Kuikomboa CCM: Watanzania huu ni wakati wa maamuzi magumu!

Malecela, lazima umchukie Lowasa, maana naamini alihusika ktk ile mbinu iliyomnyima ufalme mzee wako, unakumbuka lile tukio la Morogoro?

unakumbuka mama Anne aliporwa kiasi gani alichokuwa anakiwahisha Dodoma, kwa ajili ya kuwahonga NEC wampitishe Malecela Sr? Wewe kizazi cha wafilisi Tanzania unaweza kushika bunduki?

Chuki yako haijaanzia kwako, kwani hata maddam tulimshuhudia akijiita mpinga ufisadi, huku akisahau pesa ya kifisadi aliyopokea toka kwa fisadi papa. Chichidodo
 
Mkuu William kwa heshima yako na ya jina lako, humu forum tunakuheshimu for who you are not what you are, sasa na wewe unapojiingiza kwenye hizi siasa za maji taka, utajivunjia bure heshima yako na kuturudisha kwenye kumbukumbu za uchafu wa majina makubwa!.

Niliwahi kuuliza na leo nauliza tena, hivi Lowassa na Chenge makosa yao ni yepi hadi kustahili kusulubishwa ?!.

Kama kuna wana CCM wana mpaka kesi mahakamani mlisimama kuwaombea kura wananchi ndio wakawapiga chini!, leo mna moral authority gani ya kuwanyooshea vidole Chenge na Lawassa ambao hawajashitakiwa kwa lolote?!.

Mkuu William, una taarifa kwenye baadhi ya maeneo, CCM inashinda sio kwa sababu inapendwa sana, bali kwa mazoea tuu na ku capitalize on ignorance ya Watanzania!.

Mnajipa matumaini mkiziba viraka hilo pakacha lenu litaacha kuvuja hivyo mtatawala miaka 50 mingine!.

By now Watanzania are not as ignorant as they used to be, hivyo mtaji mkubwa ndio huo umeanza kuondoka, mikao ya Kaskazini walishaamka, kanda ya ziwa ndio hao wameamka, mikoa yenye low literacy level kama Dodoma, Singida na mikoa ya Kusini, itachukua muda zaidi lakini hatimaye watafika mahali watalibwaga pakacha la CCM na kulipiga chini puu!.

Tatizo kubwa linalotukabili Watanzania, hatuna serious opposition parties zenye serious strategies na kutuletea ukombozi toka kwenye ukoloni wa chama dola!. Vyama vyenyewe vya upinzani ndio hivi, kelele nyingi, matendo sifuri!.

Tusubiri katiba mpya ili hata sisi tusio na vyama tupate forun ya kuwafungua macho Watanzania ili mshuhudie 2015 mtabakiwa na viti vingapi ndipo uje tena humu na hizo ndoto zako za miaka 50 ijayo!.

Well ni maoni yako Pasco, isipokuwa ni muhimu tukawakumbusha wale wote wanaopewa hela huko kwa Lowassa kwamba hawezi kutununua wote na sitaki kuamini kwamba na wewe umenunuliwa pia!, maana siku hizi anawapenda sana Waandishi wa habari kama wewe na utawajua kwa maneno yao tu!

William @...NYC,USA: Mutuz Le Baharia!
 
Malecela, lazima umchukie Lowasa, maana naamini alihusika ktk ile mbinu iliyomnyima ufalme mzee wako, unakumbuka lile tukio la Morogoro? unakumbuka mama Anne aliporwa kiasi gani alichokuwa anakiwahisha Dodoma, kwa ajili ya kuwahonga NEC wampitishe Malecela Sr? Wewe kizazi cha wafilisi Tanzania unaweza kushika bunduki?
Chuki yako haijaanzia kwako, kwani hata maddam tulimshuhudia akijiita mpinga ufisadi, huku akisahau pesa ya kifisadi aliyopokea toka kwa fisadi papa. Chichidodo

Hajaninunua mkuu na hawezi kuninunua kama anavyowanunua na hizo hela zake chafu, na hawezi kutununua wananchi wote, MUCH RESPECT MKUU SANA!

William @ NYC,USA: Le Baharia!
 
