Kuosha Vyombo

Mwanakijiji

Wacha ubahili kanunue mashine ya kuosha vyombo.

BTW hivi serikali zetu bado zinaajiri wafanyakazi wa kufagia ofisi, kupika chai, madereva nk. kazi nyingine bana ndio sababu wafanyakazi wanadumaa, kazi za kupika chai maofisini sio za kuajiri mtu au kila boss kuwa na dereva wake tufike mahali tubadilike na kuondoa adha ya kutegemea shughuli kama hizi kufanywa na mtu mwingine. How do they do it in Europe? Hili ni zigo jingine kwa walipa kodi.
 
...Je, na yule anayekosha chombo kabla hajapakua, ni hila au tabia?

Hahahahha Mbu hii itakuwa katika kuitayarisha njaa...............si unajua kama hotelini vile wanaanza kukunawisha, wanaleta appetizers nusu au saa moja kabla ya chakula kuja!! Lol

Hebu tusipoteze uelekeo wa thread..................Mwanakijiji kasema ni vyombo vya kawaida.

Zamu si zamu??
 
  • Thanks
Reactions: Mbu
Mwanakijiji

Wacha ubahili kanunue mashine ya kuosha vyombo.

BTW hivi serikali zetu bado zinaajiri wafanyakazi wa kufagia ofisi, kupika chai, madereva nk. kazi nyingine bana ndio sababu wafanyakazi wanadumaa, kazi za kupika chai maofisini sio za kuajiri mtu au kila boss kuwa na dereva wake tufike mahali tubadilike na kuondoa adha ya kutegemea shughuli kama hizi kufanywa na mtu mwingine. How do they do it in Europe? Hili ni zigo jingine kwa walipa kodi.

Wacha hata ukiangalia ile report iliyotolewa na mkaguzi wa hesabu za serikali Bwana Uttouh....na badget zetu pesa nyingi zineelekezwa kwenye chai na warsha ......but on the second thought............ ukileta mimashine sijui mwaiita coffee makers ni watanzania wangapi watakosa ajira?? watakuwa redundant?? na ukichukulia uwezo wetu mdogo wa kucreate employment .................hawa wote watakuwa mzigo wa wafanyakazi wachache watakao bakia..........watu tutaigomea P.A.Y.E hapa itakuwa balaa..... naamini bado hatujafika huko.
 
Sijui kama ni swali la kizushi au uchokozi: Wote mlikuwa na njaa, mkaenda jikoni na mkapika kwa kushirikiana vilivyo na mkakipenda chakula. Mkakaa chini mkala kwa furaha zote na kuteremshia na mvinyo kidogo. Baadaye mmoja ndiye anatoka na kuanza kuosha vyombo. Hii kweli ni sahihi? Ni lazima wakati wote mshirikiane na kuosha vyombo kama mlivyoshirikiana kupika na kula? Ni swali tu.

Ha haa haa. Mwanakijiji vipi kama ilikuwa ni takeaway or fast food?
 
Hahahahha Mbu hii itakuwa katika kuitayarisha njaa...............si unajua kama hotelini vile wanaanza kukunawisha, wanaleta appetizers nusu au saa moja kabla ya chakula kuja!! Lol

Hebu tusipoteze uelekeo wa thread..................Mwanakijiji kasema ni vyombo vya kawaida.

Zamu si zamu??

unajitetea ee? LOL...mwenzio kwa msisitizo Vyombo naipigia mstari. Asiyetaka kukubali maana shauri yake.
"mwenye njaa hana miiko," na "mwosha huoshwa!"
 
Mwanakijiji si ututegulie kitendawili mkuu, maana hapa wewe ukionekana kwenye hili jukwaa basi unaletaga thread zenye "utata".
 
Vyombo hivi siyo vile
Vya huku siyo kule
Vya jikoni siyo pale
Vyomo vile vya kulia!

Vyombo siyo vya sirini
Vyombo vile vya mezani
Siyo vya kule chumbani
vyombo vile vya jikoni!

Siyo vyombo vya gizani
Vilivyong'ang'ana mwilini
Vya vyakula vya gizani
Vyenye kuliwa shukani

Vyombo hivi ni sahani,
Na vijiko vya mezani
Sufuria za jikoni
Bakuli za kabatini!

Mlivyonavyo mawazoni
Silo niwaulizeni
Sijui tatizo nini
Mmewaza ya chumbani!

Mkisha kula pamoja
Vitamu tena vya haja
Mtaosha kwa pamoja
Au aoshe mmoja?

Swali nawaulizeni.

M. M. Mwanakijiji (Sauti ya Kijiji)
Hahaha unaona sasa, Mwanakijiji watu wameingia mkenge walikuwa wanatafsiri vingine
 
Sijui nisikitike au sijui nishangae manake watu moja kwa moja walirukia huko kwenye hayo mengine wakati mzee wa watu unaongelea mambo ya kusaidiana chores za nyumbani.

Mapenzi ni kusaidiana bana. Siyo kila siku mpishi huyo huyo, mpakuzi huyo huyo, na mfuta meza huyo huyo na muosha vyombo huyo huyo. Khaaa….mapenzi gani sasa hayo? Huo ni utumwa na wala sio mapenzi.

