Kipi bora kubadilisha oil kwa kuangalia muda au kwa kuzingatia mileage?

geranteeh

JF-Expert Member
May 21, 2015
266
618
Habari zenu wakuu heri ya mwanzo wa wiki ambayo ndani yake tunatarajia sikukuu. Kama ilivo ada leo ningependa kuzungumzia kitu ambacho kuna debate kubwa sana ndani yake kwa madereva na mafundi wa magari. Kuna watu wanaamini ni bora kubadilisha oil kila baada ya km 3000 au labda 5000 hata kama hiyo oil imekaa kwa mwaka naa kwani hutegemea na mtu anatumia vipi gari yake kuna mwingine anatumia gari mara chache sana.

Lakini kuna wale wanaoamini gari inatakiwa kubadilishwa oil kila baada ya miezi sita haijalishi imefika kilometa husika au haijafika yani mtu anaweza tumia oil ya km 5000 ndan ya miezi sita akaenda km 2000 asifikishe 5000 then akabadili oil husika. Mpaka hapo nadhan kwa wale ambao hawajaelewa wameelewa mada ambayo naizungumzia hapa hivo mpaka sasa tutakuwa tunaenda pamoja.

NI NINI KAZI YA OIL KWENYE ENGINE?
Kabla hatujaenda mbele ni bora tukajua kazi ya oil kwenye gari. Kiufupi ndani ya mashine au engine kuna vitu vingi sana vinatokea ambapo kuna parts zina move na kutengeneza msuguano so oil inakua ni kama uteute ambao unapoza huu msuguano kumbuka huu msuguano ndio unaotengeneza kinetic power kuwa heat au joto ambalo ukichanganya na mlipuko wa mafuta kuelekea ufanyaji kazi wa gari yani kiufup process ni ndefu lakin najaribu kukuonesha umuhimu wa oil ni wa lazima hivo ni muhimu sana kuelewa hili somo kwani ubora wa oil huleta engine yenye afya.

Katika utumiaji wa oil tunaweza sema kwamba oil imekwisha ubora wake au si salama kuendelea kutumia kwa kadhaa ambazo ni Joto la oil, Impurities ambazo zinajumuisha (dust,water na fuel) na mwisho kabisa ni additives (viungio) ambavyo viliwekwa kweny hii oil so ikitumika basi vinapungua kama si kuisha nadhani tutakuwa tumeelewana tukisema mkuu oil yako umeitumia imepungua ubora inahitaji ubadilishe basi ukisikia hivo. Basi hivo vitu hapo juu vimepungua kama si kuisha kwenye oil yako sasa tutaiita oil chafu.

NI WAKATI GANI SAHIHI WA KUBADILI OIL? KWA KUZINGATIA MUDA AU UMBALI WA GARI ULIOTEMBEA?
1. Kubadili oil kwa kuzingatia umbali wa gari uliotembea.
Katika hili pia kuna mjadala mkubwa sana miongoni mwa watumiaji wa magari kwani kuna wataalamu ambao wanasema unatakiwa kubadili oil kila baada ya km 3000 na kuna wanaosema 5000 na kuna wale wasemao 3000 inakuwa ni usumbufu sana ni bora ubadilishe kila baada ya km 7500.

Kubadili kwa oil katika upande huu kunatokana na quality ya oil ambayo unaitumia kama ilivokua recommended na mtengenezaji wa gari yako na ndo maana tunasema kama unaipenda gari yako lazima utaisoma. Hivi ni nini kinachokuzuia ku google reccomended engine oil ya gari yako?

Ukishasoma recommended oil ya gari yako then utajua gari yako inahitaji oil ya aina gani mfano tuseme inahitaji castrol 5W30 SN oil. Baada ya hapo iangalie hiyo oil ambayo ni recomended kwa gari yako je inahitaji kutumika kila baada ya muda gani? Tukirudi kwenye mfano wa Castrol. Hapo juu hiyo oil inahitaji kubadilishwa kila baada ya km 5000 so unakua ushapata jibu.

