Tanzania inatakiwa kuvunja Mkataba wa Loliondo!

Yesu Anakuja

JF-Expert Member
Apr 10, 2019
9,488
19,288
HIli suala la Mkataba wa Loliondo halijaongelewa tu na wananchi au na wamasai tu, kuna tuhuma nyingi, zingine hatujui kama ni za kweli au za uongo. mara tuambiwe ukiwa pale Loliondo network ya simu ni ya uarabuni sio ya kibongo, mara tuambiwe kuna uwanja wa ndege kule madege huwa yanatua na kubeba wanyama wale tunaoambiwa wametengenezewa mbuga jangwani uarabuni, mara tuambiwe ardhi ile iliuzwa mazima sio part of Tanzania ni ardhi ya waarabu. Tunaomba mnaojua mtueleweshe yafuatayo:

1. Loliondo iliuzwaje, iliuzwa iwe milki ya waarabu au waliwekeza tu kitalu cha uwindaji?

2. Kuna kiwanja cha ndege? Pale kinafanya nini hasa tukizingatia tuliona lidege la kivita limedondoka pale na mfalme wa UAE wakisalimiana na Kinana?

3. Mkataba wa Loliondo ni wa milele au wa muda fulani?

4. Maaskofu walisoma kitabu cha Mwinyi, wanasema alikiri kwenye kitabu hicho kwamba alifanya makosa na anajutia mkataba wa Loliondo, manake ni mbovu, hatuwezi kuuvunja?

5. Tukivunja mkataba huo tutapata hasara gani?

6. Tukiuacha mkataba huo, watanzania tunapata shilngi ngapi? hivi tunafaidikaje nao?

7. Wanalipa kodi? au ndio ardhi yao wanaishi na wanyama kama vile wapo uarabuni tu?

8. Mkataba kama utakuwa wa aina hiyo, si unavunja katiba? kama unavunja katiba hatuwezi kuuvunja huo mkataba?

9. Tumejipangaje kwa viongozi wanaoingia mikataba mibovu ili wakiharibu waje waandike kitabu kujutia na hakuna hatua yeyote inachukuliwa dhidi yao.

10. TUAMUE KWA KUFUMBA MACHO, TUVUNJE HUU MKATABA NA LOLIONDO IBAKI MIKONONI MWA TANAPA, labda kama siuelewi vizuri. na kama kuna mtu anao huo mkataba weka hapa ili tuujadili. wanyama wale uarabuni wamefikaje? na tulishaona wanapandishwa ndege hapahapa bongo, matwiga yanapandishwa ndege wakati tunaona.

MUNGU IBARIKI TANZANIA.
 
Kwani tukivunja mkataba wa Loliondo, hata kama tutalipa pesa, tukabaki na Loliondo yetu, kuna shida gani? au haiwezekani? kwasababu Mwinyi alishaeleza kwenye kitabu chake kwamba alifanya makosa makubwa sana kuruhusu ule mkataba.
 
kwani tukivunja mkataba wa Loliondo, hata kama tutalipa pesa, tukabaki na Loliondo yetu, kuna shida gani? au haiwezekani? kwasababu Mwinyi alishaeleza kwenye kitabu chake kwamba alifanya makosa makubwa sana kuruhusu ule mkataba.
Baadae Samia naye attandika kitabu chake akijutia kuingia mkataba wa kuuza bandari kwa DP world.
 
Baadae Samia naye attandika kitabu chake akijutia kuingia mkataba wa kuuza bandari kwa DP world,
haya mambo yataendelea hivi mpaka lini? Wasiishie kujutia tu ifike mahali washtakiwe kwa makosa na hasara wanazoziingiizia taifa.
 
Baadae Samia naye attandika kitabu chake akijutia kuingia mkataba wa kuuza bandari kwa DP world.
Hakika lazima kuna siku akiona umri sasa ndio unaenda ukingoni,ataandika kitabu, atajuta kwamba kati ya makosa aliyoyafanya kwenye utawala wake ni kuingia mkataba wa DP WORLD, watu watampigia makofi, tumekula hasara na hakuna cha kumfanya.

Hiki ndicho kinachowapa kiburi. ingekuwa kama nchi zingine ambako ukifanya ujinga hata ukifa mali zako watoto wako wananyang'anywa zinarejeshwa serikalini wala wasingefanya jambo kama hili. Mkapa alifanya hivyo, Mwinyi alifanya hivyo, kikwete sidhani kama tafanya hivyo kwasababu majuto atakayojuta kwenye kitabu chake nadhani atatakiwa kuandika vitabu zaidi ya 10.
 
Mkataba wa Loliondo uvunjwe tu, ili tubaki na Loliondo yetu, na kama kweli pale hadi network za simu za uarabuni ndio zinakamata, hawa watu sio wazuri kabisa. mlioko huku tuambieni kama haya mambo ni ya kweli.
 
Dubai national park inasomba wanyama toka Loliondo si ajabu Dubai national park ikaingiza watalii wengi sana kuliko idadi ya watalii walioingia mbuga zote nchini.

Maktoum yupo vizur sana kwenye marketing. Mzungu atohitaji kuja Tanzania penye huduma mbovu atachagua kwenda Dubai national park akaangalie wanyama.

