sheria Zilizopitwa na Wakati na Zenye Migongano
  3. Kupigania Uhimilivu wa Miundo, Mifumo na Taasisi
  4. Kuendelea Kubuni Mbinu Imara Zaidi za Kukabiliana na Tatizo la Rushwa
  5. Kuhimia Uwajibikaji kwa Wananchi
  6. Kujenga Maadili na Jamii Inayoheshimu na Kulinda Utu wa Mtu kwa Kupunguza Tofauti Kubwa Kimapato, Kujenga Uchumi wa Faida kwa Wote, Umuhimu wa Kinga ya Jamii, Kuwa na Sera Rafiki kwa Familia, Kujenga Tabia ya Kujitegemea, na Kujenga Maisha ya Maadili Mema.
  7. Kugatua Madaraka ya Kupanga na Kusimamia Maendeleo Kutoka Juu Kwenda Chini kwa Kuunda Vyama Huru vya Ushirika, Kuanzisha Programu ya Kujenga Uwezo Kutoka Chini, Serikali za Vijiji na Mitaa Kusimamia Watumishi wa Umma, Kujenga Mahusiano ya Kisheria Vijijini, Kujenga Taratibu Stahiki Kusimamia Shughuli za Ustawi Vijijini, Kujenga Mazingira Yakinifu Kustawisha Biashara Vijijini, Serikali za Mitaa na Vijiji Kujengewa Mazingira ya Kujiletea Maendeleo, Miradi ya Maendeleo Vijijini Iendane na Uwezo wa Usimamizi Walengwa, Kubuni Teknolojia Wezeshi Kufanikisha Maendeleo Vijijini, na
  8. Kuandaa Utaratibu wa Hamasa kwa Serikali za Mitaa na Vijiji.
  9. Kukuza Ubunifu, na Kupanua Upeo wa Kufikiri
III. Upatikanaji wa Huduma Muhimu za Jamii kwa Wote
  1. Kuboresha Huduma za Afya
  2. Kuboresha Huduma za Elimu
  3. Kuboresha Huduma za Maji Safi, Salama na Usafi wa Mazingira
IV. Kutunza Mazingira na Kuendeleza Uadilifu wa Kiikolojia
  1. Kuboresha Usafi wa Mazingira
  2. Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi
  3. Ulinzi wa Uoto wa Asili na Bayoanwai
  4. Kulinda Mazingira ya Asili
V. Kuendeleza Mahusiano Mazuri ya Kikanda na Kimataifa
  1. Kuimarisha Fursa za Kiuchumi za Kikanda
  2. Kuimarisha Diplomasia ya Kiuchumi na Kisiasa Kimataifa
  3. Kufaidika na Fursa za Miundombinu za Masoko ya Kikanda
  4. Kuchukua Tahadhari Stahiki Dhidi ya Athari Katika Mahusiano ya Kikanda
  5. Kupanua Elimu ya Kufanikisha Utekelezaji wa Maazimo ya Kikanda.

Kuhusu umuhimu na uharaka wa “Kufufua, kuendeleza na kuhitimisha mchakato wa Katiba Mpya,” Brash alieleza kwamba, wanataaluma Wakatoliki Tanzania wanaliona suala hilo kama kipaumbele ambacho ni alfa na omega ya vipaumbele vyote vya kitaifa kuanzia sasa hadi mwaka 2050.

Kuhusu suala hili, katika kitabu kilichozinduliwa Jumamosi, CPT wanatoa angalizo lifuatalo:

“Tunarudia kusisitiza mabadiliko ya Katiba ya nchi. Tukifanikiwa kujenga utamaduni wa kuheshimu demokrasia tutakuwa wabunifu zaidi na watu wenye uwezo wa kutumia uwezo mkubwa tulionao wa kutuletea maendeleo. Mabadiliko ya katiba ni hitaji la muda mrefu na haki ya msingi ya watu iliyodaiwa kwa miaka mingi. Mchakato huu ulianza vizuri kwa kukusanya maoni ya wananchi na kuandaa rasimu ya awali. Hakuna sababu za msingi za kusitishwa kwa mchakato huu. Kwa hiyo unapaswa kuendelezwa hadi katiba mpya ipatikane. (uk. 58)”

Mapendekezo ambayo ni mapya katika Mchango wa CPT

Mapendekezo ya CPT yanahimiza maboresho makubwa katika maudhui ya ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa unaohitimishwa 2025, yaani "Tanzania Development Vision 2025" (TDV 2025).

Katika ukurasa wa 12 hadi 14 wa nakala ya Kiingereza ya "TDV 2025" zimetajwa sekta tatu za kimkakati zikiwa zinabeba vipaumbele 16 kwa pamoja. Sekta hizo ni "Ustawi wa Watu," "Utawala bora," na "Uchumi wenye nguvu za mashindano duniani." Mchanganuo wa vipaumbele hivyo 16 ni kama ifuatavyo:

I. Ustawi wa Watu

  1. Utoshelevu na usalama wa chakula.
  2. Elimu ya msingi kwa wote (UPE).
  3. Usawa wa kijinsia na uwezeshaji wa wanawake.
  4. Huduma za Afya zilizo bora.
  5. Huduma za Afya ya Uzazi zilizo bora.
  6. Upunguzaji wa vifo vya Mama na watoto.
  7. Upatikanaji wa Maji Salama kwa Wote.
  8. Watu wenye urefu wa maisha ulio sawa na watu wa mataifa ya uchumi wa kati.
  9. Kukomesha umaskini unaotweza utu.
II. Utawala bora
  1. Jamii yenye maadili bora na utamaduni wa kistaarabu.
  2. Kuheshimu utawala wa sheria.
  3. Kukomesha rushwa na utovu wa maadili ya kijamii.
  4. Jamii iliyoelimika na yenye uwezo wa kushika usukani wa ajenda yake ya maendeleo.
III. Uchumi wenye nguvu za za mashindano duniani
  1. Uchumi wa kitaifa ulio imara na wenye mfumuko mdogo wa bei
  2. Uchumi unaokua kwa kasi ya angalu 8%.
  3. Miundombinu inayotosheleza mahitaji ya sekta zote.
Hivyo, wakati andiko la TDV 2025 lilipendekeza sekta tatu za kimkkati zenye vipaumbele 16, mchango wa CPT katika Dira mpya ya Taifa Kuelekea 2050 unapendekeza sekta tano za kimkakati zenye vipaumbele 28. Kwa hiyo, kuna mapendekezo ya sekta mpya mbili na vipaumbele vipya 11. Hili ni sawa na ongezeko la 40% katika vipaumbele.

Lakini pia, andiko la TDV 2025 halikuwa na vigezo vya kupima viwango vya ufanisi wakati wa utekelezaji wake. CPT wanahimiza kwamba uandishi wa Dira ya Taifa Kuelekea 20250 usirudie kosa hili, kwa kuhakikisha kwamba Dira mpya inataja vigezo vya muda mrefu na pamoja na vigezo vya muda mfupi wa miaka mitano mitano.

Nadharia ya mabadiliko inayopendekezwa na CPT

Baada ya kupitia kitabu hiki kwa makini, tumeweza kufupisha katika ukurasa mmoja maoni ya CPT kuhusu sekta zote kwa kutumia mchoro wa ramani ya mabadiliko ya kimkakati (strategic changes map) wenye kuonyesha nadharia ya mabadiliko ya kimkakati yanayohusika (theory of strategic change), kama ifuatavyo:

1701064880526.png

Chanzo: Mchoro huu umeandaliwa na Dawati la Utafiti la Mama Amon (DUMA), baada ya kusoma kitabu kilichoandaliwa na CPT

Pia tumeweza kufupisha katika ukurasa mmoja maoni ya CPT kuhusu sekta ya uchumi kwa kutumia mchoro wa ramani ya mabadiliko ya kimkakati (strategic changes map) wenye kuonyesha nadharia ya mabadiliko ya kimkakati yanayohusika (theory of strategic change), kama ifuatavyo:

1700931895067.png

Chanzo: Mchoro huu umeandaliwa na Dawati la Utafiti la Mama Amon (DUMA), baada ya kusoma kitabu kilichoandaliwa na CPT

Kadhalika, tumeweza kufupisha maoni ya CPT kuhusu sekta ya elimu kwa kutumia mchoro wa ramani ya mabadiliko ya kimkakati (strategic changes map) wenye kuonyesha nadharia ya mabadiliko ya kimkakati yanayohusika (theory of strategic change), wenye kutoa muhtasari wa mchango husika katika ukurasa mmoja, kama ifuatavyo:

1701066099806.png

Chanzo: Mchoro huu umeandaliwa na Dawati la Utafiti la Mama Amon (DUMA), baada ya kusoma kitabu kilichoandaliwa na CPT

Wajumbe wa Tume ya mipango na hati ya majukumu yao

Zoezi la maandalizi ya Dira Mpya ya maendeleo kuelekea 2050 lilizinduliwa rasmi na Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango, Makamu wa Rais, kwa niaba ya Rais, Jijini Dodoma, tarehe 3 Aprili 2023.