- .... siku Lowassa akipitishwa kugombea Urais nitachukua Bunduki na kuingia msituni and I mean it not in my watch, nilipooona maisha yamekua magumu bongo nilikimbilia Ubaharia, na nilipooona hamsikii vilio vya wananchi nilishiriki kuanzisha kiboko yenu JF, now I am ready kuingia Msituni maana enough is enough!

MUNGU IBARIKI TANZANIA!

William @...NYC,USA: Mutuz Le Baharia!


..Bila shaka itakuwa kwa lengo la kwenda kuwinda Swala, Digidigi, n.k!
 
- Well ni lazima kuweka all the options mezani ili wanaohusika waelewe kwamba wakati wa mchezo umekwisha na no way tutachezeana tena kwenye Urais ujao!

William @..NYC,USA: Mutuz Le Baharia!
hoja ya msingi lakani kuna mwenye usafi kunyoosha mkono au kutupa jiwe la kwanza kwa hao walioza
 
- Wapo wengi ambao ameshindwa kuwanunua, otherwise amenunua wengi sana mpaka huko kwenu Upinzani!

William @...NYC,USA: Le Baharia!
kama inawezekana weka wasafi watatu hapa , lakini wasio maadui kama ni adui ni ngumu kujua ni sababu ipi imefanya hasinunulike, yaweza kuwa ni uadi au uadilifu mimi nalenga waadilifu weka majina mawili matatu kutete hoja yako

ikiwezekana tutajie wa upinzani walionunuliwa
TAIFA KWANZA
 
- Well ni maoni yako Pasco, isipokuwa ni muhimu tukawakumbusha wale wote wanaopewa hela huko kwa Lowassa kwamba hawezi kutununua wote na sitaki kuamini kwamba na wewe umenunuliwa pia!, maana siku hizi anawapenda sana Waandishi wa habari kama wewe na utawajua kwa maneno yao tu!


William @...NYC,USA: Mutuz Le Baharia!
thats what i was thinking too!!!!!!!!
 
Kama Lowassa ni Msafi; Nani Mchafu CCM?


CCM na kujivua gamba


Msomaji Raia - Raia mwema


CHAMA cha Mapinduzi (CCM) kimemaliza vikao vyake mjini Dodoma wiki iliyopita. Kama kawaida yake kwa siku za karibuni, kumalizika kwa vikao vya chama hicho, ni mwanzo wa mnyukano mpya ndani ya chama na maandalizi ya harakati mpya za kumalizana.

Kama wengi wetu tulivyotabiri tangu Aprili, mwaka huu kuwa dhana ya kujivua gamba ndani ya CCM ilikuwadaganya toto, imetokea kweli na safari hii Halmashauri Kuu ya CCM (NEC) imegwaya mbele ya ubabe wa mafisadi na kuishia kuagiza eti suala hilo lirudishwe katika vikao vya ngazi za chini.

Pamoja na utitiri na urefu wa vikao vya maandalizi ya NEC, haikuwezekana kutekeleza dhana ya kujivua gamba kama ambavyo ilikuwa ikipigiwa chapuo na watendaji wapya wa sekretariati ya CCM, wakiongozwana Katibu wa Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye.

Alikuwa ni Nape pamoja na wenzake kina John Chiligati, Wilson Mukama na Mzee Pius Msekwa waliorindima baada ya kikao cha NEC ya April 2011, wakidai mafisadi ni ama wajiondoe haraka ndani ya chama au wafukuzwe ndani ya siku 90.

Walianza kampeni hiyo baada ya kikao hicho wakisafiri kwa barabara na kufanya mikutano katika miji ya Dodoma, Morogoro, Chalinze na kupokelewa jijini Dar es Salaam kwa mbwembwe nyingi. Rais Kikwete alinukuliwa baadaye kidogo akiwa katika uzinduzi wa nyimbo za Injili kuwa aliyokuwa akiyasema Nape Nnauye yalikuwa na baraka za Chama cha Mapinduzi.

Kwa mshangao wa wengi, katika kikao kilichopita, ambacho kilitarajiwa kutekeleza azimio muhimu la NEC ya April, aliibuka Edward Lowassa na kudai bila kigugumizi kuwa alichokifanya akiwa Waziri Mkuu na kutafsiriwa kuwa ni fisadi, kilikuwa na baraka za Rais Kikwete, Baraza la Mawaziri na timu ya makatibu wakuu. Alilalamika wazi kwa jinsi alivyoendelea kudhalilishwa huku uongozi wa serikali na chama ukikaa kimya kana kwamba haujui ukweli wa mambo.

Kimsingi, Edward Lowassa alimaanisha kuwa yeye ni mtu safi kwa sababu alitekeleza yale aliyoelekezwa kutekeleza na kwa hiyo, kujiuzulu kwake kamwe kusitafsriwe kama alama ya kukubali kuwa fisadi. Alikumbusha na kuonya kuwa ikiwa tuhuma tu zinatosha kumfukuza mtu kutoka kwenye chama, basi hata Rais Kikwete asingeweza kuwa Rais, ila kwa busara na hekima za Mzee Mkapa, Rais Kikwete sasa ni Rais pamoja na tuhuma zote alizorundikiwa wakati ule. Kimahesabu, Lowassa alisema ikiwa yeye ni mchafu, basi wote au wengi sana ndani ya CCM ni wachafu, vinginevyo yeye ni msafi.

Tunaambiwa ilibidi Rais Mkapa aingilie kati ili kuzuia Rais Kikwete asijibu tuhuma alizorushiwa na Lowassa na wala watu wasiruhusiwe kuendelea na mjadala huo ulioelekea kuchafua hali ya hewa ndani ya ukumbi.
Hii ni kawaida sana katika falsafa ya utawala wa Kiafrika kwani tuhuma mbaya dhidi ya mtawala huwa haziruhusiwi kujibiwa ili kuepusha hatari ya watu wabishi kuja na ushahidi wa kuthibitisha tuhuma zao dhidi ya mtawala.

Swali la msingi tunalohitaji kujiuliza ni ikiwa Edward Lowassa anadai yeye ni msafi, na baadhi ya wajumbe wa NEC wanakubaliana naye, je ni nani ndani ya CCM ya sasa ni mchafu? Sina maana kuwa Edward Lowassa ndiye alikuwa mchafu peke yake na kwa kuwa sasa inadaiwa ni msafi, kwa hiyo wachafu hawapo! La hasha, hii si maana yangu.

Maana yangu haswa ni kuwa, Edward Lowassa tangu enzi ya hayati Baba wa Taifa, hajawahi kuwa na sifa ya usafi au uadilifu. Yeye ana sifa ya uchapakazi, uthubutu na ukarimu. Tangu enzi hizo na hasa baada ya kuzodolewa na Baba wa Taifa juu ya utajiri mkubwa usiokuwa na maelezo, Edward Lowassa aliingia katika mgogoro mwingine na Rais Benjamin Mkapa pale alipohamasisha Umoja wa Vijana (UVCCM) kugoma kumpigia kampeni baada ya kuteuliwa kuwa mgombea wa nafasi ya urais kupitia CCM, mwaka 1995.

Rais Mkapa alinyenyekea na kukubali masharti aliyopewa na ndipo vijana wakaingia katika kampeni. Hata hivyo, Mkapa aliamua kumwacha nje Edward Lowassa katika serikali yake ya kwanza hadi alipofuatwa na wazee miaka kadhaa baadaye na kumrejesha tena serikalini. Rais Mkapa alikiri baadaye kuwa alimrejesha serikalini kwa heshima ya wazee wale na wala si kwa uadilifu wake.

Edward Lowassa ana kipaji cha kuhamasisha na kutisha watawala wasiojiamini. Alifanya hivyo mwaka 2005 ili kumwingiza Jakaya Kikwete madarakani. Kama alivyodai mwenyewe wiki iliyopita mbele ya NEC, tuhuma nyingi zilimkabili Jakaya Kikwete na kutishia kuondoa jina lake katika kinyanganyiro cha urais.

Edward Lowassa kwa umahiri mkubwa, alikusanya vijana kutoka nchi nzima na kuwaleta Dodoma ili kuwatisha wazee kuwa Jakaya Kikwete asipoteuliwa, CCM ingesambaratika vibaya sana. Pamoja na jeuri yake na msimamo wake, Rais Mkapa aliogopa sana pale alipoitwa na wazee aliowakuta Dodoma na kuambiwa kuwa “chaguo ni Jakaya” vinginevyo Dodoma hapatatosha.

