Kipi Bora; Upende Zaidi Au Upendwe Zaidi? Hakuna Mia Kwa Mia!

Tatizo lingine kila mtu anatamani kupendwa,hakuna alie tayari kupenda,wote tuna njaa ya kupendwa,wote hatukufundishwa kupenda hivyo ni vigumu kujua kupenda,tunatamani kupewa kitu tusichokijua na tunadaiwa kutoa kitu tusichokijua,hapo inakuwa ni kazi sana,tungejua kupenda ni nini tusingedai kupendwa kwani hatuhitaji kupendwa jukumu letu ni kupenda tu!
 
Hivi kuna 10% au 50% au 100% kupenda???
Mimi sijali kama Ninapendwa na mimi Ninapenda inatosha, nadhani ni mawili either napendwa au sipendwi..
Na kila kitu kikizidi ni karaha..., cause sitapenda mtu anywe sumu eti sababu nimechelewa kurudi, au kunibana hadi nishindwe kupumua...
 
Kama ni kuzidiana katika kupenda basi inakuwa raha pale unapopenda na wewe unapendwa na pale unapopendwa na wewe unapenda pia, tofauti ya hapo ndio pale unapompenda mtu kumbe yeye yuko on the other side of the coin.
najua tunapendana sana lkn najiskia vzr sana pale nnapohisi kuwa unanipenda zaidi....lol
 
Yeah! Japokuwa ni relative sana kuweza kukokotoa lakini kuna imani ya kuwepo upendo au mapenzi zaidi au pungufu katika mahusiano. Mfano kuna mmoja ukimwambia partner wake kaja basi hata kama anafanya shughuli fulani ujue itamshinda ili akamwone, wakati huyo mwingine ni vigumu kwake kuacha jambo lolote analofanya just b'se mpenzi wake kaja. Mifano mizuri inakuwa katika kiwango cha kujitoa kati yenu. Baadhi tunaamini kwamba katika mapenzi mara nyingi hamuwezi kujitoa kwa kiwango sawa na yule anayejitoa kidogo kidogo huchukuliwa kama anayependa kidogo ukilinganisha na anayejitoa zaidi. That was the point.
Hivi kuna 10% au 50% au 100% kupenda???
Mimi sijali kama Ninapendwa na mimi Ninapenda inatosha, nadhani ni mawili either napendwa au sipendwi..
Na kila kitu kikizidi ni karaha..., cause sitapenda mtu anywe sumu eti sababu nimechelewa kurudi, au kunibana hadi nishindwe kupumua...
 
Nipende zaidi ila nisifanyiwe vituko tu. Hakuna kitu kinachoumiza nafsi kama kuwa na mtu anayekupenda sana halafu wewe habari huna. Napenda nipende zaidi hadi nichanganyikiwe. Lol! Ila vituko visiwepo.
 
Huyu jamaa ktk avatar yako alinusurika kufa kweli? Sorry, I couldn't help it.
its true brother i agree with u 100% .....mwanamke ukionyesha unampenda atakutesa saaaana i had proof on this
 
Back
Top Bottom