Tatizo kubwa la mgogoro wa Maasai na Serikali ulianza katika mikono ya Hayati Mwinyi kwa kuwapa familia kutoka falme ya Dubai

lukubuzo Samsis

JF-Expert Member
Nov 3, 2014
2,909
3,340
November 11, 1992, Waziri wa Utalii, Maliasili na Mazingira wa wakati huo, Abubakar Mgumia, alitoa vitalu vya uwindaji katika Maeneo ya Pori Tengefu ya Loliondo (Kaskazini na Kusini) kwa kipindi cha miaka 10 ya kalenda, vinavyongezeka kuanzia January, 1993.

Brigedia Mohammed Abdul Rahim Al Ali,sehemu ya familia ya kifalme ya UAE ambaye alikuwa mmiliki wa (OBC). Ardhi iliyonyakuliwa ni ardhi ya uzaliwa wa maelfu ya wanavijiji wa Arash, Soitsambu, Oloipiri, Ololosokwan, Loosoito na Oloirien vijiji vya Loliondo.

Vitalu hivyo vinatolewa kwa Brigedia Mohammed Abdul Rahim Al Ali kutoka Dubai, ambaye alikuwa Naibu Waziri wa ulinzi wa Falme za Kiarabu. Barua ya Waziri wa Utalii, Maliasili na Mazingira Abubakar Mgumia inaelekezwa kwa Brigedia Al Ali ya tarehe 14 Septemba 1992.

Waziri wa Utalii, Maliasili na Mazingira Abubakar Mgumia - katika barua ya kutoa kitalu cha uwindaji kwa OBC - alimshauri Brigedia kwamba “kampuni iundwe kusimamia Eneo la Makubaliano kwa mujibu wa sheria na kanuni za Kampuni ya Tanzania”.

Waziri pia alimkumbusha Al Ali kuwa makubaliano yafanyike kati yake na Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro, azingatie kikamilifu sheria na kanuni zote za wanyamapori, na TAWICO iruhusiwe kutumia eneo hilo kwa wateja wao hadi tarehe 31 Machi 1993.

Waziri wa Utalii, Maliasili na Mazingira wa wakati huo, Abubakar Mgumia aliongeza kuwa makubaliano ya Brigedia Mohammed Abdul Rahim Al Ali kuchangia asilimia 25 ya mapato kwenye Halmashauri ya Wilaya yamepita na juu ya mchango wa kawaida.

Meneja Mkuu wa OBC alifanya hivyo mwaka 2007 aliandika (MTNRE/A/100/4/97) kwamba, baada ya safari ya uwindaji kwa kibali cha Rais mwaka 2001, Brigedia Mohammed Abdul Rahim Al Ali alitoa wito kwa Waziri Mkuu wa wakati huo John Samuel Malecela,

Barua hiyo ya Meneja Mkuu wa OBC ilionesha nia ya kupata kitalu cha uwindaji Loliondo kilitolewa. Brigedia Mohammed Abdul Rahim Al Ali alikuwa tayari ameshafika Tanzania kwa ajili ya kuwinda mara kadhaa tangu mwaka 1985. (Ndaskoi, 2010)

Ngorongoro Conservation Area (NCA) kuna eneo lenye ukubwa wa 8,292 km² (mara 3 ya eneo lote la kisiwa cha Zanzibar, 2,462km2). Loliondo Game Controlled Area (LGCA) kuna eneo lenye ukubwa wa 4,000km².

Eneo la uwindaji la OBC ni eneo lote la 4,000km², na wanaweza kuwinda panya karibu na ofisi ya Mkuu wa Wilay na wasiulizwe, eneo kuu la uwindaji, ni eneo karibu na Hifadhi ya Taifa ya Serengeti, inayoelezwa kama “ukanda” wa 1,500km².

Osero au pori ni eneo muhimu la malisho ya msimu wa kiangazi kwa Wamasai. Mashirika ya uhifadhi tayari yalikuwa yamependekeza kwa nyakati tofauti kutengwa kwa eneo hili kama “buffer zone”. Lakini utawala wa Rais Ali Hassan Mwinyi uliwapa waarabu wa Dubai.