Lakini kwa upande mwingine pia kubadilisha oil kunategemea na hali ya gari yako. Kwa mfano gari ambayo ilitengenezwa mpya na mtengenezaji aka recommend kwa aina ya engine basi ubadili oil husika kila baada ya km 5000 basi huwezi fanya hivo kwa gari hiyo hiyo ambayo ishatumika kwa maelfu ya kama yani namaanisha gari ishaenda km 80,000 kwenye odo kuna vitu vingi sana vimeshaanza kuchoka kwenye parts za engine hivo basi huwez sema utabadili baada ya km 5000 hivo basi ni lazima ile interval ya kubadili ibadilike kwa mfano badala ya kumaliz km 5000 utaenda km 4000 au 3000 so kwa kibongo bongo umeweka oil ya km 6000 usijaribu kwenda hizo km nenda hata 4000 then ibadili.

2. Kubadili oil kwa kuzingatia muda uliotumia gari
Kama nilivoelezea hapo juu oil ya gari yako imeundwa na components (viambata) aina mbalimbali hivo basi kadiri unavotumia gari yako basi na viambata hivi hupungua ubora na kuelekea kuisha kabisa ubora wake na hii huathiri utendaji kazi wa gari yako.

Kuna wataalamu hushauri kubadili oil yako kila baada ya miezi sita au atleast mara moja kwa mwaka kwa estimation ya km 12000 mpaka 17000 ambazo dereva atakuwa ametumia kwa mwaka mzima. Yani kama si mtu wa safari ndefu ndefu mara kwa mara yan town trip na huna uhakika wa kumbukumbu zako ni vema ukabadili kila baada ya miez sita.

KIPI BORA KATI YA KUBADILISHA KWA MUDA AU UMBALI WA GARI?
Kwa umakini zaidi naomba niliongelee hili kulingana na source mbalimbali nilizosoma. Kumbuka tulisema katika hatua mbalimbali za mlipuko ndani ya engine yako mafuta yanatengeneza carbon na uchafu mbalimbali ambao huenda kuganda katika sehemu za engine hivo basi uchafu huu oil hubeba huu uchafu na kuugeuza kuwa katika molekuli ndogo sana na kuhifadhi katika oil so kadiri unavozidi kutumia inamaana hivi vitu vinaongezeka ndani ya oil yako na mwisho vikizidi huanza kurudi katika sehem vilipotoka yani uwezo wa kuviondoa unapungua na kupelekea kurudishwa badala ya kubeba inarudisha na kubeba so nimejitahidi kuelezea kwa namna ambayo umeelewa umuhim wa kubadili oil ya gari yako mara kwa mara.

Lakini pia wakati sahihi wa kubadili oil ya gari yako kunategemea na sababu mbalimbali kama vile ubora wa oil, Aina ya oil na uendeshaji wa gari yako kwa mfano kuna watu hutumua miez minne kufikisha km 10,000 wazee wa trip lakin kuna ambao hutumia mwaka au zaid kufikisha 10,000km nadhan hapo usjaona ugumu wa kukadiria njia sahihi kati ya muda au umbali.

Watengenezaji mbalimbali wa magari hushauri kwamba ni bora ukabadili oil ya gari yako mapema iwezekanavyo endapo gari yako umehisi tufaut hata kama hujafkisha kilometer au muda husika na ndiyo maana inashauriwa baada ya mwaka ubadili oil ya gari yako hata kama hujafikisha umbali husika yani kama oil yako ni km 5000 na hujafika hata 4000 ndani mwaka unashauriwa kubadil oil Ya gari yako japo wataalam wengi wameshikilia kwamba mwaka mmoja unatosha kubadili oil ya gari yako hata kama umeenda km 1000 katika 5000 kwani kumbuka kuna viambata ambavyo vipo so mwaka mmoja unatosha kabisa kupungua kwa ubora kwa viambata nilivoelezea hapo juu.

Nadhani utalua umejifunza kitu na unatakiwa kujua upo kwenye kundi lipi kati ya makundi hayo mawili yani kuna wale wa trip za mkoa kwa mkoa au nchi kwa nchi na kuna wale wa mjini tu ambao huchukua mda sana kufika km husika so somo hili natumai litakuwa ni funzo kubwa sana.

Makala hii imeandikwa na Hamis Mgaya

download.jpg
 
Kwa gari yenye 1000cc na kushuka chini, badili oil kila baada ya km 2000, bila kubadili oil filter. Badili oil filter kila baada ya km 4000.

Kwa gari yenye 1001cc - 1500 cc, badili oil kila baada ya km 2500, badili oil filter kila baada ya km 5,000.
Kwa gari ya 1501cc - 2500cc, badili oil kila baada ya km 3,000, badili oil filter kila baada ya km 6,000.

Kwa gari ya 3,000cc na kuendelea yenye piston sita, waweza badili oil na oil filter kila baada ya km 5000.
Hii ni kwa gari za Petrol.

Kwa gari za Diesel, waweza kubadili oil na filter kila baada ya km 5,000 kwa magari ya light duty.
Kwa heavy duty, jitahidi isizidi km 10,000 hasa kwa hizi gari za kichina. Fanya hivi ili injini ya gari yako idumu.
 
Asante mkuu lakin kumbuka hujazingatia vitu vitatu nilivovitaja kwa maana aina ya oil kwan ubora unatofautiana mfano Castrol huwez ifananisha na gp lakini je kwa hii ulosema cc 1000 imepita zaid ya mwaka sijafikisha hiyo km 2000 inakuaje?
 
Unaweza fanya unavyopenda. Lakini kama unataka gari lako lidumu, fuata niliyokuelekeza.
 
Ungesema pia kuwa maelezo yako ni kwa oil za kawaida zilizojaa mtaani ila sio kwa Synthetic Oil ambazo zimetengenezwa kwa teknologia inayoziwezesha kutembea KMS nyingi zaidi
Hicho ndicho nilichokua namwambia mfano oil ya castrol uniambie uende km 2000 kweli?
 
Tatizo lipo Kwa oil filter za bei rahisi..oil filter inauzwa Tsh 5000 - 10,000 alafu unategemea iweze kuhimili km 5000 ni ndoto
Kwangu Mimi nabadilisha Kila baada ya km 4000
 
Tatizo lipo Kwa oil filter za bei rahisi..oil filter inauzwa Tsh 5000 - 10,000 alafu unategemea iweze kuhimili km 5000 ni ndoto
Kwangu Mimi nabadilisha Kila baada ya km 4000
Kweli kabisa mkuu hapa ni kweli lakini naamini ni ile kasumba tu ya kupata vitu vya bei rahisi lakin filter original zinapatikana vizuri kabisa sawa sawa na issue ya plug
 
Boss nilichoongea si maelezo ni swali ambalo nahitaji namm kujifunza pamoja na wngine wajifunze ndo maana mwishoni kuna alama ya kuuliza
Sorry but I ve got to many things in my head to deal with.
I only talk about major things. The rest of u got deal with minor details..
 
Kwa gari yenye 1000cc na kushuka chini, badili oil kila baada ya km 2000, bila kubadili oil filter. Badili oil filter kila baada ya km 4000.

Kwa gari yenye 1001cc - 1500 cc, badili oil kila baada ya km 2500, badili oil filter kila baada ya km 5,000.
Kwa gari ya 1501cc - 2500cc, badili oil kila baada ya km 3,000, badili oil filter kila baada ya km 6,000.

Kwa gari ya 3,000cc na kuendelea yenye piston sita, waweza badili oil na oil filter kila baada ya km 5000.
Hii ni kwa gari za Petrol.

Kwa gari za Diesel, waweza kubadili oil na filter kila baada ya km 5,000 kwa magari ya light duty.
Kwa heavy duty, jitahidi isizidi km 10,000 hasa kwa hizi gari za kichina. Fanya hivi ili injini ya gari yako idumu.
Hizi ni gari au pikipiki?

Yaani uweke Oil fully Synthetic halafu uje ubadili baada ya 2000Km? Mkuu I hope hii ni joke.

Labda kama huo ushauri unautoa kwa Oils za kupima.
 
Back
Top Bottom