Malafyale
JF-Expert Member
- Aug 11, 2008
- 13,813
- 11,126
George Mwakalinga mwana Kyela aliyekuwa anaishi na kufanya kazi kama mtaalaum wa kompyuta nchini UK amewasili Kyela majuzi na tayari ametangaza kuwania ubunge wa wilaya ya Kyela ndani ya CCM!
Mwakalinga ametoka kuongea na wana Kyela sasa hivi kwenye hotel ya kisasa ya Sativa na watu waliokuwepo hapo wanasema hapana shaka Mwakalinga kaletwa Kyela na vigogo ndani ya CCM na serikalini na dhahiri anaungwa mkono na mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mzee Mwakalinga na Mwenyekiti wa CCM wa wilaya hiyo Japhet Mwakasumi!
Kwa mujibu wa habari za watu wa Kyela,kama uchaguzi wa kura za maoni ndani ya CCM utafanyila leo kwenye kata 15 zinazounda wilaya hiyo, Mwakalinga na Dr Mwakyembe watashinda kata 6 kila mmoja na kata 3 zikiwa ni "swing states".
Kata ya Kyela mjini,kata ya Matema na kata ya Ngonga sehemu ambapo wana siasa hawa wanapotokea ndiyo kata pekee za"swing states"lkn kata ya Kyela mjini ikianza kuegemea upande wa Mwakalinga na kumpa sasa likely kama anaongoza kwa kata 7 kwa 6 za Dr Mwakyembe!
Bila ubishi kata ya Ikolo,kata ya kajunjumele,kata ya Katumba Songwe,na kata 3 za mashariki ya Kyela hizo zitachukuliwa na Dr Mwakyembe ili hali kata ya Ipinda,kata ya Lusungu,kata ya Makwale na kata 3 kuzunguka upande wa Magharibi hasa kuanzia mpakani mwa Kasumulu na mgodi wa Kiwira zitachukuliwa na Mwakalinga kwa kile wanachosema Dr Mwakyembe kashindwa kazi ya kuwasadia wahanga waliofukuzwa kazi kwenye mgodi huo na vijiji jirani!
Mwakalinga,ambae pia ana vitege uchumi vingi sana wilayani Kyela zikiwemo hotel kubwa za kisasa tayari yupo Kyela,na kaanza kuzunguka kwa kasi vijijini kujinadi kwa wana CCM na kuna kila ukweli kuwa viongozi wa CCM wilayani na mkoani wamebariki kuanza huku kwake kampeni kabla ya muda wake.
Juhudi zinafanywa ili mazungumzo ya Mwakalinga akiwa kyela ambako tayari sasa kafanya ndiyo makazi yake yapatikane na yaletwe hapa ili wana JF wayachambue!

Last edited by a moderator: