Ndugu yangu alivyotapeliwa kununua matairi feki ya gari, kuweni makini

Bravo247

Senior Member
Sep 14, 2013
108
229
Habari wakuu,

Leo nimeona niwezeku-share nanyi namna ndugu yangu alivyotapeliwa mbele yangu jioni kweupe mida ya saa kumi.

Ilikuwa hivi ndugu yangu anaendesha "Bolt" na "Uber" na anamiliki gari ndogo ya kwake binafsi. Kutokana na hali ya maisha kuna matairi yalikuwa yameisha na hakuwa ameweza kuyabadili. Akiwa kwenye foleni kwenye moja ya mataa mjini hapa alifuatwa ma kijana mmoja, akamueleza amafanya kazi kwenye moja ya warehouse inayohifadhi matairi kwaajili ya kupelekea ma-agent wao (alishaona gari ya ndugu yangu haina tairi mpya).

Wakakubaliana watauziana kwa bei nzuri ambayo ni ya chini sana kuliko madukani.

Kwakuwa ndugu yangu naye aliingia tamaa akataka kununua matairi yote manne 😀😀😀

Utapeli Ulivyofanyika
Basi mtoa deal akamwambia kwakuwa hayuko kazini atamlink na dereva anayepeleka mzigo wakutane ampe mzigo wake na pesa atamkabidhi huyo dereva.

Ndugu yangu alinipitia nyumbani akakuta napiga kinywaji kidogo huku nafanya mambo yangu. Akanishirikisha nkamwambia aende ila alinishi twende wote. Nkamwambia mimi nishashtua na sina ratiba ya kutoka ila akanisihi sana basi nikakaa kushoto tukaelekea huko makutano ilikuwa maeneo ya Tandale.

Huyo dereva akasema hawezi kuja na hiyo canter yenye mzigo anaogopa anaweza kutana na maboss ama moja ya wafanyakazi hivyo mzigo upo kwenye bajaji anakuja chap sana ili aendelee na route yake.

Akafika eneo tulikuwa tumepark ila kwa akili zake akatupita akaenda kusimama barabarani kabisa. Ambapo pako busy magari, pikipiki na bajaji zinapita.

Akaelekeza tumfuate, kwakuwa ndugu yangu ndio alikuwa busy kuongea na simu mimi nikahamia kulia niendeshe kuelekea bajaji iliposimama (mtego ukawa umeanza kunasa sasa 😀).

Nikapark nyuma ya ile bajaji nikaja nyuma ya gari kufungua boot. Me sio mtaalam sana wa matairi na pia biashara ilikuwa hainihusu so nilikuwa na red cup yangu naendelea kufyonza kinywaji. Yule dereva alileta tairi moja limefungwa makaratasi vizuri tu kama yanavyokuwa mapya. Akamkabidhi ndugu yangu, jamaa akapekua sehemu ya size ya tairi kama walivyoelezana.

Mimi nikamuuliza tu ndugu yangu ndio lenyewe akasema ndiyo.

Hapo dereva alirudi kwenye bajaji kama anafuata mengine (bajaji ilikiwa silence inaunguluma tu) alikaa kidogo kama dakika mbili ila akarudi kabeba tairi zote tatu zikawekwa kwenye buti ndugu yangu akafunga buti (kumbukeni tumesimama barabarani na kuna usumbufu mwingi).

Dereva akaja akapewa pesa, hakuzihesabu akidai anamwamini ndugu yangu na akidai watafanya sana biashara mbeleni akakimbia chap kwenye bajaji akasema anawahi kupeleka order zile za agent wao.

Kilichofuatia sasa
Mimi nikarudi tena kulia akaniambia tuelekee kwa fundi Kijitonyama aweze kubadili hizo tairi mpya 😀

Tukafika kwa fundi akaambiwa vua matairi yote weka hayo mapya kwenye buti. Mimi nimekaa kando naendelea na kinywaji tunagusa stories mbili tatu.

Ghafla tukasikia fundi anauliza "Oyaa mmetoa wapi hizi tairi?" Ndugu yangu akauliza kwanini akasema "Hazifai yaani hamna kitu" akiweka kidole kinapitiliza nje ama ndani. Akawaambia waliokuwa wanafungua rims ili wabadili tairi "Wazee acheni msizitoe!"

Daah ndugu yangu akazuga tu kwa fundi kuwa kuna kaka yake kamuita tu kampa.

Tulibaki tumeduwaa ndugu yangu alikuwa amechukua hela yake ya kulipa kodi 280,000 kwa mkewe. Mke haelewi jinsi hela ilivyoenda hasa ukizingatia tulikiwa wawili akaanza kuhisi jamaa labda kafanyia kitu kingine 😀 ikabidi jamaa abebane na matairi yake apeleke kithibitisho nyumbani.

Mjini utapeli ni mwingi na wa aina tofauti.
 
Mkuu umenikumbusha niliwahi kupigwa kizembe sana. Kuna siku nimeenda kununua tairi tena zote nne pale warehouse ya Binslum hata sikua na shaka kutokana na mazingira ya pale niliyoyakuta. Nafika kwa fundi nikabadili zote fresh... nimetumia kama mwezi zikaanza kuvimba manundu ile kukagua vizuri nakuta nimeuziwa tairi za miaka mitano nyuma ambazo basically zilikua zishaisha muda wake wa matumizi.
 
Mkuu umenikumbusha niliwahi kupigwa kizembe sana. Kuna siku nimeenda kununua tairi tena zote nne pale warehouse ya Binslum hata sikua na shaka kutokana na mazingira ya pale niliyoyakuta. Nafika kwa fundi nikabadili zote fresh... nimetumia kama mwezi zikaanza kuvimba manundu ile kukagua vizuri nakuta nimeuziwa tairi za miaka mitano nyuma ambazo basically zilikua zishaisha muda wake wa matumizi.
Yaani utapeli upo inakuwa tu muda haujafika!! Ingawa tukiona habari kama hizi tunajifunza kuongeza umakini. Ama nilichojifunza kama kitu huna utaalamu nacho heri kumtumia aliye mtaalamu ama aliyebobea wakati wa kutafuta kitu unachohitaji!!!
 
Huyo jamaa yako ndio wewe,
Mtu hutapeliwa kwa tamaa zake mwenyewe,ukiletewa fursa tambua kua wewe ndio fursa yenyewe.
Ningekuwa ni mimi ningeweka wazi tu hakukuwa na haja ya kupindisha story. Ndio tamaa na kutokuwa na pesa ya kutosha kulifanya apoteze hata kidogo alichokuwa nacho!!!
 
Ndo hivo sasa hakuwa na mawasiliano na wauzaji pia nadhani!!
Mlishindwa hata kusoma namba ya Bajaji? hii issue toka mwanzo ukiisoma inaonekana kabisa kua ilikua ni utapeli,hata namba ya simu ya huyo Dereva hamkutaka kuitumia ili mumpate?
 
Back
Top Bottom