Kukodisha Airbus ni mkataba wa kipuuzi - Mwakyembe

Haya hiyo ndiyo Tanzania, eti tuambiwe tu ATC inayo ndege inaruka, tunatakiwa wananchi tujielewe tuiondoshe hii serikali ya kifisadi madarakani

Siyo tu oondoshe serikali bali uondoshe kizazi kizima kwani hapa tatizo ni watu. Watu tumekuwa na tamaa ya mali ktk nafsi zetu na mfumo huo umeanzia vyuoni. Mwanachuo anapomaliza chuo mawazo yake ni kupata kazi na mafanikio ya maisha ya fasta fasta ndio maana. Na vijana wengi ndio wamekuwa vishawishi kwahao wazee kuanza kuiba,maana wazee hawajatahamaki wanaona kijana katoka chuo juzi mara ana kila kitu.
 
Halafu akimsimamisha Chizi watu mlalamike?
Chizi amekodisha Boeing 737-500 na sio Airbus. Airbus walikodisha watu wa zamani kabla ya Chizi. Mwakyembe anachokifanya hapa ni kuongelea tuhuma za miaka mingi nyuma kuhalalisha ukabila alioufanya watu waone kachukua hatua sahihi. ATC toka ameingia Chizi ni kampuni tofauti kabisa, nashauri kama huwa hupandi ndege usiwe kinara wa kumsifia Mwakyembe kwa kuwa amekurupuka
 
Ni mkataba wa kipuuzi
ambao haujawahi kutokea. alonga Mwakyembe .. Mpaka sasa hivi serikali
inadaiwa 6.9 billion shillings..
ndege imekodiwa tumeanza kuilipia ikiwa angani hata kabla
haijatua

Mie nimemsikiliza vizuri Mwakyembe clauds, nadhani kama hivyo ndivyo alivyo kweli, ndie candidate pekee ambae angalau magamba wanaweza kumsimamisha na akapunguza kidogo kura za dr slaa mwaka 2012!
 
Anasema mikataba aliyokuta Atcl ni ya kipuuzi na hakuna mwenye akili timamu atakayoikubali.Hivyo ilimbidi aingilie kuokoa taifa ndege inatumika sehemu nyingine kwa miezi 6 halafu bado tunailipia sisi maajabu haya.Source Clouds redio

Walioingia mkataba pamoja na clouse ni wenda..wa...zm
 
Sasa hivi wanaume wenye uchungu na nchi hiii katika serikali ya J.K. tumewapata wanne, wa kwanza Mwakyembe, wa pili Kagasheki, wa tatu ni Sita na wa nne ni Magufuri japo aliteteleke katika suala la kuuza nyumba za serikali. Lakini angarau hao kinaonekana wanachokifanya.

Mwakyembe watanzania tunasubiri TAZARA, Reli ya kati na Bandari hasa hiyo kampuni ya akina Karamagi
Mwakyembe hana proven record ya kutetea maslahi ya watanzania zaidi ya maslahi binafsi. Usiamini maneno ndugu subiri vitendo. Kagasheki ameshugulikia tukio hapo hapo, huyu Mwakyembe yuko busy na viporo vya David Mataka badala ya kutueleza future ya ATC itakuwaje. Katenga fedha ya ndege mpya kwenye bajeti? Ndio vitu vya kumuuliza. Katenga fedha za kupunguza wafanyakazi? Kama vyote hakuna kamwe hataweza kuligeuza hilo shirika. Biashara ya ndege ni tofauti na siasa
 
Kiukweli kwa jinsi Mzee Mwakyembe, Balozi Kagasheki na watendaji wanavyoanza kufunguka CDM waandae agenda nyingine haraka sana. Ama sivyo watajikuta wanaimba zilipendwa wakati wananchi wanageukia Zinapendwa!
Watu kama Mwakwembe hawatakiwi CCM kwa sababu kwa CCM kila kitengo,kampuni au taasisi ni deal ambayo inawahusisha vigogo kupambana na hao mafisadi wakati umo kwenye chama tawala ni ndoto ya mwendawazimu au unajitafutia matatizo.Mfano mzuri wale wabunge wa CCM waliosaini zoezi la kumgoa Pinda mbali ya kua mazingira ya chama makini CHADEMA na wabunge hao kulipelekea mabadiliko ya baraza la mawazi.Wabunge hao hao ambao wengeliitwa mashujaa wanaandamwa kwa vitisho kutoka viongozi wa juu wa CCM na vikao vya ndani ya CCM.
 