Wananchi wote tulialikwa kushiriki kikamilifu katika maandalizi ya Dira mpya. Lakini pia, wito wa ushiriki mpana ulirudiwa na Mhe. Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan, tarehe 11 Septemba 2023, Jijini Dar Es Salaam, wakati akifungua mkutano maalumu wa Baraza la vyama vya siasa na wadau wa demokrasia.

Tayari Rais Samia ameunda Tume ya Mipango ikiwa chini ya Wizara ya Mipango. Aidha tayari ameteua wajumbe wa Tume hii. Wajumbe hao ni wafuatao:

  1. Ombeni Sefue, Katibu Mkuu Kiongozi wa zamani, Balozi Mstaafu na mwakilishi wa Tanzania wa Kudumu katika Umoja wa Mataifa, New York;
  2. Omar Issa, Mkurugenzi Mtendaji wa zamani wa Kitengo cha Rais cha "Matokeo Makubwa Sasa" (BRN) wakati wa Rais Jakaya Kikwete;
  3. Ami Mpungwe, Mkurugenzi wa zamani Katika Wizara ya Mambo ya Nje, aliyesimamia Masuala ya Ukanda wa Afrika na Mashariki ya Kati, na Balozi wa zamani wa Tanzania nchini Afrika Kusini; na
  4. Maryam Salim, Meneja Mkazi wa Benki ya Dunia huko Cambodia.
Nakala ya hati ya majukumu ya Tume ya Mipango tuliyoiona inataja majukumu 11 ya Tume ya Mipango kama ifuatavyo:
  1. Kubuni dira na miongozo ya uchumi wa Taifa;
  2. Kusanifu sera za kiuchumi, usimamizi wa uchumi, utafiti, na mikakati ya maendeleo ya Taifa;
  3. Kufanya tathmini ya hali ya rasilimali za taifa kwa ajili ya kuendeleza na kuishauri serikali juu ya matumizi bora ya rasilimali hizo;
  4. Kuchambua mwelekeo wa vigezo muhimu vya kiuchumi ikiwa ni pamoja na urari wa malipo, ujazo wa fedha na bei na kuishauri serikali ipasavyo;
  5. Kuchambua sera zilizopo kwa nia ya kuimarisha utekelezaji wake na kupendekeza sera mpya pale inapoonekana ni muhimu;
  6. Kufuatilia utendaji wa kila siku wa sekta mbalimbali za uchumi na kuhakikisha kuwa hatua zinazofaa zinachukuliwa ili kutatua matatizo yoyote ya kiutendaji yanayoweza kugunduliwa katika sekta hizo;
  7. Kuhakikisha miongozo juu ya mahusiano ya kiuchumi na mataifa mengine na mashirika ya kimataifa imeandaliwa;
  8. Kuandaa mikakati ya kitaifa ya idadi ya watu;
  9. Kutoa miongozo ya uundaji wa Mpango wa Taifa na kufuatilia mchakato wa maandalizi ya mipango ya muda mrefu, mipango ya muda wa kati na mipango ya muda mfupi;
  10. Kusimamia utekelezaji wa maamuzi ya serikali kuhusu masuala ya mipango na usimamizi wa uchumi; na
  11. Kuchambua masuala yoyote ya kijamii na kiuchumi na kupendekeza kwa serikali sera na hatua zinazofaa kuchukuliwa kwa maslahi ya taifa.
Hata hivyo, hatukuweza kuthibitisha kama Tume hii tayari imeanza kazi ya kupokea maoni ya wananchi kama Makamu wa Rais alivyolitangazia Taifa au bado.

1700474154894.png

Balozi Ombeni Sefue, Mjumbe wa Tume ya Mipango

Harakati za utume wa CPT tangu 1982

Mariam Kessy, Mratibu wa CPT Taifa, aliwaeleza wajumbe kwamba uamuzi wa CPT kuandika kitabu cha “Mchango wa Wanataaluma Wakristo Tanzania Kuelekea Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050,” ni hatua mojawapo katika safari ndefu ya chama hiki katika kutekeleza utume wake wa kutekeleza kwa vitendo mafundisho ya Kanisa Katoliki kuhusu mbinu bora za kuboresha maisha ya jamii.

Kessy alifafanua mafanikio na changamoto walizopitia tangu 1982 na maelezo yake yanafupishwa hapa chini. Alisema kuwa, safari ya utume wa CPT kwa miaka 40 ni sawa na safari ya Wanaisraeli kwa miaka 40 wakiwa jangwani kuelekea kwenye nchi ya ahadi ya Kanaani.

“Hatujafika, hatujachoka, na hatujakata tamaa. Ni safari ya matumaini yasiyochuja. Tunaimarishwa na ukweli kwamba kuna mafanikio mengi na mapungufu kidogo,” alieleza Mariam Kessy.

Kwa maoni yake Kessy, kazi za utume wa CPT zilizotekelezwa tangu 1982 zinagawanyika kwenye makundi saba. Kuna masuala ya kijamii, elimu ya uraia, siasa na chaguzi za kisiasa, usimamizi wa uchumi, na usimamizi wa maadili ya jamii.

Masuala ya kijamii yanahusu huduma za elimu, afya, nishati, maji, mazingira na miundombinu zilifanyiwa tafakari ya kipekee kwa kufanya uchambuzi wa sera, bajeti, na utolewaaji wa huduma, kwa kutumia kigezo cha ubora pamoja na upatikanaji.

Kwa mfano, changamoto ya uhifadhi wa vyanzo vya maji, uvunaji wa maji ya mvua na usambazaji wake ilitiliwa mkazo kupitia program ya CPT ya mwaka 2000 kupitia andiko “Maskini Tukomboane (2000)” lililokazia umuhimu na ulazima wa maji safi na salama kwa kila kaya.

Elimu ya uraia huleta ufahamu juu ya namna serikali inavyofanya kazi, wajibu wa raia kwa serikali na kwa jamii pamoja na haki za raia.

Hivyo, CPT imeandaa machapisho na kuyatumia kufanya uhamasishaji kwa njia mbalimbali. Machapisho hayo ni pamoja na:

  • “Sheria ya Ndoa na Mirathi (1999),”
  • “Haki na Wajibu wa Raia (1998),”
  • “Sheria ya Ardhi Tanzania(2001),”
  • “Haki za Raia na Jeshi la Polisi (2003),”
  • “Polisi Rafiki (2005),”
  • “Kitabu cha Kiada kwa Mahakimu wa Mahakama za Mwanzo(2001),”
  • “Haki za Wafungwa na Hali ya Magereza Tanzania Bara (2001),” na
  • “Utume kwa Wafungwa (2004).”
Siasa ni shughuli zote zinazohusiana na harakati za kujipatia madaraka na namna ya kuyatumia kwenye uratibu na usimamizi wa mambo ya umma, madaraka hayo yakiwa yanaambatana na uwezekano wa kufanyika kwa maamuzi yaliyo na athari chanya au athari hasi kwa maisha ya jamii.

