Kyela 2010: Mwakyembe Vs Mwakalinga kupitia CCM

Mkuu tunaomba wasifu wa Mwakalinga tafahdhali

Mchapakazi, mtiifu, mwenye mapenzi mema na nchi yake na wananchi kwa ujumla,anayependa kukosolewa na kujifunza,msikivu,mpenda maendeleo ya wezao na chachu ya maendeleo ya jirani(nenda kyela ukaone na usikie).

Mwenye miono mipana nia madhubuti ktk ujenzi ,zero tolarence kwa maovu .nk

Kama akaamuwa kugombea mimi nitakuwa bega kwa bega naye.Ukitaka ushahidi zaidi funga safari uende kyela vinginevyo sito prove hapa.
 
MkamaP amepata wasiwasi niliposema Mzumbe chuo cha kilimo na mifugo. Enzi hizo Katika chuo kikuu cha Dsm kuna watu walikuwa wanachukua course ya Angricultural Enginearing kwa miaka 4. Miaka 2 ya kwanza walikuwa wanafanyia UDSM na mingine 2 Mzumbe. Sawa mkuu?

Bado kidogo nieleweshe SOKOINE (leo SUA) ama Mzumbe?
 
Jamani imeshathibitika kuwa Mwakalinga hayupo Kyela basi tunaomba mods ufunge thread kisha toa adhabu kali kwa aliye ileta hii thread kwa kulejea kuwa Mwakalinga ni member hapa JF moja kwa moja huyu member wetu anaweza undiwa zengwe na chuki bila sababu huko aliko sasa mkoa wa Arusha kama sikosei mods kazi kwenu.
 
Hebu tupatieni wasifu wa huyu mheshimiwa mtarajiwa. Mimi namfahamu mtu mmoja anaiywa George Ambwene Mwakalinga. Lisoma rungwe secondary, Tambaza High School, Mzumbe chuo cha Kilimo na mifugo, UDSM kabla ya Kutimkia Bulgaria. Je ndiyo huyu?

Nimeambiwa ndo yeye ila sio BULGARIA bali ni POLAND na mwisho UK shule na kazi.Sasa mzee we ndo tupe wasifuu wake maana unaonekama unamwelewa vizuri

soma hapo chini
George Ambwene - Graduates.com - Reuniting School Friends Around the World. -- alumni classmates reunion high school college university.
 
Nimefanikiwa kuongea na Mwakalinga ambaye yupo Tanzania kwa mapumziko na ameshtuka kusikia haya, kwa kifupi anasema SI KWELI na yeye yupo Tanzania kwa ajili ya mapumziko na familia yake.

Anasema ni maneno ya kutungwa yasiyo na ukweli wowote na anashauri hoja ifungwe kwakuwa kathibitisha kwa kauli yake kuwa hana mpango wa kugombea Kyela.

Kwa sasa yupo Arusha.
 
Mwakalinga ni mwenzetu hivyo ni bora kuliko Mwakyembe.

Kanda2,

Acha politics na kutoa genela statements. Kuja wana JF wengi wameomba kuelezwa ubora wa Mwakalinga uko wapi hamsemi. Kwa wengi hatumfahamu mwageni data. Kumbuka JF IS A HOME OF CREATIVE THINKERS SO WE NEED SENSIBLE ARGUMENTS!. mWAGA DATA WANA KYELA TUPIME WENYEWE NA SI KUTULAZIMISHA.
 
Ndio atagombea kwani vipi?teeeeeeeeeeeeeee..Hizi kamati za ufundi zinasaidia,nasikia kamati ya ufundi ya Mwakalinga imesema nenda kwanza Arusha.Wapambe wa dr.wakakimbia kyela ,mwakalinga hayupo.
bwana weee na anayetafuta CV yake si nendeni google tuu?heee bwana kamati ya ufundi imefanya kweli...kwanza Arusha na baadaye kyela and then tangaza kugombea...heee bwana we DR. chali...maana nyie sela zenu ni ufisadi, lowassa , RA
 
Mods fungeni mjadala maana habari imesha potoshwa si ukweli imetiwa chumvi nyingi mno hata kusoma ni chungu.
 