Eneo la uwindaji la OBC lina 4,000km² na linajumuisha tarafa yote ya Loliondo na sehemu ya tarafa ya Sale Ngorongoro. Kuna sehemu tatu za Wamasai Loliondo - Purko, Loita na Laitayok - ambayo imewezesha matumizi ya mbinu za kugawanya na kutawala.

Tarafa ya tatu ya Wilaya ya Ngorongoro, kusini mwa Loliondo, haipo katika eneo la uwindaji, ni Hifadhi ya Ngorongoro. Katika eneo hili, jamii ya Wamasai wanaishi chini ya utawala mkali na vikwazo vikali kutoka kwa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro,

Mbunge wa wakati huo wa Ngorongoro, Richard Koillah, Mkuu wa Wilaya Leban Makunenge na viongozi wengine wa serikali walifanya na walizunguka katika vijiji sita vya Tarafa ya Loliondo vinavyopakana na Hifadhi ya Taifa ya Serengeti na Ngorongoro, kushawishi wananchi.

Walizunguka wakijaribu bila mafanikio kuwashawishi wanakijiji hao kutia saini makubaliano ya kuruhusu Brigedia Mohammed Abdul Rahim Al Ali kuwinda katika ardhi ya kijiji chao. Wananchi walikataa ushawishi huo wa kugawa ardhi yao kwa waarabu wa OBC.

Baada ya kushindwa waliendelea na kusaini mkataba kati ya Al Ali na Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro kwa ajili ya “uhifadhi wa wanyamapori, usimamizi na maendeleo ya kijiji cha Pori Tengefu la Loliondo” wenyewe, bila kuwashirikisha wanakijiji.

Ahmed Saeed Abulrahman Alkhateeb alitia saini kwa niaba ya Brigedia Mohammed Abdul Rahim Al Ali. Mkuu wa Wilaya Ngorongoro, Kanali Leban Makunenge, alitia saini kwa niaba ya Serikali Kuu. Mkurugenzi Mtendaji wa halmasgauri akisaini kwa niaba ya halmashauri.

Richard Koillah, aliyekuwa Mbunge wa Ngorongoro wakati huo, alisaini mkataba huo kwa niaba ya vijiji sita; yaani, Ololosokwan, Soitsambu, Oloipiri, Olorien-Magaiduru, Loosoito-Maaloni na Arash Vijiji vya Piyaya na Malambo havitajwi popote kwenye mkataba.

Mkataba huo wa kuuza ardhi 4,000km² kwa waarabu wa Dubai ulijulikana kama (Mkataba kwa Ajili ya Kuhifadhi na Kusimamia Maendeleo ya Wanyamapori Ili kuleta Maendeleo ya Vijiji katika Eneo la Loliondo Game Controlled Area: South and North, 1992)

Vijiji vilivyosajiliwa kwa mujibu wa Sheria ya Tamisemi Na.7 ya mwaka 1982 (TAMISEMI Act No.7 of 1982) vingeweza kwa wakati huo kuingia mikataba yenye dhamana kwa niaba yao wenyewe. Lakini mbunge wao, Richard Koillah akawauza kwa waarabu wa Dubai.

Mkataba huo uligubikwa na ufisadi ulifuatiliwa kwa ukaribu kwenye vyombo vya habari Tanzania hususani magazeti na ukaja kupewa jina la “Loliondogate”. Mbali na vijijini kashfa hii ilihusisha kupewa vitalu vya uwindaji kwa miaka 10 badala ya miaka 5 iliyozoeleka,

Kufanya hivyo wakati TAWICO (shirika la serikali lililokuwa linasimamia vitalu vya uwindaji nchini Tanzania hadi Idara ya Wanyamapori ilipochukua mamlaka mwaka 1988) ilikuwa tayari imepewa. mkataba kutoka 1991 hadi 1996.