Hivyo, CPT imekuwa ikitoa mchango wa kuelimisha jamii kuusudi watu waelewe haki na wajibu wao kabla, wakati na baada ya chaguzi za kisiasa zinazoongozwa na demokrasia ya vyama vingi. Hivyo, machapisho yafuatayo yaliandaliwa na CPT na kusambazwa:

  • “Historia ya Tanzania na Sifa za Demokrasia(1994),”
  • “Mamlaka na Wasio na Mamlaka: Uzoefu wa Tanzania(1994),”
  • “Ushiriki wa Wananchi(1995),”
  • “Kuwajibika Katika Jamii(1995),”
  • “Uchaguzi wa Kisiasa: Kwa nini Tujali? (2000),”
  • “Kwa nini Tujali Manufaa na Ustawi wa Wote (2004),”
  • “Mada za Kuongoza Maandalizi ya Uchaguzi Mkuu wa 2010 (2009),”
  • “Ilani ya Mapendekezo ya Vipaumbele vya Kitaifa (2009),”
  • “Tudhamirie Siasa Adilifu (2010),”
  • “Tudhamirie Kujenga Jamii Yenye Utu (2013),” na
  • “Mwalimu Nyerere Conference of People Centred Development (2019).”
Usimamizi wa maadili ya jamii ni kazi nyingine ya serikali. Kanuni zote za maadili zilizotungiwa sheria za Bunge na kutambuliwa kama jinai zinapaswa kusimamiwa na serikali kwa kuwakamata na kuwashitaki watu wanaotuhumiwa kuzivunja, na hatimaye kuwafunga wote watakaotiwa hatiani na mahakama. Kwa hiyo, CPT waliandaa machapisho yafuatayo na kusambazwa:
  • “Thomas Moore and the Tanzanian Intellectual (1999),”
  • “Teolojia ya Pesa, Madaraka na Kazi (2002),”
  • “Misingi ya kuishinda rushwa(2004),”
  • “Msukumo wa Wanataaluma Wakristo Tanzania Katika Kukabiliana na Rushwa(2005),”
  • “Ulevi ni Ugonjwa: Je Unataka Kupona? (2011),”
  • “Tafakari Kuhusu Misingi ya Kimaadili (2018),” na
  • “Njia Ndogo ya Kawaida Kufikia Utakatifu (2020).”
Usimamizi wa uchumi wa nchi ni kazi mojawapo ya serikali. Michakato ya uzalishaji, usambazaji, uuzaji na ununuzi lazima ifanyike kwa kuzingatia kanuni za haki sawa katika mabadilishano, majukumu sawa katika kuchangia pato ya Taifa, haki sawa katika kugawana pato la Taifa, usawazishaji wa tofauti za kipato ili kulinda umoja wa kitaifa, na kutoa fidia stahiki kwa wote wanaoonewa kiuchumi. Kwa sababu hizi, machapisho yafuatayo yaliandaliwa na CPT na kusambazwa:
  • “Uchumi Unaojali (1998),” kitabu kilichoandaliwa wakati wa mchakato wa kuandaa dira ya Taifa ya 2000-2025, kwa ajili ya kuhimiza “Uchumi unaoweza kuwa mtumishi wa jamii,”
  • “Maskini unganeni kuondokana na Umaskini (2001),”
  • “Maskini Tukomboane (2002),”
  • “Motisha Hujenga Utashi wa Utekelezaji (2020),”
  • “Kujengea Watu Ari ya Kutambua Uwezo Wao na Kuutumia (2021),”
  • “Jinsi ya Kuanzisha saccos na kuziendesha kwa mafanikio (2007),”
  • “Wito wa kukuza usawa (2022),”
  • Na hivi karibuni “Mchango wa Wanataaluma Wakristo Tanzania Kuelekea Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 (2023),” ambacho ni kitabu kilichozinduliwa Jumamosi iliyopita.
1700473870957.png

Omary Issa, Mjumbe wa Tume ya Mipango

Historia fupi ya mipango ya Taifa

Naye Mjumbe wa Kamati ya Ushauri (CPT Taifa), Paschal Kessy, aliwaeleza wajumbe juu ya historia ya mipango ya maendeleo nchini Tanzania.

Tulifanya utafiti kwa ajili ya kujibu swali lifuatalo: "Ni kwa kiasi gani sekta ya umma nchini Tanzania inazingatia mbinu za kisasa za utengenezaji wa mipango mikakati?" alisema Kessy.

Yaani, "“To what extent does the Tanzanian public sector adopt best practices in strategic planning?” alifafanua Kessy.

Alisema kwamba, tangu Tanzania tupate uhuru tumeandaa na kutekeleza mipango 14 ya Maendeleo ya muda mfupi. Mipango hiyi ni kma ifuatavyo:

  • Mpango wa kwanza wa miaka mitatu wa maendeleo baada ya uhuru (1962-1964);
  • Mpango wa kwanza wa maendeleo ya miaka mitano (1964-1969);
  • Mpango wa Pili wa maendeleo ya kiuchumi na kijamii wa miaka mitano (1969-1974);
  • Mpango wa tatu wa maendeleo kiuchumi na kijamii wa miaka mitano (1975–1979).
  • Programu ya Taifa ya Kunusuru Uchumi (NESP) (1980–1982);
  • Programu ya Taifa ya Marekebisho ya Uchumi (SAP) (1983–1985);
  • Mpango wa Kwanza wa miaka 3 wa Kufufua Uchumi (ERP I) (1986–1988);
  • Mpango wa Pili wa Kufufua uchumi (ERP II au ESAP) (1989–1992);
  • Mipango ya Miaka Mitatu Mitatu Inayopokezana na Bajeti ya Maoteo (RPFB) (1993–2012).
  • Mpango wa Kwanza wa Maendeleo wa Miaka Mitano (FYDP I) (2011–2015);
  • Mpango wa Pili waTaifa wa Maendeleo wa Miaka Mitano (FYDP II) (2016–2020); na Mpango ya Tatu wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano (FYDP II) (2021–2025).
Kwa maoni ya Kessy, utengenezaji wa mipango mkakati katika sekta ya umma unaonyesha kwamba mipango mingi tuliyoiandaa tangu uhuru haina nadharia ya mabadiliko ya kimkakati (theory of strategic changes) yenye kuongoza utengenezaji wake.

"Kuna haja ya kuondoa dosari hii wakati wa kutengeneza mkakati wa sasa kuelekea 2050," alisema Kessy.

Dawati la Utafiti la Mama Amon (DUMA) linafahamu kwamba mbinu ya utengeneza wa mikakati iitwayo "Balanced Score Card (BSC) Model of Strategic Planning" inaweza kumaliza dosari hii.

BSC ni mbinu ya kimkakati ya kupanga na kusimamia utekelezaji wa mipango mikakati iliyobuniwa katika miaka ya 1990 na Dkt. Robert Kaplan akishirikiana na Dkt. David Norton, wote kutoka Shule ya Biashara ya Harvard, Marekani.

Mbinu ya Kaplan-Norton inatumiwa na idara mbalimbali za serikali, mashirika ya kitaifa na kimataifa, na serikali kadhaa za Asia, Afrika, Amerika na Ulaya.

Mfano, mwaka 2010 serikali ya Dubai iliutumia utaratibu huu wa BSC kuunda mkakati wake wa kitaifa kuelekea mwaka 2030. Ni mpango wenye kuvutia.

Katika mazingira haya, Kessy aliwaomba Watanzania wote kutumia uzoefu wetu wa kihistoria wa miaka zaidi ya 60 kuandaa mpango mkakati wa muda mrefu wenye kutaja dira, dhima, malengo, madhumuni, mbinu, mikakati, vigezo vya ufanisi, rasilimali na mgawanyo wa majukumu ulio sahihi.

“Dira imetafsiriwa kama mtanzamo wa kina sana wa mwenendo wa hali ya sasa ili kutoa ubashiri sahihi wa mwenendo wa hali ya baadaye. Mafanikio ya Dira yanahitaji, pamoja na mengine, ubashiri ulio karibu na ukweli wa mwenendo wa hali ya baadaye, matakwa halisi ya jamii kimaendeleo na uchaguzi yakini wa vipaumbele vitakavyoiwezesha jamii kujenga uwezo wa kufikia mafanikio ya pamoja kijamii,” alimaliza taarifa yake Kessy.

