Kukodisha Airbus ni mkataba wa kipuuzi - Mwakyembe

Huyu mzee wa Ukurutu nimekuwa simwamini tokea aseme kwenye ile ripoti yake ya Richimond kuna mambo ambayo ameficha ili serikali isianguke inamaana alitusaliti sisi wananchi. halafu turudi kwenye mada yeye ni mtaalamu wa mikataba ya kukodisha ndege?

nakuona kama huna nidhamu na hukufunzwa maadili kwenu. Unajuaje kama hutoweza kupata ugonjwa kama huo ilihali hujamfa? Tumia bongo japo ya kimtaani taani kama hujafunzwa kwenu. Kumbuka humu wanajoin watu wenye bongo zao na si wahuni. Mwacheni Mwakyembe awasaidie kuokoa shirika.
 
Tanzania Tanzania, ni kosa gani ulilifanya kwa Mungu hadi uadhibiwe?
 
..

Naomba nikusahihishe kidogo kwanza kabisa mwakyembe hakuenda redioni kama unavyosema pale ni JKIA terminal 2 na alikuwa akiongea na wafanyakazi wa ATCL hapo uwanjani..ulichosikia ni recorded sound ya tukio zima...
La pili Mwakyembe kamuondoa Chizi si kutokana na kashfa hizo tajwa hapo juu..kashfa hizi ni zile za waliotangulia Chizi kaondolewa kwa sababu uteuzi wake unakinzana na sheria yaani kwa ufupi Uteuzi wako haupo kisheria..

Ugonile malafyale...
Kama utaratibu haukufuatwa kwa mtu kukaimishwa yeye kafuata utaratibu gani kumuweka binamu yake Lusajo? Mwakyembe aliugua na kulazwa India kwa karibu miezi 6 na sheria za kazi zinasema miezi mitatu ya kwanza unalipwa mshahara mzima na miezi mitatu inayofuata unapokea nusu mshahara, lakini yeye aliendelea kupokea mshahara wote kwa miezi yote aliyokuwa kitandani hafanyi kazi. Je huu sio ukiukwaji wa sheria. Masuala ya kupiga mikwala kujustify maslahi binafsi watanzania tuyakatae. Hajaeleza mpango wowote wa kuinua shirika zaidi ya longolongo ambazo hazitaleta ndege mpya wala kupunguza wafanyakazi
 
nakuona kama huna nidhamu na hukufunzwa maadili kwenu. Unajuaje kama hutoweza kupata ugonjwa kama huo ilihali hujamfa? Tumia bongo japo ya kimtaani taani kama hujafunzwa kwenu. Kumbuka humu wanajoin watu wenye bongo zao na si wahuni. Mwacheni Mwakyembe awasaidie kuokoa shirika.

Sasa kwavile wewe unampenda unataka na mimi niwe upande wako kwani kuwa na bongo ni kumpenda Mwakyembe?
 
Jamani.... ya Airbus... si basi sasa ... si tuendelee mbele... au ndio hivyo tuchukue hizo ndio deliverables zako Dr. Mwakyembe... kiongozi mzuri ni yule ana-kubali hali halisi aliyoikuta na kuanza na strategy zake....

Mfano kama nikiwa rais wa hii nchi,halafu nikanyonga watu kama wewe..hata bila kuwasikiliza sana,potelea mbali..bado nitakwenda mbinguni
 
Hebu angalia hapo ambapo wino umekolezwa. Hivi kweli sare moja inunuliwe kwa dola karibu 50,000?

Mwakyembe alipuka tena





WAZIRI wa Uchukuzi, Dk. Harison Mwakyembe, ameendelea kuwasha moto ndani ya Shirika la Ndege (ATCL) ambapo jana aliweka bayana sababu kadhaa za kutengua uteuzi wa aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika hilo, Paul Chizi.


Akizungumza na wafanyakazi wa shirika hilo katika karakana ya uwanja wa ndege jijini Dar es Salaam, Mwakyembe alisema kamwe hawezi kufanya kazi na watendaji wabovu na kuwataka wale walioumizwa na maamuzi yake kuacha kazi mara moja.
Huku akionyesha kukasirika, waziri huyo aliapa kuendelea kufukuza watendaji wengine zaidi watakaobainika kwenda kinyume na sheria.
Akitaja sababu zilizomwondoa Chizi, alisema kuwa uteuzi wake haukuzingatia tarartibu za utumishi wa umma.


“Chizi katika ripoti yake ya uzoefu wa kazi inaonekana kuwa alishastaafu kwa mujibu wa sheria ambapo kwa wafanyakazi wa aina yake kuna taratibu za kuwaajiri, hivyo anatakiwa azifuate ili kuajiriwa tena,” alisema.


Mbali na hilo, sababu nyingine iliyomponza mkurugenzi huyo ni kuingia mkataba wa kukodi ndege bila ridhaa ya serikali wala wizara husika.


Hata hivyo, Dk. Mwakyembe alipotakiwa aeleze kwa nini mkurugenzi huyo alifanya hivyo, alisema anaogopa kusema kwani huenda akazidi kuibua mjadala zaidi katika taifa.


“Inasikitisha sana kuona kuwa ilifika mahali watu wakaona shirika ni mali yao na kufanya maamuzi vile wanavyotaka huku wakisahau kwamba wananchi wanaliangalia shirika hilo linavyouawa,” alisema.


Alisema kuwa serikali mbali na kutoridhia pia ukodishwaji huo haukufuata taratibu za manunuzi ya umma kwani ndege hiyo ilinunuliwa nchini Liberia ambako bidhaa zote chakavu ‘mikweche’ kama baiskeli, pikipiki na ndege zimekuwa zikipelekwa huko na nchi zilizoendelea.


Alieleza kukerwa na kitendo cha watendaji wa shirika hilo kujinunulia magari ya kifahari wakati serikali ilitoa fedha ili shirika lifufuke.


“Maana inashangaza iweje idara na kampuni ndogo zinaweza kujiendesha na kusimama zenyewe lakini ATCL imekuwa ikibebwa hadi leo pamoja na kuwa na wafanyakazi wazuri ambao wakienda kufanya kazi katika makampuni mengine wanafanya vizuri,” alihoji.


Alisema kuwa serikali inajua wako mawakala wa makampuni ya ndege binafsi, wanaodhani wataiua ATCL kumbe wanajiua wenyewe, na hivyo kuwaonya akisema kama bado wapo ni bora waondoke wenyewe kabla hajawaondosha.


Alisema yuko tayari kufikishwa mahakamani kwa ajili ya suala hilo kwani wanaofanya hivyo ni sawa na kuchezea sebuleni kwake.


Akifafanua zaidi madudu ndani ya ATCL, Mwakyembe alisema kuwa fedha za bima ya ndege iliyodondoka mkoani Kigoma takriban dola bilioni saba, tatu za awali zililipwa na iliagizwa ziingizwe katika akaunti ya Shirika Hodhi la Mashirika ya Umma(CHC) lakini watendaji wakafanya kinyume.


“Watendaji hao hawakufanya hivyo na kuamua kuziingiza katika akaunti ya ATCL, ambapo kati ya fedha hizo tumekuta dola bilioni mbili na dola bilioni moja zilizosalia hazijulikani zilipopelekwa,” aliongeza.


Waziri huyo aligusia pia hatua ya baadhi ya maafisa kwenda nchini China na kukaa huko takriban siku 45 kwa ajili ya kusimamia sare za wafanyakazi, jambo ambalo alidai ni ufujaji wa fedha za umma kwa kugharamia sare moja dola 49,900.


Kuhusu ajira ndani ya ATCL, Dk. Mwakyembe alisema kuna waajiriwa wengi waliokwishastaafu na pia ajira mpya zilitolewa bila kufuata tararibu ikiwemo kutangaza nafasi zilizopo ili wenye sifa washindane.


Alisema kuwa badala yake watu wamekuwa wakipeana ajira hizo kwa kufahamina na kuacha wale walio na sifa, jambo alilodai kuwa walikuwa wameamua kufukuza menejimenti yote, lakini wakahisi wangekosa kumbukumbu za urushwaji ndege.
“Baada ya kupitia baadhi ya mafaili ya watendaji hao tulikuta mwenye afadhali ni Kaimu Mkurugenzi huyu niliyemteua, Kapteni Lusajo Lazaro,” alisema.


Aliwaonya wanaozusha kuwa ametumia ukabila kumteua mkurugenzi huyo, akidai kuwa amebebwa na sifa pamoja na uwezo wake kiutendaji.

Waziri huyo alisema kuwa wameunda tume ambayo anaamini itakuja na majibu mazuri yatakayoliwezesha shirika hilo kusonga mbele.


Aliwataka wafanyakazi waliobaki, kuchapa kazi ili kumrahisishia pale anapoomba fedha serikalini aeleweke na kuongeza kwamba tayari wameshakabidhiwa sh bilioni 4.9 kutoka hazina kwa ajili ya matengenezo ya ndege.


Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Shirika hilo aliahidi kuyafanyia kazi yale yote waziri huyo aliyowaagiza, na kutimiza malengo ndani ya miezi mitatu waliyopewa.