Mwanachama Mwandamizi wa Jamii FORUM ambaye anaishi Uingereza Bwana Mwakalinga ametangaza rasmi nia yake ya kugombea ubunge jimbo la Kyela 2010.

Kwa Mwakyembe moto!

*Mpizani wake Uchaguzi Mkuu 2010 ajitangaza
*Ni Mtanzania mtaalamu wa kompyuta anaishi Uingereza

Monday, 03 August 2009 07:27

Na Israel Mwaisaka, Kyela

MWANACHAMA mmoja wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) anayefanya kazi nchini Uingereza Bw. George Mwakalinga ametangaza rasmi nia yake ya kugombea ubunge Jimbo la Kyela kwenye Uchaguzi Mkuu ujao wa 2010

Akizungumza na gazeti hili juzi, Bw. Mwakalinga, alisema ameamua kuweka wazi nia yake baada ya kuona Jimbo la Kyela linazidi kudorora kimaendeleo kama yatima asiye na mlezi.

Alisema Chama Cha Mapinduzi wilayani Kyela katika kipindi chote cha awamu hii, kimekumbwa migogoro mikubwa ambayo imeathiri kwa kiasi kikubwa ukuaji maendeleo kutokana na viongozi kuelekeza nguvu zao katika suala hilo.

Alisema hali hiyo imekuwa ikiendelea hivyo kuzidi kupoteza matumaini ya wananchi wa jimbo hilo ndio maana ameamua kuchukua fomu ya kugombea nafasi hiyo muda utakapofika.

Bw. Mwakalinga alidai kuwa Wilaya Kyela imekuwa na huduma hafifu zitolewazo na Serikali zikiwemo za afya, elimu na kilimo kisichokuwa na tija kwa wananchi na ubadhilifu wa fedha za umma mambo ambayo yametokana na kukosekana usimamizi wa kutosha kiuongozi.

Alisema kutokana na uzoefu wake wa uongozi na kufanya kazi mbalimbali barani Ulaya na elimu aliyonayo, anaamini kuwa ataweza kusimamia maendeleo ya wananchi wa Wilaya Kyela na kuhakikisha matabaka yaliyopo sasa kisiasa ndani ya CCM, yanakwisha.

Alisema binafsi mbali ya kuwa na kazi nzuri nchini Uingereza ameamua kuiacha na kurudi nyumbani ili kuwaendeleza watu wa Kyela baada ya kubaini mapungufu mengi yanayosababishwa na kukosekana uongozi thabiti kutokana na migogoro.

Alisema uzoefu wake kiuongozi alioupata ndani na nje utasaidia kwa kiasi kikubwa kufikia malengo yake ya kuwatumikia wananchi wa Kyela kwa kiwango kinachotakiwa na kuwaondolea kero ambazo zimekuwa 'donda ndugu' lisilopona

Alisema kutokana na huduma duni za afya wananchi wengi wamekuwa wakilazimika kukimbilia wilaya jirani ya Rungwe kupata huduma hizo.

Kazi alizowahi kufanya Bw. Mwakalinga nchini Uingereza ni pamoja na kuwa Mhazini wa Jumuia ya Watanzania Waishio Nje ya Nchi (Tanzanet) kwa muda wa miaka 4 na kuwa mmoja wa wanachama waanzilishi na mdhamini wa mtandao wa Jamii Forum.

Bw. Mwakalinga ambaye ni mtaalamu mwandamizi wa kompyuta na simu ana shahada ya pili ya Sayansi ya Kompyuta aliyoipatia katika Chuo Kikuu cha Wroelaw nchini Poland pia ni mtaalamu ya Biashara.

