Kinachoendelea Loliondo: Shame on them! - Mwinyi, Mkapa, and Kikwete!

Wamasai wa Loliondo lazima waletwe kwenye karne ya 21 kama watanzania wengine. Mambo ya kuwafanya kama kivutio cha watalii kama nyumbu hayana ubinaadamu.

Mbuga ya Loliondo ni hifadhi ambayo inaleta fedha za kigeni, kwa hiyo lazima watu waondolewe kama maeneo ya makabila menginr yalivyo chukuliwa kuwezesha miradi ya maendeleo kwa manufaa ya watanzania wote.
Unachojaribu kusema ni kuwa unatamani kuua utamaduni wa kimasai sio? Unajua kwanini UNESCO iliitangaza Ngorongoro kuwa urithi wa Dunia?
 
Baada ya kuligusa suala la Meremeta nilidokeza kuwa ripoti tunayoifanyia kazi sasa ni ile ya kuelezea historia ya ufisadi wa makuwadi wa wizi wa kimataifa ulioanzia Loliondo na kugusa Ikulu yetu (chini ya Mwinyi) hadi suala Meremeta ambalo nalo liligusa utawala wa Mkapa, na suala la Dowans linalogusa utawala wa Rais Kikwete.

Lakini kabla hatujafika huko kote hatuna budi kusikitishwa na taifa letu kurudi nyuma tena karibu miaka 17 sasa kwenye kashfa ya Loliondo. Kama nilivyodokeza kwenye suala la Loliondo::connections watu wale wale waliokuja kama wawekezeji wamerudi tena na watarudi tena na kutufanya sisi tuwe watumwa katika nchi yetu.

Kampuni ya OBC ya UAE mdau wake mkubwa ni Brigadier wa jeshi la UAE na mtu wa karibu wa familia ya mtawala wa huko. Kwenye Dowans kampuni hewa ya Dowans (ambayo JK hakufuatilia kama vile hakufuatilia Richmond) nayo inamilikiwa na Generali wa jeshi hilo hilo la UAE na ambaye naye ana ukaribu na watu wa familia hiyo.

Kama vile tulio na wazimu katika vichwa vyetu tukawa tayari kupiga magoti mbele ya watu hawa hawa na kuwanyanyasa watu wetu ili tuwafurahishe makuwadi wa ufisadi wa kimataifa. Wamasai wa Loliondo leo hii wanaitwa wakimbizi katika nchi yao na malalamiko yao hayapewi kipaumbele wala kutiliwa maanani!

Na ni watu hawa hawa wa familia ile ile waliojaribu kuchukua eneo la Yaeda Chini na kusababisha njaa kwa watu wetu na watawala wetu wakawatetea; watu wa familia ile ile ya kina Zayed. Angalau kwenye kesi ya Bonde la Yaeda Chini tuliweza kupiga kelele na kuwatimua lakini Loliondo na Dowans hawako tayari kutuachilia.

Hawa watu wanatuahidi vitu gani hadi tuwe wanyonge na dhaifu mbele zao utadhani mbwa mbele ya chatu? Hawa majenerali wenye nyotanyota wanawaahidi nini watawala wetu na wanalainika mbele zao kama waliolishwa limbwata za kitanga?

Hadi inafika mahali waliochaguliwa na wananchi wanawatetea makuwadi wa ufisadi wa kimataifa ambao rekodi yao iko wazi ya jinsi gani wametumia vibali tulivyowapa vibaya, jinsi gani wameua wanyama wetu kiholela na kutorosha wanyama hai kwenda makwao kwa fahari ya watawala wa huko.

Kama vile watawala hawa hawa walivyoruhusu madini yetu kule Buhemba kuchotwa na mamluki wa kivita wa Afrika ya Kusini na kuendelea kutuimbia wimbo wa umaskini wetu huku tukijichekelesha mbele yao.

Nani alitulaani? Tuache kupiga kelele ili wauze hadi nepi za watoto wetu, na vitanda vya vikongwe vyetu vipigwe mnada? Tuache kuandika na kuhoji yanayotokea nchini mwetu kwa vile wao ni watawala? Tuache kuliamsha taifa kutoka katika usingizi wake kwa sababu tukifanya hivyo tunawaudhi wanaotembea na ving'ora na kutetemewa wakitembea?