Naye Askofu Mkuu Paul Ruzoka, wa Jimbo Kuu la Tabora, akiandika katika dibaji ya kitabu kilichozinduliwa, anasema:

“Mchango wetu katika kuelekea Mchakato wa Kuandaa Dira ya Maendeleo Tanzania Kuelekea 2050, una vishawishi kadhaa: mosi, kushahidia haja ya kuwa na mwendelezo wa kujiwekea Dira yenye malengo dhahiri; pili, kuhimiza nidhamu ya kusimamiana katika kutekeleza kwa dhati tuliyonuia kufikia; tatu, kurejea na hivyo kujikosoa pale ambapo tunaona hatukufanya vizuri ili tuweze kujisahihisha na kuepuka kukosea tena, na; nne, kuwasilisha maono ya vipaumbele vyetu katika mustakabali wa maendeleo ya Taifa na wananchi wake kuelekea mwaka 2050.”

1700932594484.png

Balozi Ami Mpungwe, Mjumbe wa Tume ya Mipango

Kanuni ya tafakari za CPT na Chimbuko lake

Profesa Beda Mutagahywa, ni miongoni mwa wanachama waasisi wa CPT, na aliwahi kuwa Mwenyekiti wa CPT. Yeye alitoa maelezo kuhusu chimbuko la CPT na mantiki ya methodolojia ya kuchunguza maisha ya jamii inayotumika hadi leo. Maelezo yake yanafupishwa hapoa chini.

Ndani ya Kanisa Katoliki, kuna vyama vya utume wa walei kama vile Chama cha CPT, Wawata, Viwawa, Rejio Maria, na vyama vingine vya kitume kama hivi, ni watoto tofauti katika familia moja.

Kila chama kina mbinu zake malum za kutekeleza utume wa walei wa kujenga “ufalme wa Mungu” wa haki, utu, usawa, amani na maendeleo, kwa “kuyatakatifuza malimwengu.”

Mwezi huu wa Novemba 2023, chama cha CPT kinaadhimisha miaka 40 tangu kianzishwe, kama chama kingine cha kutekeleza utume wa walei chini ya Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC) lililokipokea rasmi mwaka 1982.

Katika ngazi ya kitaifa, hatua za mwanzo za kuanzishwa kwa CPT zilifanywa na kukundi cha wana TYCS kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam waliohitimu katika miaka ya 1960 na 1970 na kuajiriwa sehemumbalimbali serikalini.

Kikundi cha wahitimu hawa kilizoea kufanya tafakari mbalimbali kuhusu masuala yanayohusu sera za kiuchumi na kijamii kwa kutumia kurunzi ya enjili, michakato hiyo ikiwa inaongozwa na spairo yenye maduara yaliyo na hatua tatu za tafakari, yaani, spairo yenye mizunguko kadhaa ya “Kuona, Kuamua na Kutenda.”

Majadiliano yalijikita kwenye uhusiano unaopaswa kuwepo kati ya Imani ya Kanisa, kwa upande mmoja, na Sera za Serikali kuhusu Ujamaa na Kujitegemea, kwa upande mwingine. Matokeo ya tafakari hizi yalikuwa yanachapishwa kwenye Jarida la wakati huo lililoitwa “Mwamko wa Utu.”

Wanachama waasisi waliohudhuria vikao vya kwanza kati ya 1978 na 1982 vilivyofanyika kwa ajili ya kuunda CPT walikuwa tayari ni waajiriwa serikalini na sekta binafsi.

Leo hii, chama cha CPT kinaunganisha Wakristo wa taaluma mbalimbali zinazotambuliwa kisheria kuanzia ngazi ya cheti, stashahada, shahada ya kwanza, shahada ya uzamili, shahada ya uzamivu nd uprofesa.

Katika ngazi ya kimataifa, vuguvugu la kuasisiwa kwa CPT lilichochewa na Mtaguso Mkuu wa Pili wa Vatikani wa mwaka 1962-1965 ulioleta mwamko na hamasa ya ushiriki wa walei katika kutekeleza utume wa Kanisa kwa kutumia maarifa na stadi za kitaaluma walizo nazo. Mtaguso unawaalika walei kuutakatifuza ulimwengu kwa kutumia kanuni za mafundisho ya Kanisa kuhusu misingi na mbinu za kuboresha maisha ya jamii.

Katika kipindi cha miaka 40, kazi za utume zilizofanywa na CPT zinagusa haki na majukumu katika sekta za uchumi, jamii, siasa, maadili, na uraia. Kazi hizi zimetekelezwa na wanachama wa CPT kwa njia ya machapisho, semina, warsha, makongamano, mijadala ya redioni, na kwa kutoa huduma za kisheria na kitabibu bure.

Mwisho, yatupasa pia kuomba toba kwa makosa tuliyofanya kwa kutojitoa ipasavyo wakati tukitimiza wajibu wa utume. Tunaamini, kupitia msamaha huo tutapata nguvu Zaidi ya kufanya utume kwa namna iliyo bora zaidi.

Profesa Beda alihitimisha maelezo yake kwa kusisitiza kwamba, CPT kama Jumuiya ya Walei Wakristu na Wanataaluma, ni chama chenye majukumu makuu matatu.

Kwanza, kuinjilisha walimwengu kwa vitendo tukitumia kwa ustadi, weledi na uadilifu taaluma na uzoefu wetu.

Pili, kama Wanataaluma wenye uzoefu katika nyanja mbalimbali, tuna wajibu wa kusaidia jamii katika jitihada zake za kutafuta ufumbuzi wa changamoto za maisha wanazokabiliana nazo.

Na tatu, tuna wajibu wa kuibua na kuchokoza mijadala inayolenga, hususan, kuleta mtazamo na mfumo mpya wa utendaji ili kuharakisha kufikia malengo tuliyojiwekea kama nchi au kuboresha malengo yaliyopo na utendaji wake.

“Hii ina maana kwamba vilevile tuna wajibu wa msingi wa kutafuta mbinu za kuinua maendeleo ya Taifa letu na hali za maisha ya wananchi wengi na sio baadhi tu,” alimalizia Profesa Beda.

1700474074851.png

Maryam Salim, Mjumbe wa Tume ya Mipango

Mapadre saba waitaka CPT kufukuza giza la utumwa kwa kutumia mwanga wa taaluma

Tukio la kumbukizi ya miaka 40 ya CPT na uzinduzi wa kitabu maalum lilifunguliwa kwa ibada ya Misa iliyoongozwa na mgeni rasmi, Padre Vitalis Kasembo, ambaye ni Mwenyekiti wa Utume wa Walei Jimbo Kuu la Dar es Salaam. Padre Kasembo alisindikizwa na mapadre wengine sita. Kwa ujumla timu ya mapadre wote saba ilikuwa kama ifuatavyo:

  • Padre Vitalis Kasembo, ambaye ni Mwenyekiti wa Utume wa Walei Jimbo Kuu la Dar es Salaam;
  • Padre Richard Tiiganya (C.PP.S) kutoka Seminari Kuu ya Segerea, Dar es Salaam;
  • Padre Nicodemus Mayalla kutoka Seminari Kuu ya Segerea, Dar es Salaam;
  • Padre Dkt. Joseph Matumaini kutoka Chuo Kikuu cha SAUT;
  • Padre Justin Ramde ambaye ni Mmisionari wa Afrika anayeishi Atman House, Dar es Salaam;
  • Padre Fulbert Mtunguja (OSB) kutoka Parokia ya Mt. Paul Majengo, Jimbo Katoliki Mtwara; na
  • Padre Vic Missiaen, Mlezi wa CPT Taifa.
Siku hiyo, mahubiri yalitolewa na Padre Dkt. Joseph Matumaini. Mahubiri yake yaliongozwa na vitabu viwili vya Biblia. Somo la kwanza lilitoka kitabu cha Nabii Ezekiel, sehemu inayoongelea maisha ya Wanaisraeli wakiwa katika giza la utumwa wa Babeli (36:22-28).

Na Somo la pili lilitoka Kitabu cha Enjili ya Luka, sehemu ya Wimbo wa Maria akimtukuza Mungu kwa uamuzi wake wa kuwakomboa wanaisraeli kutoka utumwani (1:46-55).

