Lowassa and Co., waliteka Bunge; Sitta, Mwakyembe kudhibitiwa

January Makamba alijitafutia Ujiko juzi. Amepewa haki yake lakini sidhani kama atafanya chochote ila kwa maelekezo tu. Lyatonga sidhani kama kuna jipya hapa. Zitto anaweza sana, tunamhitaji.

Kumbe alikuwa ndiyo ameanza kampeni!wanasiasa bwana!they can turn stone into bread,nothing is impossible to them!!
 
lowassa ameshinda uenyekiti kamati ya mambo ya nje.wakati huo huo serukamba amemshinda ANNA KILANGO kwa kura 1 na kuwa mwenyekiti wa miundombinu.zitto ameshinda POC

What do you expect from a Mafia state,ofcourse the opposite of what is expected.Frankly speaking I did not expect anything different.
 
Tunashangaa ameukwaa uenyekiti? 2015 nchi ni yake!!!! Kweli nimekosa pumzi.
 
Kwa wale waijua virefu vya PAC etc.

Types of Parliamentary Committees

Tanzania Parliament possesses an organised system of committees which comprises standing committees and Select Committees.

  1. Finance and Economic Affairs
  2. Public Accounts - John Cheyo
  3. Social Services - Margreth Sitta
  4. Social Welfare & Community Development
  5. Constitutional, Legal and Public Administration
  6. Standing Orders
  7. Parliamentary Privileges, Ethics and Powers
  8. Energy and Minerals - January Makamba
  9. HIV/AIDS Affairs
  10. Infrastructurec - Serukamba
  11. Public Corporation Accounts - Zitto Kabwe
  12. Miscellaneous Amendments
  13. Land, Natural Resources and Environment
  14. Agriculture, Livestock and Water
  15. Foreign Affairs, Defence and Security - Edward Lowassa
  16. Industries and Trade
  17. Local Government Accounts -

EL noma kaanza mchakato jeshini(monduli)! 2015 kazi ipo.
 
DUh EL kiboko.. Kwahiyo ulinzi na usalama vyote kakabidhiwa FISADI?? kazi ipo!!!
 
Kwangu mimi ni mara mia ya kuwa na Cheyo na Lyatonga kuliko Kafulila na Hamad Rashid. Hao wawili kuwadhibti ni rahisi ukizingatia Baraza kivuli lote litatoka CDM
 
lowasa atatawala makaburi yetu mwaka 2015, kamwe hatakuwa rais wa nchi hii damu zetu bado zikizunguka kwenye mishipa ya arti na veins!!!!!!!!!! never never even on our dead bodies
 
What do you expect from a Mafia state,ofcourse the opposite of what is expected.Frankly speaking I did not expect anything different.


Watanzania wenzangu,

Leo tunacheka naomba tujiulize implication na outcome ya huu uteuzi uliofanyika.

1.Yatupasa kutegemea vifo vya gafla kwa watu wetu wengi ambao ni against goverment will.
2. wizi wa madini na fedha za serikali kwa kiasi ambacho hatuwezi kukieleza.

Watu hawa (CCM ) ni watu waliojaa hila kila kunapoitwa leo hawajafanya makosa kumteua Lowassa katika nafasi hii,naamini atakwenda kusimamia mauaji kwa ufasaa zaidi kama yalivyokusudiwa,na kutengeneza njia chafu nyingi za kutuangamiza kwa mauwaji ya kinyama kama alivyo kwisha anza.

Lakini pia Eneo la madini,wapo watu wangependa kuendelea kulinda uwozo wa mikataba mibovu ya madini,ili mradi tu percent yao ya kila siku iendelee kuwapo.

Hali hii ni hali ambayo siyo nzuri inatisha na kuhuzunisha,ni msiba mzito wa kitaifa ambao kila mtu kilio hiki kitamgusa.

Watanzania tuamke na kutoa tafsiri ya haya yote kwani ndani ya mda mdogo mengi twaja kuyashuhudia.


Ee Mungu Nusuru Taifa letu la Tanganyika.
 