Mnatupa uchaguzi rahisi; mnatupa uchaguzi ambao hatuwezi kuacha kuuchukua; ni uchaguzi usiohitaji shahada za Harvard wala utaalamu wa fizikia ya anga za mbali. Hatuwezi kufumba macho yetu na vinywa vyetu ili mtutawale mpendavyo.

Jifunze kuhusu original Loliondo Scandal ambayo inahisiwa kuhusishwa na kifo cha mwandishi mahiri wa uchunguzi Stan Katabalo hapa Bonyeza Hapa

View attachment 1021624

Napenda kujua msimamo wa wabunge wafuatao kuhusu Loliondo:

Dr. Harrison Mwakyembe
Lucas Selelii
mama Anna Kilango
Mzee Yusuph Makamba
John Chiligati
Samwel Sitta (Spika)

NB: Nilituma salamu kwa Apson na Mboma wiki chache zilizopita; nikatoa wito kwa RO juu ya kuwadi wenu. Mtu wenu mliyemtuma (DB) nimempa ujumbe wangu wa ana kwa ana wiki moja sasa (bahati mbaya kwenu, taarifa za ujio wake zilimtangulia); natumaini ameufikisha pasipo kuongeza chumvi. Endeleeni tu, kwani historia yenu imeonesha mmesimama upande wa kushindwa mara zote.
Ka mwinyi ni kazee ila kajiziii, kana laana sana na moto wa jehenamu lzm ukaangazie
 
Mwanakijiji political analysis zimeshindwa kuelezea tatizo letu. Hata sociological analysis zimegonga mwamba. Kilichobaki ni psychoanalysis/psychological analysis - we must be very very sick upstairs! Kumbuka adui wakuu 2 kati ya wale 3 ni Maradhi na Ujinga!
Wengine tunaposikia ya bandari tunaangalia na kusema "ni wale wale "...Kuna jipya Tanzania?
 
tulipokuwa wadogo kuna mafundi hasa mafundi mbao na ujenzi au fundi redio,ambao walikuwa mafundi wabovu tulikuwa tunawaita "fundi mangungu"
sasa naona huyu waziri wa jk nae tumwite
"waziri mangungu"
Heshima yako mkuu
 
Heshima yako mkuu

Thread hii ni moja ya thread zilizompa umaarufu Mwanakijiji Hadi Akanunuliwa kumtetea Magufuli yeye na DK Slaa...sasa wameanza tena kutafuta masifa wanunuliwe au aje Rais mkristo mwenzao wanyamaze kimyaa kabisa kama walivyo nyamaza wakati wa JPM
 
nyererer alishiriki kuwachagua mwinyi na mkapa.he must share the blame.....

Na alikuwa kwenye nafasi ya kuweka Katiba yenye kukidhi mahitaji ya wananchi wengi lakini aliishia kusema “ kwa Katiba hii akija kupatikana Rais kichaa itakuwaje sijui”

Bila kuchukua tahadhari ya vitendo akatuachia msala .

Matharani kusema Rais asishitakiwe ni kosa kubwa la kikatiba.

Kwamba Rais hakosei yeye anafanana Na Mungu?

Hivi WaTZ wamerogwa?

Ona sasa yanayoendelea
 
Dhana ya kuzuia Rais asishitakiwe ililenga kufanya asilazimishe kubaki madarakani hasa kama ana madudu anajua akitoka Tu mahakamani...

Ililenga kufanya ajione safe hata baada ya kutoka madarakani...ili aje mwingine arekebishe
 
Japokuwa sijakuelewa lakini naomba nijibu,

Je Kwa hiyo kwa nyakati hizi Kuna haja iendelee kuwepo au imeshapitwa na wakati kwa mtazamo wako?

Na kwa kuangalia huko Duniani wenzetu wanawashitaki marais kila leo maana Dunia sasa imekuwa kijiji sababu ya technology.
 
Aisee
Baada ya kuligusa suala la Meremeta nilidokeza kuwa ripoti tunayoifanyia kazi sasa ni ile ya kuelezea historia ya ufisadi wa makuwadi wa wizi wa kimataifa ulioanzia Loliondo na kugusa Ikulu yetu (chini ya Mwinyi) hadi suala Meremeta ambalo nalo liligusa utawala wa Mkapa, na suala la Dowans linalogusa utawala wa Rais Kikwete.