Mkapa alinywea na kujikuta anaimba wimbo wa Jakaya huku Lowassa akiwa anachekelea kwa kejeli ya hali ya juu. Akiwa ni kamanda wa mtandao uliomwingiza Kikwete Ikulu, Lowassa kwa wema na ubaya, aliufahamu udhaifu wa Kikwete na kuufanya mtaji wa kumhujumu wakati wowote. Alichokifanya wiki iliyopita ni utangulizi wa makubwa yajayo.

Mbinu aliyoitumia Lowassa mwaka 2005 kumtisha Mkapa ili kumwachia Jakaya aingie bila mikwaruzo, ndiyo hiyo hiyo aliyoitumia ‘kummaliza’ Kikwete wiki iliyopita mjini Dodoma. Alikusanya makundi ya vijana kutoka sehemu mbalimbali na kuwaleta Dodoma huku akiwachochea kuwa umoja wao unafutwa; aliwakamata wazee kadhaa maarufu katika chama na kuwafadhili; akawakamata baadhi ya wenyeviti wa mikoa; akaigawa sekretariati ya CCM na kisha akawapata Wazanzibari wengi upande wake.

Hii ilitosha kumtisha Kikwete mpaka akawatosa majemedari wake waaminifu akina Nape, Chiligati, Sitta, Membe, Makongoro Nyerere na Kinana. Tishio la kuenguliwa katika nafasi ya uenyekiti wa chama lilimfanya hata amtose katibu wake Mkuu, Wilson Mukama, ambaye ndiye mjenzi wa dhana ya kurejesha hadhi ya chama kwa kuwaondoa wanaokichafua.

Kama ilivyokuwa kwa Mkapa mwaka 2005 kwa watu kudhani amerogwa na nguvu za giza, ndivyo ilivyokuwa kwa Jakaya Kikwete wiki iliyopita ambaye watu wengi wa karibu naye wanaamini amerogwa na nguvu ya “TV Emmanuel” au nguvu ya aina fulani inayomfanya awe na kigugumizi kisicho cha kawaida.

Waafrika ni wepesi wa kuamini ushirikina lakini kilichofanyika si kigeni katika siasa za makundi. Wanasiasa wajanja hutumia mbinu za kuwafitini wenzao kwa kuwatisha kuwa watatoa hadharani madhambi yao na kuwafanya wafyate mikia yao. Edward Lowassa anajua vema kutumia nafasi hii na anaelekea kufanikiwa. Pigo alilotoa kwa Kikwete wiki iliyopita linatishia kabisa kuua fikra zozote za kuibua tena dhana ya ufisadi katika nafasi na haiba ya Edward Lowassa.

Pigo hilo lilimfanya Kikwete akatae au asahau hata kuwapa nafasi ya kuongea wale aliokuwa amewapanga waongee ili kumtetea yeye binafsi au kummaliza Edward Lowassa. Baadhi ya marafiki zake wanaomboleza kwa kunyimwa nafasi ya kumsaidia baada ya Edward Lowassa kuwa amemrushia makombora mazito sana.
Mpaka hapa, bado swali linabaki, ikiwa Edward Lowassa amefanikiwa kujinasua katika tuhuma za ufisadi na kuwafanya washtaki wake wagwaye, ni nani basi anaweza kumzuia kuwa Rais ajaye kupitia CCM?

Je, wale waliokuwa msitari wa mbele kumtuhumu hadharani watafanya nini watakapotakiwa kupanda jukwaani kumnadi kama “tumaini la pili lililorejea”? Jambo moja ni wazi: Uongozi dhaifu waweza kuwafanya mamluki kuwa mashujaa na wahenga wa kizazi husika.








My Take:

Nadhani hiki kipande kinatoa picha kamili!
 
- Wapo wengi ambao ameshindwa kuwanunua, otherwise amenunua wengi sana mpaka huko kwenu Upinzani!

William @...NYC,USA: Le Baharia!

