Kilimo cha vitunguu kilivyonitia hasara

Wapi huko? Morogoro?
Kitunguu nmelima kilosa, Lumumba
Nkapigaga kaela fulani ila syo zile zao wanazosema
Nkaja tena nkalamiga kitungu mvumi, Kilosa maeneo ya mangombole...kuna mashamba yana scheme ya umwagiliaji

Nlipata kdg sema hapo dongo halikuwa zuri kwa kitungu.

Ufutq nlilimaga dodoma,mlowa kuna pori linaitwa madimo,hilo pori sisi ndy watu wa kwanza kwenda huko kulisafisha na kuanza kulima...nakumbuka kulima tulitumia ngombe,tena tuliwafatq mpunguzi kuwakodi
Ila ufuta nlikula za uso.

Sema badaye watu wote huko nao wakalivqmiq pori hilo kuanza nao kulima.

Ukienda huko mkuranga mwarusembe tumelima sana tikikiti na matango.

Mpunga nmelima kwenye mashamba ya mstaafu rip mwinyi dakawq.

Nyanya nmelima morogoro sehemu za magole ,kuna Estate farm ya Don mmoja
Nkiendelea kutoa cv ya kulima himu ntajaza server ya jf 😄
Hawa wanaohifqnyq sjui bbm bbt sjui wanazungumzia kilimo tunawa zoom tu

Ova
 
Kitunguu nmelima kilosa,lumumba
Nkapigaga kaela fulani ila syo zile zao wanazosema
Nkaja tena nkalamiga kitungu mvumi,kilosa maeneo ya mangombole...kuna mashamba yana scheme ya umwagiliaji
Nlipata kdg sema hapo dongo halikuwa zuri kwa kitungu
Ufutq nlilimaga dodoma,mlowa kuna pori linaitwa madimo,hilo pori sisi ndy watu wa kwanza kwenda huko kulisafisha na kuanza kulima...nakumbuka kulima tulitumia ngombe,tena tuliwafatq mpunguzi kuwakodi
Ila ufuta nlikula za uso....
Sema badaye watu wote huko nao wakalivqmiq pori hilo kuanza nao kulima
Ukienda huko mkuranga mwarusembe tumelima sana tikikiti na matango
Mpunga nmelima kwenye mashamba ya mstaafu rip mwinyi dakawq
Nyanya nmelima morogoro sehemu za magole ,kuna Estate farm ya Don mmoja
Nkiendelea kutoa cv ya kulima himu ntajaza server ya jf 😄
Hawa wanaohifqnyq sjui bbm bbt sjui wanazungumzia kilimo tunawa zoom tu

Ova
Mkuu wewe ni fighter. Lini mwaka gani tikiti maji ulilima Mwalusembe? Pia mimi nilijaribu 2014 hapo Mwalusembe nilikula za uso. Pia Ufuta Nikala za uso. Pia vitunguu Mang'ola nikala za uso. Mahindi usiseme nikala za uso. Nikaamua tu kuendelea na kubeba boksi. Halafu majitu yalionipiga pesa hayana aibu bado yanaendeleaga kuniombaga hela.

Ila napenda sana kilimo na ufugaji. Siku umri ukienda nataka nitulie kwenye hiyo sekta.
 
Kilimo Cha mitandaoni ni kizuri,ingia kwenye uhalisia ndo utajua hujui
 
Mkuu wewe ni fighter. Lini mwaka gani tikiti maji ulilima Mwalusembe? Pia mimi nilijaribu 2014 hapo Mwalusembe nilikula za uso. Pia Ufuta Nikala za uso. Pia vitunguu Mang'ola nikala za uso. Mahindi usiseme nikala za uso. Nikaamua tu kuendelea na kubeba boksi. Halafu majitu yalionipiga pesa hayana aibu bado yanaendeleaga kuniombaga hela.

Ila napenda sana kilimo na ufugaji. Siku umri ukienda nataka nitulie kwenye hiyo sekta.
Mwalusembe ulilimia wapi,mm nlilimia maeneo ya mainge
Tikitiki nlipiga sana bao...
Sema sahv nna miaka 3,4 sjajishugulisha na mitkasi hizo

Ova
 
Inawezekana uliiiga. Hahaha usinichekeshe na kunikumbusha. Mang'ola nini?

