Kuweni makini, utapeli mpya umeibuka Dar

Yaani ukisikia "Bongo Dar es Salaam" ndio hii, watu wanaishi kwa kutumia Ubongo wao, na siyo elimu. Unaweza ukawa na Elimu ya degree kwa DSM na usiwe na pesa. Lakini ukashangaa kijana aliyeishia darasa la 3 shule ya msingi akakuajiri wewe.

"BONGO DAR ES SALAAM"
mtu yeyote hata awe mzee au ni mlemavu akikusimamisha na kukuuliza kitu mchunguze kwanza kabla hujamuhurumia.

MIZAMBWA
INANIUMA SANA!!!
 
Yaani wewe ndo umeijua leo????
Mbona hii issue ya Longi sana???!!!
 
Mjini mipango,mjini hakuna mashamba mjini kuna lami tu mdomo ndo unakuweka mjini,anyway hii habari ni ya mda sana hapa JF hila kuna member wengine wapya itawafaa sana hii
 
Kumbe hawajabadilisha staili hii ina mika sita sasa watu laki mbili walishalizwa sana hata wabunge wetu na wanasheria, wanakupiga kufuatana na wewe ulivyo wanaanzia laki nne mpaka million sita. Wanakaa sinza na Ubungo, hata hivyo police ishawatia mbaroni wakakosa ushahidi wa kuwatia hatia maana na wewe ulitaka kuiba kwa njia ya udanganyifu.
 
washawahi kunipigia mwaka 2009 nikawashtukia na kutaka kuwakamata lakini baadae wakashtuka hawakutokea sehemu niliyowambia tukutane...nikaambiwa hawa jamaa kijiwe chao ni sinza mapambano
 
Wewe kama unaishi DSM unatakiwa kuwa macho kuliko swala wa serengeti ambaye hofu yake siyo simba tuu, kuna threats nyingi sana mafisi, mwewe ,tai , mbwa mwitu, wawindaji haramu na kadhalika. DAR nako kuna utapeli wa kila namna kuanzia huo wa madawa ya mifugo, wauzaji wa bidhaa fake, wezi wa mfukoni,vibaka, majambazi, wauzaji wa viwanja fake, watoza ushuru(TRA) fake, mapolisi fake, michango ya harusi fake, michango ya ujenzi wa makanisa ambayo haifiki kanisani, tegemeza jimbo, changia jumuia ndogo ndogo,wezi wa majumbani wanaoingia kama wasoma mita wa tanesco, changia ujenzi wa madarasa ya shule za msingi na sekondari za kata, michango ya kila siku isiyoisha kwa ajili ya watoto wetu wanaosoma shule zetu za msingi za kayumba, nk,nk,..orodha ni ndefu cha msingi ukitaka kuishi DAR kwa raha usimwamini mtu yoyote sii padri, shehe, mwenyekiti wa mtaa, katibu kata, katibu tarafa wala mzee wa upako ....Napendekeza ianzishwe thread kila mtu aweke kila aina ya utapeli anaoufahamu upo DAR ili tuwanusuru members wenzetu.
 
Wakuu,
kama dk 3 zilizopita nimepigiwa simu kwa namba 0657751049 jamaa kajitambulisha kama Dr kutoka WFP kigoma. Anahitaji preserving food chemical inaitwa Gustavic liquid from Germany. The guy sound weird na mimi kwa kuwa naujua huu mchezo long way back. Na hapa jamvini pia imesharipotiwa sana. Pia namba nyingine anayodai ni ofisa Msd ni 0713925380 jina athuman pazi. Mimi nawasubiri nione mwisho wao. Update later as saga continues
 
Kila la kheri. uwa wanaenda likizo na watu wakisahau wanarudi kwa gia ile ile
 
Tengeneza mazingira uwakamate mkuu , tena uwe na polisi na waandishi wa habari . Wamezoea sana .
 
My Advices kama utafanikiwa kuwakamata ni kujua nani katoa information zako kwani huyo ndo mbaya wako. Mara nyingi ni mtu wa karibu na wewe na si mtu mwema naweza kukulengesha kwa watu wabaya zaidi ya hao matapeli.
 
hata mimi walishwahi kumpigia, yaani nimcheka sana jamaa mpaka akajiona mjinga aisee. Namba za watu wanzitoa kwenye media mbalimbali za matangazo. we kama ulishawahi kuweka namba yako in public au kwenye gazeti au mtandao wowote ndio wanaanziaga hapo.
 
5 Reactions
Reply
Back
Top Bottom