Bodi ya wakurugenzi ya TAWICO na mkurugenzi wa wanyamapori waligoma, lakini bila mafanikio. Mary Ndosi mwakilishi wa OBC Tanzania alitumia P.O Box ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali na kulikuwa na madai kuwa Al Ali alikuwa rafiki binafsi wa Rais Mwinyi.

Januari 1993 Brigedia Mohammed Abdul Rahim Al Ali alifanya safari ya kuwinda Longido pamoja na mtawala wa sasa wa Dubai, Sheikh Mohammed bin Rashid Al Maktoum, wakati huo alikuwa Waziri wa Ulinzi wa UAE. Waliandamana na balozi wa Tanzania UAE na watu 67.

Waziri wa Utalii, Maliasili na Mazingira, Abubakar Mgumia alikiri kwenye gazeti la Mfanyakazi kulikuwa na uwindaji mkubwa, na wawindaji walisafirisha pundamilia na swala, mmoja alianguka na kufa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro.

Katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro alikuwepo Abdulrahman Kinana, Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa wakati huo, akiwakilisha Serikali ya Tanzania wakati wanyamapori hao (wakiwa hai kabisa) wakisafirishwa kwenda Dubai.

Hata gazeti la New York times liliripoti kwamba wawindaji kutoka Dubai walipunguza kwa kiasi kikubwa idadi ya gerenuk huko Longido. Vyombo vya habari vya Tanzania mara nyingi vichanganya Longido na Loliondo, lakini haikuwa hivyo kwa Mfanyakazi mwaka 1993.

Tarehe 7 Februari 1993 Waziri wa Utalii, Maliasili na Mazingira, Abubakar Mgumia alitangaza Otterlo Business Corporation (OBC) ingeanza shughuli zake za uwindaji katika Eneo Lililodhibitiwa la Loliondo (Loliondo Game Controlled Area) tarehe 1 Aprili 1993.

Mwandishi wa habari aliyefuatilia kwa karibu mchongo wote wa ufisadi huo alikuwa Stanislaus Katabalo, katika gazeti la Mfanyakazi kuanzia tarehe 20 Januari 1993, hadi alipofariki dunia (kuuwawa) katika mazingira ya kutatanisha tarehe 26 Septemba 1993.

Stanislaus Katabalo alikuwa mwandishi wa habari wa ukweli, alithubutu akatupa habari za ukweli , akachimbua haswa , akatueleza jinsi twiga wetu walivyokwenda Arabuni. Akauwawa, hadithi za kusafirishwa twiga ikafa, naye pia tukamsahau.

Stanislaus Katabalo alikuwa anaandika kupitia gazeti la MFANYAKAZI kila jumamosi jinsi mkataba huo wa magumashi ulivyoingiwa kati ya serikali na waarabu kutoka Dubai ilikuwa kipindi cha Ali Hassan Mwinyi... Katabalo alifariki na kuacha simanzi kubwa.

Stanislaus Katabalo alikuwa akifanya uandishi wa habari wa uchunguzi (investigative journalism) kwenye developing story. Aliandika na kuibua kashfa nyingi ikiwepo ya mchele mbovu wa Mohammed Enterprises Tanzania Limited (METL) na Tanzania Breweries Ltd.

Lakini, Muhidin Ndolanga (mkurugenzi wa wanyama pori wakati ule na Waziri wa Utalii, Maliasili na Mazingira wa wakati huo, Abubakar Mgumia Rais Mstaafu Ali Hassan Mwinyi) mmoja kati yao, anaweza kutueleza vizuri kilichomkuta Stanislaus Katabalo.

Stan Katabalo alipata taarifa nyingi kutoka kwa Moringe ole Parkipuny, mbunge wa kwanza wa Ngorongoro ambaye alizidiwa ujanja na kukatishwa tamaa na siasa za chama kimoja, na kuanzisha NGO ya kwanza ya wafugaji huko Loliondo, na Tanzania, mwaka 1990.

Tarehe 2 Mei 1993 wakati Parkipuny alipokuwa akirudi nyumbani kutoka Loliondo “mji”, umbali wa mita 300 kabla ya kumaliza kituo cha polisi cha Loliondo, polisi walifyatua risasi gari lake kwa nyuma. Risasi hiyo ilivunja glasi ya mlango wa nyuma, ikapita katikati ya bega lake na sikio, na kuvunja kioo cha mbele.

Polisi aliyefyatua risasi hiyo alijulikana. Alipewa amri na officer commanding district (OCD) kupiga risasi. Hakuna hatua iliyochukuliwa dhidi ya askari polisi huyo ambaue alimpiga risasi mbunge wa Ngorongoro, Moringe ole Parkipuny au mtu mwingine yeyote.

17 Aprili 1993 Idhaa ya Kiswahili ya BBC ilitangaza kwamba Rais Ali Hassan Mwinyi amemuondoa Abubakar Mgumia kutoka Wizara ya Utalii, Maliasili na Mazingira kutokana na kashfa ya Loliondogate akateuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Singida.

Mwaka wa 1994 Kamati Teule ya Bunge ilitoa bungeni Ripoti ya Marmo inayoelezea unyanyasaji na kasoro kuhusu OBC (Report detailing abuse and irregularities concerning OBC). 1996 ripoti ya Warioba iliitaja OBC kama moja ya kampuni fisadi zaidi nchini Tanzania

Baada ya mabishano hayo, kibali cha miaka 10 cha Otterlo Business Corporation (OBC) kilifutwa wakati fulani, lakini kisha kikafanywa upya kwa muda wa kawaida wa miaka 5 kuanzia mwaka 1995 na tangu wakati huo kimekuwa kikifanywa upya.

Hivyo, ni vyema wakati tunatoa sifa kede-kede kwa Rais wa awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi, pia, tukumbuke kwamba tatizo kubwa la mgogoro wa Maasai na Serikali ulianza katika mikono yake kwa kuwapa familia kutoka falme ya Dubai 4,000km² za ardhi ya Loliondo.

Eneo lote la kisiwa cha Zanzibar lina ukubwa wa 2,462km². Eneo ambalo Otterlo Business Corporation (OBC) waliuziwa Loliondo na serikali ya Ali Hassan Mwinyi ni 4,000km². Hii ni karibu mara mbili (1.624) ya eneo lote la kisiwa cha Zanzibar. Kapewa mwarabu.

Kwa taarifa za sasa ni kwamba; waarabu kutoka familia ya falme ya Dubai (Otterlo Business Corporation (OBC)) wameongezewa 1,500km² kutoka 4,000km² zilizokuwa kwa wananchi wa Loliondo wao ambao wamebaki na 2,500km² na eneo lote. Wameporwa ardhi yao.

Martin Maranja Masese, MMM.
 
20240305_000144.jpg
 

Attachments

  • 20240305_000147.jpg
    20240305_000147.jpg
    86.8 KB · Views: 5
Baelezee nimesoma kipande cha bandiko ye SYLLOGIST! akisema loliondo imeuzwa na nyingineo akisema kuhusu mwarabu ambaye ss anaonekana ni Brigedia Mohammed Abdul Rahim Al Alinaamini alisema piya walipelekwa kwa kuwinda na kula nyama ya nyati na maranja msese amesema piya , likambo yi kokomwa kumbe ile stori yake ni kweli. Wachaneni ni mtafute ile post nione tena. Ètonnant

nzambe azali kotala
 
Inashangaza unawapa kampuni moja eneo kubwa kama hilo na kila anachunguza anapotezwa. Unawapa watu exclusive eneo kubwa kuliko nchi ndogo nyingi huku ukiwatimua Wamasai.

Angeweza kuwapa hata 1/10 ( 400km square). Kinana, Abubakar Mgumia, washikaji wenzake wameanza mbali kuuza maliasili za Tanzania na kuiuza Tanzania wakishiriana na kiongozi namba moja Tanzania, Rais mwenyewe.
 
Kinachofurahisha na kusikitisha wakati huo huo ni kwamba kamwe hutosikia chochote humu kuhusu Buzwagi, Bulyanhulu, accasia, yule mzungu anayemiliki eneo kanda ya kusini kwa miaka 99, yule bilionea wa kimarekani anayemiliki eneo maridadi kabisa kule kaskazini n.k. Na kama utasikia basi itakuwa kwa lugha nyepeesi mno yenye kupamba na hutosikia maneno 'mwingereza' wala 'mmarekani', bali 'muwekezaji'!! Majina ya viongozi wa tz waliohusika ndo hutoyasikia kabisaaaaa!!
 
Kinachofurahisha na kusikitisha wakati huo huo ni kwamba kamwe hutosikia chochote humu kuhusu Buzwagi, Bulyanhulu, accasia, yule mzungu anayemiliki eneo kanda ya kusini kwa miaka 99, yule bilionea wa kimarekani anayemiliki eneo maridadi kabisa kule kaskazini n.k. Na kama utasikia basi itakuwa kwa lugha nyepeesi mno yenye kupamba na hutosikia maneno 'mwingereza' wala 'mmarekani', bali 'muwekezaji'!! Majina ya viongozi wa tz waliohusika ndo hutoyasikia kabisaaaaa!!

Duh, hapa kwa mfano unataka kusemaje...?

Unalo Jambo lako hapa....embu limwage ...umepigaje hapo?
 
Kinachofurahisha na kusikitisha wakati huo huo ni kwamba kamwe hutosikia chochote humu kuhusu Buzwagi, Bulyanhulu, accasia, yule mzungu anayemiliki eneo kanda ya kusini kwa miaka 99, yule bilionea wa kimarekani anayemiliki eneo maridadi kabisa kule kaskazini n.k. Na kama utasikia basi itakuwa kwa lugha nyepeesi mno yenye kupamba na hutosikia maneno 'mwingereza' wala 'mmarekani', bali 'muwekezaji'!! Majina ya viongozi wa tz waliohusika ndo hutoyasikia kabisaaaaa!!
Labda kwasababu kichwa chako kimejaa wadudu



 
Baelezee nimesoma kipande cha bandiko ye SYLLOGIST! akisema loliondo imeuzwa na nyingineo akisema kuhusu mwarabu ambaye ss anaonekana ni Brigedia Mohammed Abdul Rahim Al Ali naamini alisema piya walipelekwa kwa kuwinda na kula nyama ya nyati na maranja msese amesema piya , likambo yi kokomwa kumbe ile stori yake ni kweli. Wachaneni ni mtafute ile post nione tena. Ètonnant

nzambe azali kotala

Nzambe asali ndio nini?

Nimeiona kijana, tulia.

As a matter of fact naijua

Huyo Ali akiwa kule Ilala sebuleni mwake alikuwa ana RPG (bazuka)na AK-47 Jambia na gobole, silaha hizo zote zilikuwa...

Ukutani zimening'inizwa, hebu fikiria miaka hiyo na silaha kama bazuka ziko sebuleni Kwa ajili ya kuwindia.
 
Hivi huwa mnafaidika na nini hasa..?? Kwa kuleta mada kama hizi juu ya wale ambao tayari wameshamaliza majukumu yao duniani
ukweli lazima usemwe ili Taifa lijue.Kama mnapenda kusifiwa mpende pia kukosolewa.
 
Wawejezaji wapo Tanzania hata Leo.

hao waarabu wamewekeza au wamepabdisha Hadi benders Yao?
 
Hivi huwa mnafaidika na nini hasa..?? Kwa kuleta mada kama hizi juu ya wale ambao tayari wameshamaliza majukumu yao duniani
Tukiwa hapa duniani basi ndugu zangu tujitahidi tuwe na hadithi nzuriiii
 
Back
Top Bottom