Lakini kabla hatujafika huko kote hatuna budi kusikitishwa na taifa letu kurudi nyuma tena karibu miaka 17 sasa kwenye kashfa ya Loliondo. Kama nilivyodokeza kwenye suala la Loliondo::connections watu wale wale waliokuja kama wawekezeji wamerudi tena na watarudi tena na kutufanya sisi tuwe watumwa katika nchi yetu.

Kampuni ya OBC ya UAE mdau wake mkubwa ni Brigadier wa jeshi la UAE na mtu wa karibu wa familia ya mtawala wa huko. Kwenye Dowans kampuni hewa ya Dowans (ambayo JK hakufuatilia kama vile hakufuatilia Richmond) nayo inamilikiwa na Generali wa jeshi hilo hilo la UAE na ambaye naye ana ukaribu na watu wa familia hiyo.

Kama vile tulio na wazimu katika vichwa vyetu tukawa tayari kupiga magoti mbele ya watu hawa hawa na kuwanyanyasa watu wetu ili tuwafurahishe makuwadi wa ufisadi wa kimataifa. Wamasai wa Loliondo leo hii wanaitwa wakimbizi katika nchi yao na malalamiko yao hayapewi kipaumbele wala kutiliwa maanani!

Na ni watu hawa hawa wa familia ile ile waliojaribu kuchukua eneo la Yaeda Chini na kusababisha njaa kwa watu wetu na watawala wetu wakawatetea; watu wa familia ile ile ya kina Zayed. Angalau kwenye kesi ya Bonde la Yaeda Chini tuliweza kupiga kelele na kuwatimua lakini Loliondo na Dowans hawako tayari kutuachilia.

Hawa watu wanatuahidi vitu gani hadi tuwe wanyonge na dhaifu mbele zao utadhani mbwa mbele ya chatu? Hawa majenerali wenye nyotanyota wanawaahidi nini watawala wetu na wanalainika mbele zao kama waliolishwa limbwata za kitanga?

Hadi inafika mahali waliochaguliwa na wananchi wanawatetea makuwadi wa ufisadi wa kimataifa ambao rekodi yao iko wazi ya jinsi gani wametumia vibali tulivyowapa vibaya, jinsi gani wameua wanyama wetu kiholela na kutorosha wanyama hai kwenda makwao kwa fahari ya watawala wa huko.

Kama vile watawala hawa hawa walivyoruhusu madini yetu kule Buhemba kuchotwa na mamluki wa kivita wa Afrika ya Kusini na kuendelea kutuimbia wimbo wa umaskini wetu huku tukijichekelesha mbele yao.

Nani alitulaani? Tuache kupiga kelele ili wauze hadi nepi za watoto wetu, na vitanda vya vikongwe vyetu vipigwe mnada? Tuache kuandika na kuhoji yanayotokea nchini mwetu kwa vile wao ni watawala? Tuache kuliamsha taifa kutoka katika usingizi wake kwa sababu tukifanya hivyo tunawaudhi wanaotembea na ving'ora na kutetemewa wakitembea?

Mnatupa uchaguzi rahisi; mnatupa uchaguzi ambao hatuwezi kuacha kuuchukua; ni uchaguzi usiohitaji shahada za Harvard wala utaalamu wa fizikia ya anga za mbali. Hatuwezi kufumba macho yetu na vinywa vyetu ili mtutawale mpendavyo.

Jifunze kuhusu original Loliondo Scandal ambayo inahisiwa kuhusishwa na kifo cha mwandishi mahiri wa uchunguzi Stan Katabalo hapa Bonyeza Hapa

View attachment 1021624

Napenda kujua msimamo wa wabunge wafuatao kuhusu Loliondo:

Dr. Harrison Mwakyembe
Lucas Selelii
mama Anna Kilango
Mzee Yusuph Makamba
John Chiligati
Samwel Sitta (Spika)

NB: Nilituma salamu kwa Apson na Mboma wiki chache zilizopita; nikatoa wito kwa RO juu ya kuwadi wenu. Mtu wenu mliyemtuma (DB) nimempa ujumbe wangu wa ana kwa ana wiki moja sasa (bahati mbaya kwenu, taarifa za ujio wake zilimtangulia); natumaini ameufikisha pasipo kuongeza chumvi. Endeleeni tu, kwani historia yenu imeonesha mmesimama upande wa kushindwa mara zote.
Duh haya yalisemwa zamani sana na hivi karibuni tumeshuhudia, jweli lisemwalo lipo😭
 
Back
Top Bottom