Kwa kuzingatia maudhui ya masomo haya mawili, Padre Dkt. Joseph Matumaini alisema kwamba kitendo cha Mungu kuwakomboa wanaisraeli kilikuwa ni kitendo cha “kusimika utaratibu mahali penye vurugu.” Hivyo akawahoji maswali mengi wana-CPT:

"Kila mara ninapofikiria juu ya dhima yenu na kuangalia mnayoyafanya huwa siwaelewi vizuri.

"Hivi nyie mnao uwezo wa kusimika utaratibu mahali penye vurugu? Mnaweza kupanda maarifa penye ombwe la kimaarifa? Sauti yenu ya unabii inayo nguvu hiyo?

"Machapisho yenu yanawafikia wasomaji au mnayaficha makabatini? Dhima yenu ni kuperemba na kukosoa kazi za wengine pekee au mnashirikiana na wengine katika kutafuta maslahi ya pamoja?

"Mnafanya uwezeshaji kwa wengine katika kutafuta maslahi ya pamoja? Nyie ni waibua ajenda na kisha kubaki watazamaji au mnafuatilia 'movie' hadi mwisho?"

Lakini hakuishia hapo. “Kesho Jumapili tutasikia enjili ya talanta. Basi, mtukuzeni Mungu kwa njia ya vipaji vyenu,” alimaliza homilia Dkt. Matumaini.

Kwaya ya Mtakatifu Don Bosco inayoundwa na wanafunzi wa Chuo cha Usafirishaji (NIT) cha Mabibo, Jijini Dar es Salaam, ndiyo ilitumbuiza wakati wa ibada ya Misa Takatifu.

“Tunaamini kwamba, aimbaye vizuri husali mara mbili,” alisema Anthony Shitente, ambaye ni kwayamasta wake.

Na katika sala ya kufunga siku, Padre Kasemba aliwakumbusha CPT kwamba, Kanisa sio chombo cha kusimamia mabadiliko ya kiroho kama maandalizi ya maisha yajayo baada ya kifo cha mwili.

“Badala yake, Kanisa lina jukumu la msingi katika maisha ya kawaida ya watu wenye mwili hai na hasa katika kuboresha ustawi wa jamii,” alisema Padre Kasembo.

Alifafanua kwamba, jukumu hili lilibainishwa rasmi katika Mtaguso Mkuu wa Pili wa Vatikani uliofanyika mwaka 1962-65.

“Na baadaye limefafanuliwa kwa kina katika kitabu cha Mkusanyiko wa Mafundisho ya Kanisa Kuhusu Mbinu Bora za Kuboresha Maisha ya Jamii,” alimalizia Padre Kasembo.

Taarifa hii imeandaliwa na:

Mama Amon
Afisa Mtendaji Mkuu
Dawati la Utafiti la Mama Amon (DUMA)
S.L.P. P/Bag
"Sumbawanga Town"

Sumbawanga.
 
Attachments

  • KITABU CHA CPT. DIRA 2050--NOVEMBA 2023.pdf
    997 KB · Views: 6
Somo la umuhimu wa upatikanaji wa katiba mpya ni gumu sana kueleweka kwa ccm
Katiba ndiyo inayojenga utawala wa haki, kutoa fursa kwa usawa na kuweka mwongozo mkuu namna nchi inavyotakiwa kwenda kwa kuzingatia matakwa ya umma.

Kosa kubwa ni kutarajia kuwa CCM ambayo ni kinara wa kukanyaga haki, ndiyo ituongoze katika kupata katiba, ambayo kwa vyovyote itauweka wazi uovu wao.

Lakini tukitaka Taifa lenye ustawi kwenye nyanja zote, ni lazima.na ni muhimu sana, katiba mpya ipatikane.
 
Hii Katiba Mpya inapendeza sana inapopigiwa kelele na makundi mengine zaidi ya wanasiasa, ni hitaji la watanganyika la muda mrefu.

Naona sasa huu ni wakati wa makundi mengine nayo kuungana kuidai, kwasababu kuwaachia wanasiasa peke yao inaonekana ni hitaji la kisiasa kwa ajili ya manufaa ya chama fulani cha siasa, jambo ambalo sio kweli.

Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app
 
View attachment 2819106
Profesa Kitila Alexander Mkumbo, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, Waziri mwenye dhamana ya kusimamia utendaji wa kazi za Tume ya Mipango
Chama cha Wanataaluma Wakristo Tanzania (CPT) kimeadhimisha kwa kishindo kumbukizi ya 40 tangu kilipozaliwa mwaka 1982.

Tukio hilo limeambatana na uzinduzi wa kitabu kipya chenye kupendekeza nguzo kumi na mbili katika ujenzi wa Taifa la Tanzania, huu ukiwa ni mchango wao wa kitaaluma katika mchakato wa maandaizi ya Dira ya Taifa ya Maendeleo kuelekea mwaka 2050.

Akiongea katika ukumbi wa Vijana wa Don Bosco, Upanga jijini Dar es Salaam, Jumamosi ya tarehe 18 Novemba 2023, Mwenyekiti wa CPT, Thomas Brash, ambaye kitaaluma alijitambulisha kama Mwanasheria, alisema kwamba, wanataaluma wametafiti na kuandika kitabu hiki ili kukazia umuhimu wa masuala yapatayo kumi na mbili.

Kwa kuanzia na masuala yaliyo muhimu zaidi, mambo hayo aliyataja kama ifuatavyo:

Kufufuliwa, kuendelezwa na kuhitimishwa kwa mchakato wa Katiba Mpya; Kufanyika kwa mapitio ya sheria kandamizi, tata, zilizopitwa na wakati na zenye migongano; kujengwa kwa uchumi wenye uwezo wa kuishirikisha na kuitumikia jamii pana; na kuimarishwa kwa utawala bora kwa kujenga taasisi imara na kugatua madaraka ya kupanga na kusimamia maendeleo.

Pia, Brash alieleza haja ya kupanuliwa kwa upatikanaji wa huduma muhimu za jamii kwa watu wote; kukuzwa kwa ubunifu kwa kupanua uwezo wa jamii katika michakato ya kufikiri, kuamua na kutenda; kutunzwa kwa mazingira kwa kutumia misingi thabiti ya uadilifu wa kiikolojia; na kujenga maadili ya jamii kwa kukuza na kuhami tunu ya utu wa kila binadamu.

Kadhalika, Brash aliongelea kumalizwa kwa upungufu mkubwa wa miundombinu, wataalamu na huduma za kibingwa katika ngazi zote za utoaji wa huduma za afya; Kuimarishwa kwa huduma za elimu kwa kuongeza ubora na wingi wa wahitimu kwa kila ngazi na kila sekta ya elimu; na kupanuliwa kwa huduma za maji safi na salama, na kukoleza usafi wa mazingira, ili huduma hizi ziweze kuwafikia watu wote majumbani kwao, mijini na vijijini.

Aidha, CPT wanahimiza kuyakabili ipasavyo mabadiliko ya tabianchi kwa kuchukua hatua madhubuti za kukabiliana na tishio hili kubwa la mazingira; na Kujengwa kwa maadili na jamii inayoheshimu na kulinda utu wa kila binadamu kwa kupunguza tofauti kubwa za kimapato, kujenga uchumi wa faida kwa wote, umuhimu wa kinga ya jamii, na kuwa na sera rafiki kwa familia.

Kuhusu umuhimu na uharaka wa “Kufufuliwa, kuendelezwa na kuhitimishwa kwa mchakato wa Katiba Mpya,” Brash alieleza kwamba, wanataaluma Wakatoliki Tanzania wanaliona suala hilo kama kipaumbele ambacho ni alfa na omega ya vipaumbele vyote vya kitaifa kuanzia sasa hadi mwaka 2050.