Kuna hizi zingine chini.

-Dengu
-Tikiti maji
-Mbaazi
-Alizeti
-Korosho
-Mayai ya Kware
-Vanilla
😆😁👌🏿👊🏿🙌🏿🤜🏿🤛🏿
Za uso mjegeje
 
Kitunguu nmelima kilosa, Lumumba
Nkapigaga kaela fulani ila syo zile zao wanazosema
Nkaja tena nkalamiga kitungu mvumi, Kilosa maeneo ya mangombole...kuna mashamba yana scheme ya umwagiliaji

Nlipata kdg sema hapo dongo halikuwa zuri kwa kitungu.

Ufutq nlilimaga dodoma,mlowa kuna pori linaitwa madimo,hilo pori sisi ndy watu wa kwanza kwenda huko kulisafisha na kuanza kulima...nakumbuka kulima tulitumia ngombe,tena tuliwafatq mpunguzi kuwakodi
Ila ufuta nlikula za uso.

Sema badaye watu wote huko nao wakalivqmiq pori hilo kuanza nao kulima.

Ukienda huko mkuranga mwarusembe tumelima sana tikikiti na matango.

Mpunga nmelima kwenye mashamba ya mstaafu rip mwinyi dakawq.

Nyanya nmelima morogoro sehemu za magole ,kuna Estate farm ya Don mmoja
Nkiendelea kutoa cv ya kulima himu ntajaza server ya jf 😄
Hawa wanaohifqnyq sjui bbm bbt sjui wanazungumzia kilimo tunawa zoom tu

Ova
We noma sana na bado hujatoboa, na dijaona dehemu umetoa poditive ni negatice tu, kwa hiyo unataka kusema wtuu wasilime kilimo hakilipi kabisa
 
Kama habari inavyoeleza hapo juu,

Mimi ni mkulima mzuri wa nyanya, nimelima zao hili kwa zaidi ya miaka kadhaa kutokana na changamoto za hapa na pale zilinifanya kuwa mzoefu na mtaalamu sana wa kilimo hiki, hivyo ilikuwa nikiweka mbegu shambani.

Ililazimu jirani angalie nitaivisha wakati gani Ili tusikutane naye hii ni kutokana tu na kutengeneza Jina la uzalishaji wa bidhaa bora,kama wahenga walivyosema "Mwenye nguvu mpishe "kauli hii ilinipa kujiamini kutokana na kile tulichokuwa tunakizalisha, zama huwa zinabadilika.

Mabadiliko ya Kila Leo ya soko la nyanya na vijana wengi kuhisi tunapiga pesa nyingi basi kulianza kunifikirisha kulihana zao hilo, baada ya kuona vijana wengi wakiiga pasi na ujuzi juu ya uzalishaji wa zao hili,kulileta mafuriko katika soko letu kiasi kwamba kwa mtu unayezalisha kwa kutumia gharama kubwa.

Huwezi kushindana na mtu aliyezalisha kwa gharama ndogo na anauza anavyojisikia, ukizingatia walaki wetu wa mwisho Wana angalia quantity na si quality, hivyo mtu aliyezalisha kwa gharama ndogo atapima mfuko ule unaouzwa kwa Shilingi mia tatu(Magufuli)Wasukuma Wa Meatu Mwandoya Simiyu.

Huwa wanaita hivyo, mtu aliyezalisha kwa gharama ndogo atauuza Shilingi 500,huku Mimi na rafiki yangu Makoye kibarua wangu tukiuza nyanya 5 kwa Shilingi mia 500, Tuliona kabisa kuwa tunakoelekea tutakwenda kukwama.tuliamua kulihana zao hilo na kuamua kuhamia kwenye vitunguu.

Hamasa ya kutiana mioyo ilikuwa kubwa tulikuwa tukipiga stori za kupata mamilioni ya pesa kwani wakati huo gunia lilikuwa likinunuliwa 350k, tulijipa matumaini makubwa kuwa hata kama tutakuta bei imeshuka basi tutakuta angalau ngunia linanunuliwa 150k.

Haiwezekani bei iporomoke kutoka 350k mpaka liivuke 150k, mjadala juu ya Nini tufanye uliishia Mwanaume nikajitosa kwenda kununua mbegu,nilikwenda maduka kadhaa kufanya ulinganifu wa bei na upelelezi wa Kila walaka unaozungumuzia kilimo hiki nilisoma kwa makini huku nikiulizia Kila uzoefu na changamoto za hapa na pale juu ya zao hili.

Nilibahatika kupata mzoefu wa zao hili kwa kuuza mbegu,kulima na mrejesho wa wakulima mbali mbali aliokuwa anaupata kwa wakulima walikuwa wakichukua mbegu kwake.

ITAENDELEA...
Mkuu nipe bei ya hiyo solo pump inatumia betri na kwa mwanza nazipata wapi? kama una mawasiliano nao naomba unipm au hapahapa
 
Jamaa yangu alikopa m15 akaemda eti kulipa mbogamboga ruvu akakodi na shamba kabisa hahahaaaaaa naogopa kumalizia maana ilikuwa makasiriko kwa kila mtu.
Alilima mboga gani? Manake sie tupu huku na tunaingiza pesa
 
Mtaalamu wa zao hili na Bwana shamba anayeishi Mwanhuzi -Meatu, alinishauri nilime mbegu iitwayo Red Bombay(Mang'ora) kama ulivyokuwa ikiitwa na wakulima wazoefu niliowakuta kwenye game, kwasababu shauku ilikuwa ni kufanikiwa niliulizia juu ya kipimo kinachotosha hekari Moja.

Mtaalamu wa kilimo hiki Samson Luzege ( afisa kilimo) alinishauri kuchukua angalau kilo 5 kwa mbegu hii ya kienyeji nilimwambia apime ndebe Zima kilo 9 hivi. Safari ya kilimo hiki ilianza mbegu ziliota zikapendeza kweli,hapo ndipo hesabu mezani za mamilioni ya pesa zilikuwa zikizunguka kichwani Mwangu niliwaza kukunja zaidi ya Milioni 10 Hadi 20 za Kitanzani maana mawazo makubwa yalilenga kupata gunia zaidi ya mia Moja kwa hekari Moja.tulijituma usiku na mchana tukifanya Kila linalowezekana kufanikisha zoezi hili,shamba likalimwa,safu zikatengenezwa.

Kwakweli kama ni ajira tulitoa kwa vijana, kwakuwa sikutaka kufeli hata kidogo nilisafiri kutoka ninapoishi kwenda kutafuta vijana wazoefu wa kupanda zao hili Semu( mto Semu) eneo maarufu kwa kilimo Cha vitunguu Wilaya ya Meatu-Simiyu tuliweka mikakati lini zoezi lifanyike, baadae hatukuwatumia vijana hao kwani walianza kuonyesha maringo huku mbegu zikiwa zimeshaanza kutuonesha dalili ya malalamiko kuwa zinahitaki kuhamishiwa shambani.

Tulipata ushauri wa wataalamu mbalimbali kuwa upandaji wa vitunguu na mpunga utofauti ni kidogo mno kuwa vitunguu visizamishwe angalau basi sm2 kama vilivyokuwa kwenye vitalu ,tulijitahidi kutoa taaluma hii hasa kwa kuwatumia akina mama wa pale kijijini kazi waliifanya vizuri upandaji wa vitunguu ukaenda vizuri, vikamea vizuri shamba likapendeza kweli,tulifika wakati wakuanza kupalilia kwahofu ya kuunguza vitunguu ilibidi kutuliza kichwa nilimuomba ushauri mtaalamu wa zao hili na muuzaji wa mbegu ya vitunguu kutoka Mwanza, Charles Mangula.

Alinishauri kununua dawa inayoitwa predator ni dawa ambayo huua majani na kuviacha vitunguu vikiwa na uhai wake kwenye uso wa ardhi, vilinyon'gonyea kwa muda wa wiki nzima ilibidi tuwekee mbolea ya Urea Kg 75 kwaajili ya kurudisha Ile ukijani uliotoweka baada ya kupulizia dawa hii ya kuua magugu, ikumbukwe pia hapo awali tuliweka mfuko mmoja na nusu wa mbolea ya DAP kg75.