Kwa niaba ya wanafanyakazi hao, Nelson Kalinga, alisema kusuasua kwa ATCL kumechangiwa na serikali kutowasikiliza wafanyakazi, kwani tangu awali walipinga kununuliwa kwa ndege hiyo ya Air Bus, ambapo waliandamana na kuandika barua wizarani lakini hawakusikilizwa.


Source: Tanzania Daima
 
mwakyembe anachapa kazi lakini ushauri wake kwa chizi juu ya kupokea malipo ya insurance nje ya account za atcl,hauku-sound ki- professional

Ha haaa usishangae sana hawa ndio wachakachuaji wenyewe ,hana tofauti na UDA .huo ushauri ulikuwa wa hovyo kabisa kwani dawa ya deni ni kulipa sio kupitisha hela pembeni pembeni.
 
tungelikua na mawaziri nusu ktk wizara tulizonazo wenye misimamo na kutetea nchi,tungefika mbali sana sana
yani nimesikitishwa kwa jinsi hii ATCL na akina chizi walivofanya,jamani ndege hata haijaja watu wamechakachua?ivi tunaitakia nini hii nchi?hawa waliopewa madaraka si watanzania wezetu?wazee ni noma sana kweli nimeamini!!

na aliyemchagua chizi na wale wakurugenzi nae achunguzwe ana lake jambo si bure,watu wanakula kwa kupitia ATCL
natamani tu lisiwepo hili shirika sioni sababu linatunyonya tu
 
Mh.Mwakyembe wewe piga kazi kwa nguvu zote,iga mfano wa mh.magufuli,maadam dhamira yako ni njema hata wapinge namna gani wewe utang'aa tuu! Maombi ya watanzania yanatafuta mtu kama wewe...Mungu anatafuta mtu atakayesimama sehemu iliyobomoka.... hao wanaokupinga ni mafisadi ama wanafaidika na mafisadi.
endelea mbele mkuu.
Katika eneo ambalo ninamuunga mkono Rais msaafu wa mwaka 2015 nipale alipomteuwa Dr Harrison Mwakyembe kuwa waziri wa uchukuzi. Ninaamini atatusaidia sana. Kaza uzi.
 
Mwakyembe

Piga kazi achana na hao Wasomi lkn ni Wezi wa Mali za Taifa hili

Hongera sana na Kaza Buti hivyo2
 
hapana naomba unijuze Edson

Moja ya sababu ni kutekeleza maagizo ya Kikwete wakati wa kuwateua mawaziri wapya, alisema sasa wanakwenda kuwashughulikia watendaji wa mashirika wanaosababisha mawaziri wa Kikwete kulalamikiwa na kisha kuondolewa.

Kwa hiyo ni mkakati maalum sio wa kumaliza ufisadi Tanzania bali kulipiza kisasi. CCM na mkulu wake hawana nia ya dhati ya kuung'oa wizi na ubadhirifu kwa sababu ndio unaowastawisha.
 
Mbona tulishawapigia sana kelele humu hawakuchukua hatua! Hadi Mwakyembe afanye jitihada binafsi!
 
Tanzania Tanzania, ni kosa gani ulilifanya kwa Mungu hadi uadhibiwe?
 
Moja ya sababu ni kutekeleza maagizo ya Kikwete wakati wa kuwateua mawaziri wapya, alisema sasa wanakwenda kuwashughulikia watendaji wa mashirika wanaosababisha mawaziri wa Kikwete kulalamikiwa na kisha kuondolewa.

Kwa hiyo ni mkakati maalum sio wa kumaliza ufisadi Tanzania bali kulipiza kisasi. CCM na mkulu wake hawana nia ya dhati ya kuung'oa wizi na ubadhirifu kwa sababu ndio unaowastawisha.



mmmmmh haya kaka
 
Huyu mzee wa Ukurutu nimekuwa simwamini tokea aseme kwenye ile ripoti yake ya Richimond kuna mambo ambayo ameficha ili serikali isianguke inamaana alitusaliti sisi wananchi. halafu turudi kwenye mada yeye ni mtaalamu wa mikataba ya kukodisha ndege?

Yeye ni mwanasheria......na Mtanzania pia....halafu ndugu lower the tone please!
 
kuondolewa kwa chizi ni kutokana na mikataba mibovu, ajira yake haikufata taratibu au kushindwa kusimamia shirika?

Hivi mnamwamini mwakyembe??

unataka tukuamini wewe? Kwa lipi kubwa ulilolifanya? Au hiyo kauli yako ya kupinga kila jambo? Kama rais wako kamuamini na kumpa cheo wewe ni nani? Inawezekana hata mjumbe wa nyumba kumi haujawahi kupewa sasa tukuamini kwa lipi? Acha chokochoko na majungu.
 
Back
Top Bottom