Kyela 2010: Mwakyembe Vs Mwakalinga kupitia CCM

Hapa ndipo ninapouona umuhimu wa waraka wa kanisa katoliki.

Haya masuala ya kumpigia debe mtu kwa kisingizio cha mwenzetu ndo yametufikisha katika mtafaruku wa ufisadi, matokeo yake vyeo vinakwenda kwa ushikaji badala ya uchapa kazi. apimwe kwa kigezo cha ufanisi
 
Mwakalinga ni mwenzetu hapa JF kwa muda mrefu,michango yake ni muhimu sana amekuwa hakosi kuwepo hapa kila siku masaa karibu 18 kwa siku.
ana exposure kubwa sana akiingia bungeni hata wabunge wengine watanufaika na Mwakalinga ambaye kwake Utaifa ni mbele kwa kila kitu.
Mwakalinga Utanzania umemjaa kuliko Ukyela.

naomba wote tumuunge mkono kama hapa kijiweni kwake tunaanza kumuombea mabaya nani atamsupport?

Mwalimu Nyerere mwaka 1995 alipiga kampeni nchi nzima isipokuwa Arusha Mjini. alipofika Arusha akasema kuwa pale anagombea mtoto wake-Makongoro Nyerere hata kama wako vyama tofauti hawezi kwenda kumpinga mtoto wake jimboni Arusha mjini.kama kuna mtu anaweza kuniambia tofauti aje hapa.

tufanye uzalendo kama wa Nyerere kwa kumsupport mwenzetu.
Mwakalinga hata michango tutakupa.kwetu sisi wewe ni bora mara elfu kwa Mwakyembe.

Simjui Mwakalinga na sitaki kuburuzwa kumuunga mkono. Mmeombwa kutuwekea CV yake hapa ili tumjue kwa karibu hamtaki kazi ni kupiga debe tu. Tupe CV yake ili tupate nafasi ya kumliganisha na Mwakyembe. JF sio chama cha siasa eti tumuunge mkono Mwakalinga kwa kuwa ni mwana JF.

Kwa mawazo yangu mepesi, huyu ni chaguo la mafisadi akina Lowassa na RA ili asaidie kumtoa Mwakyembe bungeni kazi ambayo sio rahisi kama wanavyofikiria kwani Mwakyembe, kama wengine walivyochangia anao uwezo wa kugombea popote na kupitia chama chochote na akashinda kiti cha ubunge.

Dokezo: Kipindi cha kampeni kimefika?

Tiba
 
George Mwakalinga mwana Kyela aliyekuwa anaishi na kufanya kazi kama mtaalaum wa kompyuta nchini UK amewasili Kyela majuzi na tayari ametangaza kuwania ubunge wa wilaya ya Kyela ndani ya CCM!

Mwakalinga ametoka kuongea na wana Kyela sasa hivi kwenye hotel ya kisasa ya Sativa na watu waliokuwepo hapo wanasema hapana shaka Mwakalinga kaletwa Kyela na vigogo ndani ya CCM na serikalini na dhahiri anaungwa mkono na mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mzee Mwakalinga na Mwenyekiti wa CCM wa wilaya hiyo Japhet Mwakasumi!

Kwa mujibu wa habari za watu wa Kyela,kama uchaguzi wa kura za maoni ndani ya CCM utafanyila leo kwenye kata 15 zinazounda wilaya hiyo, Mwakalinga na Dr Mwakyembe watashinda kata 6 kila mmoja na kata 3 zikiwa ni "swing states".

Kata ya Kyela mjini,kata ya Matema na kata ya Ngonga sehemu ambapo wana siasa hawa wanapotokea ndiyo kata pekee za"swing states"lkn kata ya Kyela mjini ikianza kuegemea upande wa Mwakalinga na kumpa sasa likely kama anaongoza kwa kata 7 kwa 6 za Dr Mwakyembe!

Bila ubishi kata ya Ikolo,kata ya kajunjumele,kata ya Katumba Songwe,na kata 3 za mashariki ya Kyela hizo zitachukuliwa na Dr Mwakyembe ili hali kata ya Ipinda,kata ya Lusungu,kata ya Makwale na kata 3 kuzunguka upande wa Magharibi hasa kuanzia mpakani mwa Kasumulu na mgodi wa Kiwira zitachukuliwa na Mwakalinga kwa kile wanachosema Dr Mwakyembe kashindwa kazi ya kuwasadia wahanga waliofukuzwa kazi kwenye mgodi huo na vijiji jirani!

Mwakalinga,ambae pia ana vitege uchumi vingi sana wilayani Kyela zikiwemo hotel kubwa za kisasa tayari yupo Kyela,na kaanza kuzunguka kwa kasi vijijini kujinadi kwa wana CCM na kuna kila ukweli kuwa viongozi wa CCM wilayani na mkoani wamebariki kuanza huku kwake kampeni kabla ya muda wake.

Juhudi zinafanywa ili mazungumzo ya Mwakalinga akiwa kyela ambako tayari sasa kafanya ndiyo makazi yake yapatikane na yaletwe hapa ili wana JF wayachambue!

Almost 90% Ya habari hii ni uongo na majungu!

Nitathibitisha. Please give me a few minutes!
 
Kumbe kampeni za uchaguzi wa ubunge ndani ya ccm zimeshaanza, au nimesoma hiyo habari vibaya vile! Naona huyu keshashindwa hata kabla ya kuingiza mguu katika hatua zake. Nampa pole

Yaani wewe kusoma hiyo habari ya uongo ndo umeamini? watu wameanza kuogopa vivuri vyao
 
Mtanzania we need you Most now.....Engineer wa majungu upo wapi teh teh teh teh teh.....
 
George Mwakalinga mwana Kyela aliyekuwa anaishi na kufanya kazi kama mtaalaum wa kompyuta nchini UK amewasili Kyela majuzi na tayari ametangaza kuwania ubunge wa wilaya ya Kyela ndani ya CCM!
Hapa kuna ukweli. George ameishi hiyo nchi ya Uingereza na anajua mambo mengi kwenye mitambo ya telecoms.

Mwakalinga ametoka kuongea na wana Kyela sasa hivi kwenye hotel ya kisasa ya Sativa na watu waliokuwepo hapo wanasema hapana shaka Mwakalinga kaletwa Kyela na vigogo ndani ya CCM na serikalini na dhahiri anaungwa mkono na mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mzee Mwakalinga na Mwenyekiti wa CCM wa wilaya hiyo Japhet Mwakasumi!

Uongo mtupu. Ndugu Mwakalinga bado hajafika Kyela wala Mbeya katika hii safari. Hiyo hotel ya Sativa, ndiyo ipo huko Kyela, nadhani ina branch kule Dar pia.

George hajaletwa na mtu yeyote. Kama yuko hapa Bongo basi kaja kwa bidii zake na kama likizo kujionea yaliyomo hapa nchini mwake. BTW, RC Mbeya ni Mwakipesile..... hiyo ya Mzee Mwakalinga ni majungu yako tu mkuu. Naomba wanaJF makini wasiyape nafasi.

Kwa mujibu wa habari za watu wa Kyela,kama uchaguzi wa kura za maoni ndani ya CCM utafanyila leo kwenye kata 15 zinazounda wilaya hiyo, Mwakalinga na Dr Mwakyembe watashinda kata 6 kila mmoja na kata 3 zikiwa ni "swing states".

Uongo mwingine huo technically! Kura za maoni za chama mkoani ni 21 na zile za serikali ni 15. Hiyo idadi unayoitaja umeitoa wapi?!

Kata ya Kyela mjini,kata ya Matema na kata ya Ngonga sehemu ambapo wana siasa hawa wanapotokea ndiyo kata pekee za"swing states"lkn kata ya Kyela mjini ikianza kuegemea upande wa Mwakalinga na kumpa sasa likely kama anaongoza kwa kata 7 kwa 6 za Dr Mwakyembe!

Bila ubishi kata ya Ikolo,kata ya kajunjumele,kata ya Katumba Songwe,na kata 3 za mashariki ya Kyela hizo zitachukuliwa na Dr Mwakyembe ili hali kata ya Ipinda,kata ya Lusungu,kata ya Makwale na kata 3 kuzunguka upande wa Magharibi hasa kuanzia mpakani mwa Kasumulu na mgodi wa Kiwira zitachukuliwa na Mwakalinga kwa kile wanachosema Dr Mwakyembe kashindwa kazi ya kuwasadia wahanga waliofukuzwa kazi kwenye mgodi huo na vijiji jirani!
Haya nadhani mengi ni majungu tu pia!!

Mwakalinga,ambae pia ana vitege uchumi vingi sana wilayani Kyela zikiwemo hotel kubwa za kisasa tayari yupo Kyela,na kaanza kuzunguka kwa kasi vijijini kujinadi kwa wana CCM na kuna kila ukweli kuwa viongozi wa CCM wilayani na mkoani wamebariki kuanza huku kwake kampeni kabla ya muda wake.
Bana eeee.... kwanini watu mnakuwa waongo namna hii?!!! Dayyym! George wala hajafika huko Kyela. Bado yuko safarini, na kwa taarifa yako tu, George yuko Ngorongoro leo hii, alikuwa Dar, akazuka Manyara na baadae kujionea maendeleo anayofanya Dr. Slaa kule Karatu, maana ndiko aliko lala.

Juhudi zinafanywa ili mazungumzo ya Mwakalinga akiwa kyela ambako tayari sasa kafanya ndiyo makazi yake yapatikane na yaletwe hapa ili wana JF wayachambue!

Ndugu Malafyale, I think you are totally misinformed or simply in for character assassination! Kama huna contacts na watu wa Kyela I suggest upige simu hii,

0784431748. Ni ya mwandishi wa habari wa magazeti mbalimbali atakufahamisha what's happening in Kyela leo hii.

Am out!
 
eeeh stivi dii tutafutane mkuu nami ni mwana kyela.....najua una fungu kwa 2010......
 
malafyale kumbe alitulisha sumu? naona GT alimpa thanks.......ngoja tumsubiri labda na steveD nazo sumu.....

btw stev unataka kusema kuwa mwakalinga hana mpango kabisa wa kugombea ubunge?
 
malafyale kumbe alitulisha sumu? naona GT alimpa thanks.......ngoja tumsubiri labda na steveD nazo sumu.....

btw stev unataka kusema kuwa mwakalinga hana mpango kabisa wa kugombea ubunge?

Hilo la kuwa na mpango au kutokuwa sijasema. Hata hivyo kwa umakini wa George hilo bado ni jambo jema na mimi nitamtakia mafanikio tu kama anaamua kufanya.

Mkuu miye si mtu wa maangamizi, nikiamua kukulisha sumu ujue kuwa kuna antidote ninayo mkononi, hivyo usighafirike sana mkuu.

Btw, you seen the opt out clause ya GT...!!
 
....George Mwakalinga mwana Kyela aliyekuwa anaishi na kufanya kazi kama mtaalaum wa kompyuta nchini UK amewasili Kyela majuzi .\
Si kweli! nina ushahidi wa 100%,ukitoa angalau picha yake 1 akiwa huko Kyela nakupa 1000USD.Waandishi uchwara!Huna cha kufanya au huna habari?Au unataka kugombanisha watu kwa kifupi kwa kuwa hayuko Kyela hayo uliyoandika yote na kuwasumbua watu minds zao ni utumbo!
 
Haya masuala ya kumpigia debe mtu kwa kisingizio cha mwenzetu ndo yametufikisha katika mtafaruku wa ufisadi, matokeo yake vyeo vinakwenda kwa ushikaji badala ya uchapa kazi. apimwe kwa kigezo cha ufanisi

Nyie vipimo vyenu vikoje?

Ikifika Zitto,Slaa ,Mnyika wakichangia hapa utasikia wenzetu wa hapa jf ,wengine wakisema hivyo hivyo inakuwa nong'wa hii iko je?

Wanaosema Kanda2 kumsapoti Mwakalinga eti atashindwa kwa sababu hizi na zile hao ndio wadini wakuu,mtu si mdini kwa kusema mambo ya kidini ila anaye practice udini huyo ndiyo mdini.

Kanda2 na Mwakalinga uwezekano mkubwa ni wa dini tofauti sasa Kanda2 kumuunga Mwakalinga anaonyesh jinsi gani asivyo mdini anaangalia mtu mjenga hoja na aliye na nia madhubuti ya kuwaletea wananchi maendeleo na si mviziaji wa kulipua mabomu kama mwakyembe.
 
Hebu tupatieni wasifu wa huyu mheshimiwa mtarajiwa. Mimi namfahamu mtu mmoja anaiywa George Ambwene Mwakalinga. Lisoma rungwe secondary, Tambaza High School, Mzumbe chuo cha Kilimo na mifugo, UDSM kabla ya Kutimkia Bulgaria. Je ndiyo huyu?
 
Hapo juu ni sahihi kweli?
 
MkamaP amepata wasiwasi niliposema Mzumbe chuo cha kilimo na mifugo. Enzi hizo Katika chuo kikuu cha Dsm kuna watu walikuwa wanachukua course ya Angricultural Enginearing kwa miaka 4. Miaka 2 ya kwanza walikuwa wanafanyia UDSM na mingine 2 Mzumbe. Sawa mkuu?
 
Ebwana binafsi nafikiri linapokuja suala la uchaguzi hasa katika mfumo wa kidemokarasia kila mtu anao uhuru wa kugombea nafasi yeyote anayoipenda,sasa kama mwakalinga analitaka hilo jimbo la kyela basi atakuwa anatimiza wajibu wake kama mwananchi,labda kikubwa tu ni kwamba wale ambao wanataka kugombea nafasi za ubunge basi wawe wanaharakati wa kweli katika kuwaletea wananchi maendeleo katika majimbo yao, maana siasa za kibongo zimetawaliwa sana na uongo,ushirikina na rushwa kwa wingi saaana,labda nitoe rai tu kwa wale wanaotaka kugombea wabadilike,vileile wananchi na sisi tubadilike tusikubali kutumiwa,tuchague watu ambao ni wazalendo na sio chama,mtu kama anakuja na rushwa zake we kuleni tuuuuuuuuu, lakini kura msimpe kwani mtu kama huyo hawezi kuwa kiongozi bora hata kidogo.
 
Back
Top Bottom