Te te te! wale waliokuwa wanasema n ukabila waje hapa waseme sasa, huu n upuuziii! nchi haina mwema kila mtu tapeli! kamua mwakyembe wala usiangalie nyuma. we nchi gani hatuna shirika la ndege! we toka mwanza mpaka dar nauli ilikuwa 380,000 mpaka 499,000 kwa precision na 540. wametuharibia ndege yetu ipo hapa mwanza! fukuza wote
Mkuu inaelekea hujapanda ndege muda mrefu sana. Nauli ni kati ya 320,000 na 350,000 kwenda na kurudi. Chizi akatuletea Twiga akaanza na mkwara wa 200,000 kwenda na kurudi then matapeli wa Precision na 540 chu.pi zikawabana wakashusha hadi 280,000. Leo Mwakyembe amemuondoa kwa ukabila sasa hivi tutasikia Twiga amepaki kwa vile amewashika pabaya washindani
 
Kiukweli kwa jinsi Mzee Mwakyembe, Balozi Kagasheki na watendaji wanavyoanza kufunguka CDM waandae agenda nyingine haraka sana. Ama sivyo watajikuta wanaimba zilipendwa wakati wananchi wanageukia Zinapendwa!
Mbona hawa wanatekeleza ajenda ya Chadema? Actually wanaipaisha chati.
 
Huyu mzee wa Ukurutu nimekuwa simwamini tokea aseme kwenye ile ripoti yake ya Richimond kuna mambo ambayo ameficha ili serikali isianguke inamaana alitusaliti sisi wananchi. halafu turudi kwenye mada yeye ni mtaalamu wa mikataba ya kukodisha ndege?

hapo juu,,,,,,,dah naona wadau bado mnamwita vibaya sana
 
Mkuu inaelekea hujapanda ndege muda mrefu sana. Nauli ni kati ya 320,000 na 350,000 kwenda na kurudi. Chizi akatuletea Twiga akaanza na mkwara wa 200,000 kwenda na kurudi then matapeli wa Precision na 540 chu.pi zikawabana wakashusha hadi 280,000. Leo Mwakyembe amemuondoa kwa ukabila sasa hivi tutasikia Twiga amepaki kwa vile amewashika pabaya washindani

uphhhhhhhhhhhh
 
Miaka karibu mitano baadaye? Really? mbona this one haikutahiji hata tume kuundwa? Tuliwaandikia, tuliwapigia kelele, tuliwaambia acheni wakang'ang'ania? magenius wetu wa Bongo!

Chakushangaza kipi hapo ?nakumbuka kama leo Rais Mkapa aliposema wananchi wa Tanzania wapo tayari hata kula majani lakini ndege ya Rais wao inunuliwe sasa kwa hili la kukodi ndege kwa hali yoyote ile alimradi Tz ionekane nayo inarusha ndege inaminisha kuwa Nchi na wananchi wake wapo tayari kula hata kama ni kinyesi lakini nchi ijipatie sifa inarusha ndege nayo
 