Kuhusu suala hili, katika kitabu kilichozinduliwa Jumamosi, CPT wanatoa angalizo lifuatalo:

“Tunarudia kusisitiza mabadiliko ya Katiba ya nchi. Tukifanikiwa kujenga utamaduni wa kuheshimu demokrasia tutakuwa wabunifu zaidi na watu wenye uwezo wa kutumia uwezo mkubwa tulionao wa kutuletea maendeleo. Mabadiliko ya katiba ni hitaji la muda mrefu na haki ya msingi ya watu iliyodaiwa kwa miaka mingi. Mchakato huu ulianza vizuri kwa kukusanya maoni ya wananchi na kuandaa rasimu ya awali. Hakuna sababu za msingi za kusitishwa kwa mchakato huu. Kwa hiyo unapaswa kuendelezwa hadi katiba mpya ipatikane. (uk. 58)”

Kitabu hiki ambacho kimebatizwa jina “Mchango wa Wanataaluma Wakristo Tanzania Kuelekea Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050,” kimeandikwa kuitikia wito wa serikali ya awamu ya sita nchini Tanzania, yenye kuongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan. Nakala peke ya kitabu hiki imeambatanishwa hapa chini.

Tayari Rais Samia ameunda Tume ya Mipango ikiwa chini ya Wizara ya Mipango. Aidha tayari ameteua wajumbe wa Tume hii.

Wajumbe wa Tume ya mipango na hati ya majukumu yao

Wajumbe hao ni wafuatao: Ombeni Sefue, Katibu Mkuu Kiongozi wa zamani, Balozi Mstaafu na mwakilishi wa Tanzania wa Kudumu katika Umoja wa Mataifa, New York; Omar Issa, Mkurugenzi Mtendaji wa zamani wa Kitengo cha Rais cha "Matokeo Makubwa Sasa" (BRN) wakati wa Rais Jakaya Kikwete; Ami Mpungwe, Mkurugenzi wa zamani Katika Wizara ya Mambo ya Nje, aliyesimamia Masuala ya Ukanda wa Afrika na Mashariki ya Kati, na Balozi wa zamani wa Tanzania nchini Afrika Kusini; na Dada Maryam Salim, Meneja Mkazi wa Benki ya Dunia huko Cambodia.

Nakala ya hati ya majukumu ya Tume ya Mipango tuliyoiona inataja majukumu 11 ya Tume ya Mipango kama ifuatavyo:

(1) Kubuni dira na miongozo ya uchumi wa Taifa;

(2) Kusanifu sera za kiuchumi, usimamizi wa uchumi, utafiti, na mikakati ya maendeleo ya Taifa;

(3) Kufanya tathmini ya hali ya rasilimali za taifa kwa ajili ya kuendeleza na kuishauri serikali juu ya matumizi bora ya rasilimali hizo;

(4) Kuchambua mwelekeo wa vigezo muhimu vya kiuchumi ikiwa ni pamoja na urari wa malipo, ujazo wa fedha na bei na kuishauri serikali ipasavyo;

(5) Kuchambua sera zilizopo kwa nia ya kuimarisha utekelezaji wake na kupendekeza sera mpya pale inapoonekana ni muhimu;

(6) Kufuatilia utendaji wa kila siku wa sekta mbalimbali za uchumi na kuhakikisha kuwa hatua zinazofaa zinachukuliwa ili kutatua matatizo yoyote ya kiutendaji yanayoweza kugunduliwa katika sekta hizo;

(7) Kuhakikisha miongozo juu ya mahusiano ya kiuchumi na mataifa mengine na mashirika ya kimataifa imeandaliwa;

(8) Kuandaa mikakati ya kitaifa ya idadi ya watu;

(9) Kutoa miongozo ya uundaji wa Mpango wa Taifa na kufuatilia mchakato wa maandalizi ya mipango ya muda mrefu, mipango ya muda wa kati na mipango ya muda mfupi;

(10) Kusimamia utekelezaji wa maamuzi ya serikali kuhusu masuala ya mipango na usimamizi wa uchumi; na

(11) Kuchambua masuala yoyote ya kijamii na kiuchumi na kupendekeza kwa serikali sera na hatua zinazofaa kuchukuliwa kwa maslahi ya taifa.

Hata hivyo, hatukuweza kuthibitisha kama Tume hii tayari imeanza kazi ya kupokea maoni ya wananchi kama Makamu wa Rais alivyolitangazia Taifa au bado.

Harakati za utume wa CPT tangu 1982

Mariam Kessy, Mratibu wa CPT Taifa, aliwaeleza wajumbe kwamba uamuzi wa CPT kuandika kitabu cha “Mchango wa Wanataaluma Wakristo Tanzania Kuelekea Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050,” ni hatua mojawapo katika safari ndefu ya chama hiki katika kutekeleza utume wake wa kutekeleza kwa vitendo mafundisho ya Kanisa Katoliki kuhusu mbinu bora za kuboresha maisha ya jamii.

Kessy alifafanua mafanikio na changamoto walizopitia tangu 1982 na maelezo yake yanafupishwa hapa chini. Alisema kuwa, safari ya utume wa CPT kwa miaka 40 ni sawa na safari ya Wanaisraeli kwa miaka 40 wakiwa jangwani kuelekea kwenye nchi ya ahadi ya Kanaani.

“Hatujafika, hatujachoka, na hatujakata tamaa. Ni safari ya matumaini yasiyochuja. Tunaimarishwa na ukweli kwamba kuna mafanikio mengi na mapungufu kidogo,” alieleza Mariam Kessy.

Kwa maoni yake Kessy, kazi za utume wa CPT zilizotekelezwa tangu 1982 zinagawanyika kwenye makundi saba. Kuna masuala ya kijamii, elimu ya uraia, siasa na chaguzi za kisiasa, usimamizi wa uchumi, na usimamizi wa maadili ya jamii.

Masuala ya kijamii yanahusu huduma za elimu, afya, nishati, maji, mazingira na miundombinu zilifanyiwa tafakari ya kipekee kwa kufanya uchambuzi wa sera, bajeti, na utolewaaji wa huduma, kwa kutumia kigezo cha ubora pamoja na upatikanaji.

Kwa mfano, changamoto ya uhifadhi wa vyanzo vya maji, uvunaji wa maji ya mvua na usambazaji wake ilitiliwa mkazo kupitia program ya CPT ya mwaka 2000 kupitia andiko “Maskini Tukomboane (2000)” lililokazia umuhimu na ulazima wa maji safi na salama kwa kila kaya.

Elimu ya uraia huleta ufahamu juu ya namna serikali inavyofanya kazi, wajibu wa raia kwa serikali na kwa jamii pamoja na haki za raia.

Hivyo, CPT imeandaa machapisho na kuyatumia kufanya uhamasishaji kwa njia mbalimbali. Machapisho hayo ni pamoja na: “Sheria ya Ndoa na Mirathi (1999),” “Haki na Wajibu wa Raia (1998),” “Sheria ya Ardhi Tanzania(2001),” “Haki za Raia na Jeshi la Polisi (2003),” “Polisi Rafiki (2005),” “Kitabu cha Kiada kwa Mahakimu wa Mahakama za Mwanzo(2001),” “Haki za Wafungwa na Hali ya Magereza Tanzania Bara (2001),” na “Utume kwa Wafungwa (2004).”

Siasa ni shughuli zote zinazohusiana na harakati za kujipatia madaraka na namna ya kuyatumia kwenye uratibu na usimamizi wa mambo ya umma, madaraka hayo yakiwa yanaambatana na uwezekano wa kufanyika kwa maamuzi yaliyo na athari chanya au athari hasi kwa maisha ya jamii. Hivyo, CPT imekuwa ikitoa mchango wa kuelimisha jamii kuusudi watu waelewe haki na wajibu wao kabla, wakati na baada ya chaguzi za kisiasa zinazoongozwa na demokrasia ya vyama vingi.

Hivyo, machapisho yafuatayo yaliandaliwa na CPT na kusambazwa: “Historia ya Tanzania na Sifa za Demokrasia(1994),” “Mamlaka na Wasio na Mamlaka: Uzoefu wa Tanzania(1994),” “Ushiriki wa Wananchi(1995),” “Kuwajibika Katika Jamii(1995),” “Uchaguzi wa Kisiasa: Kwa nini Tujali? (2000),” “Kwa nini Tujali Manufaa na Ustawi wa Wote (2004),” “Mada za Kuongoza Maandalizi ya Uchaguzi Mkuu wa 2010 (2009),” “Ilani ya Mapendekezo ya Vipaumbele vya Kitaifa (2009),” “Tudhamirie Siasa Adilifu (2010),” “Tudhamirie Kujenga Jamii Yenye Utu (2013),” na “Mwalimu Nyerere Conference of People Centred Development (2019).”

