Kinachoendelea Loliondo: Shame on them! - Mwinyi, Mkapa, and Kikwete!

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,478
40,000
Baada ya kuligusa suala la Meremeta nilidokeza kuwa ripoti tunayoifanyia kazi sasa ni ile ya kuelezea historia ya ufisadi wa makuwadi wa wizi wa kimataifa ulioanzia Loliondo na kugusa Ikulu yetu (chini ya Mwinyi) hadi suala Meremeta ambalo nalo liligusa utawala wa Mkapa, na suala la Dowans linalogusa utawala wa Rais Kikwete.

Lakini kabla hatujafika huko kote hatuna budi kusikitishwa na taifa letu kurudi nyuma tena karibu miaka 17 sasa kwenye kashfa ya Loliondo. Kama nilivyodokeza kwenye suala la Loliondo::connections watu wale wale waliokuja kama wawekezeji wamerudi tena na watarudi tena na kutufanya sisi tuwe watumwa katika nchi yetu.

Kampuni ya OBC ya UAE mdau wake mkubwa ni Brigadier wa jeshi la UAE na mtu wa karibu wa familia ya mtawala wa huko. Kwenye Dowans kampuni hewa ya Dowans (ambayo JK hakufuatilia kama vile hakufuatilia Richmond) nayo inamilikiwa na Generali wa jeshi hilo hilo la UAE na ambaye naye ana ukaribu na watu wa familia hiyo.

Kama vile tulio na wazimu katika vichwa vyetu tukawa tayari kupiga magoti mbele ya watu hawa hawa na kuwanyanyasa watu wetu ili tuwafurahishe makuwadi wa ufisadi wa kimataifa. Wamasai wa Loliondo leo hii wanaitwa wakimbizi katika nchi yao na malalamiko yao hayapewi kipaumbele wala kutiliwa maanani!

Na ni watu hawa hawa wa familia ile ile waliojaribu kuchukua eneo la Yaeda Chini na kusababisha njaa kwa watu wetu na watawala wetu wakawatetea; watu wa familia ile ile ya kina Zayed. Angalau kwenye kesi ya Bonde la Yaeda Chini tuliweza kupiga kelele na kuwatimua lakini Loliondo na Dowans hawako tayari kutuachilia.

Hawa watu wanatuahidi vitu gani hadi tuwe wanyonge na dhaifu mbele zao utadhani mbwa mbele ya chatu? Hawa majenerali wenye nyotanyota wanawaahidi nini watawala wetu na wanalainika mbele zao kama waliolishwa limbwata za kitanga?

Hadi inafika mahali waliochaguliwa na wananchi wanawatetea makuwadi wa ufisadi wa kimataifa ambao rekodi yao iko wazi ya jinsi gani wametumia vibali tulivyowapa vibaya, jinsi gani wameua wanyama wetu kiholela na kutorosha wanyama hai kwenda makwao kwa fahari ya watawala wa huko.

Kama vile watawala hawa hawa walivyoruhusu madini yetu kule Buhemba kuchotwa na mamluki wa kivita wa Afrika ya Kusini na kuendelea kutuimbia wimbo wa umaskini wetu huku tukijichekelesha mbele yao.

Nani alitulaani? Tuache kupiga kelele ili wauze hadi nepi za watoto wetu, na vitanda vya vikongwe vyetu vipigwe mnada? Tuache kuandika na kuhoji yanayotokea nchini mwetu kwa vile wao ni watawala? Tuache kuliamsha taifa kutoka katika usingizi wake kwa sababu tukifanya hivyo tunawaudhi wanaotembea na ving'ora na kutetemewa wakitembea?

Mnatupa uchaguzi rahisi; mnatupa uchaguzi ambao hatuwezi kuacha kuuchukua; ni uchaguzi usiohitaji shahada za Harvard wala utaalamu wa fizikia ya anga za mbali. Hatuwezi kufumba macho yetu na vinywa vyetu ili mtutawale mpendavyo.

Jifunze kuhusu original Loliondo Scandal ambayo inahisiwa kuhusishwa na kifo cha mwandishi mahiri wa uchunguzi Stan Katabalo hapa Bonyeza Hapa

Screenshot 2019-02-13 at 20.30.00.png


Napenda kujua msimamo wa wabunge wafuatao kuhusu Loliondo:

Dr. Harrison Mwakyembe
Lucas Selelii
mama Anna Kilango
Mzee Yusuph Makamba
John Chiligati
Samwel Sitta (Spika)

NB: Nilituma salamu kwa Apson na Mboma wiki chache zilizopita; nikatoa wito kwa RO juu ya kuwadi wenu. Mtu wenu mliyemtuma (DB) nimempa ujumbe wangu wa ana kwa ana wiki moja sasa (bahati mbaya kwenu, taarifa za ujio wake zilimtangulia); natumaini ameufikisha pasipo kuongeza chumvi. Endeleeni tu, kwani historia yenu imeonesha mmesimama upande wa kushindwa mara zote.
 
Last edited:
Haya na Nyerere pia! (bahati mbaya hayupo hai hawezi kusikia wala kujua tumemwambia shame on him! isipokuwa kwa ajili ya sisi kujisikia vizuri!)
Probably his mistake was not to have multifaced succession plan. Aliwaachia nchi watu waliokuwa walafi kuliko maelezo. Wanalindana kwa nguvu zote ili wanayoyafanya yasijulikane na wasiwajibishwe. Ila hii sauti inayolia..inaita kulipa kisasi. Ipo siku mtakuja ona kisasi chake kitakavyokuwa. Naomba Mungu iwe during my life time. Wanatengeneza time bomu, wanalifukia chini ya nyumba halafu wao wanaendelea kuishi ndani. Lazima huo ni ujuha sio akili timamu
 
Mwanakijiji political analysis zimeshindwa kuelezea tatizo letu. Hata sociological analysis zimegonga mwamba. Kilichobaki ni psychoanalysis/psychological analysis - we must be very very sick upstairs! Kumbuka adui wakuu 2 kati ya wale 3 ni Maradhi na Ujinga!
 
Mwanakijiji political analysis zimeshindwa kuelezea tatizo letu. Hata sociological analysis zimegonga mwamba. Kilichobaki ni psychological/psychoanalytical analysis - we must be very very sick upstairs! Kumbuka adui wakuu 2 kati ya wale 3 ni Maradhi na Ujinga!
Collective strategies should address the problem in all dimensions. We should continue educating people about their rights. They can't continue ignoring these voices if they want to stay in power longer
 
Nahisi prediction za system haziko sawasawa maana hawajajua ukubwa na athari za matatizo yaliyopo..Wameweka nguvu katika ku counter attack any truth that surfaces
 
tulipokuwa wadogo kuna mafundi hasa mafundi mbao na ujenzi au fundi redio,ambao walikuwa mafundi wabovu tulikuwa tunawaita "fundi mangungu"
sasa naona huyu waziri wa jk nae tumwite
"waziri mangungu"
 
Mwanakijiji political analysis zimeshindwa kuelezea tatizo letu. Hata sociological analysis zimegonga mwamba. Kilichobaki ni psychoanalysis/psychological analysis - we must be very very sick upstairs! Kumbuka adui wakuu 2 kati ya wale 3 ni Maradhi na Ujinga!

sometimes I wonder how would Freud and Maslow and other psychoanalysts of earlier days would describe the mental condition of our people and especially that of our our leaders? Didn't they get enough hugs from their mothers or the viboko during their utoto left them with unhealed scars in their subconscious minds which has left them unable to live a well adjusted life?

could this be a psychoanalyst explanation of ufisadi as is practiced by Tanzanians?
 
sometimes I wonder how would Freud and Maslow and other psychoanalysts of earlier days would describe the mental condition of our people and especially that of our our leaders? Didn't they get enough hugs from their mothers or the viboko during their utoto left them with unhealed scars in their subconscious minds which has left them unable to live a well adjusted life?

could this be a psychoanalyst explanation of ufisadi as is practiced by Tanzanians?

Baada ya kumsikiliza Waziri wa Uwindaji akiwatetea Majangili wa Loliondo nadhani nadharia hii ya Saikolojia ya Jamii inaelezea matatizo yetu 'Miafrika Ndivyo Tulivyo' - katika ngazi ya nafsi inafanya mtu awe fisadi ila katika ngazi ya jamii inasababisha watu wawe na hasira kali dhidi ya mafisadi:

Relative Deprivation Theory

Description
We tend to decide how well-off or deprived we are not from any absolute standard or how hungry are, but by comparing ourselves with other people.

In particular, we decide on what we deserve and what we should expect from looking at other people. We then compare ourselves with this standard.
------------------

[ame="http://en.wikipedia.org/wiki/Relative_deprivation"]Relative Deprivation[/ame]

Relative deprivation is a situation in which a person is deprived of something which they think they are entitled to, while another person possesses it. The deprivation is relative between the two parties as a person possesses the item while the other does not.

