Lowassa and Co., waliteka Bunge; Sitta, Mwakyembe kudhibitiwa

so???? sasa sisi tufanyeje wamchague na HAMAD kuwa kiongozi wa Upinzani basi yaishe
 
Kama kweli kachaguliwa nilikuwa nategemea hilo maana CCM walikuwa wamekwishapanga nani akae wapi na kwa maslahi yapi ndio maana ikakubalika kubadilisha kanuni,tunasubiri tuone Hamad Rashid nae atapewa kamati gani.
 
so puppet cheyo has got it finally!!

Hizo zingine wampe hamad na kafulila, ccm wasidhani wamefanya lolote la maana hapo, we are watching closely hata wakizima umeme 24 hrs ili tusijue yanayojiri huko tunawafuatilia sana.... Shame on politicians who depend on the system to oppress what is right.
 
Muda mfupi uliopita CHEYO WA UDP Amechaguliwa kuongoza kamati ya PAC.

Kafulila, Cheyo, Hamad wanayumbisha upinzani kwa sababu majimboni kwao wananchi huwa hawachagui chama ---wanachagua mtu.

Let's take note of all thise shit.

CCM will pay more price in 2015.

Enzi za ufala kwa Watanzania zilishapita.

Kila wanachofanya CCM na washirika wao tunajua kama ni dhambi ama haki.

Wanachofanya sasa ni dhambi, na Mshahara wa dhambi ni Mauti.
 
amechaguliwa its comfermed.utata upo LAC ambapo lyatonga na kafulila walionyesha kugombea. POC wanaendelea na uchaguzi ZITTO Anagombea
 
Lowassa ameshinda uenyekiti kamati ya mambo ya nje. Wakati huo huo Serukamba amemshinda ANNA KILANGO kwa kura 1 na kuwa mwenyekiti wa miundombinu. Zitto ameshinda POC

ZAIDI wasome wakuu Fareed na Kagemro hapa chini:

Kuchaguliwa kwa Edward Lowassa, waziri mkuu aliyejiuzulu kwa kashfa ya Richmond/Dowans, kuwa mwenyekiti wa the most powerful committee in the National Assembly -- Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama, ina maana kuu zifuatazo:

1. Anajitengenezea CV ya kuwa mgombea Urais wa CCM 2015. Moja ya vigezo vikubwa vya CCM ni mgombea wa Urais kuwa na uzoefu wa mambo ya nje. Hapa Lowassa anajipatia CV hiyo kupitia kamati hii ya Bunge.


2. Akiwa mwenyekiti wa kamati ya mambo ya nje, ulinzi na usalama, atakuwa anapata security briefings na issue zote nyeti, kama Meremeta, rada, Kagoda, usalama wa taifa, Takukuru, polisi, jeshi, nk, vinapitia kwake. Anakuwa na powers ku-summon wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama hapa nchini.


3. Anapata meno ya kumshuhulikia adui wake mkuu kwenye mbio za urais, Waziri wa Mambo ya Nje, Bernard Membe, kwani kamati ya mambo ya nje ndiyo inayosimamia wizara ya Membe. Pia Waziri wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta, naye anakuwa anasimamiwa na kamati hiyo ya Lowassa.


4. Mpambe wa Lowassa, Peter Serukamba, amechaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Miundombinu ili awashuhulikie kina John Magufuli na Dk. Harisson Mwakyembe wa wizara ya ujenzi.


5. Mpambe mwingine wa Lowassa na Rostam Aziz, January Makamba, amechaguliwa kuwa mwenyekiti wa kamati ya nishati na madini ili amfukuze kazi Ngeleja na kumuweka waziri wao mwingine na azime issue za Dowans/Richmond.


6. Zitto Kabwe, ambaye ni mtu wa kina Rostam kabaki kamati ya mashirika ya umma kama kanyaboya. Kamati za PAC na local government wamepewa TLP na UDP ambao ni vibaraka wa CCM kama CUF.


Lowassa, January na Serukamba na wapambe wao wa kamati za upinzani (Zitto, Augustino Mrema, John Cheyo) wanaingia kwenye kamati ya uongozi wa Bunge wakiwa wenyeviti wa kamati za Bunge. Watakuwa na majority vote kwenye kamati ya uongozi wa Bunge. Hii ina maana kuwa watakuwa wana uwezo wa kuamua moja kwa moja shuhuli za Bunge, kanuni, miswada, mwenendo na hoja mbali mbali za Bunge.


Anne Makinda ndiyo aliyewateuwa kina Lowassa, January, Serukamba, etc kuwa kwenye kamati hizi kwa maelekezo ya Rostam Aziz aliyemuweka kuwa Spika. Amewateuwa wajumbe wachovu kwenye kwenye kamati hizi ili watu hawa wakamate uongozi wake.


Ni dhahiri kuwa mafisadi sasa wameliteka Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania!