Mwakyembe hana proven record ya kutetea maslahi ya watanzania zaidi ya maslahi binafsi. Usiamini maneno ndugu subiri vitendo. Kagasheki ameshugulikia tukio hapo hapo, huyu Mwakyembe yuko busy na viporo vya David Mataka badala ya kutueleza future ya ATC itakuwaje. Katenga fedha ya ndege mpya kwenye bajeti? Ndio vitu vya kumuuliza. Katenga fedha za kupunguza wafanyakazi? Kama vyote hakuna kamwe hataweza kuligeuza hilo shirika. Biashara ya ndege ni tofauti na siasa

mmmm,,,,,mwakyembeeeee
 
Kitendo cha Mwakyembe kwenda redioni kuongelea mkataba wa kukodisha Airbus miaka mitano iliyopita ni unafiki uliopitiliza. Mi nilidhani ataongelea mapungufu ya sasa ya shirika na kueleza namna ya utatuzi wake. Nawashauri watanzania mlio wavivu wa kufuatilia mambo muwe makini sana na watu wa aina hii, wanacheza na public opinions kwa maslahi binafsi na cheap popularity. Kwanza akina Mataka si wana kesi mahakamani? Jamani shikeni maneno yangu huyu Mwakyembe ni msanii, makosa ya miaka mitano iliyopita hayahalalishi kumpa nafasi binamu yake kuongoza shirika
 
Maswali mengi kuliko majibu, mkataba wa miaka mitano iliyopita unahusiana vipi na Chizi? Hii mbona kama danganya toto!:sick:
 
Kiukweli kwa jinsi Mzee Mwakyembe, Balozi Kagasheki na watendaji wanavyoanza kufunguka CDM waandae agenda nyingine haraka sana. Ama sivyo watajikuta wanaimba zilipendwa wakati wananchi wanageukia Zinapendwa!

hata kama wangemnunulia kila mtanzania gari, tunachotaka ni mabadiliko, waje watawala wengine tuone mikakati yao ikoje ya kubadili maisha ya watanzania, halafu ngoma ya upinzani ndo itanoga wakati huo ccm atakuwa mpinzani. watanzania watafaidika, sababu upinzani ni kuhit pale mwenzio amevuruga, amefisadi basi wewe unatake advantage, miaka 50.
 
Wakuu Mh. Mwakyembe hakupindisha maneno juu ya uovu wa Mr. Chizi na wenzie. sasa hizo uniform za staff za dola za obama 50,000 kwa wafanyakazi wangapi hapo ATCL? tena bila tendering process? Tumpe nafasi na kama ametupiga changa la macho soon tutajua tu maana hata huyo Chizi ameyasikia yaliyosemwa.

lakini Chizi alishastaafu kwa mujibu wa sheria na Mwakyembe anasema utaratibu wa kumuajiri mstaafu haukufatwa. hapo napo kuna ukabila?

Amesema mwenyekiti wa bodi mpya atatangazwa na JK soon, ngoj tuone hiyo bodi mpya na hao watakaoajiriwa kwenye menejiment mpya ndo tujue ukabila uko upande gani.

Issue hapa sio kupeleka ndege yenye picha ya twiga angani. Issue tunaipeleka kwa gharama gani na utaratibu upi?

Watu mnalalmikia picha ya twiga angani wakati watu wamepeleka twiga hai angani!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
Tanzania bwana utasikia ooh udini oooh ukabila huku watu wanaiba.
 
Mkuu wangu nimeandika ktk sredi moja hapa inayohusu ATCL kwamba mwaka jana nilikua mmojawapo aliyepinga uteuzi wa Paul Chizi kuwa kaimu CEO,lakini sasa kutokana na kazi ameifanya nasema ulikua uteuzi sahihi hata kama taratibu zilikiukwa. Chizi hasiusishwe na mikataba ya kihuni ya miaka iliyopita. Tumechangia sana hapa,lakini kama kawaida ya Watanzani wameisha sahau. Sitashangaa kwa watu wenye kumbukumbu kidogo kiasi hiki kuwarudisha CCM madarakani!!
Maswali mengi kuliko majibu, mkataba wa miaka mitano iliyopita unahusiana vipi na Chizi? Hii mbona kama danganya toto!:sick:
 
Back
Top Bottom