Frank Wanjiru

JF-Expert Member
Apr 12, 2012
21,838
38,729
Edward Ngoyai Lowasa ameondoka. Yuko mahali salama pasipo na mgao wa umeme wala usanii wa treni za umeme. Amepumzika baada ya kazi ngumu. Anapokufa mtu mzito kama Lowassa, kuna makundi matatu hujitokeza;
1. Wanaolia
2. Wanaofurahia
3. Wasiojua kama walie au wafurahie.

Makundi yote matatu tunayo katika kifo cha Edward Lowasa. Mimi sijui nipo kundi gani lakini niseme mambo manne ninayokumbuka:

1. Dola yetu ina mihimili mitatu: Bunge, serikali na mahakama. Lakini Lowassa alisababisha kuzaliwa kwa mihimili mitatu ndani ya mhimili wa bunge:
  • Wa kwanza ni Spika Samwel Sitta
  • Wa pili ni Wabunge mitume wakiongozwa na Mwakyembe
  • Mhimili wa 3 ulikua Edward Lowasa mwenyewe.
Hakika Bunge la 9 halitasahaulika kwa WEMA na UBAYA wake.

2. Alikuwa mtetezi asiye na mtetezi. Alikitetea chama chake, kikamtelekeza. Alimtetea Rais wake akamsaliti. Aliitetea nchi lakini nchi ikawatetea watesi wake.

3. Aliwapenda Wamasai, lakini Watesi wake wakamchonganisha na Wamasai. Wakahoji umasai wake na kudai Lowassa ni Mmeru. Lakini upendo wake kwa Wamasai ukawa na nguvu kuliko fitina za watesi wake. Akiwa hai na akiwa maiti Edward amebaki kuwa Mmasai.

4. Alisalitiwa na wengi aliowasaidia. Baada ya kumtumia kwa maslahi yao na kumtelekeza alibaki na Regina. Tujifunze kujali familia zetu. Mwisho wa yote, mzigo unabebwa na familia. Mambo ya “Pengo halitazibika” ni ulaghai mtupu. Kufa uone watakavyoziba pengo hata kabla ya mazishi.

LOWASSA KATIKA UBINADAMU WAKE:
A. Aliwaamini watu kuliko walivyomuamini.

B. Aliuchukia umaskini kwa vitendo. Watesi wake wakatumia hoja hii kumchonganisha na wananchi maskini. Wakasahau kuwa hata maskini wanauchukia umaskini wao na wanatamani kutoka.

C. Aliamini uzalendo si umaskini. Unaweza kuwa tajiri na ukawa mzalendo.

D. Alitumikia vyama 2 vikubwa. Vikamchafua na kumsafisha. Vikambeza na kumtukuza. Ameondoka akiwa mshindi kwa vyama vyote viwili.

E. Ameishi duniani miaka 70. Lakini Historia yake ni ndefu kuliko miaka yake. Ni mfupi wa umri lakini mrefu wa historia. Nenda Edward. Pole kwa Mama Regina, Watoto na wajukuu.!
 
Kwa kweli ilikua huzuni kipindi cha 2006-2010 hapo ukisoma gazeti la Mwanahalisi ulitamani ufe sababu tuliaamini umaskin wetu umeletwa na akina Lowasa kumbe ni Chama Cha Mapinduzi, tulimchukia bure , nilikuja kumpenda badae kwa sababu alisema mwenye ushahidi apeleke mahakamani hakuna aliyepeleka wala kukamatwa hata Magufuli aliyetesa watu alishindwa kumfunga.
Lowasa ni msindi
Lowasa ni bingwa wa vita
Lowasa ni bingwa wa uvumilivu
 
Edward Ngoyai Lowasa ameondoka. Yuko mahali salama pasipo na mgao wa umeme wala usanii wa treni za umeme. Amepumzika baada ya kazi ngumu. Anapokufa mtu mzito kama Lowassa, kuna makundi matatu hujitokeza;
1. Wanaolia
2. Wanaofurahia
3. Wasiojua kama walie au wafurahie.

Makundi yote matatu tunayo katika kifo cha Edward Lowasa. Mimi sijui nipo kundi gani lakini niseme mambo manne ninayokumbuka:

1. Dola yetu ina mihimili mitatu: Bunge, serikali na mahakama. Lakini Lowassa alisababisha kuzaliwa kwa mihimili mitatu ndani ya mhimili wa bunge:
  • Wa kwanza ni Spika Samwel Sitta
  • Wa pili ni Wabunge mitume wakiongozwa na Mwakyembe
  • Mhimili wa 3 ulikua Edward Lowasa mwenyewe.
Hakika Bunge la 9 halitasahaulika kwa WEMA na UBAYA wake.

2. Alikuwa mtetezi asiye na mtetezi. Alikitetea chama chake, kikamtelekeza. Alimtetea Rais wake akamsaliti. Aliitetea nchi lakini nchi ikawatetea watesi wake.

3. Aliwapenda Wamasai, lakini Watesi wake wakamchonganisha na Wamasai. Wakahoji umasai wake na kudai Lowassa ni Mmeru. Lakini upendo wake kwa Wamasai ukawa na nguvu kuliko fitina za watesi wake. Akiwa hai na akiwa maiti Edward amebaki kuwa Mmasai.

4. Alisalitiwa na wengi aliowasaidia. Baada ya kumtumia kwa maslahi yao na kumtelekeza alibaki na Regina. Tujifunze kujali familia zetu. Mwisho wa yote, mzigo unabebwa na familia. Mambo ya “Pengo halitazibika” ni ulaghai mtupu. Kufa uone watakavyoziba pengo hata kabla ya mazishi.

