Kuweni makini, utapeli mpya umeibuka Dar

Wakuu,
kama dk 3 zilizopita nimepigiwa simu kwa namba 0657751049 jamaa kajitambulisha kama Dr kutoka WFP kigoma. Anahitaji preserving food chemical inaitwa Gustavic liquid from Germany. The guy sound weird na mimi kwa kuwa naujua huu mchezo long way back. Na hapa jamvini pia imesharipotiwa sana. Pia namba nyingine anayodai ni ofisa Msd ni 0713925380 jina athuman pazi. Mimi nawasubiri nione mwisho wao. Update later as saga continues

peponi kuna network leo?
 
sijaona mtu akitoa maelezo wanatapeli vp? yani kw mfano wakishakupgia wat next? akisema anahtati hzo chemical so ndo inakuaje? anakuagza ukutane nae au anataka umtumie hela. bado sijawapata vizuri, weken wazi
 
Mimi cjaona utapeli hapa!kwani wewe mi supplier wa chemicals au madawa?Elezea utapeli wao uko wapi ili tujihadhari,maana ninachokiona kwako ni labda ulipigiwa wrong number,na ungejibu hivyo tu.
 
Mimi cjaona utapeli hapa!kwani wewe mi supplier wa chemicals au madawa?Elezea utapeli wao uko wapi ili tujihadhari,maana ninachokiona kwako ni labda ulipigiwa wrong number,na ungejibu hivyo tu.
Kashindwa kujieleza lakini hawa jamaa wanawapata sana watu wenye tamaa. Mfanyakazi mwenzangu bado nusu aingie mtegoni baada ya huyo jamaa anaetaka hizo chemicals kujifanya anamjua na alishawai kukutana nae kwenye project moja na kumuunganisha na Mzungu (thru mobile phone) ambaye ndio Supplier( anaejifanya) anayekubalika na Taasisi hiyo inayotaka chemicals ili anunue toka kwake kwa bei rahisi na wapeleke kwenye Taasisi ya WFP kwa kuongezea bei ili wapate faida mara mbili. Alipoambiwa atatuma dolla kwenye account namba ndio akaanza kutuuliza na kumshauri aache ****** ingawa alissisitiza hilo jina la ofisa wa WFP ni common kwake kwa sababu wanatoka sehemu moja kwao Moshi na kweli alishashiriki kwenye project moja yule tapeli anayoitaja.
Ndugu yangu hawa jamaa huwa waanzia mbali sana jambo la muhimu hapa ondoa tamaa yeyote ile na kumbuka kwamba hakuna pesa ya rahisi kwa wakati huu wa sasa.
Sasa hivi wameanza mpaka mbinu za blackmailing. Tatizo hawa jamaa hata wakikamatwa na Polisi kesi zao ni taabu sana kuwatia hatiani sijui kwa nini labda ushahidi au nini sijui labda wanasheria kwenye JF watusaidie.
 
Hawa jamaa wajanja sana na wanajua namna ya kujiprotect,wewe ushaexpose mtego hadi hapa jf,unadhani utawakamata,thubutuuuu,kuna ndugu yangu pamoja na ujanja wote majuzi wamempiga Tshs.3,500,000/= anakuja kushtuka wanataka pesa zingine,nilimshangaa sana sasa tatizo hata namna ya kuwapata ni tatizo,japo pesa inaweka kwenye akaunti yao lakini ngumu kuwatia hatiani kwa sababu pesa unakuwa umeweka kwa hiari yako mwenyewe bila kulazimishwa ndio sabb kesi nyingi hata zikienda mahakamani zinashindwa.
 
Haina haja ya kuwaambia polisi....hao wanashirikiana nao....juzi kati hapa lija maa limemtapeli dada flani tena lilisema litakuja toka south africa kwa email....then dada akaenda kulipokea airport likidai limeshuka na ndege na kutumia namba za tanzania....likamwambia limeleta mzigo wa kumpa zawadi dada huyo afunguo saloon. Dada akaenda airport akalipokea wakaenda jivinjari hotel moja ya gharama likagharamia kama laki mbili hivi likamwambia limeleta mzigo wa milioni ishirini na atoe milioni mbili tu wakautoe mzigo huo. Pale pale dada mpaka akakopa na kuuza baadhi ya vitu vyake, akalikabidhi jamaa milioni mbili lifuate mzigo.......weeeee jamaaa limetokomea na namba haipatikani....
 
hili lijamaa litakuwa ni lizimbabwe ndio utapeli wao, nafikiri hata kuoaoa limeoa kwa muda (yaani kutoa kamzigo)
 
WanaJF,
Juzi nimepigiwa simu na mtu aliyejitambulisha kwa jina kwa ananifahamu vizuri sana.
Kisha akanieleza kuwa kuuna Deal la biashara inayohusisha wizara moja hivi.
Nilishawahi kusikia watu kibao wametapeliwa kwa njia ya watu kama hawa hivyo sikuwasikiliza hadi mwisho nikakata simu.
Napenda kuuliza hivi hawajulikani na hawakamatiki?
Namba aliyonipigia nayo ni 0783156703
Mimi nipo jijini mwanza kwa sasa ili alisema ananifahamu tangu nikiwa wizara ya mambo ya nje jijini Dar es salaam
Nawasilisha
 
Jamaa wanakupa details zako zoote na wanakujua kila kitu...then wanakuingiza mkenge wako so smart ila kwa sasa nadhani wamepunguza sana maana watu wengi wameshalizwa na habari zimesambaa
 
he! Nilidhani ni braza wangu papaa msoffe karudia tena utapeli maana siku hizi ameokoka
sio bure,hawezi kuokoka tu hivihivi.huyu lazima kuna jambo la kiafya alikumbana nalo.wakat fulani mkongoman mmoja aliniambia kuwa anauguwa kisukari.wale wakongoman wa FM academia sijui watapata wapi pesa ya ''MABANGA''(kutaja majina ktk wimbo).
 
Msofe kaokoka wapi? Juzi hapa amejenga fensi na servant kota kwenye kiwanja cha mama mmoja jirani yangu huku mbezi beach. Bahati nzuri huyu mama nae ni mtu wa mjini ameshinda kesi.
 
Back
Top Bottom