Kuchaguliwa kwa Edward Lowassa, waziri mkuu aliyejiuzulu kwa kashfa ya Richmond/Dowans, kuwa mwenyekiti wa the most powerful committee in the National Assembly -- Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama, ina maana kuu zifuatazo:

1. Anajitengenezea CV ya kuwa mgombea Urais wa CCM 2015. Moja ya vigezo vikubwa vya CCM ni mgombea wa Urais kuwa na uzoefu wa mambo ya nje. Hapa Lowassa anajipatia CV hiyo kupitia kamati hii ya Bunge.

2. Akiwa mwenyekiti wa kamati ya mambo ya nje, ulinzi na usalama, atakuwa anapata security briefings na issue zote nyeti, kama Meremeta, rada, Kagoda, usalama wa taifa, Takukuru, polisi, jeshi, nk, vinapitia kwake. Anakuwa na powers ku-summon wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama hapa nchini.

3. Anapata meno ya kumshuhulikia adui wake mkuu kwenye mbio za urais, Waziri wa Mambo ya Nje, Bernard Membe, kwani kamati ya mambo ya nje ndiyo inayosimamia wizara ya Membe. Pia Waziri wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta, naye anakuwa anasimamiwa na kamati hiyo ya Lowassa.

4. Mpambe wa Lowassa, Peter Serukamba, amechaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Miundombinu ili awashuhulikie kina John Magufuli na Dk. Harisson Mwakyembe wa wizara ya ujenzi.

5. Mpambe mwingine wa Lowassa na Rostam Aziz, January Makamba, amechaguliwa kuwa mwenyekiti wa kamati ya nishati na madini ili amfukuze kazi Ngeleja na kumuweka waziri wao mwingine na azime issue za Dowans/Richmond.

6. Zitto Kabwe, ambaye ni mtu wa kina Rostam kabaki kamati ya mashirika ya umma kama kanyaboya. Kamati za PAC na local government wamepewa TLP na UDP ambao ni vibaraka wa CCM kama CUF.

Lowassa, January na Serukamba na wapambe wao wa kamati za upinzani (Zitto, Augustino Mrema, John Cheyo) wanaingia kwenye kamati ya uongozi wa Bunge wakiwa wenyeviti wa kamati za Bunge. Watakuwa na majority vote kwenye kamati ya uongozi wa Bunge. Hii ina maana kuwa watakuwa wana uwezo wa kuamua moja kwa moja shuhuli za Bunge, kanuni, miswada, mwenendo na hoja mbali mbali za Bunge.

Anne Makinda ndiyo aliyewateuwa kina Lowassa, January, Serukamba, etc kuwa kwenye kamati hizi kwa maelekezo ya Rostam Aziz aliyemuweka kuwa Spika. Amewateuwa wajumbe wachovu kwenye kwenye kamati hizi ili watu hawa wakamate uongozi wake.

Ni dhahiri kuwa mafisadi sasa wameliteka Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania!
 
Silipendi lilowassa..natamani apotee kwenye ramani ya tz
Mtu wangu BJ, haya sio mambo usimchukie mtu mpaka kumuita lijitu!. Hebu mfikirie Bwana Wetu Yesu Kristo, aliwasamehe mpaka waliomsulubisha na kusema wasameeni kwa vile hawajui watendalo.

Yote yanayosemwa kuhusu EL ni tuhuma tuu, kwa sisi tunaomjua in person ni mtu mwenye utu, mwenye huruma, mpenda haki, mtetezi wa wanyonge and besides all, ni mchapakazi wa ukweli. Mimi nampenda na silazimishi umpende ila usimchukie. Chuki ni moja ya vitendea kazi vya shetani!?
 
Kuna umuhimu wa kutoa elimu ya jinsi ya kujitoa muhanga some people are supposed to be dead ..hakuna maelezo ambayo unaweza ukamwambia mtu akakuelewa ....how come EL ?
 
Yaani ni upuuzi kwenda mbele. Pamoja na kelele zote hizi hawa wabunge wanampa post EL? hawa ni wa kuwazomea wakipita mitaani mpaka waelewe kuwa hatuwathamini tena kama wawakilishi wetu (namaanisha wale wa chama twawala)

Kwa taarifa yako asilimia kubwa ya wabunge wamefadhiliwa na Lowasa na RA. Baada ya kuiteka NEC ya CCM kipindi hiki walitaka kuliteka bunge kutokana na jinsi lile la 19 lilivyowaadhibu.
 
Back
Top Bottom