Jimbo la Kyela hivi sasa lipo chini Mbunge wake Dkt. Harrison Mwakyembe ambaye amejipatia umaarufu mkubwa kutokana na msimamo wake katika kupambana na ufisadi.

Chati ya mwanasiasa huyo msomi wa sheria aliyebobea, ilipanda zaidi pale alipoteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Kamati Teule ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania iliyochunguza kashfa ya mkataba kati ya Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) na Kampuni ya Kufua Umeme wa dharura ya Richond LLC, ambayo ilisababisha mawaziri watatu wa Serikali kujiuzulu.

Mbali ya kujiuzulu mawaziri hao akiwemo, aliyekuwa Waziri Mkuu, Bw. Edward Lowassa, aliyekuwa Waziri wa Nishari na Madini Bw. Mustafa Karamagi na aliyekuwa Waziri wa Wizara ya Afrika Mashariki, Dkt. Ibrahim Msabaha, 'mzimu' wa Richmond bado 'umeikaba koo' Serikali baada ya Bunge mwishoni mwa wiki kukataa Taarifa ya Utekelezaji wa Maazimio ya Bunge kuhusu sakata hilo na kutaka iwasilishwe upya kwenye Mkutano wa 17 wa Bunge, Novemba mwaka huu.

habari kamili someni gazeti la Majira.co.tz.
 
Last edited by a moderator:
Mwanachama Mwandamizi wa Jamii FORUM ambaye anaishi Uingereza Bwana Mwakalinga ametangaza rasmi nia yake ya kugombea ubunge jimbo la Kyela 2010.

shime tumuunge mkono mwenzetu kwani yeye ni mwanachama muanzilishi na mdhamini wa JF.

habari kamili someni gazeti la Majira.co.tz.
thanks mkuu....jamaa kama msanii msanii hivi mara alikataa mara katangaza vipi tumuelewe elewe vipi?
huyu ana uzoefu mkubwa sana huko UK eeh?
Kazi alizowahi kufanya Bw. Mwakalinga nchini Uingereza ni pamoja na kuwa Mhazini wa Jumuia ya Watanzania Waishio Nje ya Nchi (Tanzanet) kwa muda wa miaka 4
lol kazi kweli kweli huko kyela kama kichwa ndio hiki lazima wana kyela wafulie....

na kuwa mmoja wa wanachama waanzilishi na mdhamini wa mtandao wa Jamii Forum.
wow!
Bw. Mwakalinga ambaye ni mtaalamu mwandamizi wa kompyuta na simu ana shahada ya pili ya Sayansi ya Kompyuta aliyoipatia katika Chuo Kikuu cha Wroelaw nchini Poland pia ni mtaalamu ya Biashara.
kutokana na uzoefu wake wa kuwa mhazini wa tanzanet inaelekea hata hii degree yake ya computer hajaifanyia kazi.....na sasa anarukia kwenye siasa....jamaa dizaini namna gani vile.....

huyu jamaa aje atueleze sera zake hapa hatutaki wana kyela wafulie....sisemi dr harison awe mbunge wa maisha kyela lakini mwakalinga aanonekana ni mweupe sana.....
 
Ni habari nzuri na kufurahiwa.

Tupo pamoja katika kutaka kuleta mageuzi ya kisiasa Tanzania.
 
thanks mkuu....jamaa kama msanii msanii hivi mara alikataa mara katangaza vipi tumuelewe elewe vipi?
huyu ana uzoefu mkubwa sana huko UK eeh?

lol kazi kweli kweli huko kyela kama kichwa ndio hiki lazima wana kyela wafulie....

wow!

kutokana na uzoefu wake wa kuwa mhazini wa tanzanet inaelekea hata hii degree yake ya computer hajaifanyia kazi.....na sasa anarukia kwenye siasa....jamaa dizaini namna gani vile.....

huyu jamaa aje atueleze sera zake hapa hatutaki wana kyela wafulie....sisemi dr harison awe mbunge wa maisha kyela lakini mwakalinga aanonekana ni mweupe sana.....

