Aibu: Viongozi wote wa CCM, wastaafu na sasa wanaogopa kusema hadharani kwamba Lowassa alihamia Chadema na kugombea Urais 2015

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
117,703
218,247
Screenshot_2024-02-14-16-35-44-1.png
Screenshot_2024-02-14-16-35-34-1.png

Nimefuatilia Hotuba za viongozi karibu wote wa CCM na serikali wa sasa na wastaafu, sijasikia hata mmoja anayesema kwamba Lowassa aliwahi kuhamia Chadema na kugombea Urais kupitia Chama hicho 2015.

Bado sijajua kama wanaogopa kusema au wanaona aibu, hata Warioba anayesifiwa kwa hotuba yake kwenye msiba huo, hakusema baada ya Lowassa kukatwa na ccm 2015 alienda wapi, wala hakusema kilichotokea, aliishia tu kusema Lowassa alikatwa 1995.

Bali kinachofichwa ni kwamba Lowassa alijiunga na CHADEMA august 2015 na kugombea Urais na kushinda kwa kishindo , kabla ya kunyang'anywa Ushindi wake kwa msaada wa "ofisi" ya Masaki iliyoongozwa na watu watatu ambao tutawataja hadharani baada ya mazishi (Liwalo na liwe)

Baada ya dhuluma hiyo " watu wa system " waliofichua uchafu wote uliotendwa hadi Lowassa kuporwa ushindi wakakamatwa na kutupwa gereza la KEKO , bila kufikishwa Mahakamani, japo waliachiwa baada ya miaka mingi , huku wachache wakifa kwa presha na visukari, CCM inafanya siasa za kishamba sana !(HAKUNA ASIYELIJUA HILI)
 
Hiyo maana yake bado tuna siasa za kuwindana nchi hii, ajabu sana, uwepo wa vyama vingi unakaribia miaka thelathini lakini mpaka leo bado CCM hawataki kukubali hilo, mindset yao inaonesha ni jinsi gani hata hilo wazo la uwepo wa vyama vingi lilivyopata upinzani huko CCM.

Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app
CCM ni chama cha kishamba sana !
 
Ni Aibu sana kwa familia kuiruka historia ya Baba yao na kimsingi ni kujitafutia laana
Ni mambo ya kulinda maslahi, kulipa fadhila na kukaa kimkakati wa kujilinda zaidi.

Familia imepitia mengi kipindi cha Magufuli mpaka kurudi kundini.

Kuna jambo fulani lilinisikitisha sana mwaka jana. Kuna kitu Samia alifanya, ah, ilikuwa mkataba wa bandari.

Fredrick Lowassa (MP) mwaka jana alitoa kauli akasema hivi, "kama Mama Samia kaamua hivyo, mimi ni nani nipinge?".

Nikamtafuta na kumpaka sana Freddy kwa kauli ile. Nikamwambia, Freddy, kwa nini unajishusha hivi kwa Samia? You don't need to kowtow kwa Samia hivyo. Wewe ni mbunge.

Baadaye, yale maneno naona niliyafikiria sana. Nikayafikiria kwa empathy, nikayaangalia kutoka upande wa Freddy.

Naona niliyafikiria sana mpaka nikaota ndoto usiku.

Nikaota niko na Freddy shule (tulisoma wote) tunaangalia mpira. Kwenye ndoto nikamfuata Freddy, nikawa bado namlaumu. Namwambia Freddy mbona unajishusha sana kwa Samia? You dont need to do that.

Sasa, kwenye ndoto hapo, Freddy akawa ananiambia, unajua kaka, kwa sasa familia inapitia wakati mgumu sana, Mzee anaumwa sana, inabidi tuwe watiifu kwa serikali tu. Nikajikuta kuwa, badala ya kumshambulia Freddy, nimeanza kumuonea huruma.

Basi kwenye ndoto tukawa tume ji organize shule tunachapisha T-Shirts za charity ya kumuenzi na kum support Lowassa.

Hii ni ndoto tu, lakini ilikuwa kama nachambua mambo mwenyewe at a deeper psychological level.

Nikaifikiria sana ile ndoto. Nikamuhadithia rafiki yangu mmoja anayetujua wote. Akaniambia mtafute Freddy umuulizie hali. Hapo ni mwaka jana mwishoni.

Nikasema nitamtafuta Freddy. Baadaye nikawa na kazi nyingi nikasahau. Nikasema haya ni mambo ya ndoto tu. Freddy is a busy MP, sitaki kumsumbua kwa mambo ya ndoto tu.

Juzi kwenye msiba, nikamsikia Freddy anavyosema bila Samia Mzee Lowassa asingefika hata hiyo siku aliyofariki. Kwamba serikali imewapa msaada mkubwa.