Unajua Nyani we mjanja sana; wewe ndio umewapandikizia watu wazo fulani halafu ukakaa pembeni unawashangaa wanavyovingirishana nalo kama yale madudu ambayo huvingirisha mavi ya ng'ombe kwa kuyasukuma kwa miguu ya nyuma! Halafu baadaye unawashangaa!
 
Mwanakijiji si ututegulie kitendawili mkuu, maana hapa wewe ukionekana kwenye hili jukwaa basi unaletaga thread zenye "utata".

duh kwa kweli mnanilaumu bure tu.. watu wenyewe ndio wanamatatizo. Miye nimeuliza kitu kiko wazi kabisa; wengine wenye mawazo tata ndio hao wakaanza "zikapanda zikashuka" huku wengine wanatabasamu na kujisikia sikia hivi..
 
Sawa sawa kabisa maana kwa sisi tuliosoma yale masomo ya Maarifa ya nyumbani au was it Sayansi Kimu tumeelewa na sharti baada ya vyombo kukoshwa shurti viwekwe kwenye chanja na hata maji yakauke na vizuri haya majukumu yasiachwe kwa watoto wa kike tu bali wa kiume zamu ni jambo muafaka kabisa, tulipokuwa wadogo tulikuwa na zamu kibao ya kuondoa vyombo, kukosha hata kuandaa chakula.
 
Mh hiki chombo oshwa kisiwe kifanyiro changu? by the way mie naosha na mama anaosha chombo chake after MLO stahimilifu....
 
Mwanakijiji Kama nimekuwa nikizielewa makala zako mahili na
hakika leo sijabadilika na kushindwa kuelewa maudhui yako.

Ni wazi ulishatoa kidokezo hapo chini nilipo kunakili kuwa swali
ni la kizushi. Maneno, "sijui kama" ni kufumba ili kuondoa
ukali wa maneno swali la kizuishi au uchokozi.

Sijui kama ni swali la kizushi au uchokozi:
 
Mwanakijiji Kama nimekuwa nikizielewa makala zako mahili na
hakika leo sijabadilika na kushindwa kuelewa maudhui yako.

Ni wazi ulishatoa kidokezo hapo chini nilipo kunakili kuwa swali
ni la kizushi. Maneno, "sijui kama" ni kufumba ili kuondoa
ukali wa maneno swali la kizuishi au uchokozi.

Hivi nani anaweza kutueleza kwa vielelezo kuwa aliyeamini ni vyombo vya ndani au aliyechukulia ni vyombo vya kibailojia (kama mimi) nani yuko sahihi na akatumia hivyo vielelezo kutoa alama (marks) zisizo na utata? Naamini hata Mwanakijiji mwenyewe hawezi.

Ila pia sina shida kuwa miongoni mwa wale tulioonekana tunawaza sana ngono...kwani naamini ndiyo inafanya maisha yawe kama yalivyo (especially kwa upande wangu). Hata sijui maisha bila hiyo kitu yangekuwaje au kama yangekuwa na maana yoyote kwangu!!

Huyo ni mimi......Mzee DC.
 
Aaaah DC usiwe hivyo bana....hapa ilikuwa kufurahi tu.
 
Sijui kama ni swali la kizushi au uchokozi: Wote mlikuwa na njaa, mkaenda jikoni na mkapika kwa kushirikiana vilivyo na mkakipenda chakula. Mkakaa chini mkala kwa furaha zote na kuteremshia na mvinyo kidogo. Baadaye mmoja ndiye anatoka na kuanza kuosha vyombo. Hii kweli ni sahihi? Ni lazima wakati wote mshirikiane na kuosha vyombo kama mlivyoshirikiana kupika na kula? Ni swali tu.
Kila mmoja akaoshe vyombo alivyotumia mwenzie....! Japo kwa kutumia beseni moja, sabuni moja... na hata kuvifuta kwa kutmia kitambaa kimoja...!
 
Aaaah DC usiwe hivyo bana....hapa ilikuwa kufurahi tu.

Najua mkuu....... ila tena wewe ndo umelianzisha, ... halafu tunaonekana tunapenda sana ngono na hadithi zinazohusiana nazo....!!!!!

Don't take it serious or personal ...ilikuwa ni kutaka kuweka mambo sawa......Hata hivyo mimi binafsi napenda sana hiyo kitu na ukipagusa unaweza kunitoa kwenye mstari......LOL!!
 
mim nilijua tokea mwanzo ni vyombo vya mezani,niliwashangaeni saaaaana kudhani hili ni fumbo,
mim kama mim mpenzi wangu akinisaidia kupika hata asiponisaidia vyombo sitamlaumu,sbb wakaka wengine(hasa wa kibongo) hata jiko hawajui linawashwaje,mke akiumwa kama hakuna housegirl itabidi wale vya kununua,so nikisaidiwa kupika mengine ya jikon nitamalizia mwenyewe bila hiyana.
 
Back
Top Bottom