Karibu tena mkuu

turudi nyuma kidogo
nakukumbusha niliwai kuuuliza kuwa ukipata nafasi ya kukutana na rais wetu Kikwete akakuliza kama mwana CCM unashauri afanye nini. Ukajibu kuwa utamwambia tatizo letu Tanzania ni sheria tu

Lakini naona One or two year later sasa unasogea sogea na kukubaliana na reality na unakubali kuna maamuzi magumu yanatakiwa kufanyika.(Kuhusu uongozi na viongozi) So sad ungekuwa kwenye postion hiyo ungepoteza miaka kama miwili kudeal na sheria wakati kichama kilikuuwa na kina uwezo kuwatimua wasiofaa. ( Isipokuwa mwenyekiti) teh teh teh teh

But hamjachelwa sana maamuzi ya 2011 yanaweza kuwa msaada mkubwa kwa chama mwaka 2015
 
- CCM ni lazima ijivue magamba ili kushinda kwa kishindo Mwaka 2015, ni lazima ifike mahali Lowassa na Chenge waondolewe katika nafasi zozote za uongozi wa chama. Lengo la CCM ni lazima liwe ku-invest more in Waheshimiwa kama Januari Makamba, Nape under Supervision ya Wazee kama Sitta, Mwakyembe, na Mwandosya hapa the goal ni kutawala 50 more years. Kwa sababu by then the Nyerere generation itakuwa imekwisha, tutakua na wananchi wasiomjua Mwalimu kabisaa ndipo for the first time CCM tutaanza kupigania kura kwa jasho, my point ni kwamba CCM for that goal haiwezi kuwekeza kwenye mafisadi kina Lowassa.

- CCM ni lazima ijivue kwa sababu kama hawajivui, then Ninawashauri Waheshimiwa Nape na Sitta wajitoe na kuivunja CCM kwa sababu tupo wengi ambao tunalijali hili taifa tutajiunga nao, Lowassa na mihela yake yote hawezi kuanzisha chama cha siasa, he knows that kwamba ni Dead end, na akitoka CCM anajua kwamba CCM haiwezi kuvunjika, lakini for sure 100%, Waheshimiwa Nape na Sitta wakitoka CCM inavunjika vipande, Je Mh. JK yuko radhi kuona CCM inavunjika under his watch? No! So hawa magamba ni lazima waondoke soon as possible or else!

- People this is our Nation na saa ya kuhesabiwa ni sasa, hatuwezi kukaa pembeni kuwaachia mafisadi watuamulie the National agenda, kwanza tuliambiwa Rostam hawezi kuguswa cause ana siri nyingi sana za Mkuu wa Kaya, lakini akavuliwa sasa ni wakati muafaka na Lowassa, Chenge na wengine wengi wakavuliwa, we understand the campaign ya Mafisadi kununua watu wengi kila kona ya taifa, ninasema Wenyeviti wote wa CCM Mikoa kuacha Mheshimiwa Makongoro, na Makatibu wao waondolewe na ikibidi wafukuzwe Chama, wote ni compromise wa Lowassa, Wamenunuliwa tayari. Kuondoka kwa mafisadi wote hakumalizi matatizo yote ya CCM, lakini kunafungua njia ya kujipanga kelekea kwenye utawala wa Respect of the Law!

- Lowassa hajatununua wananchi wote, ninawajua a lot of my friends walionunuliwa tayari shame on you, wewe ndugu yangu ninayesikia umenunuliwa na Shillingi Millioni 100 hivi karibuni na kwamba siku hizi unapewa habari za kuandika na Tanzania Daima, I am shocked na ninakuja soon ninataka tukae uso kwa uso uniangaliae usoni uniambie kwamba hii habari sio kweli, ninajua kwamba Wabunge 75% ya Wabunge wa CCM wamenunuliwa tayari wakiongozwa na Kagasheki ambaye hutamba sana bungeni kwamba hakuna wa kumgusa Lowassa, maaan! you are dead wrong!

- CCM this is my promise to you, siku Lowassa akipitishwa kugombea Urais nitachukua Bunduki na kuingia msituni and I mean it not in my watch, nilipooona maisha yamekua magumu bongo nilikimbilia Ubaharia, na nilipooona hamsikii vilio vya wananchi nilishiriki kuanzisha kiboko yenu JF, now I am ready kuingia Msituni maana enough is enough!

MUNGU IBARIKI TANZANIA!

William @...NYC,USA: Mutuz Le Baharia!

najua unamiliki jf, last time nilijaribu kukuambia ukweli ukamtuma brutus akanipa ban. Wewe ndie ulikua unajifanya unakipenda chama, mwana ccm halisi (kisa mdingi). Sikia, (hata ukinipa ban na leo) na wewe ni mnafiki, mzandiki na mfitini mkubwa. Huna jipya, ni magamba yale yale kafie baharini.
 
Back
Top Bottom