Usimamizi wa maadili ya jamii ni kazi nyingine ya serikali. Kanuni zote za maadili zilizotungiwa sheria za Bunge na kutambuliwa kama jinai zinapaswa kusimamiwa na serikali kwa kuwakamata na kuwashitaki watu wanaotuhumiwa kuzivunjwa, na hatimaye kuwafunga wote watakaotiwa hatiani na mahakama.

Kwa hiyo, CPT waliandaa machapisho yafuatayo na kusambazwa: “Thomas Moore and the Tanzanian Intellectual (1999),” “Teolojia ya Pesa, Madaraka na Kazi (2002),” “Misingi ya kuishinda rushwa(2004),” “Msukumo wa Wanataaluma Wakristo Tanzania Katika Kukabiliana na Rushwa(2005),” “Ulevi ni Ugonjwa: Je Unataka Kupona? (2011),” “Tafakari Kuhusu Misingi ya Kimaadili (2018),” na “Njia Ndogo ya Kawaida Kufikia Utakatifu (2020).”

Usimamizi wa uchumi wa nchi ni kazi mojawapo ya serikali. Michakato ya uzalishaji, usambazaji, uuzaji na ununuzi lazima ifanyike kwa kuzingatia kanuni za haki sawa katika mabadilishano, majukumu sawa katika kuchangia pato ya Taifa, haki sawa katika kugawana pato la Taifa, usawazishaji wa tofauti za kipato ili kulinda umoja wa kitaifa, na kutoa fidia stahiki kwa wote wanaoonewa kiuchumi.

Kwa sababu hizi, machapisho yafuatayo yaliandaliwa na CPT na kusambazwa: Kitabu cha “Uchumi Unaojali (1998)” kiliandaliwa wakati wa mchakato wa kuandaa dira ya Taifa ya 2000-2025, kwa ajili ya kuhimiza “Uchumi unaoweza kuwa mtumishi wa jamii,” “Maskini unganeni kuondokana na Umaskini (2001),” “Maskini Tukomboane (2002),” “Motisha Hujenga Utashi wa Utekelezaji (2020),” “Kujengea Watu Ari ya Kutambua Uwezo Wao na Kuutumia (2021),” “Jinsi ya Kuanzisha saccos na kuziendesha kwa mafanikio (2007),” “Wito wa kukuza usawa (2022),” na hivi karibuni “Mchango wa Wanataaluma Wakristo Tanzania Kuelekea Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 (2023),” ambacho ni kitabu kilichozinduliwa Jumamosi iliyopita.

Historia fupi ya mipango ya Taifa

Naye Mjumbe wa Kamati ya Ushauri (CPT Taifa), Paschal Kessy, aliwaeleza wajumbe juu ya historia ya mipango ya maendeleo nchini Tanzania.

Alisema kwamba, tangu Tanzania tupate uhuru tumeandaa na kutekeleza mipango 14 ya Maendeleo ya muda mfupi. Maipango hiyi ni Mpango wa kwanza wa miaka mitatu wa maendeleo baada ya uhuru (1962-1964); Mpango wa kwanza wa maendeleo ya miaka mitano (1964-1969); Mpango wa Pili wa maendeleo ya kiuchumi na kijamii wa miaka mitano (1969-1974); na Mpango wa tatu wa maendeleo kiuchumi na kijamii wa miaka mitano (1975–1979).

Kadhalika, alifafanua kuwa, kuna Programu ya Taifa ya Kunusuru Uchumi (NESP) (1980–1982); Programu ya Taifa ya Marekebisho ya Uchumi (SAP) (1983–1985); Mpango wa Kwanza wa miaka 3 wa Kufufua Uchumi (ERP I) (1986–1988); na Mpango wa Pili wa Kufufua uchumi (ERP II au ESAP) (1989–1992); na Mipango ya Miaka Mitatu Mitatu Inayopokezana na Bajeti ya Maoteo (RPFB) (1993–2012).

Aidha, alisema kwamba, kuna Mpango wa Kwanza wa Maendeleo wa Miaka Mitano (FYDP I) (2011–2015); Mpango wa Pili waTaifa wa Maendeleo wa Miaka Mitano (FYDP II) (2016–2020); na Mpango ya Tatu wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano (FYDP II) (2021–2025).

Hatimaye, akwaomba Watanzania wote kutumia uzoefu huu wa miaka Zaidi ya sitini kuandaa mpango mkakati wa muda mrefu wenye kutaja dira, dhima, malengo, madhumuni, mbinu, mikakati, vigezo vya ufanisi, rasilimali na mgawanyo wa majukumu ulio sahihi.

“Dira imetafsiriwa kama mtanzamo wa kina sana wa mwenendo wa hali ya sasa ili kutoa ubashiri sahihi wa mwenendo wa hali ya baadaye. Mafanikio ya Dira yanahitaji, pamoja na mengine, ubashiri ulio karibu na ukweli wa mwenendo wa hali ya baadaye, matakwa halisi ya jamii kimaendeleo na uchaguzi yakini wa vipaumbele vitakavyoiwezesha jamii kujenga uwezo wa kufikia mafanikio ya pamoja kijamii,” alimaliza taarifa yake Kessy.

Naye Askofu Mkuu Paul Ruzoka, wa Jimbo Kuu la Tabora, akiandika katika dibaji ya kitabu kilichozinduliwa, anasema:

“Mchango wetu katika kuelekea Mchakato wa Kuandaa Dira ya Maendeleo Tanzania Kuelekea 2050, una vishawishi kadhaa: mosi, kushahidia haja ya kuwa na mwendelezo wa kujiwekea Dira yenye malengo dhahiri; pili, kuhimiza nidhamu ya kusimamiana katika kutekeleza kwa dhati tuliyonuia kufikia; tatu, kurejea na hivyo kujikosoa pale ambapo tunaona hatukufanya vizuri ili tuweze kujisahihisha na kuepuka kukosea tena, na; nne, kuwasilisha maono ya vipaumbele vyetu katika mustakabali wa maendeleo ya Taifa na wananchi wake kuelekea mwaka 2050.”

Kanuni ya tafakari za CPT na Chimbuko lake

Profesa Beda Mutagahywa, ni miongoni mwa wanachama waasisi wa CPT, na aliwahi kuwa Mwenyekiti wa CPT. Yeye alitoa maelezo kuhusu chimbuko la CPT na mantiki ya methodolojia ya kuchunguza maisha ya jamii inayotumika hadi leo. Maelezo yake yanafupishwa hapoa chini.

Ndani ya Kanisa Katoliki, kuna vyama vya utume wa walei kama vile Chama cha CPT, Wawata, Viwawa, Rejio Maria, na vyama vingine vya kitume kama hivi, ni watoto tofauti katika familia moja.

Kila chama kina mbinu zake malum za kutekeleza utume wa walei wa kujenga “ufalme wa Mungu” wa haki, utu, usawa, amani na maendeleo, kwa “kuyatakatifuza malimwengu.”

Mwezi huu wa Novemba 2023, chama cha CPT kinaadhimisha miaka 40 tangu kianzishwe, kama chama kingine cha kutekeleza utume wa walei chini ya Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC) lililokipokea rasmi mwaka 1982.

Katika ngazi ya kitaifa, hatua za mwanzo za kuanzishwa kwa CPT zilifanywa na kukundi cha wana TYCS kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam waliohitimu katika miaka ya 1960 na 1970 na kuajiriwa sehemumbalimbali serikalini.

Kikundi cha wahitimu hawa kilizoea kufanya tafakari mbalimbali kuhusu masuala yanayohusu sera za kiuchumi na kijamii kwa kutumia kurunzi ya enjili, michakato hiyo ikiwa inaongozwa na spairo yenye maduara yaliyo na hatua tatu za tafakari, yaani, spairo yenye mizunguko kadhaa ya “Kuona, Kuamua na Kutenda.”

Majadiliano yalijikita kwenye uhusiano unaopaswa kuwepo kati ya Imani ya Kanisa, kwa upande mmoja, na Sera za Serikali kuhusu Ujamaa na Kujitegemea, kwa upande mwingine. Matokeo ya tafakari hizi yalikuwa yanachapishwa kwenye Jarida la wakati huo lililoitwa “Mwamko wa Utu.”