Mkuu, lakini unamfahamu vizuri huyu mwanachama mwenzetu au unahitaji maelezo zaidi kuhusu yeye?

Jaribu kuwa "responsible" katika haya ulioandika.
 
pitieni na habari kuu ya Tanzania Daima kuhusu Kyela inaonekana Mwakalinga amejipanga vizuri.
nadhani wana JF wajitokeze kwa wingi Yebo yebo,Mwanakijiji, kada mpinzani,GT kachukueni majimbo.
 
Mkuu, lakini unamfahamu vizuri huyu mwanachama mwenzetu au unahitaji maelezo zaidi kuhusu yeye?

Jaribu kuwa "responsible" katika haya ulioandika.
mkuu nimefata maelezo alionukuliwa na gazeti la majira.....jamaa atakuwa msanii tu kama wengine tuliowazoea...alimwambia maxence maneno haya
Maxence Melo
user_online.gif

Maxence Melo :A friend to everyone
JF Founder
Join Date: Mon Mar 2006
Location: Dar es Salaam
Posts: 1,768
Thanks: 377
Thanked 896 Times in 322 Posts
Rep Power: 100000
reputation_pos.gif
reputation_pos.gif
reputation_pos.gif
reputation_pos.gif
reputation_pos.gif
reputation_highpos.gif
reputation_highpos.gif
reputation_highpos.gif
reputation_highpos.gif
reputation_highpos.gif
reputation_highpos.gif

Credits: 965,629,550

icon1.gif
Re: Mwakalinga Awasili Kyela Kumuangusha Dr Mwakyembe
Nimefanikiwa kuongea na Mwakalinga ambaye yupo Tanzania kwa mapumziko na ameshtuka kusikia haya, kwa kifupi anasema SI KWELI na yeye yupo Tanzania kwa ajili ya mapumziko na familia yake.

Anasema ni maneno ya kutungwa yasiyo na ukweli wowote na anashauri hoja ifungwe kwakuwa kathibitisha kwa kauli yake kuwa hana mpango wa kugombea Kyela.

Kwa sasa yupo Arusha.

leo kaibuka na kutaka kuingia mjengoni sina tatizo na hilo.....huyu mzoefu wa kuwa mhazini wa tanzanet anaweza ku solve matatzio ya wana kyela kama alivyosema mwenyewe kuwa wana kyela wana matatizo makubwa....
 
MOD umeondoa kichwa cha habari nilichoweka.nilipenda iwe Mwanajf sio Mwakalinga kwani mwenyewe kakiri kuwa ni Mwanajamii forum.
 
Jaribu kuwa "responsible" katika haya ulioandika.
mkuu soma alichokisema unless aseme tena hakuwa yeye..

Bw. Mwakalinga alidai kuwa Wilaya Kyela imekuwa na huduma hafifu zitolewazo na Serikali zikiwemo za afya, elimu na kilimo kisichokuwa na tija kwa wananchi na ubadhilifu wa fedha za umma mambo ambayo yametokana na kukosekana usimamizi wa kutosha kiuongozi.
mheshimiwa mwakalinga kawasaidia nini wana kyela mpaka sasa...maana nijuavyo kuleta maendeleo sio lazima uwe mbunge,mkurugenzi au waziri.....yeye keshawafanyia nini wana kyela?
 
MOD umeondoa kichwa cha habari nilichoweka.nilipenda iwe Mwanajf sio Mwakalinga kwani mwenyewe kakiri kuwa ni Mwanajamii forum.

Hawa ma mods waqchemfu sana wakati mwingine. Kila mtu anamjua huyo mtu kuwa ndio Mtanzania sasa wamefuta post yangu sijui kwa nini.
 
Back
Top Bottom