The term can be used in social sciences to describe feelings or measures of economic, political, or social deprivation that are relative rather than absolute.

The concept of relative deprivation has important consequences for both behaviour and attitudes in a society, including feelings of stress, political attitudes, & participation in collective action.
 
Nchi hii tupiganie kuiondoa mikononi mwa CCM. Mkuu M.M.M hao unaotaka kujua msimamo wao, well, wanaweza kusema kitu lakini hawawezi kuibadili CCM. CCM inawenyewe ndo hao mafisadi wakubwa wanaitwa wafadhili wa chama.

Hakuna dallili zozote za kuonyesha mabadiliko ndani ya CCM, you can see Mwinyi - Mkapa - Kikwete - anayefuata ... hali haitabadilika. Mungu atuwezeshe kuikomboa nchi toka mikononi mwa CCM.
 
Haya na Nyerere pia! (bahati mbaya hayupo hai hawezi kusikia wala kujua tumemwambia shame on him! isipokuwa kwa ajili ya sisi kujisikia vizuri!)
.
Mzee Mwanakijiji, asante kwa connecting the dots ya Loliondo, Yaeda Chini na Dowans lakini hili la kumuunganisha Nyerere, haliwezi kupita hivi hivi bila kupingwa. Yes sio mtakatifu, kuna maeneo alikosea na alikiri makosa kwa kusema " kufanya kosa si kosa, kosa kurudia kosa"
Please kwa heshima yako Mzee Mwanakijiji, please ondoa hii shame on him kwenye hili!.
Yes alimnyooshea njia Mwinyi na Mkapa, lets be genuine, alijua watafanya madudu waliyofanya?. Was he part to it?. Please mwacheni Mzee wetu apumzike kwa amani.
 
Mzee Mwanakijiji hawa jamaa unaweza kutaka kujua msimamo wao, wako kwenye kundi moja na hata kama watafanya hivyo wanaweza kusema kwa ajili ya political agenda pekee na sio vingine. ukitaka kujua kuwa na wao wapo walikuwa wapi kipindi chote mpka mambo haya yanakuja kutokea Tanzania, Jaribu kuunganisha docs zao na utaona kuwa wanaingia moja kwa moja
 
NB: Nilituma salamu kwa Apson na Mboma wiki chache zilizopita; nikatoa wito kwa RO juu ya kuwadi wenu. Mtu wenu mliyemtuma (DB) nimempa ujumbe wangu wa ana kwa ana wiki moja sasa (bahati mbaya kwenu, taarifa za ujio wake zilimtangulia); natumaini ameufikisha pasipo kuongeza chumvi. Endeleeni tu, kwani historia yenu imeonesha mmesimama upande wa kushindwa mara zote.
Katika yote, nimeipenda zaidi hii. Ni uthibitisho JF sio tunapiga kelele for nothing, its for something na kelele zetu zinafika haswa kule kunako. Thanks MMKJJ, Thanks JF.
 
Kama sisi wenyewe hatujipendi wala kujionea huruma kwa nini mgeni atupende na kutuonea huruma?

Amandla........
 
Last edited:
.
Yes alimnyooshea njia Mwinyi na Mkapa, lets be genuine, alijua watafanya madudu waliyofanya?. Was he part to it?. Please mwacheni Mzee wetu apumzike kwa amani.

Hapo mkuu ume sound kama mkuu wa kaya! heheheh
 
Kwa aina ya wanasiasa tulionao ni ngumu kupata tumaini kwamba hivi karibuni mambo yatakuwa tofauti. Tatizo kubwa kwangu ni kuwa hata kama kiongozi aliyepo hafai, yule basi wa kumfikiria kama anaweza kufaa naye haonekani. Nakubaliana na mtu aliyesema pengine bado hajazaliwa mtu anayefaa kuondoa haya matakataka tuliyoyaza chini ya kapeti yakitoa uvundo mkali, huku wenyewe tuko juu ya meza twala chakula bila kuona karaha ya harufu za takataka hizo.
Nani atazizoa takataka hizi tulizojaza kila kona ya Taifa letu?
 
labda kosa kubwa la Nyerere ni kumpinga Mrema kuwa raisi wakati ule (1995), ile nguvu aliyokuwa nayo Mrema wakati ule angeingia nayo madarakani nadhani adabu ingekuwepo katika hii nchi
 
Back
Top Bottom