Wanachama waasisi waliohudhuria vikao vya kwanza kati ya 1978 na 1982 vilivyofanyika kwa ajili ya kuunda CPT walikuwa tayari ni waajiriwa serikalini na sekta binafsi.

Leo hii, chama cha CPT kinaunganisha Wakristo wa taaluma mbalimbali zinazotambuliwa kisheria kuanzia ngazi ya cheti, stashahada, shahada ya kwanza, shahada ya uzamili, shahada ya uzamivu nd uprofesa.

Katika ngazi ya kimataifa, vuguvugu la kuasisiwa kwa CPT lilichochewa na Mtaguso Mkuu wa Pili wa Vatikani wa mwaka 1962-1965 ulioleta mwamko na hamasa ya ushiriki wa walei katika kutekeleza utume wa Kanisa kwa kutumia maarifa na stadi za kitaaluma walizo nazo. Mtaguso unawaalika walei kuutakatifuza ulimwengu kwa kutumia kanuni za mafundisho ya Kanisa kuhusu misingi na mbinu za kuboresha maisha ya jamii.

Katika kipindi cha miaka 40, kazi za utume zilizofanywa na CPT zinagusa haki na majukumu katika sekta za uchumi, jamii, siasa, maadili, na uraia. Kazi hizi zimetekelezwa na wanachama wa CPT kwa njia ya machapisho, semina, warsha, makongamano, mijadala ya redioni, na kwa kutoa huduma za kisheria na kitabibu bure.

Mwisho, yatupasa pia kuomba toba kwa makosa tuliyofanya kwa kutojitoa ipasavyo wakati tukitimiza wajibu wa utume. Tunaamini, kupitia msamaha huo tutapata nguvu Zaidi ya kufanya utume kwa namna iliyo bora zaidi.

Profesa Beda alihitimisha maelezo yake kwa kusisitiza kwamba, CPT kama Jumuiya ya Walei Wakristu na Wanataaluma, ni chama chenye majukumu makuu matatu.

Kwanza, kuinjilisha walimwengu kwa vitendo tukitumia kwa ustadi, weledi na uadilifu taaluma na uzoefu wetu.

Pili, kama Wanataaluma wenye uzoefu katika nyanja mbalimbali, tuna wajibu wa kusaidia jamii katika jitihada zake za kutafuta ufumbuzi wa changamoto za maisha wanazokabiliana nazo.

Na tatu, tuna wajibu wa kuibua na kuchokoza mijadala inayolenga, hususan, kuleta mtazamo na mfumo mpya wa utendaji ili kuharakisha kufikia malengo tuliyojiwekea kama nchi au kuboresha malengo yaliyopo na utendaji wake.

“Hii ina maana kwamba vilevile tuna wajibu wa msingi wa kutafuta mbinu za kuinua maendeleo ya Taifa letu na hali za maisha ya wananchi wengi na sio baadhi tu,” alimalizia Profesa Beda.

Mapadre saba waitaka CPT kupanda matumani mahali penye hofu

Tukio la kumbukizi ya miaka 40 ya CPT na uzinduzi wa kitabu maalum lilifunguliwa kwa ibada ya Misa iliyoongozwa na mgeni rasmi, Padre Vitalis Kasembo, ambaye ni Mwenyekiti wa Utume wa Walei Jimbo Kuu la Dar es Salaam. Padre Kasembo alisindikizwa na mapadre wengine sita.

Mapadre hao ni Padre Richard Tiiganya (C.PP.S) kutoka Seminari Kuu ya Segerea, Dar es Salaam; Padre Nicodemus Mayalla kutoka Seminari Kuu ya Segerea, Dar es Salaam; Padre Dkt. Joseph Matumaini kutoka Chuo Kikuu cha SAUT; Padre Justin Ramde ambaye ni Mmisionari wa Afrika anayeishi Atman House, Dar es Salaam; Padre Fulbert Mtunguja (OSB) kutoka Parokia ya Mt. Paul Majengo, Jimbo Katoliki Mtwara; na Padre Vic Missian, Mlezi wa CPT Taifa.

Siku hiyo, mahubiri yalitolewa na Padre Dkt. Joseph Matumaini. Mahubiri yake yaliongozwa na vitabu viwili vya Biblia. Somo la kwanza lilitoka kitabu cha Nabii Ezekiel, sehemu inayoongelea maisha ya Wanaisraeli wakiwa katika giza la utumwa wa Babeli (36:22-28).

Na Somo la pili lilitoka Kitabu cha Enjili ya Luka, sehemu ya Wimbo wa Maria akimtukuza Mungu kwa uamuzi wake wa kuwakomboa wanaisraeli kutoka utumwani (1:46-55).

Kwa kuzingatia maudhui ya masomo haya mawili, Padre Dkt. Joseph Matumaini alisema kwamba kitendo cha Mungu kuwakomboa wanaisraeli kilikuwa ni kitendo cha “kusimika utaratibu mahali penye vurugu.” Hivyo akawahoji maswali mengi wana-CPT:

"Nyie mnao uwezo wa kusimika utaratibu mahali penye vurugu? Mnaweza kupanda maarifa penye ombwe la kimaarifa? Sauti yenu ya unabii inayo nguvu hiyo?

"Machapisho yenu yanawafikia wasomaji au mnayaficha makabatini? Dhima yenu ni kuperemba na kukosoa kazi za wengine pekee au mnashirikiana na wengine katika kutafuta maslahi ya pamoja?

"Mnafanya uwezeshaji kwa wengine katika kutafuta maslahi ya pamoja? Nyie ni waibua ajenda na kisha kubaki watazamaji au mnafuatilia 'movie' hadi mwisho?"

Lakini hakuishia hapo. “Kesho Jumapili tutasikia enjili ya talanta. Basi, mtukuzeni Mungu kwa njia ya vipaji vyenu,” alimaliza homilia Dkt. Matumaini.

Kwaya ya Mtakatifu Don Bosco inayoundwa na wanafunzi wa Chuo cha Usafirishaji (NIT) cha Mabibo, Jijini Dar es Salaam, ndiyo ilitumbuiza wakati wa ibada ya Misa Takatifu. “Tunaamini kwamba, aimbaye vizuri husali mara mbili,” alisema Anthony Shitente, ambaye ni kwayamasta wake.

Na katika sala ya kufunga siku, Padre Kasemba aliwakumbusha CPT kwamba, Kanisa sio chombo cha kusimamia mabadiliko ya kiroho kama maandalizi ya maisha yajayo baada ya kifo cha mwili.

“Badala yake, Kanisa lina jukumu la msingi katika maisha ya kawaida ya watu wenye mwili hai na hasa katika kuboresha ustawi wa jamii,” alisema Padre Kasembo.

Alifafanua kwamba, jukumu hili lilibainishwa rasmi katika Mtaguso Mkuu wa Pili wa Vatikani uliofanyika mwaka 1962-65.

“Na baadaye limefafanuliwa kwa kina katika kitabu cha Mkusanyiko wa Mafundisho ya Kanisa Kuhusu Mbinu Bora za Kuboresha Maisha ya Jamii,” alimalizia Padre Kasembo.

Taarifa hii imeandaliwa na:

Mama Amon
Afisa Mtendaji Mkuu
Dawati la Utafiti la Mama Amon (DUMA)
S.L.P. P/Bag
"Sumbawanga Town"

Sumbawanga.
Okay !
 
Hii Katiba Mpya inapendeza sana inapopigiwa kelele na makundi mengine zaidi ya wanasiasa, ni hitaji la watanganyika la muda mrefu.

Naona sasa huu ni wakati wa makundi mengine nayo kuungana kuidai, kwasababu kuwaachia wanasiasa peke yao inaonekana ni hitaji la kisiasa kwa ajili ya manufaa ya chama fulani cha siasa, jambo ambalo sio kweli.

Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app
Kama TEC wataanza kuzungumzia umuhimu wa Katiba mpya hapo ndio nitajua sasa watu wapo serious na Katiba mpya !
 
Back
Top Bottom