Je, ni sahihi baba mwenye nyumba naye kupangiwa zamu ya kupika na kuosha vyombo?

DR HAYA LAND

JF-Expert Member
Dec 26, 2017
17,992
45,497
Habari za Muda huu

Nipo na rafiki yangu, nimekua nikiona ana ratiba yake ya kupika na kuosha vyombo.

Watu huku wenzetu wanamapenzi ya kizungu yaani huyu rafiki yangu kila Jumapili huwa anashinda Nyumbani na kufanya shughuli za kupika na kuosha vyombo achilia mbali kufua na kufagia uwanja.

Je hii ni Sahihi?

NB: Nyumba yao ipo na Furaha kubwa Sana na Ndoa Yao ipo na miaka mitatu.

1666599688785.png

Picha kutoka maktaba
 
Tunapika ndio, ila sio kwa ratiba, hatufui kwa ratiba, tunafanya kwa mapenzi na tukijisikia ili kunogesha penzi, siku tukizifanya hizo kazi tunapewa mbususu kupitiliza tunapika siku za nyama roast au kuchoma nyama...hatupiki maharage wala mboga za majani.
 
Mimi nafanya sana kipindi nikiwa mapumziko, siwezi kulala baada ya saa 12 asb hivyo nikiamka nashindwa kukaa tuu, nafanya siyo namsaidia mpaka ziishe.
 
Nilijaribu kufanya hivyo mke akaona kama tuko sawa, akaona nami napaswa kubeba majukumu yake kama yeye asipojisikia. Akafikia hadi hatua ya kuniamsha asubuhi eti nikachote maji kisa yeye amechoka kipindi maji yalikata kama wiki hivi🤣🤣

Asubuhi naamka mapema kuliko yeye, hanifulii, hanipasii nguo, kifupi nikawa kama sijaoa.

Kilichofuata, nilimpigia "ABOUT TURN" moja matata mpaka yeye akabaki anashangaa tu.
 
inategemea kila nyumba na taratibu zake ila kwangu hapana nitapika nitafanya kila kazi ninapojisikia na inapobidi ila sio kwa ratiba
 
Back
Top Bottom