Ndugu yangu unayenifuatilia katika Uzi huu nakutahadharisha ,si Kila eneo linafaa kulima vitunguu au zao lolote ,epuka kabisa kwenye mfumo wa maisha Yako kuwa mfano wa majaribio juu ya jambo fulani.Kwasababu ya kutaka mafanikio ya hara Mimi na kibarua wangu tulitegemea mvua zitakuwa msaada kwenye kumwagilia bahati mbaya sana mwaka huo mvua ziligoma.

Ardhi ya Meatu-Simiyu ilikuwa inatulazimisha kumwagilia angalau Mara tatu kwa wiki maana ukiacha ardhi inakuwa ngumu na vitunguu vinasinyaa mno tulipambana usiku na mchana tukihangaika Ili angalau tujikwamue katika shida Ile maana ake iligeuka kuwa shida badala ya fursa,ikumbukwe kuwa baada ya kuona mbegu zimebaki ililazimu kutafuta shamba la dharula Ili tuinusuru mbegu iliyokuwa kitaluni, tulikuwa tumejiandaa vya kutosha kwa vifaa na mtaji wakutosha hatukuwa na dhiki kabisa ya mahitaji.

Kwani kwa mkati tulio uweka tulitaka tupunguze usumbufu wa umwagiliaji wa mashamba yote mawili hivyo, ililazimu kuwa na Generator Moja iliyokuwa ikihudumia mashamba yote mawili, pipes mita 300 mita 150 Kila heka ,Mashine ya kupulizia dawa " kishani mariama"Moja ya pump nzuri sana, Mashine ya kutumia betri hivyo unapokuwa umechoka hunahaja ya kusukuma pump, pamoja na pump 6 manual "Matabi"Moja ya pump imara sana,na box la Kila aina ya dawa utafikiri tulitaka kuanzisha duka, tulikuwa tikijituma sana na kijana wangu wa kazi,rulishauriana kulala masaa kadhaa tu.

Ililazimu kulala saa 10 za jioni na kuamka saa 6 za usiku Ili kwenda kuwaangamiza wadudu waharibifu wa zao hili wanao anza mashambulizi nyakati za jioni na usiku mzima hivyo kuwapulizia dawa nyakati za usiku ni wazo lililo kuwa sahihi zaidi.

Hata hivyo mbali na changamoto hizi za kuvizia wadudu ililazimu Mimi nikamsaidie mfanyakazi wangu Ili asubhi niamkie majukumu mengine ya utumishi wa imma tulifanya hivyo kwa mafanikio makubwa lakini changamoto kubwa ikiwa ni kupishana na wanyama hatari na wakali kama vile tembo na fisi ukizingatia kuwa eneo la Meatu lote ni sehemu iliyomegwa kuwa makazi ambapo hapo awali ilikuwa ni makazi ya wanyama ( Maswa game reserve) hivyo wanyama kama tembo huwa wanaweka historia ya kurudia kupita eneo Moja kwa vizazi na vizazi.

Kwa historia Iko hivi tembo akipita eneo fulani akifa watoto wajukuu na vitukuu,watarudia kupita eneo hilohilo na njia Ile Ile walimopita ukoo wa mababu zao, hivyo ilikuwa hatari mno kwasababu hatukuweza kufahamu kuwa tembo anaweza kuwa wapi kwa wakati huo ukikumbuka kuwa tembo dume akisimama bila kukubughudhi unaweza kupita kwenye uvungu wa miguu yake ukidhani ni upenyo wa njia kwenye kichaka fulani.

Tulipambana kwa nguvu nyingi mno tukikabiliana na wanyama wadogo wadogo kama fisi ambao kwa mwanga wa tochi kali tulizikuwa tukizitumia wasingweza kuhimi maana zilikuwa na uwezo wa kumilika kilometers kadhaa kama hakuna kizingiti Cha vichaka na makazi ya watu.

ITAENDELEA...
Poleeee sana
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom