Kwa waliomaliza form 4, kama una roho ndogo usiende kusoma special schools (shule za vipaji maalumu)

Mimi nakumbuka miaka ya 2005 mimi na washkaji wangu wawili tumetokea shuke moja ya kata tukaenda Ilboru kufanya discussion hapo tupo form 4..

Tukaanza kusolve maswali tunapiga paper nzima discussion.. kwenye vipengele vya multiple choice bwana nilijifunza kitu sana kwao na kilinisaidia sana.

Tulisove paper moja tukafika kwenye kipgele hicho cha multiple choice tukakutana na swali ambalo majibu yake yanatuchanganya jamaa wa ilboru akamtuma mwenzake kwenda kufuata kitabu ili tupate jibu lake.. kitabu kililetwa akamwamvia fungua ukurasa flani tukasoma ukurasa huo mpaka tukapata jibu sahihi.

Wakati huo kule kwetu katani kama swali halieleweki tunatafuta jibu kwa kura au kufumba macho kisha unapandisha mkono unashusha taratibu kuelekea eneo la swali kidole ikiangua A tunahitimisha kuwa ndiyo jibu .

Ila kuanzia pale nilijifunza kitu na ilinisaidia sana na nikafaulu bhana
 
Pcb ilikua mziki sana ukizingatia bam nayo sio ya kitoto

Practical nilikua bingwa wa kufoji practical aisee, necta nilipangiwa sehemu ya kuanza kufanya practical ya umeme yule msimamizi alinichek mpaka akacheka, yaani sikuunga kitu chochote jamaa anakuja kuniambia muda unaenda mbona hufanyi practical anakuta ndo namalizia kuchora graph nishamaliza saa nyingi...

Akaishia kucheka tu ananiuliza sasa we hizi data umezipataje
Mimi aliniulizaga hivyo hivyo nikamwambia Mambo magumu sijui chochote akanambia pole huku Mimi nishatafuta data siku nyingi kwa kifoji
 
Wahanga wakubwa wa nacte ni 2012 4m 4 na 2013 4m 6, lilipita gharika ikabidi warudie rudie kupachika pachika tu, wapo waliobahatika na wengine walilalia kuti kavu. Ndio ikaletwa BRN baada ya hapo ufaulu ni kupaa tu toka hapo mpka leo.
Form six 2007 ulikuwa Bado hujazaliwa?
 
IPO nami nilibance nikaona hiyo imetiki sasa yeye anadai PCB nikamwambia haiwezekani kwa Sie wahenga A level 90s huko nikashangaa kuwa tcha wake amemwambia possible
Kama ni wa kike hizo points 10 anaweza kuchaguliwa PCB, wa kiume labda atasubiri second selection Au mpeleke private. Muache mtoto asome anachokipenda, kwanza CBG Haina dili Siku hizi

Pia anaweza kuchaguliwa CBG na akahamia PCB Kama Shule aliyopangiwa wanayo hiyo combination
 
Umenikumbusha kijana mmoja anaitwa Rajabu ndegeulaya.

Tuna report advance Azania yeye alipitisha tangazo la kuwa anafundisha tuition Kwa WANACHUKUA PHYSICS, CHEMISTRY NA PURE MATHEMATICS.

WATU walizani ni form six kumbe ni form five alishamaliza topic zote mpaka za six basi ikabidi tuendelee kupiga mapindi kwa Ndegeulaya.

Saivi unatusumbua kwenyejukwaa la Sports jamii,Kenge wewe
 
Hizi shule(mzumbe,pugu,kisimiri,ilboru,kibaha and the likes) japokua siku izi nyingi zimepoteza sifa zake aisee kama una moyo mwepesi usiende huko unaweza kupata depression au pressure ukashindwa kusoma

Miaka Hio mwisho wa miaka ya 2000 niliripoti Moja ya shule tajwa hapo combination ya pcm... Kipindi hicho special school wamejaa watoto wa dar kutoka (kibaha, Azania, pugu) aisee Hawa madogo wana sifa kishenzi.... Mtu anakuja kuripoti form 5 ameshamaliza topic zote za form 5 anakaribia kumaliza za form 6

Sasa si matozi tulivyomaliza form 4 vitabu tukatupa Kule mpaka siku ya kuripoti hujawahi kupiga pindi lolote... Unakutana na vitoto vimesoma sijui mchikichini huko aisee wamefuta topic zote, aisee nilipata presha sana mpaka kuzoea ile Hali.... Nakuta madogo wanapiga integration kama hawana akili, ukikaa bwenini wanaulizana kwa nguvu reaction za organic. Chemistry huko....