Nikasema kuwa, ingawa sikumtafuta Freddy kumjulia hali, ila yale maongezi yangu naye niliyoyaota ni kama nilikuwa naongea naye, kwa sababu ndiyo mule mule alipokuja kusema katika msiba.

So, familia ipo karibu sana na serikali kiasi kwamba hata wao wanaogopa kui embarass serikali kwa kutaja historia ya Lowassa upinzani.
 
Ni mambo ya kulinda maslahi, kulipa fadhila na kukaa kimkakati wa kujilinda zaidi.

Familia imepitia mengi kipindi cha Magufuli mpaka kurudi kundini.

Kuna jambo fulani lilinisikitisha sana mwaka jana. Kuna kitu Samia alifanya, ah, ilikuwa mkataba wa bandari.

Freddy mwaka jana alitoa kauli akasema hivi, "kama Mama Samia kaamua hivyo, mimi ni nani nipinge?".

Nikamtafuta na kumpaka sana Freddy kwa kauli ile. Nikamwambia, Freddy, kwa nini unajishusha hivi kwa Samia? You don't need to kowtow kwa Samia hivyo. Wewe ni mbunge.

Baadaye, yale maneno naona niliyafikiria sana. Nikayafikiria kwa empathy, nikayaangalia kutoka upande wa Freddy.

Naona niliyafikiria sana mpaka nikaota ndoto usiku.

Nikaota niko na Freddy shule (tulisoma wote) tunaangalia mpira. Kwenye ndoto nikamfuata Freddy, nikawa bado namlaumu. Namwambia Freddy mbona unajishusha sana kwa Samia? You dont need to do that.

Sasa, kwenye ndoto hapo, Freddy akawa ananiambia, unajua kaka, kwa sasa familia inapitia wakati mgumu sana, Mzee anaumwa sana, inabidi tuwe watiifu kwa serikali tu. Nikajikuta kuwa, badala ya kumshambulia Freddy, nimeanza kumuonea huruma.

Hii ni ndoto tu, lakini ilikuwa kama nachambua mambo mwenyewe at a deeper psychological level.

Nikaifikiria sana ile ndoto. Nikamuhadithia rafiki yangu mmoja anayetujua wote. Akaniambia mtafute Freddy umuulizie hali. Hapo ni mwaka jana mwishoni.

Nikasema nitamtafuta Freddy. Baadaye nikawa na kazi nyingi nikasahau. Nikasema haya ni mambo ya ndoto tu. Freddy is a busy MP, sitaki kumsumbua kwa mambo ya ndoto tu.

Juzi kwenye msiba, nikamsikia Freddy anavyosema bila Samia Mzee Lowassa asingefika hata hiyo siku aliyofariki. Kwamba serikali imewapa msaada mkubwa.

Nikasema kuwa, ingawa sikumtafuta Freddy kumjulia hali, ila yale maongezi yangu naye niliyoyaota ni kama nilikuwa naongea naye, kwa sababu ndiyo mule mule alipokuja kusema katika msiba.

So, familia ipo karibu sana na serikali kiasi kwamba hata wao wanaogopa kui embarass serikali jwa kutaja historia ya Lowassa upinzani.
Sawa sawa nimependa hiyo connection ya ndoto na alichosema Fredy

Kifupi familia inacheza mdundo mpya isingependa kurudi nyuma ...
 
Inapofikia stage ya kuogopa kutaja jina la Chadema kwenye msiba wa Lowassa, wakati mwingine naona ni uoga tu usiokuwa na maana kwa wahusika, hasa familia ya marehemu.

Sitaki kuamini kwamba familia ya marehemu "ingeadhibiwa" simply kwa kulitaja jina la Chadema msibani.

Lakini baadae naona kama inawezekana yote yaliyotokea yalikuwa planned, na haikuwa huruma tu ya familia ya Lowassa kwa serikali bila sababu.

Nasema hivyo kwa sababu, hata nikitazama matukio yaliyotangulia msiba.

Mfano: mwakilishi wa Chadema kutopewa nafasi ya kuhutubia msibani, na jina la Chadema kutotajwa msibani kama marehemu aliwahi kupita kule.

Hayo yanaonesha familia ya Lowassa inawezekana kabisa ilipewa maelekezo wafanye hivyo, hata kama wenyewe hawakupenda.

Naamini Chadema ilimuinua Lowassa na familia yake, ikawarejeshea tabasamu na tumaini walilopoteza wakati wakiwa, na kuondoka CCM, sijui mioyo ya hii familia ina hali gani wakikumbuka hayo.

Back
Top Bottom