Mkuu Bitabo,binafsi sifahamiani na Paul Chizi,lakini nadhani badala ya Mwakyembe kumfuta kazi angesimamia mchakato huru na haki kulifufua shirika letu la ndege. Kama kawaida ya Mwakyembe na wenzake ametumia taratibu kumwondoa mtu ambaye mimi naamini alikua anafanya kazi kizalendo na analipenda shirika! Walioua ATCL ni wanasiasa na watendaji serikalini. Inaumu sana kwetu sisi ambao tumetumia huduma za shirika ili toka tukiwa watoto wadogo!
Wakuu Mh. Mwakyembe hakupindisha maneno juu ya uovu wa Mr. Chizi na wenzie. sasa hizo uniform za staff za dola za obama 50,000 kwa wafanyakazi wangapi hapo ATCL? tena bila tendering process? Tumpe nafasi na kama ametupiga changa la macho soon tutajua tu maana hata huyo Chizi ameyasikia yaliyosemwa.
lakini Chizi alishastaafu kwa mujibu wa sheria na Mwakyembe anasema utaratibu wa kumuajiri mstaafu haukufatwa. hapo napo kuna ukabila?
Amesema mwenyekiti wa bodi mpya atatangazwa na JK soon, ngoj tuone hiyo bodi mpya na hao watakaoajiriwa kwenye menejiment mpya ndo tujue ukabila uko upande gani.
Issue hapa sio kupeleka ndege yenye picha ya twiga angani. Issue tunaipeleka kwa gharama gani na utaratibu upi?
Watu mnalalmikia picha ya twiga angani wakati watu wamepeleka twiga hai angani!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
Tanzania bwana utasikia ooh udini oooh ukabila huku watu wanaiba.