A
Anonymous
Guest
Kuna njia ya hii ya utapeli ambapo mtu anatengeneza urafiki na wewe kupitia mtandaoni. Kadri siku zinavyoenda mnatengeneza ukaribu na ka imani kanaanza kukuingia kiasi fulani kuwa umepata rafiki mzuri kutoka nchi jirani japokuwa wakati mwingine inaweza kuwa hapa hapa bongo.
Sasa akishaona umemuamini anakwambia fulani nina zawadi kwaajili yako nataka nikutumie, anakuonesha zawadi hizo na mara nyingi zinakuwa ni za gharama kubwa sana. Anakupigia picha akizipaki mpaka siku anazituma na anakupa mawasilianao ya mtu au kampuni inayotakiwa kudeliver mzigo huo.
Mzigo ukifika mtu au kampuni uliyoambiwa itakupatia mzigo huo wanakupigia simu kukujulisha kuwa mzigo umefika, lakini mzigo huwa unakuwa umepelekwa mji tofauti na wewe, na hapo utaambiwa, address ilikosewa au imetokea kutoelewana/sintofamu mzigo umetumwa sehemu nyingine, ili utumiwe mzigo huo unatakiwa kutuma pesa ya usafiri.
Ukiangalia pesa ya usafiri unayotajiwa na thamani ya vitu ulivyotumiwa unaona pesa ya usafiri ni ndogo sana, hivyo huoni hata shida ya kutuma! Ukishatuma tu imekula kwako, kampuni au mtu huyo anakublock inakuwa imetoka hiyo, ushaliwa!
Jambo la kuzingatia ili usije kuingia mkenge, watu hawa huwa hawataki kutumia video call, utabaki kuona profile picture zao na kusikia sauti lakini katu hawakubali kufanya video call ili ujue utambulisho wao.
Watu hawa wamekuwa wakitumia udhaifu wa watu kuwa wapweke kihisia kutapeli watu, sio upande wa mapenzi tu hata urafiki wa kawaida, jinsi wanavyokuchota utaona nimepata rafiki wa kweli kumbe mtu yupo kazini.
Kuweni makini.