Mabadiliko yoyote ya mkataba wa DP World ni kiashiria cha uonevu kwa Dkt. Slaa

Nsanzagee

JF-Expert Member
Jun 28, 2023
1,939
4,118
Songombingo la kuvuliwa hadhi ya Ubalozi wa Dkt. Slaa, lilianzia pale kwenye kuvujishwa kwa mkataba wa hovyo kabisa kuwahi kutokea duniani, wa DPWORD na TPA kuhusu bandari za Tanganyika

Kama kawaida, viongozi wa Kiafrika huwa hawapendi kushindwa na hata wakishindwa, lazima watoe makucha yao kwa hao, wanaodhani wamewadhalilisha, licha kwamba ni ukweli wa makosa yao! Huwa inawauma kiasi cha kutamani kumeza watu kuonesha kwamba, wao ni malaika hawapaswi kushauriwa kwa kukosolewa, kujishusha katika jambo ambalo wao wamejikwaa kwa bahati mbaya, shariti wawaangushie wengine zigo la misumari ili roho zao ziwe kwatu!

Dk Slaa ameondolewa hadhi ya Ubalozi kwa kosa ambalo limetokana na kuwa na msimamo tofauti na viongozi wetu hapa waliosain mkataba mbovu wa DPWORD na Tanzania kuhusu bandari za Tanganyika, Misimamo yake ya kutetea haki ya watanganyika kuhusu mali zao, ndio imekuwa Tanzi kwake!

Najiuliza, ikiwa Dk Slaa ameondolewa hadhi hiyo ya ubalozi na mkataba ukafanyiwa maboresho kinyume na ilivyo kuwa awali, Hii haitakuwa ni uonevu kwa Dk Slaa kwa kuwa yeye alichokuwa akikipigania ni ubovu wa sheria zilizopo kwenye mkataba wa DPWORD na TPA kuhusu bandari zetu?

Nahitimisha kusema kuwa, Dk Slaa, atakuwa ni mshindi na itaonekana ameonewa pindi tu, kutakapotokea maboresho yoyote ya baadhi ya sheria za mkataba wa dp world!
 
Back
Top Bottom