The Analyst
JF-Expert Member
- Feb 26, 2011
- 464
- 246
Si lazima iwe kweli lakini inaonekana zaidi kwamba Couples wengi wanapendana kwa viwango vinavyotofautiana. Hata kama wote wanakiri kupendana kwa dhati namna gani, bado ni ngumu kuthibitisha kwamba kwa wakati wowote mmoja katika kuishi kwao, wawili hawa watakuwa wanapendana kwa viwango sawa. Binafsi nimejijengea theory kwamba atakayefall kwanza atakuwa mpendaji mkubwa siku za mwanzo na atakuwa mbembelezaji wakati huyu mwingine atafall taratibu kwa kubembelezwa. Akinogewa na raha na kufall basi atamjali sana huyu wa mwanzo na wakati huo wa mwanzo atajihisi kupumzika baada ya kukamilisha kazi ngumu. Atafurahia kwa deko za kila aina na wakati huu yeye hata wivu hupungua na huyo wa pili kufall inawezekana akawa na wivu sana wakati huu.
Pia wapo ambao muda mwingi utagundua eidha mke au mume pekee ndiye mwenye kujali vitu vingi na vidogovidogo katika mahusiano yao.
Unamkuta mama kwa mfano, ndiye siku zote analalamika bwana kutokuwa romantic na kutomjali wakati bwana anaishi kwa staili kama vile Bora liende. Hajali sana mambo kama mara ya mwisho amebusiwa lini nk.
Kwa ufupi (hata kama mifano hailipi saana!) kuna kupendwa zaidi ya unavyopenda na kupo kupenda zaidi ya unavyopendwa. Ndiyo maana basi swali langu likawa hivi Kipi bora; Upende zaidi au upendwe zaidi? Hakuna kupendana kuliko lingana kama mia kwa mia. Tafadhali wanajamvi, naomba tujadili hili.