Pantomath
JF-Expert Member
- Jan 4, 2019
- 789
- 3,230
Tafakari utagundua, kama ni mtu unayetumia mda wako vizuri basi utagundua unapokua unaishi mwenyewe, ukaamua kujipikia iwe kwa mtazamo huuu
1. Ni kitu unapenda kutoka moyoni,
2. Unapoishi hakuna mgahawa karibu
3. Uchafu wa migahawa inayokuzunguka
4. Huwezi kutunza pesa hivyo bora ununue chakula hata ukiishiwa unachakula n.k lakini sio sababu ya Saving.
5. Mgahawani hawapiki chakula kizuri.
Lakini kinyume na hapo kama unaamini una save chochote basi unajidanganya, unapoamua kujipikia basi kwa kujua au kutojua umekubali haya :
1. Kupoteza mda,
Hiki ndio kipengele kikubwa, kuanzia manunuzi/maandalizi, kupika kwenyewe, kuosha vyombo, kusafisha jikoni, kupanga na shughuli nyingne zote zinazofanyika jikoni...
2. Kero za takataka,
Hasa ndugu zangu wa mjini, umepika ushamaliza mambo yako tumbo limejaa, kipengele ukiangalia makololo ya mabaki ya vyakula, hapo ndio unafikiria pakuyapeleka, Nyumba nyingne hazina Waste disposal nzuri, ni timing ifike usiku ukatupe barabarani.
3. Kero ya kucheza na bajeti,
Mda wote wewe kuwaza, unga nusu shilling kadhaa,mafuta nusu bei ile, Sukari kilo sijui sh ngapi, kesho ukienda bei imebadirika unakua mkali..
4. Gharama,
Kujipikia ni gharama, usijidanganye kabisa eti kuna kitu una save, Leo hii unaweza ukaenda mgahawani ukala chakula cha Buku, niambie ni katika mazingira gani utajipikia chakula baadae ukijumlisha mboga, chakula, gas, viungo, Chumvi n.k utakua umetumia chini ya buku? Nipe hio bajeti hapa na kweli iwe applicable.
5. Hasara,
Katika upikaji sio mda wote unachopika unakila chote, kuna kubakia, kuharibika, kuharibu, kuunguza n.k zote hizo ni lost ambazo ukiziweka kwenye mahesabu unazidi kuongeza budget..
6. Ratiba,
Upo sehemu unafanya hili na lile, kichwani unawaza kwenda kugombana na masufuriaa, unalazimika kufunga hata ofisi sababu umekua mfungwa wa kujipikia
Faida za kula mgahawani..
1. Unaokoa mda, hili ndio kubwa, utatumia huu mda kufanya mambo mengine ya msingi
2. Unaokoa pesa, hapa sitii neno
3. Unakua flexible na nini ule, Nyumbani mda mwingine unalazimika kula kitu ambacho kuhutaka sababu tuu ndio kimebaki hutaki kukiharibu
4. Unakua huru na ratiba zako mda ukifika unaenda kula unaendelea na ratiba.
5. Usafi, mda mwingi ndani panakua pasafi, unapofanya usafi ni wakawaida, Kinyume na hapo unatembea njiani vidole vinanuka vitunguu..
6. Unaepuka kero za takataka na maji taka n.k
Katika hayo yote simaanishi ndio usijue kupika, simaanishi usiwe na chombo hata kimoja,
Jifunze kupika, mana hujui na mazingira gani utalazimima kupika..
Nunua vyombo vyote, siku kwa kujiachia ukaona leo na mimi nijipikie, hio pia iko poa
ILA SIO KUA MTUMWA WA MAPISHI..
Pia kwa kiasi kikubwa hapa nazungumzia wale tuliopanga, wale wenye ratiba ngumu, wale tunaoishi mijini,
Familia au mpo zaidi ya mmoja kupika yaweza kua options nzuri, Pia katika hili Sijalenga wanawake.
Niko tayari kukosolewa na kurekebishwa kwa hoja itapendeza.
Najua ni maisha yako, Sijakupangia namna ya kusihi, ni mtazamo tuu.
Bachelor Pika For leisure.