Kukodisha Airbus ni mkataba wa kipuuzi - Mwakyembe

Kumbe tukiwa na 100billion twaweza kuwa na brand new Ndege!
So yule jamaa yetu wa vitisho wakati wa 2010 election anaweza nunua izo kama kumi ivi.
Naona kuna haja ya kujenga ushirika nao watukopeshe maana kuwakamata tumeshindwa!
 
Chiziiiiiiiiiiiiii

Mkataba anaouzungumzia Mwakyembe ulitiwa sign enzi za Mattaka na sio Chizi; kitu kinachoshangaza ni kuwa uchunguzi haugusi kabisa ili kufahamu kwa uwazi ni nani aliyeamuru ndege ile ya Air Bus 320 ikodiwe na ATCL!!Tafuteni ukweli kwa kufuatilia na kumuuliza katibu mkuu Chambo awaeleze yule Mchina wa Sonangol alikuwa anakutana na nani alipokuwa anakuja nchini na nani anaamuru kuwa hazina wamlipe hayo mahela WALLIS TRADING?? Mwakyembe anazungumza juu ya Air Bus without knowing the facts, he should investigate and find out who was behind that deal before making wild allegations.
 
Don't dare compare a giant (Dr.Slaa) with a pygmy (Dr.Mwakyembe or anybody in CCM circles). Nchi hii imefirisiwa na kukamuliwa kila ilicho nacho hawa kina Mwakyembe wakiwa ndani ya CCM. Hawajwahi thubutu kunyosheana kidole na wala hawajahi kuweka strategies za kuzuia mianya ya rushwa, uzembe, ubadhrifu, wizi na machafu yote kama haya.Hawahawa kina Ssita, Mwakymebe, Kilango, Magufuri wameshuhudia benki kuu yetu ikivunjwa na pesa kuchukuliwa mithili ya cha mgema huliwa na mlevi. Wameshuhudia madudu ya IPTL, Buzwagi, Richmond, Mikataba yote ya madini, mistu yetu inayovunwa kama shamba la bibi, viwanda vyetu vinagawiwa na kugeuzwa maghala ya bidhaa toka nje, mbuga za wanyama zimeuzwa. Wote hawa wamo ndani ya chombo kinachozama.

Kumsimamisha Chizi ndio Mwakyembe apungunze kura za Dr.Slaa come 2015? You are kidding. CDM ni nyumba iliyojengwa kwa muda mrefu chini ya concrete strategies na ideologies. CCM haina ideology practically bali theoretically ni ujamaa na kujitegemea bali kwa vitendo wanacheza ngoma nyingine. Sasa watu wanaendeleza unafiki kwa vitendo na kuweka katika kumbukumbu za historia wanaweza kutuletea good candidate. Si rahisi hivyo hata kama watu aina yako na Rutashubanyuma wanaaamini hivyo basi.

dr. Slaa mwenyewe anamkubali mwakyembe. Kpnd cha uchaguzi uliopita ktk kuomba kura kyela slaa alisema anaomba kura za urais lkn kura za mbunge mpeni mwakyembe na akatoa cfa za mwakyembe japo cdm walicmamisha mgombea ubunge kyela.
 
ila kwa hili wenye uzoefu na mikataba ya kukodi ndege watueleze kwa sababu waweza kuta mwakyembe kachemka.kwamba unaanza kulipia kabla ya ndege kufika nchini au la?
 
Nakubaliana na wewe kabisa, lakini zaidi ya hayo yawezekana Mwakyembe anafanya maagizo ya hao wenye nchi maana nasikia Chizi alikuwa anakuja juu kwenye sekta ya anga hata kuwatishia waliokuwa wanatawala hilo anga.

Just thinking.

Maamuzi anayofanya Mwakyembe kuhusu ATCL ni lazima tuyaone kwa kuangalia the BIG PICTURE. Katika vita dhidi ya ufisadi makundi ndani ya CCM yanafadhiliwa na watu wenye interest mbalimbali; moja ya makundi hayo linafadhiliwa na Reginald Mengi ambae anauhusianao wa karibu na wamiliki wa Precision Air ambao kila siku wanaomba kwa Mungu wao ATCL ipotee katika biashara ya kutoa huduma za ndege na Mengi ni mmoja wa watu walioonesha msimamo huo hadharani!! Hivyo basi sio jambo la ajabu kuona kuwa Mwakyembe kwa kujua au kutokujua anaingia kwenye mtego huo wa kuwaondoa wafanya kazi wazalendo ambao walikuwa na moyo wa kulifufua shirika. Mwakyembe anasema management ya Chizi haikuwa transparent katika ukodishaji wa ndege lakini hajui kuwa kwenye commercial transactions secrecy is the norm na kwa bahati mbaya watendaji wakuu wa wizara yake ambao Cizi alipashwa kuwapa taarifa wako kwenye payroll ya Precision!! Kitu alichotakiwa kukifanya ni kuungakia mkataba ulioleta hiyo ndege ya boeing na kuona kama ni mzuri au ulikuwa na kasoro na hiyo ndio ingekuwa sababu ya kuchukua uamuzi na sio suala la kufuata procurement procedures kwani the Airline industry sio sawa na kuendesha kampuni ya Daladala ina characteristics ambazo zinahitaji uamuzi wa haraka. Juu ya hayo Katibu mkuu Chambo ndio anahusika na shirika kutokuwa na bodi kwa muda mrefu ikiwa mbinu yake ya kutaka kuendesha shirika toka wizarani kitu ambacho ndio chanzo cha chokohoko zote zinazolikumba shirika!!
 
ni aibu kwa nchi kama tanzania yenye GAS,MADINI lakini hatuna ndege..wenzetu jirani kenya wana KQ ni aibu jamani. precision sasa hivi ndio kama vile ni ndege ya kitaifa. Watu wanafikiria matumbo yao tu bora mwakyembe kafanya mambo na bado awatimue na wengineo wengi na wafikishwe mahakamani.

Hata hiyo Precision uanzishwaji wake ulitokana na fedha zilizokapuliwa kwenye kodi zetu. Wenye shares Precision ni wenye tuhuma za kuifisadi nchi. Ngoja tupate uhuru mtatukoma.
 
Back
Top Bottom