Kama wanyama wa Africa wanapatikana uarabuni waje kufanya nini Africa.
 
HIli suala la Mkataba wa Loliondo halijaongelewa tu na wananchi au na wamasai tu, kuna tuhuma nyingi, zingine hatujui kama ni za kweli au za uongo. mara tuambiwe ukiwa pale Loliondo network ya simu ni ya uarabuni sio ya kibongo, mara tuambiwe kuna uwanja wa ndege kule madege huwa yanatua na kubeba wanyama wale tunaoambiwa wametengenezewa mbuga jangwani uarabuni, mara tuambiwe ardhi ile iliuzwa mazima sio part of Tanzania ni ardhi ya waarabu. Tunaomba mnaojua mtueleweshe yafuatayo:

1. Loliondo iliuzwaje, iliuzwa iwe milki ya waarabu au waliwekeza tu kitalu cha uwindaji?

2. kuna kiwanja cha ndege? pale kinafanya nini hasa tukizingatia tuliona lidege la kivita limedondoka pale na mfalme wa UAE wakisalimiana na Kinana?

3. Mkataba wa Loliondo ni wa milele au wa muda fulani?

4. Maaskofu walisoma kitabu cha Mwinyi, wanasema alikiri kwenye kitabu hicho kwamba alifanya makosa na anajutia mkataba wa Loliondo, manake ni mbovu, hatuwezi kuuvunja?

5. tukivunja mkataba huo tutapata hasara gani?

6. tukiuacha mkataba huo, watanzania tunapata shilngi ngapi? hivi tunafaidikaje nao?

7. wanalipa kodi? au ndio ardhi yao wanaishi na wanyama kama vile wapo uarabuni tu?

8. mkataba kama utakuwa wa aina hiyo, si unavunja katiba? kama unavunja katiba hatuwezi kuuvunja huo mkataba?

9. tumejipangaje kwa viongozi wanaoingia mikataba mibovu ili wakiharibu waje waandike kitabu kujutia na hakuna hatua yeyote inachukuliwa dhidi yao.

10. TUAMUE KWA KUFUMBA MACHO, TUVUNJE HUU MKATABA NA LOLIONDO IBAKI MIKONONI MWA TANAPA, labda kama siuelewi vizuri. na kama kuna mtu anao huo mkataba weka hapa ili tuujadili. wanyama wale uarabuni wamefikaje? na tulishaona wanapandishwa ndege hapahapa bongo, matwiga yanapandishwa ndege wakati tunaona. MUNGU IBARIKI TANZANIA.
Kwani tukivunja mkataba wa Loloondo na UAE tutapata faida gani?
 
Kwani tukivunja mkataba wa Loloondo na UAE tutapata faida gani?
Tunatakiwa kujua kwanza nini tunafaidika nao, what do we gain out of it, shilingi ngapi tunapata kila mwaka, Loliondo ipo Tanzania, ni mali yetu, kama hatufaidiki hatutakiwi kuendelea kuwashikilia hawa jamaa, ikiwa mikononi mwetu watalii wataneda ka uhuru kama wanavyoenda ngorongoro na serengeti na wanyama wetu hawatakuwa wanabebwa kila siku kupelekwa uarabuni. mbona rahisi sana hii kuelewa, au akili yako imejaa sperms?
 
Dubai national park inasomba wanyama toka Loliondo si ajabu Dubai national park ikaingiza watalii wengi sana kuliko idadi ya watalii walioingia mbuga zote nchini.
Maktoum yupo vizur sana kwenye marketing.
Mzungu atohitaji kuja Tanzania penye huduma mbovu atachagua kwenda Dubai national park akaangalie wanyama.
Kama wanyama wa Africa wanapatikana uarabuni waje kufanya nini Africa.
Hawa viongozi waswahili kuwaingiza kingi ni rahisi sana, maana elimu dunia hawaitilii maanani sana hivyo hawana critical thinking, ona sasa utalii umehamia dubai kwa kutumia wanyama wetu.
 
Hawa viongozi waswahili kuwaingiza kingi ni rahisi sana, maana elimu dunia hawaitilii maanani sana hivyo hawana critical thinking, ona sasa utalii umehamia dubai kwa kutumia wanyama wetu.
Wakishapewa apartment Dubai ya milioni 400 hawajali hasara ya bilioni 900,wao ukishawashangaza ukiwapa mapokezi ya VIP,plus warembo wakali,ukiwapa kibunda Cha dollar kuwapofusha macho Huwa hawasomi mkataba wasaini tu.
 
Dah! Nasikia hiyo mbuga iliuzwa kwa hao Waarabu enzi za utawala wa Mwinyi eti! Na sasa na Ngorongoro nayo iko mbioni kupigwa mnada! Ukiunganisha matukio, unaweza kujikuta umenunua ugomvi na ndugu zetu katika Imaan.

Nchi ngumu sana hii!
 
Wakishapewa apartment Dubai ya milioni 400 hawajali hasara ya bilioni 900,wao ukishawashangaza ukiwapa mapokezi ya VIP,plus warembo wakali,ukiwapa kibunda Cha dollar kuwapofusha macho Huwa hawasomi mkataba wasaini tu.
Kwa sasa tunalo la ngorongoro na bandari, mulemule.....
 
Back
Top Bottom