ndege JOHN
JF-Expert Member
- Aug 5, 2015
- 19,573
- 44,803
Assume una mke mdogomdogo mama wa nyumbani na bado hamjapata mtoto, sasa mnaishi kwenye nyumba moja mko wapangaji wawili tu; yaani mtu na mkewe ambao hawana pia mtoto ila wenyewe hawana kazi ya kipato cha kati, wanaunga unga maisha yaendelee.
Mara nyingi mume wake anatoka asubuhi anarudi usiku leo kapata kidogo kesho kakosa nyakati nyingi hamuachii mkewe hela yoyote ya mezani.
Sasa wewe kipato chako sio haba sana unapata salary mpaka ya kuwa na na uwezo wa kununua vitu vya jumla ukaweka ndani mchele, mafuta, unga, gas,nyanya,vitunguu na kadhalika.
Sasa inaibuka tabia ya mkeo kuanza ku share kupika na yule mdada mpangaji..na mke anakutamkia wazi kabisa kwamba wanashirikiana kupika jirani yake huyo ananunua mboga na viungo vya mchana halafu mimi tanunua mboga za usiku.
Anadai kwamba hata kwao kijijini ulimpomtoa huwa wanapika na wifi yake wanakula pamoja na kwamba hajazoea maisha ya choyo. Anadai niwaache waendelee kushirikiana kwa sababu chakula cha kula mwenyewe hakimnogei ikumbukwe me huwa natoka asubuhi na mchana nakula kazini narudi usiku tu.
swali langu wakuu wenye uzoefu mnaonaje je hapo hakuna kuhujumiana kweli maana me nahisi kwa uwezo wangu ndo natoa mchango mkubwa sijawahi kuona wao wanunue vitu kwa jumla.
Je, nimkubalie mke wangu tu alivyozoea kumsaidia jirani yake? Maana kweli kuna siku za kuishiwa pengine jirani yake atamsaidia pia chakula alichonach,o ila sasa roho inauma maana nahisi kama mke wangu hana uchungu na maisha yalivyo magumu; anahisi me napata hela nyingi huku kazini.
Hali hio ni ya kawaida kweli kwa mke kusaidiana kupika na kuosha vyombo na mpangaji mwenzake wa pekee na umri wa mke ni miaka 18.