NDUGU ZANGU NIMESTUSHWA SANA NA HAYA JAPO NILIYATEGEMEA LAKINI SI KWA KIWANGO HIKI,(Hii ni kambi ya watu wanaomuunga mkono Lowasa.)

BUNGE LIMETEKWA!

Kutokana na mambo ambayo leo yametokea mjini Dododma ni dhahiri kuwa kumekuwa na mapinduzi ya wazi ya kuliteka Bunge letu na kuanzia sasa litakuwa halina nguvu tena za kuwawajibisha mafisadi wala hakutakuwa na mtu wa kuzungumza lolote juu ya Mafisadi na ufisadi.

Nayasema haya kutokana na mambo yafuatayo;

1. Uchaguzi wa wenyeviti wa kamati za kudumu za Bunge ni kama ifuatavyo;

(i) Mwenyekiti wa kamati ya fedha na uchumi ni Abdallah Kigoda
(ii) Mwenyekiti wa kamati ya katiba, sheria na utawala ni Pindi Chana
(iii) Mwenyekiti wa kamati ya mambo ya nje, Ulinzi na Usalama ni Edward Nyoyai Lowassa
(iv) Mwenyekiti wa kamati ya huduma za jamii ni Magreth Sitta
(v) Mwenyekiti wa kamati ya maendeleo ya jamii ni Jenista Mhagama
(vi) Mwenyekiti wa kamati ya ardhi, maliasili na mazingira ni ………….
(vii) Mwenyekiti wa kamati ya kilimo,mifugo na maji ni Prof.David Mwakyusa
(viii) Mwenyekiti wa kamati ya Miundombinu ni Peter Serukamba.
(ix Mwenyekiti kamati ya hesabu za za serikali za mitaa ni Augustino Mrema.
(x) Mwenyekiti wa kamati ya hesabu za mashirika ya umma ni Zitto Kabwe
(xi) Mwenyekiti wa kamati ya heswabu za serikali ni John Momose Cheyo.
(xii)Mwenyekiti wa kamati ya viwanda na Biashara ni Mahamoud
(xiii) Mwenyekiti wa kamati ya nishati na madini ni January Makamba.

Baada ya kuwaangalia wenyeviti hao ni kuwa kamati ya uongozi ya Bunge huwa ina wajumbe ambao ni wenyeviti wote kamati za kudumu pamoja na wafuatao;

(i) Spika – Anne Makinda
(ii) Naibu Spika- Job Ndugai
(iii) Kiongozi wa Upinzani- Freeman Mbowe.
(iv) Mwanasheria Mkuu wa Serikali - Fredrick Werema
(v) Waziri wa Nchi Bunge na uratibu - Willium Lukuvi.

Hivyo basi utaona kuwa kamati ya uongozi ya Bunge ambayo ina wajumbe 18 .

Kazi za kamati ya uongozi ya Bunge ni;

(i) Kuendesha bunge siku hadi siku
(ii) Kuamua ni hoja gani zipelekwe Bungeni kujadiliwa
(iii) Kuamua nini kifanywe na Bunge na nini kisifanywe na Spika huwa ni msemaji wake wakishaamua .

Hivyo basi kati ya wajumbe 18 wa kamati ya uongozi ambayo kimsingi ndio Bunge lenyewe utaona kuwa Edward Lowassa amejigeuza na kuwa yeye ndiiye atakuwa anafanya maamuzi yote ndani ya Bunge na kuamua lipi lifanyike na lipi lisifanyike kwani wajumbe 13 wanamuunga mkono yeye ama ni watu wake. hao ni pamoja na ;

(i) Lowassa
(ii) Cheyo
(iii) Serukamba
(iv) January
(v) Pindi Chana
(vi) Jenister
(vii) Mrema
(viii) Zitto
(ix) Makinda​
(x) Ndugai
(xi Lukuvi
(xii) Werema
(xiii) Mahamoud – huyu ni mbunge wa Kilwa Kasikazini.


Hivyo utaona jinsi Bunge lilivyotekwa. Lowassa ataweza kufanya yafuatayo;

(i) Kumuita Membe na kumpa maelekezo ya kibunge
(ii) Kumuita Sitta na kumpa maelekezo
(iii) Kuita upya hoja ya Richmond kupitia January
(iv) Kumuita Magufuli na Mwakyembe kupitia Serukamba
(v) Kumuita IGP, DG-TIS kumpa briefing kama mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama.

Hivyo hii inaonyesha kuwa tutakuwa na Bunge la kumi la aina gani.

Yafaa kila mmoja akatafakari na kuchukua hatua nini kifuate baada ya hapo.
 
lowassa ameshinda uenyekiti kamati ya mambo ya nje.wakati huo huo serukamba amemshinda ANNA KILANGO kwa kura 1 na kuwa mwenyekiti wa miundombinu.zitto ameshinda POC

it is just the begining of his come back.......
 
halafu mnasema mna wabunge wa kutumikia wananchi kweli? How the hell did they give EL that post? Its absurdy, absurdy.. Absurdy!!!
 
Back
Top Bottom