LOWASSA KATIKA UBINADAMU WAKE:
A. Aliwaamini watu kuliko walivyomuamini.

B. Aliuchukia umaskini kwa vitendo. Watesi wake wakatumia hoja hii kumchonganisha na wananchi maskini. Wakasahau kuwa hata maskini wanauchukia umaskini wao na wanatamani kutoka.

C. Aliamini uzalendo si umaskini. Unaweza kuwa tajiri na ukawa mzalendo.

D. Alitumikia vyama 2 vikubwa. Vikamchafua na kumsafisha. Vikambeza na kumtukuza. Ameondoka akiwa mshindi kwa vyama vyote viwili.

E. Ameishi duniani miaka 70. Lakini Historia yake ni ndefu kuliko miaka yake. Ni mfupi wa umri lakini mrefu wa historia. Nenda Edward. Pole kwa Mama Regina, Watoto na wajukuu.!
Hata mm sijui nilie au nisilie.. Neno pengo halizibiki ni ulaghai mtupu kufa uone kama pengo lako litakavyozibwa haraka
Bagonza na nyundo yake kwenye wanafiki wengi
 
Leo ndio nimejua hakuna ulazima wala kidini kumfunua marehemu na watu kupita kumuangalia
Familia hii imeonyesha Dini haswa inavyotaka
Mbadilike sasa mmefunguliwa macho maana wengi walikuwa wanajua ni lazima kumuanika ila mnaweza kutufafanulia zaidi
Screenshot_20240214_122129_Instagram~2.png
 
Lowasa ni msindi
Lowasa ni bingwa wa vita
Lowasa ni bingwa wa uvumilivu
Hizi ni sifa za kinafiki. Ushindi gani kaupata ktk vita hii ya wasaliti wakati mhe. Chegeni amesema Lowasa angeuahi zaidi asingepata ajali za kisiasa??

Hii maana yake afya yake imetetereka kutokana na usaliti aliyofanyiwa.
 
Edward Ngoyai Lowasa ameondoka. Yuko mahali salama pasipo na mgao wa umeme wala usanii wa treni za umeme. Amepumzika baada ya kazi ngumu. Anapokufa mtu mzito kama Lowassa, kuna makundi matatu hujitokeza;
1. Wanaolia
2. Wanaofurahia
3. Wasiojua kama walie au wafurahie.

Makundi yote matatu tunayo katika kifo cha Edward Lowasa. Mimi sijui nipo kundi gani lakini niseme mambo manne ninayokumbuka:

1. Dola yetu ina mihimili mitatu: Bunge, serikali na mahakama. Lakini Lowassa alisababisha kuzaliwa kwa mihimili mitatu ndani ya mhimili wa bunge:
  • Wa kwanza ni Spika Samwel Sitta
  • Wa pili ni Wabunge mitume wakiongozwa na Mwakyembe
  • Mhimili wa 3 ulikua Edward Lowasa mwenyewe.
Hakika Bunge la 9 halitasahaulika kwa WEMA na UBAYA wake.

2. Alikuwa mtetezi asiye na mtetezi. Alikitetea chama chake, kikamtelekeza. Alimtetea Rais wake akamsaliti. Aliitetea nchi lakini nchi ikawatetea watesi wake.

3. Aliwapenda Wamasai, lakini Watesi wake wakamchonganisha na Wamasai. Wakahoji umasai wake na kudai Lowassa ni Mmeru. Lakini upendo wake kwa Wamasai ukawa na nguvu kuliko fitina za watesi wake. Akiwa hai na akiwa maiti Edward amebaki kuwa Mmasai.

4. Alisalitiwa na wengi aliowasaidia. Baada ya kumtumia kwa maslahi yao na kumtelekeza alibaki na Regina. Tujifunze kujali familia zetu. Mwisho wa yote, mzigo unabebwa na familia. Mambo ya “Pengo halitazibika” ni ulaghai mtupu. Kufa uone watakavyoziba pengo hata kabla ya mazishi.

LOWASSA KATIKA UBINADAMU WAKE:
A. Aliwaamini watu kuliko walivyomuamini.

B. Aliuchukia umaskini kwa vitendo. Watesi wake wakatumia hoja hii kumchonganisha na wananchi maskini. Wakasahau kuwa hata maskini wanauchukia umaskini wao na wanatamani kutoka.

C. Aliamini uzalendo si umaskini. Unaweza kuwa tajiri na ukawa mzalendo.

D. Alitumikia vyama 2 vikubwa. Vikamchafua na kumsafisha. Vikambeza na kumtukuza. Ameondoka akiwa mshindi kwa vyama vyote viwili.

E. Ameishi duniani miaka 70. Lakini Historia yake ni ndefu kuliko miaka yake. Ni mfupi wa umri lakini mrefu wa historia. Nenda Edward. Pole kwa Mama Regina, Watoto na wajukuu.!
Ukisoma passage ya lucas unaona kabisaa Chanzo Cha Matatizo wamefurahia kuondoka kwa jamaa
 
Ukiona familia inakataa kumfunua mpendwa wao jua kaisha sana(kaumwa kipindi kirefu mno)Mtamsimanga hali itakayoiumiza familia
Leo ndio nimejua hakuna ulazima wala kidini kumfunua marehemu na watu kupita kumuangalia
Familia hii imeonyesha Dini haswa inavyotaka
Mbadilike sasa mmefunguliwa macho maana wengi walikuwa wanajua ni lazima kumuanika ila mnaweza kutufafanulia zaidi View attachment 2903846
 
Back
Top Bottom