Kuweni makini, utapeli mpya umeibuka Dar

Msofe kaokoka wapi? Juzi hapa amejenga fensi na servant kota kwenye kiwanja cha mama mmoja jirani yangu huku mbezi beach. Bahati nzuri huyu mama nae ni mtu wa mjini ameshinda kesi.

Ni kweli, halafu we waweza kuwa jirani yangu, nami naishi mitaa hiyo, vibia tunagonga GMB au Juliana na T-Square!
 
Haya jamaa bado wanapiga sana tu hasa huku mikoani,na watumia simu,pamoja account numbr,shemeji kalizwa 3.5milions majuzi tu hapa!
 
sio bure,hawezi kuokoka tu hivihivi.huyu lazima kuna jambo la kiafya alikumbana nalo.wakat fulani mkongoman mmoja aliniambia kuwa anauguwa kisukari.wale wakongoman wa FM academia sijui watapata wapi pesa ya ''MABANGA''(kutaja majina ktk wimbo).
Maana ya neno hilo kwenye red ni Mawe kama ambavyo utasikia kwenye nyimbo zao nyingi wana sema "Mbula ya Mabanga" maana ya ke "Mvua ya Mawe"
 
Hawa jamaa wamejitambulisha kuwa wana kampuni ya uchimbaji mabwawa na wamepata tenda ya kuchimba mabwawa kwa ajili ya maji ya kunywa wanyama katika mbuga zetu hapa Tanzania.

Wanadai ujuzi wa uchimbaji mabwawa waliusomea ujerumani. wanadai wakati wapo ujerumani waliongea na mjerumani mmoja ambaye ni mtaalam wa madawa ya kusafisha maji.

Wakadai zaidi kuwa waliongea na huyo mjerumani kuwa, mara watakapomaliza maliza kozi hiyo mjerumani huyo aliwaahidi kuwa angeweza kusupply hayo madawa ya kusafisha maji kwa bei ya dola 4,900 kwa ujazo walinitajia nimesahau.

Wakaniambia kuwa madawa hayohayo yanaweza patikana katika kiwanda kimoja hapahapa tz kwa dola 4,100. Hivyo wameniambia nifikirie kama nina uwezo wa kusupply hayo madawa na baadae niwasiliane nao.

Naomba ushauri wandugu nisije kupiga penalti ikageuka kuwa kona.
 
Ni matapeli hao margin ya dolla 700.00 isikudanganye ukaliwa dolla 4900.00. Pls be carefull waambie wewe huna mtaji wa kusupply watafute mtu mwingine.

Kama una dolla hizo unaweza kuanzisha biashara nyingine ukaisimamia na ikakulipa zaidi kuliko kujiingiza katika biashara hewa ambayo si ajabu ni rafiki zako ndiyo wamekuchongea deal hilo ili uliwe fedha yako.
 
Walikuwa kwenye madawa ya kuifadhia mazao sasa wamegeukia kwenye maji

kuwa mwangalifu ni matapeli hao
 
Wewe ukitaka kuwajua ni simple!fanya kama unawatumia M Pesa kiasi ambacho huna!then itakuja sms yenye jina la mwenye namba ya simu kama wamejisajili!ila angalia utaliwa!wao wamekujuaje kama una hizo hela?hilo ni changa
 
matapeli hao..... Ukiwatumia hela huwaoni, kawaida wanapata details zako kwa mtu wa karibu, na siku hizi kuna wimbi jingine oikipata details zako wanakupigia wakikwambia wana faili lako lenye makosa yako uwaone uwape kitu kidogo la sivyo watalifikisha mbele.....

Wote ni matapeli
 
Huyu wa namba inayoishia na 040 alijitambulisha kuwa mimi na yeye tunatoka kijiji kimoja huko upareni alipatia kweli na anaongea kipare vizuri, ila nilipombana eneo gani hapo kijijini au jirani na mzee gani maarufu alibabaika hakuweza kujinibu ipasavyo hapo ndipo nikaanza kujipanga.


matapeli hao..... Ukiwatumia hela huwaoni, kawaida wanapata details zako kwa mtu wa karibu, na siku hizi kuna wimbi jingine oikipata details zako wanakupigia wakikwambia wana faili lako lenye makosa yako uwaone uwape kitu kidogo la sivyo watalifikisha mbele.....

Wote ni matapeli
 
Mie walinipigia wiki mbili zilizopita,wakijaribu kuulizia habari za watu ninaofanya nao kazi,wakanieleza hii story ya madawa nikawaambia nitawajibu:Niliamua kuwashirikisha mume wangu na kaka yangu ndipo waliponifungua macho kuwa ni matapeli wakubwa na wameshaliza watu wengi hapa mjini.Jiadhari nao
 
mm nawatamani kweli hawa watu..., yani nataka nikimshika mmoja namfanya kitu nikimuachia anaenda kujinyonga mwenyewe kwa hiyari yake....,
 
Back
Top Bottom