Kukodisha Airbus ni mkataba wa kipuuzi - Mwakyembe

Saint Ivuga

JF-Expert Member
Aug 21, 2008
54,363
58,386
Ni mkataba wa kipuuzi ambao haujawahi kutokea. alonga Mwakyembe .. Mpaka sasa hivi serikali inadaiwa 6.9 billion shillings..
ndege imekodiwa tumeanza kuilipia ikiwa Hungary hata kabla haijatua
 
Haya hiyo ndiyo Tanzania, eti tuambiwe tu ATC inayo ndege inaruka, tunatakiwa wananchi tujielewe tuiondoshe hii serikali ya kifisadi madarakani
 
Anasema mikataba aliyokuta Atcl ni ya kipuuzi na hakuna mwenye akili timamu atakayoikubali.Hivyo ilimbidi aingilie kuokoa taifa ndege inatumika sehemu nyingine kwa miezi 6 halafu bado tunailipia sisi maajabu haya.Source Clouds redio
 
Huyu mzee wa Ukurutu nimekuwa simwamini tokea aseme kwenye ile ripoti yake ya Richimond kuna mambo ambayo ameficha ili serikali isianguke inamaana alitusaliti sisi wananchi. halafu turudi kwenye mada yeye ni mtaalamu wa mikataba ya kukodisha ndege?
 
Ni mkataba wa kipuuzi ambao haujawahi kutokea. alonga Mwakyembe .. Mpaka sasa hivi serikali inadaiwa 6.9 billion shillings..
ndege imekodiwa tumeanza kuilipia ikiwa angani hata kabla haijatua


Kuna jamaa mmoja humu alikuwa anasema eti Mh.Mwakyembe ni mkabila, nafikiri majibu yake sasa atayapata....!
 
Yaani management ya ATCL imeoza kabisa, tena bora alivyowasimamisha kazi hao top officials. Ingekuwa matakwa yangu, wasirudishwe tena kazini hata kama watashinda tuhuma zinazowakabili -kwani najua watachakachua tu. Wakishinda walipwe haki zao wasepe zao, shirika lisukwe upya!
 
Jamani kuna fundamentals kwenye kila mkataba unaposign!
Sasa gullu wa sheria kama mwakyembe awe ameshindwa kuinterprete sheria kisa ni mkataba wa ndege ya Airbus mkuu Presice dharau hiyo.
Huyu ni DR wa Sheria alikamau Ugerumani uko
 
Mtu anaitwa Chizi? Mhh jina baya hilo maana mkimlaumu anaweza kutoa jibu rahisi mkakosa la kumfanya.
 
Toka mwanzo niliwahi kusema humu kuna ulazima gani wa Tanzania kumiliki ndege kwasasa ikiwa gharama za usafiri hazina tofaut na mashirika mengine ambayo hayaja kodi ndege,sasa tunadaiwa bil 6 kwa nini tusitunze hizo pesa zikitimia bei ya ndege tukanunue yetu
 
Mh.Mwakyembe wewe piga kazi kwa nguvu zote,iga mfano wa mh.magufuli,maadam dhamira yako ni njema hata wapinge namna gani wewe utang'aa tuu! Maombi ya watanzania yanatafuta mtu kama wewe...Mungu anatafuta mtu atakayesimama sehemu iliyobomoka.... hao wanaokupinga ni mafisadi ama wanafaidika na mafisadi.
endelea mbele mkuu.
 
Anasema mikataba aliyokuta Atcl ni ya kipuuzi na hakuna mwenye akili timamu atakayoikubali.Hivyo ilimbidi aingilie kuokoa taifa ndege inatumika sehemu nyingine kwa miezi 6 halafu bado tunailipia sisi maajabu haya.Source Clouds redio

Hivi ndege ni zetu kwanini tunalipia tena? Kwani tunazikodisha? Kama tunazikodisha kwanini tuwe nazo tusiwarudishie wenyewe? Kama nimekodisha kitu kimenishinda kugaramia si nrudishia mwenye nacho?
mbona ni atcl? What does it mean?
 
Back
Top Bottom