Dah yaani mwezi wa kwanza form 5 watu wanasolve necta review nikasema hapa nimeyatimba... Aisee ile presha ya ku catch up nilipata shida Sana sio Siri... Ukiwa na roho nyepesi unaweza kukata tamaa Moja kwa Moja

Kuna dogo tumeingia form 5 alikua anaitwa T.O (Tanzania one) alitukimbiza wote form 4 aisee huyu Jamaa mpaka Leo hua namuogopa. Hua namwambia hata hii kazi ya u engineer unayofanya unastahili kua somewhere else una potential kubwa sana, picha linaanza tumeingia form 5 hapo.... Sasa form 6 walikua wanafanya fitness tests (hii anatokea mwanafunzi mmoja au wawili wanatunga mtihani alafu wengine wanafanya japo sio lazima)

Ujinga wa hii mitihani wanafunzi wanajua kukomoana yaani maswali yote unakuta ya kibabe... Kuzungusha 0 huku ni kawaida tu ndo maana wengi walikua hawataki huu ujinga, dogo bana tunafika form 5 kaskia form 6 wanafanya fitness test ya physics dogo akazamia akapiga Pepa... Matokeo yanatoka form 6 karibu wote wamefeli dogo kawakimbiza.... Wote wanaulizana hili jina nani mbona hatumjui... Kuja kuulizia wakaja kugundua ni dogo wa form 5 aisee jamaa walimind kinoma akapigwa marufuku kabisa kusogeza pua kwenye fitness tests za form 6

Huyu dogo tulipofika form 6 sidhani kama aliwahi kukaa akasoma, jamaa alikua anakaa zake class watu wamepanga foleni na maswali Yao yaliowashinda dogo anapiga yote tu hajali kama ni ya physics, chemistry, pure au bam ye anasolve tu. Alikuja kua Tanzania one tena form 6 jamaa walimtangaza hesabu paper 1 na 2 zote alipiga 100%.

Huku kama una roho ndogo sio pa kwenda mi nusura panishinde nilitaka nirudishe mpira kwa kipa(kuhamia private)
Haha dah umenikumbusha mbali sana , kuna watu walikuwa na mikwara balaa ila baada ya muda mnakuwa sawa
 
Umenikumbusha kijana mmoja anaitwa Rajabu ndegeulaya.

Tuna report advance Azania yeye alipitisha tangazo la kuwa anafundisha tuition Kwa WANACHUKUA PHYSICS, CHEMISTRY NA PURE MATHEMATICS.

WATU walizani ni form six kumbe ni form five alishamaliza topic zote mpaka za six basi ikabidi tuendelee kupiga mapindi kwa Ndegeulaya.
Ndegeulaya alikua na kipaji cha kufundisha ila kuanzia O level mpaka advance alikimbizwa na wadau ambao walikua hawan kelele.
 
Alikua headboy wangu MKUU nimesoma nae O level na Na advance nimepiga nae yeye alipiga PCM Mimi nilikua napiga EGM tulikua tunakutana kwenye Pure mathematics.
Hivi ndege aliwahi kua headboy azania? mbona sikumbuki.
 
Broo umenikumbusha mbali pigo inaanza nafauli comb za science basi nikaanza kupiga mapindi nilikuwa bitozi san enzi hizo mapind sifiki pesa ya tuition naishia kulamba mademu...... basi nikapangiwa advance nikatimba maskuli fresh kufika nakutana na mwana mmja alikuwa pcb enzi hizo.....
Jamaa akanikuta nimelal kweny kitanda bwenini akanitukana dogo unazingua umekuja sayansi na unalal sa3 sijui alikuja bwenini kufanyaje lakin stor ndo ilianzia hapo.
Mimi sikujali sana nikaendelea kulala freshi siku ya pili akanikuta tena akasimama bwenini dogo boya huyu analala sa3 humu amekuja kusoma au laa niliogop sana sem nilikuwa mtukutu ...... badae nikaenda darasani nakutana na wanafunzi wana solve organic ma chandi nikapagawa nikasem nimeyatimba lakin nashukur mungu nili adpt mazingira nikaanza kukata mapindi
Pigo ikaenda jamaa alikuwa form six nikawa nasem daah huyu jmaaa anajua sana maan kulala kwake ni sa9 usik mimi nikijiona sa3 nimejitahid
Jamaa akapiga ascee matokeo kutoka amelamba 17 three nikakaa kitandani nilicheka mpka machozi sijui yupo wapi sasa ingawa mimi pia sikufany vyema nilipat dv 2
 
Back
Top Bottom